Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mkanhdara,
Asante kaka. Naona huyu PM ana lengo la kutuondoa kwenye issue. Umeona leo yule mwandishi wa makala gari lake limevunjwa na wameondoka na laptop? Huyu jamaa alikuwa anamwaga data hatua kwa hatua. Kuna mengi ambayo bado hatujui, na hawa wameanza kuhaha. PM usituhadae. Ukweli utadhihiri tu.
 
kaka mukandara hata ingekua miaka 5 au sita iliyopita ..si ajabu kwani mapinduzi ya nyumba upanga [kupanda bei kwa kasi ] hayana hata miaka mitano...hivi karibuni bei ya nyumba imepanda kwa kasi..kuhusu kubomoa ..kwa nini hakubomoa ni uamuzi wake kwani ile nyumba haikua CONDEMNED BUILDING..sasa kama hivi mnapiga kelele angedevolop ghorofa 15...kama hawa ESTATE DEVOLOPERS wengine ingekuwaje....
tofautisha bei ya nyumba kariakoo na upanga ..kariakoo imevamiwa na devolopes waarabu wanajenga maghorofa up to kumi..tatizo ambalo hawajui na serikali haijui linaliokimbiza wapangaji serious kariakoo ni parkin..mtu anajenga 10 storeyed but haweki parking....bei ya nyumba mbavu kariakoo haikuti upanga kaka...kariakoo mnazi mmoja ni 400 million leo..huku mission kota kama unazo 150million unapata ..kule gerezani ni hadi 200 million...umenipata...
kaka jasusi tuko wote hapa mimi sina uwezo wa kuhamisha attention za watu ..wanaohamisha attention ni hao ambao leo mwaka unakaribia wa pili HAWAJAFUNGUA HATA BARABARA MOJA [ILIYOKAMILIKA]......ZAIDI YA MANENO TU...WE NEED OUTPUT NOW!!!!!!!!!!!!!!!
 
kaka mukandara hata ingekua miaka 5 au sita iliyopita ..si ajabu kwani mapinduzi ya nyumba upanga [kupanda bei kwa kasi ] hayana hata miaka mitano...hivi karibuni bei ya nyumba imepanda kwa kasi..kuhusu kubomoa ..kwa nini hakubomoa ni uamuzi wake kwani ile nyumba haikua CONDEMNED BUILDING..sasa kama hivi mnapiga kelele angedevolop ghorofa 15...kama hawa ESTATE DEVOLOPERS wengine ingekuwaje....
tofautisha bei ya nyumba kariakoo na upanga ..kariakoo imevamiwa na devolopes waarabu wanajenga maghorofa up to kumi..tatizo ambalo hawajui na serikali haijui linaliokimbiza wapangaji serious kariakoo ni parkin..mtu anajenga 10 storeyed but haweki parking....bei ya nyumba mbavu kariakoo haikuti upanga kaka...kariakoo mnazi mmoja ni 400 million leo..huku mission kota kama unazo 150million unapata ..kule gerezani ni hadi 200 million...umenipata...
kaka jasusi tuko wote hapa mimi sina uwezo wa kuhamisha attention za watu ..wanaohamisha attention ni hao ambao leo mwaka unakaribia wa pili HAWAJAFUNGUA HATA BARABARA MOJA [ILIYOKAMILIKA]......ZAIDI YA MANENO TU...WE NEED OUTPUT NOW!!!!!!!!!!!!!!!


MMh mwanangu weeh!! Kamua kamua kamua! na kanyaga twende........
 
Phillemon Mikael,
nafikiri una miss point hapa. Kariakoo nyumba zinazouzwa ni nyumba za watu binafsi sio nyumba za serikali..makosa mengine yote ni makosa ya city na wizara ya ardhi. makosa ya utendaji kazi SIO rushwa ama WIZI wa mali ya Umma. Mkapa mwizi kaiba hana tofauti na Mobutu wa Zaire!
Hilo swala la bei limekuja baada ya wewe kutoa uhalali wa Mkapa kununua nyumba ile kwa 500,000. Ambayo wewe leo hii unadai inaweza kuuzwa kwa 1.2/m. Nyumba ambayo Mkapa hakuijenga wala kuingiza senti tano yake zaidi ya mkopo (usio halali pia).. leo hii iina maana kajizalishia zaidi ya 500,000 bila kutoka jasho. Hilo ni jumba moja tu acha mengine ambayo yanamilikiwa na mkewe!..
Wewe kwa akili yako huoni kama huu ni wizi mkubwa? wizi ambao viongozi wote wa Kiafrika wamekuwa wakitumia nguvu ya wananchi kujitajirisha wao!..Trust me, hiyo nyumba ingewekwa 1,000,000 wakati akinunua ingeondoka kama upepo wa alfajiri!...Unajua kodi wanayolipa benki pale?.. unajua Mkapa anaingiza ngapi tena bila kulipa kodi! and you think it's OK!
Na nakuhakikishia kwamba leo hii ukienda na USd 2/m - Mkapa hakupi nyumba hiyo!... Sio swala la market value ni swala la kuibia wananchi mali yao kodi halipi na bado tunamlipa mafao yake kama rais mstaafu.
 
Kuna hoja kwamna upo uwezekano wa kumshitaki Mkapa kwa jinai na kwa madai. Wapo wanasheria wanaosema kwamba katiba ya Tanzania inatoa kinga kwa Rais anapokua katika kazi zake za URAIS. Sasa kama mtu anapatikana na tuhuma zinazohusu kula rushwa, kuua mtu kwa ugomvi nyumbani kwake, kufanya uhalifu wowote usiohusiana na kazi za URAIS, a nakua hana kinga yoyote. Hapo kuna kila sababu sasa wanasheria wakaweka wazi kama kuna rushwa ama jinai kumhusu Mkapa, basi hakutakua na sababu ya kutomshitaki.

Kuhusu jinai ikiwa wananchi wataona kwamba Mkapa ama yeyote alichukua mali za umma, wanna haki ya kufungua kesi ya jinai mahakamani na kutaka mali hizo zirudishwe mikononi mwa umma zikalipie elimu na hospitali kwa wasio na uwezo.

Kaka Halisi naomba nikushauri kidogo.

Ingawa kwa kiasi kikubwa nakubaliana na fikira zako na haswa ile ya kuwa CCM haiponyeki kutoka katika hali iliyonayo sasa lakini ukweli unabaki palepale kuwa kubomoka kwa CCM kwa sasa ni hatari kwa taifa letu. Mazingira tuliyonayo haswa ukaribu wa Asasi zetu za Kiusalama, manyang'au wa nje na wa ndani na hili genge la CCM ni dalili isiyopingika kuonyesha nini kitakachotokea katika nchi yetu mara genge hili litakapoboka vipande vipande kama ambavyo mikakati hii na mingine mingi inayoendelea inavyolenga.

Unajua wazi kuwa hadi sasa hakuna mbadala makini wa CCM kimfumo. Ni vizuri kuendelea kulinda busara za kuwaheshimu viongozi wetu wastaafu hadi hapo tutakapokuwa tayari tumefanyia kazi ya kuandaa mazingira ya Tanzania bila ya CCM.

Inasikitisha kuwa ushauri wangu unatia uchungu mno lakini ndio ukweli wa hali halisi na ni mujibu wetu kuthamini busara hizi hata kama tunatambua kuwa ni usaliti kwa walalahai na walalahoi wa Tanzania.

Tanzanianjema
 
Tanzanianjema,

Maelezo yako yamepokelewa lakini haitawezekana tukaacha sheria kuwa chini ya viongozi..hadi lini?
Lazima tufanye mabadiliko na siku kiongozi mmoja ataweza kusimamishwa mahakamani ndio siku mapinduzi ya kifikra yatapata mwanya na sheria kuanza kutumika. Malawi na Zambia wameweza bila machafuko..nchi kibao zimeweza kufanya yasiyowekana kwa kupitia korti zao!
Labda nambie hatari ni pale Mkapa atiwe ndani bila kupitia mahakama!...
Vyovyote vile kama kesi inaweza kufunguliwa basi na ifanyike mengine yatajitokeza...
Wa Tanzania ni watu wa kusikiliza zaidi ya ku-react!
 
Kaka Mkandara Malawi na Zambia ni vurugu tupu. Usanii kibao. Nimetembelea huko hivi karibuni na kupata wasaa wa kuangalia hali ya mambo kutoka jikoni. Hawana tofauti na watani wetu Kenya na usanii wa NARC yao.

Nadhani jukumu la ku-prioritise lisiwe linaelekezwa kwa watawala tu. Hata sisi watawaliwa" tunapaswa kujifunza hilo. Priority sasa iwe kupunguza makali ya unyang'au miongoni mwa waliopo madarakani sasa wakati tukiandaa mazingira ya mabadiliko makini na salama. Tukiweza hilo tutakuwa na nafasi ya kuwawajibisha hao waliopita hata kama itakuwa ni vizazi vyao vinavyojifaragua na utamu wa "mafanikio" ya wazee wao.

Tusipoangalia tutakuwa tunapiga mark time huku tukiwasaidia wajanja wa sasa kutupiga bao kiulaini.

Tusiache kusema lakini lazima tuwe na mstari mnyoofu wa kutokiuka kwa sasa. Kuna vitu ambavyo hali ya kimazingira inatulazimu kuvivumilia tuu kwa sasa kwa manufaa ya baadae. Mabadilko makini yanakuja kwa jitihada za muda mrefu. Tuepuke na kupenda njia za mkato ambazo kitu pekee tutakachopata ni kufurahisha nyoyo zetu kwa muda mchache na kuhatarisha usalama wa hata hicho kidogo tulichonacho.

Inauma lakini ndio ukweli...

Tanzanianjema
 
Kaka Mkandara Malawi na Zambia ni vurugu tupu. Usanii kibao. Nimetembelea huko hivi karibuni na kupata wasaa wa kuangalia hali ya mambo kutoka jikoni. Hawana tofauti na watani wetu Kenya na usanii wa NARC yao.

Wait a minute, ya huko Malawi na Zambia siyajui, lakini hivi kweli tunaamini we are doing better than Kenyans politically, economically and otherwise?

Kwa maoni yangu hatuhitaji profesa wa sayansi ya siasa kujua kwamba wenzetu Kenya kidemokrasia wapo juu. Leo hii wananchi wa Kenya angalau wametambua nguvu walizo nazo dhidi ya serikali yao, kwamba anytime uchaguzi ukija wana uwezo wa kuwatoa viongozi kwenye madaraka kwa kura. Watanzania hatuna ung'amuzi huu na pengine taasisi zetu ni tete katika hili.

Vilevile hatuhitaji Mwalimu Moshi kutusomesha ili kujua kuwa uchumi wa Kenya umekua mara mbili na umaskini umepungua kwa asilimia 18 tangu hiyo NARC mnayoikiandia iingie madarakani.

Jamani, tusidanganyane, wakenya hawajuti kuitoa KANU madarakani. These guys are ever optimistic of their future, wakati sisi matumaini yanazidi kutoweka kila kukicha.

It is a lazy execuse to say that the situation is not ripe for the CCM to go on the pretext that there is no alternative as yet. Hivi TN nieleze hawa genge la wahuni la viongozi wa CCM akina JK, Kamala, Membe, Rostam, etc wanafanya kitu gani cha maana ambacho watu kama akina Lipumba, Mbowe,Zitto, Mnyika, Bimani, Lwakatare, Slaa, Akwilombe, etc wasingekifanya? Put it differently, hawa jamaa wa CCM wana qualifications zipi special ambazo watu wa upinzani hawana?
 
Kwa maoni yangu hatuhitaji profesa wa sayansi ya siasa kujua kwamba wenzetu Kenya kidemokrasia wapo juu. Leo hii wananchi wa Kenya angalau wametambua nguvu walizo nazo dhidi ya serikali yao, kwamba anytime uchaguzi ukija wana uwezo wa kuwatoa viongozi kwenye madaraka kwa kura. Watanzania hatuna ung'amuzi huu na pengine taasisi zetu ni tete katika hili.

Sipingi kuwa hawa jamaa kiuchumi wameweza kuamka wakati sis tumeanza kurudi usingizini lakini kisiasa ni vurugu na usanii tuu. Mafanikio yote unayosema yanaonekana sasa ni mafanikio tete ambayo anytime yanasubiri muwasha kibiriti katika ghala la petroli.

We need and deserve better than that and only with long term strategy we can achieve sio oppurtunism.

Tanzanianjema

Tanzanianjema
 
Tanzanianjema,
matokeo ya kiuchumi hiyo ni hatua nyingine kabisa ktk kumuwajibisha Mkapa!... inaweza kuwa sera za Jk hazifanyi kazi awepo Mkapa ama asiwepo. Nilidhani hapo awali ulikuwa ukimaanisha kutokea kwa machafuzi kama Mkapa atawajibishwa lakini kama una maana ya maendeleo baada ya operation ya Rushwa! Hilo tena linategemea na sera za chama na wananchi wenyewe. lakini kuondoa doa ktk utawala na sheria kukamata ni muhimu kwanza kabla ya matumaini ya maendeleo ya kiuchumi. Who knows labda kinachoturudisha nyuma Tanzania ni Rushwa peke yake! Bila rushwa tunaweza kupata viongozi imara na wenye uzalendo!.
 
It is a lazy execuse to say that the situation is not ripe for the CCM to go on the pretext that there is no alternative as yet. Hivi TN nieleze hawa genge la wahuni la viongozi wa CCM akina JK, Kamala, Membe, Rostam, etc wanafanya kitu gani cha maana ambacho watu kama akina Lipumba, Mbowe,Zitto, Mnyika, Bimani, Lwakatare, Slaa, Akwilombe, etc wasingekifanya? Put it differently, hawa jamaa wa CCM wana qualifications zipi special ambazo watu wa upinzani hawana?

Kaka nchi haiendeshwi kwa personality. Mfumo wa utawala Tanzania ni komavu mno kiasi kwamba kuubadilisha kunahitaji umakini wa hali ya juu. Naijua vizuri CHADEMA na ingawa nawaheshimu sana hawa ndugu zangu lakini huwezi kuniambia tu risk kubomoa tulichonacho kutegemea wao kama mbadala. Wanahitaji kujijenga zaidi na kama kweli una uchungu na Tanzania yako timiza wajibu wako kutimiza mipango yao amabyo nakubali kuwa ukiacha usanii mchache ina dalili nzuri.

Tusiwe kama wamarekani wanaojidai kuwa tatizo ni Bush wakati ni wazi tatizo ni mfumo mzima wa kisiasa na kimaisha wa wamarekani ambao ndio umezaa kina BUsh na wengineeo wenye sura tofauti lakini dugu moja.

Tanzanianjema
 
Tanzanianjema,
Who knows labda kinachoturudisha nyuma Tanzania ni Rushwa peke yake! Bila rushwa tunaweza kupata viongozi imara na wenye uzalendo!.

Sina upinzani na hoja hii lakini jee mfumo mbadala upo wapi? Je tunaweza kujenga nchi kama yetu ambayo ipo katika dunia hii ya dola tete kwa kubahatisha?

Tusikwepe majukumu ya kujenga mbadala makini. Na ujenzi huo unaanza nasi binafsi kujenga uthubutu wa kuwa tofauti hata kama tupo ndani ya tabaka tawala ama tuna uhusiano maalumu na watwala na hata kuwaunga mkono wale walio mstari wa mbele badala ya kuwadharau na kuwadhihaki kila kukicha.

Tusipoangalia tutawafaidisha mademagogue ambao wapo mkao wa kula tuwafanyie kazi wao wajikingie.

Tuthubutu kujenga Tanzania mbadala itakayoweza kutusuluhushia changamoto tunazokumbana nazo sasa na sio mbadala wa kufurahisha nyoyo zetu tu.

Tanzanianjema
 
Tanzanianjema,

Mimi nina hakika Tanzania ina mifumo Mbadala ktk makbrasha ambayo inahitaji Viongozi bora tu. Ardhi tunayo, watu wapo na hata siasa safi bado tunayo pamoja na kwamba tobo zipo.. Ila tatizo kubwa la Tanzania ni viongozi wabovu ambao wanatumia ardhi yetu na watu wake kupindisha sheria ambayo imetokana na mfumo huu unaozingatia Soko huria.

Sasa kama hatuweza kuwawajibisha viongozi waliopendisha sheria za nchi kwa manufaa yao kutokana na kuwepo soko huria itakuwa tunafanya suicide!.. na jinsi tunavyoendelea kuogopa uyoga huu sumu unazidi kukua.

Kama Sokoine alivyokuja na Ufagio wa Chuma, Tanzania tulipumua kidogo kwa Rushwa lakini bahati mbaya mfumo wetu wa Kijamaa hauweza kufanya kazi ktk dunia yenye vita baridi...
leo hii hakuna tena vita baridi, tumepata wawekeshaji wa kila namna na nchi yetu kila siku inazidi kuvumbua Utajiri mbali kabisa na uwezo wa wananchi kuzalisha ktk kilimo na viwanda. Tunahitaji uzio wa kuzuia nyani hawa kutoingia shambani lakini tukianza kutunga sababu za kumwondoa nyani shambani basi mavuno yetu hayawezi kuwa mazuri na umaskini utaendelea kuwepo. Utathubutu kuijenga vipi nchi hali pakacha letu limetiwa tobo?... huoni kama nguvu ya mwananchi kufikiria sio kulijaza maji pakacha ila kuliziba pakacha hilo...

Tanzanianjema hata uwe mjuzi vipi wa kuendesha gari huwezi kwenda mbali na gari lenye pancha!... ziba pancha mengine yatafuata, ktk abiria yupo mwenye uwezo wa kuliendesha kama wewe umechoka!
 
Mzee Mkandara,

Somo lako ni kali sana. Hii mifano yako ya kuzuia nyani kuvamia shamba na
hili la pancha na mifano hai ambayo hata haihitaji kuelezea mara mbili.

Bahati mbaya sisi wananchi wengi tunahangaika kubugia Ugimbi kiasi kwamba
hatuna muda na kuyafukuza hayo manyani. Baada ya miaka hakutakuwa na mahindi, ugimbi utakuwa bei mbaya, manayani yatakuwa yamejazana na yana nguvu hata uwezo wa kuyafukuza hatutakuwa nao tena. I hope hatutafika huko kama hatujafika bado.

Mwalimu alimwambia Shivji anaandika uongo kuhusu class struggle in Tanzania. Huenda alikuwa sahihi, class struggle sasa ndio ipo na inazidi kupanda.

Si umesikia hata bodi ya mikopo imekuja na makundi A, B,C,D,E na F. Hata huku Ulaya hakuna makundi mengi kiasi hicho. Kundi A nafikiri ndilo la Manyani
angekuwa Nyerere angeita Manyang'au, hayana aibu, yanavamia kilicho cha wazee, kilicho cha watoto hata kilicho cha Wagonjwa. Wanaita fursa sawa kwa wote kumbe ni utajiri kwa wachache. Haya ndiyo Manyani yanayofanya biashara bila aibu mpaka Ikulu.

Mkandara wewe uko wapi kwenye hayo makundi? I hope sio mtoto wa Nyani (kundi B) Ha ha haaaa!!!
 
Mtanzania,

Duuuuh! mimi kundi langu halina hata pepo!... Unajua waislaam ukiwa na jina Mahmood at least malaika wanaweza kuelewa wakakupa Asalaam aleikum lakini jina Mkndara mjomba hao malaika itabidi waniweke kando kunitoa ktk mstari wa immigration kuingia peponi. Haya Upande wa wakristu ndio kabisaaa jina Mkandara linahitaji Ubatizo!.... sina pepo! Haya huko peponi..

Hapa duniani Mkandara ni jina lisilo kuwa na Address...ndio yaleyale ya kuulizwa Makanda what? ...I mean wewe mtoto wa nani?..mmmmmnnnhhh! mara unakatiwa simu kama Mzee wetu Mwanakijiji.
 
ACTIVISTS RAIL ANBEM LTD BUSINESS DEALINGS AS: Abuse of office

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


OPPOSITION leaders and legal experts have accused former president Benjamin Mkapa and his wife of abuse of office following their controversial establishment of their own private company and actively doing business as entrepreneurs while still in public office at State House.

Several political and legal commentators have maintained that while the act of registering a company wasn’t illegal in itself, doing business as sole directors of a company while serving the nation at the highest level was unacceptable.

The national chairman of the opposition Civic United Front, Prof. Ibrahim Lipumba, has now challenged the former president to publicly declare his wealth. This comes in the wake of revelations that Mr Mkapa and the former First Lady, Anna Mkapa, registered their own private company, ANBEM Limited in 1999, just four years into his presidency.

The CUF leader accused Mr Mkapa of abuse office, saying the decision of the former president to call himself an ’’entrepreneur’’ while entrusted with the full-time job of leading Tanzania was scandalous.

’’Mkapa declared his wealth in 1995 when entering office, but I haven’t heard him listing his assets after leaving public office,’’ Prof. Lipumba said.

He added: ’’The act of starting his own private company and operating as sole directors of the company with the First Lady while still at State House amounts to abuse of that public office.’’

Dr. Sengondo Mvungi, an opposition leader and law lecturer from the University of Dar es Salaam, criticised the former president for starting a company with the First Lady well into their first term in office.

’’When Mr Mkapa registered his own company before even finishing his first term in office, did this mean that the state could not adequately provide for him and his family?’’ He queried.

’’I think it was nothing other than the selfishness of our political leaders in office.’’

Like Prof. Lipumba, Dr Mvungi also stated that doing business while at State House constituted abuse of public office.

’’I will be surprised if no action is taken ... this will send a wrong message to Tanzanians and set a bad precedence that our leaders can do anything with impunity while in office,’’ he charged.

’’You cannot just do as you wish and hide under the cover of presidential immunity.’’

A top government official told THISDAY that while there is no specific law prohibiting a sitting president from starting an own company while at Ikulu, the practice was inherently unethical.

’’To have a sitting president and First Lady actually start their own company in the middle of their presidency and serve as sole directors of the company is quite extraordinary,’’ said the government official who preferred not to be named.

The Code of Ethics Act (Amended) of 2001, which is also cited as Act No. 5 of 2001, covers issues of code of conduct and ethics for civil servants.

The Executive Director of the Legal and Human Rights Centre (LHRC), Ms Helen Kijo-Bisimba, said she was personally shocked by revelations of the former State House couple doing business from Ikulu.

’’It is totally unbelievable ... this is against principles of good governance and public leadership ethics,’’ she said.

Ms Kijo-Bisimba said the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, had set ’’very high standards for integrity, modesty and sacrifice to the nation.’’

It now appears that all these noble ideals died with Mwalimu in 1999, noted Ms Kijo-Bisimba, echoing the sentiments of many other activists.

Likewise, Mr Tundu Lissu from the Lawyers Environmental Action Team (LEAT), criticised the Mkapa family’s business dealings while at Ikulu, saying the presidency was a full-time job and demanded all the concentration and attention of the incumbent.

’’There is no immunity for abuse of office ... Tanzanians as lawful citizens of this nation can rightly decide to take legal action,’’ he remarked.

A veteran lawyer and politician, Mr Mabere Marando, noted that while the law is silent on business dealings done by a sitting president, there were issues of conflict of interest and undue influence to consider.

’’Tanzanian laws are silent on the issue of the president doing business while in office ... But is there any bank manager who will say no to the president when he applies for a loan?’’ He queried.

The company owned by former president Benjamin Mkapa and first lady Anna Mkapa applied for and was granted a hefty $500,000 loan from the National Bank of Commerce Limited in 2002.

With the then State House couple acting as sole directors, ANBEM Limited also received an additional loan of 250m/- from CRDB Bank Limited in the same year.

THISDAY has sent written questions to Mr Mkapa’s office in Dar es Salaam regarding the nature of the business transactions conducted by himself and Mrs Mkapa while at Ikulu. No response has been forthcoming so far.
 
Hawa THISDAY wajue kwamba Mkapa ana kesi ya kujibu:

1. Hiyo kampuni ilikua ikiendesha shughuli zake katika majengo ya EOTF, mali ya serikali bila kulipa kodi ya pango wala bili ya umeme, mai na hata watumishi na samani za serikali
2. Hiyo kampuni ilipewa pesa (ilizoita mkopo) hata kabla ya kuwa na hati ya nyumba na hivyo kupata fedha za kununulia nyumba
3. Waliopo ndani kabisa ya mfumo wanasema hata fedha zilizotolewa kama mkopo ni mazingaombwe kwani zilikua ni ahsante kwa kufanikisha upatikanaji wa NBC, lakini pia kuna ushahidi wa maandishi kwamba uongoozi wa NBC ulikua ukiipa kampuni ya Ben fedha bila maelezo
4. Mkapa na mkewe walidanganya (kinyume cha sheria ya makampuni) kwamba wao ni Wajasiriamali na baadaye kujiita wakurugenzi hata kabla ya kampuni kusajiliwa. Hilo ni kosa la jinai

5. matumizi mabaya ya madaraka kisheria ni rushwa chini ya sheria ya Kuzuia rushwa. Kosa lingine la jinai

Wananchi wafahamishwe ili waweze kuchukua hatua kama walivyofanya wenzao wa Zambia
 
Waende BRELA wakaangalie, Adress ya ANBEM ni Plot namba 15, Luthuli Road, Upanga, Ilala District, Dar es Salaam, halafu waende katika website ya EOTF au waende tu pale zilipo sasa ofisi za NGO ya Wanawake na MAendeleo (WAMA) ya Salma Kikwete
Equal Opportunities for All Trust Fund (EOTF)
15 Luthuli Road
P.O.Box 78262 Dar-es-Salaam
T a n z a n i a

Tel.: +255-22-2114512

Fax.: +255-22-2114793

eMail: eotf@raha.com or eotf@cats-net.com
Web: EOTF.OR.TZ

http://www.eotf.or.tz/modules.php?n...r.tz/modules.php?name=News&file=article&sid=4
 
Halisi,

Shukrani nyingi sana na nimefurahi sana kuona mwanzo huu mpya wa wananchi kutokubali kuburuzwa (Kutawaliwa)...Shukrani zaidi kwa Lipumba na LEAT kwa kuongoza madai haya mbele ya sheria!
JF tuongeze nguvu zetu, sauti zetu na hakika wapo waungwana wanaoweza kuyapeleka malalamiko yetu mbele. Madai yetu dhidi ya Mkapa ni halali kabisa na huu ndio uwe mwanzo wa kufichua viongozi woote waliotumia nafasi zao kujitajirisha!....Hii ni dhulma!.... dhulma ya nguvu na jasho la wananchi maskini ambao hata kula yao ni shida...

LAZIMA tuzibe pakacha!...tumeanza kwa Mkapa nina imani wengi watabainika chini ya darubini za mwananchi wenye machungu na nchi yao!
 
Huyu Mkapa anakiburi cha hali ya juu. Pamoja na waandishi wa habari wa THIS DAY kumuomba kiungwana kujibu tuhuma za kufanya biashara wakati akiwa Ikulu, yeye kwa kujua hakuna lolote litakalofanyika dhidi yake ameamua kukaa kimya kama yote aliyoyatenda hayana walakini.

Huyu alipoingia Ikulu aliita awamu yake ni "awamu ya uwazi na ukweli" na akamteua Mh Warioba afanye uchunguzi wa kina kuhusiana na rushwa Tanzania. Wote tunajua ripoti hiyo ilipowakilishwa kwa Mkapa aliifanya nini.

Tuhuma mbali mbali zilianza kujitokeza katika "awamu hii ya uwazi na ukweli"

Kwanza kabisa ilikuwa ni kuiingiza kampuni ya makaburu pale TANESCO kwa mtutu wa bunduki. Pamoja na kuthibitika kwamba wale makaburu hawakuwa na uzoefu wowote katika kuendesha shirika kubwa kama TANESCO, Mkapa hakusikia la jini wala la shetani. Pia kulikuwa na tuhuma kwamba kampuni ya shemeji yake Mkapa ambayo mkurugenzi ni huyo shemeji yake na watoto wake ndiyo ilihusika na kuwaleta makaburu wale. Pamoja na kulipwa mabilioni ya pesa hatima ya "Net group Problems" ilikuwa ni kuicha TANESCO ikiwa hoi bin taabani.

Tuhuma zikaendelea katika mikataba ya madini. Minon'gono ikaanza kwamba mikataba ilisayosainiwa na Tanzania na "wawekezaji" haina maslahi yoyote kwa Tanzania, kwani Tanzania ilikuwa inapata asilimia tatu tu nao "wawekezaji" hawakutakiwa kulipa kodi. Juhudi za wabunge kuiona mikataba hiyo ziligonga ukuta, pale Mkapa alipodai kwamba mikataba imeshasainiwa na hakuna haja ya kujadiliwa bungeni.

Tuhuma za ununuzi wa Rada, pamoja na kuonekana Rada iliyonunuliwa ilikuwa ni gharama kubwa na wananchi wengi kupinga ununuzi wa Rada ile, Mkapa kwa mara nyingine tena hakusikiliza vilio vya Watanzania. Rada ilinunuliwa kwa $40 millioni na baada ya miaka michache bomu likalipuka kwamba muhindi ambaye ndiye alikuwa wakala wa ununuzi wa Rada ile alijipatia $12 milloni kama commission, mpaka sasa hivi hatujui hatima ya "uchunguzi" kuhusiana na ununuzi wa Rada ile.

Hivi karibuni pia kulizuka tuhuma za kuhusiana na ununuzi wa magari ya jeshi, ambao pia ulionekana kufanyika katika mazingira ya kutatanisha na yule yule muhindi ndiye alikuwa wakala wa ununuzi wa magari ya jeshi na ndege ya Rais iliyonunuliwa wakati Mkapa amebakisha miezi michache kumaliza muda wake.

Tukifuatilia kwa makini tunaona kabisa kwamba tuhuma ni nzito dhidi ya Mkapa. Hata siku moja hakuwa tayari kusikiliza vilio vya wananchi pale ambapo walikuwa wanaona hakuna maslahi ya nchi au matumizi yalikuwa makubwa ukilinganisha na uwezo wa nchi yetu. Vilio vya wanachi Mkapa alivibeza kwamba "Watanzania wamejawa na wivu."

Ukiweka na shutuma za karibuni kama vile Richmonduli n.k. inaelekea viongozi wetu hawana woga wala simile katika kufanya wanavyotaka ili kujitajirisha wao na familia zao. Hali kama hii inatishia sana mwelekeo wa nchi yetu kwani wananchi wanaona wanapuuzwa tu, viongozi wamekuwa kama wafalme chochote wanachoamua hata kama ni kinyume na maadili ya uongozi au hakina maslahi kwa Tanzania kinaendelea kufanyika tu bila woga wowote.

Mungu apishilie mbali, lakini kitendo cha Mkapa kukaa kimya dhidi ya tuhuma nzito zinazomkabili (kufungua biashara akiwa Ikulu, ununuzi wa Rada, Ndege na magari ya jeshi ambapo inaonyesha alikuwa mshiriki kuu katika maamuzi) na kitendo cha kuzuia tuhuma za Richmonduli zisijadliwe Bungeni ni ishara kwamba Tanzania inaelekea kubaya.
 
Back
Top Bottom