Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mimi kinachonishangaza ni hawa viongozi wetu kutokuwa na huruma wala utu kwa watu wanaowaongoza, Mimi huwaga sipati picha kabisa kwa hawa viongozi kwenda kuchota fedha za watu (NSSF/PPF nk)ambazo watu wamezitolea jasho kwa kuzifanyia kazi usiku na mchana na manyanyaso ya kila aina makazini, na siku mtu anapokwenda kufuata pension yake inakuwa ni shida mno kuzipata hizi fedha ambazo ni zako, lakini kwa upande mwingine hawa wanaojihita viongozi wetu ndio wanakuwa mstari wa mbele kwenda kuzichota bila ugumu wowote, inauma sana
 
Mimi Nafikiria kuwa Labda kura ya maoni iitishwe ndio labda sisi Watanzania tunaweza kusema kuwa yeye ni msafi, Ukweli unabaki kuwa ni Fisadi tu hata kama wamsafishe kwa kutumia maji ya baharini bado ni fisadi au mahakama
 
Sakata la watumishi hewa wizara ya elimu,wahasibu wote wamehamishwa kama kafara. Lakini wahusika wakuu waliosuka ule mpango wameachwa bila kuguswa. Hakuna aliyepelekwa mahakamani wala kuhojiwa.

Viongozi wetu wana matatizo ya akili, narudia tena wala sijakosea VIONGOZI WETU WANA MATATIZO YA AKILI.
 
Sasa hiki ndo kipimo cha hawa wapiganaji wa Ufisadi wa CCM, wenyewe lengo lao ni kupambana na ufisadi. Sio kupanda majukwaani tu kuongelea ufisadi hewa! kuanzia kwa Spika na wabunge wenzake wapambanaji, huu ndo wakati wa kuwaona kwenye Bunge lijalo kwani hii issue ya Kiwira ililala kipolo hadi Bunge la November 2009.

Isiwe Dr. Slaa kila mara ndo akae anastua serikali na huku tunawabunge wanaojiita ni wapambanaji wa Ufisadi. Ukiwachunguza tokea mwanzo mara nyingi wenyewe wanakimbizana na watu wawili RA na EL na kuacha viongozi walioasisi ufisadi.
 
Tunao wapambanaji wa aina mbili. Wale wanaopambana kulinda maslahi ya mwananchi na wale wanaopambana kulinda nafasi zao za kisiasa ambazo zinaonekana kutishiwa na hao mafisadi!
Hata hivyo ipo siku Mkapa atasimama kizimbani, ni suala la muda tu.

Na hawa NSSF nashindwa kabisa kuwaelewa. Wanakopesha sana kwa makampuni, inakuwaje wanashindwa kuwakopesha wanachama wa mfuko ambao kimsingi ndio wenye hizo fedha? Ni vema sheria ya NSSF ikaangaliwa upya ili wanachama waweze kukopa kwa dhamana ya akiba yao.
 
Hakuna dalili yoyote ya kunishawishi kwamba serikali ina nia ya kuchukulia hatua uovu wowote unaofanywa na vigogo wake. Kama kungekuwa na nia hiyo tungeshaona ya sasa yakifanyiwa kazi. Kama kweli serikali imeshindwa kushughulikia matatizo yanayotokea sasa, ndio itajifanya kuwa na ubavu wa kushughulikia ya uongozi uliopita?

Kikwete aanze kwanza kudhibiti ujinga unaoendelea kwenye uongozi wake kabla ya kusingizia yaliyopita. Hawa ni watu wake amewaweka mwenyewe na ana mamlaka nao directly. Mbona hawakemei? Mbona hawawajibishi? Kila siku kisingizio chake ni ushahidi - eti asije akmwonea mtu asiye na hatia. Tumeona akina Lowasa, Chenge et al ambao ni watu wake; ushahidi upo lakini bado wanaitwa waheshimiwa na wako kwenye nyadhifa mbalimbali. Tumeona ya mabomu Mbagala, hakuna hatua hadi leo. Hayo tena ya mishahara hewa ya walimu, hutasikia chochote mpaka kesho. Na mengine mengi maovu usiyotaka kuyajua maana unaweza kutamani kuhama nchi.

Kama yote hayo yameachiwa, halafu utuambie eti kuna kesi mahakamani? Kesi za nani kwa nini? Tunajua kesi zenyewe viini macho tu! Ndio maana anamtetea Mkapa kwamba asipelekwe mahakamani maana anajua kesi yake haitaenda popote.

Ili kurudisha imani kwa wananchi, serikali ingefungua ukurasa mpya. Kwamba kuanzia leo kwenda mbele tunaongoza kwa kuonyesha mfano wa usafi. Atakayechemsha, zembea au kuiba hatua hapo kwa papo. Then tuangalie ya nyuma na kuwachukulia hatua walioharibu miaka hiyo (baada ya sisi wa leo kuonyesha usafi wetu). Itakuwa ngumu sana kumshitaki mtu aliyefanya kitu kilekile unachofanya wewe sasa hivi!

NB: Wapenda ufisadi na dhuluma waendelee tu; iko siku watafikishwa mbele ya vyombo visafi vya haki hapahapa duniani. Kuna mfaransa mmoja anashikiliwa kwa kosa alilotenda zaidi ya miaka 30 iliyopita! Mungu atujalie uzima, kama rekodi zao zipo tutawashughulikia tu. Wapiganaji msichoke wala msikate tamaa.
 
Sasa hiki ndo kipimo cha hawa wapiganaji wa Ufisadi wa CCM, wenyewe lengo lao ni kupambana na ufisadi. Sio kupanda majukwaani tu kuongelea ufisadi hewa! kuanzia kwa Spika na wabunge wenzake wapambanaji, huu ndo wakati wa kuwaona kwenye Bunge lijalo kwani hii issue ya Kiwira ililala kipolo hadi Bunge la November 2009.

Isiwe Dr. Slaa kila mara ndo akae anastua serikali na huku tunawabunge wanaojiita ni wapambanaji wa Ufisadi. Ukiwachunguza tokea mwanzo mara nyingi wenyewe wanakimbizana na watu wawili RA na EL na kuacha viongozi walioasisi ufisadi.
Na ndio hapo kwenye matatizo na CCM tunataka list yao ya mafisadi au ndiyo ile ya Dr.Slaa
 
• Serikali yatakiwa kuiacha mahakama iamue

na Sauli Giliard
Tanzania Daima

SIKU moja baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Sophia Simba, kuzishutumu nchi wahisani kwa kuvitumia vyombo vya habari kushinikiza kushtakiwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, baadhi ya wasomi na wanasiasa wamesema waziri huyo hamtakii mema kiongozi huyo mstaafu.

Wakizungumza na Tanzania Daima, kwa nyakati tofauti, wameeleza ya kuwa ni vema mkondo wa sheria ukachukua nafasi yake katika suala hilo la Mkapa, kuliko serikali kuendelea kumkingia kifua dhidi ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili.

Juzi, Waziri Simba, alisema Mkapa hawezi kufikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa matumizi mabaya ya madaraka, kwa kuwa tuhuma dhidi yake hazina msingi wowote na serikali haina mpango wa kumshitaki.

Profesa Mwesiga Baregu, aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kiongozi huyo anaweza kusafishwa iwapo mchakato wa kimahakama utafuatwa na kile kitakachoamuliwa ndicho kitaaminika.

Alisema Mkapa anahusishwa na kashfa kadhaa, ikiwemo ile ya kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira wakati akiwa madarakani pamoja na kuruhusu misamaha mbalimbali ya kodi isiyo na tija kwa taifa.

"Tuache mahakama imsafishe Mkapa na wala si serikali kama inavyofanyika hivi sasa, amefanya mambo mengi mazuri, lakini kama ana kashfa kwa nini asiwajibishwe?" alihoji Profesa Baregu.

Aliongeza kuwa, mengi yamefanyika chini ya utawala wake, ikiwemo ununuzi ya ndege ya rais kwa bei ya juu, huku baadhi ya watendaji wake wakihusishwa na rushwa.

Alisema kama Waziri Simba anampenda na kumtakia mema kiongozi huyo mstaafu, hana budi kuruhusu apandishwe kizimbani ili asafishwe moja kwa moja.

"Sophia hamtakii mema Mkapa, angeiachia mahakama imsafishe na Watanzania waweze kumwamini kwani amehusishwa na tuhuma nyingi. Naona kushtakiwa ni mchakato wa kumsafisha.

"Anapaswa kusafishwa na mahakama pekee kwani Watanzania wataweza kujisikia ya kwamba kweli kiongozi huyo alikuwa na mchango," alisisitiza mwanazuoni huyo.

Akielezea zaidi, Prof. Baregu alipingana na hoja ya Waziri Simba kuwa, kiongozi huyo analindwa na uadilifu wake, na kusisitiza kwamba tuhuma zilizoelekezwa kwake ni nzito, ikiwemo kufanya biashara akiwa Ikulu, na hazina uhusiano na madaraka yake kama rais.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, alilieleza Tanzania Daima kuwa, kitendo cha waziri huyo kuzifananisha shutuma dhidi ya Mkapa na zile zilizokuwa zinamkabili Rais wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba, ni upotoshaji.

Alisema kila taifa lina katiba yake ambayo kwa vitendo alivyofanya Mkapa, havihusiani na nafasi yake kama urais, hivyo hana kinga ya kutoweza kupandishwa kizimbani.

"Zambia ina katiba yake na sisi tunaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katiba ya nchi iachwe ifanye kazi yake. Ya Chiluba na Zambia yaachwe," alisistiza mwanasiasa huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akisisitiza mstaafu huyo hana kinga ya kutoshtakiwa.

Dk. Slaa alisema jambo ambalo linamfanya kiongozi huyo kuonekana kuwepo sababu ya kumshtaki, ni kufanya biashara akiwa Ikulu, jambo alilolielezea kuwa ni ukiukwaji wa maadili ya uongozi.

Aliongeza kuwa, kamwe hawezi kupoteza muda kubishana na Waziri Simba, akisema kwamba hoja zake zinaonyesha hajui dhana nzima ya wadhifa wake (ya utawala bora).

"Sina sababu ya kuendelea kubishana naye… nimekwishaeleza kipengele kwa kipengele kwamba Mkapa ana mengi ya kujibu. Suala la Kiwira na NSSF anapaswa ajibu," alisema Dk. Slaa.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, alisema kauli ya Waziri Simba kuwa serikali haiwezi kumshitaki Mkapa, ni ishara ya wazi ya kulindana inayofanywa na viongozi wa serikali na chama tawala (CCM).

Alisema rushwa imewaandama viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna weledi wa kumshtaki Mkapa kwa kuwa, nao wanaogopa kufanyiwa hivyo pindi watakapomaliza madaraka yao.

Aliipuuza kauli ya Waziri Simba kwa kusema hajui anachokiongea licha ya kupewa ofisi nyeti inayohusu masuala ya maadili ya viongozi wa umma.

Alisema Mkapa hawezi kukwepa kupanda kizimbani, kwa kuwa kashfa ya ununuzi wa ndege na rada ambayo mchakato wake umegubikwa na rushwa ya dola za Marekani milioni 12 kutoka kwa mfanyabiashara Sailesh Vithlani, ni ushahidi tosha, kwamba anapaswa kuwajibishwa.

"Kwa sasa baadhi ya watendaji na viongozi katika baraza lake la mawaziri (Basil Mramba, Daniel Yona na Gray Mgonja) walioutumikia utawala wake, wamepelekwa kizimbani, hii inaonyesha ni kwa vipi asivyoweza kukwepa kashfa hizi," alisema.

Aliongeza kuwa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alipokwenda Uingereza hivi karibuni na kuulizia kashfa ya rada inayopelelezwa na ofisi inayoshughulikia ufisadi mkubwa (Serious Fraud Office-SFO), alithibitishiwa ya kwamba kulikuwa na ufisadi wakati wa ununuzi wa rada hiyo iliyogharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha.

Katika suala hilo la ukiukwaji wa miiko ya uongozi, Jussa alisema, wakati kiongozi huyo akiingia madarakani, alitangaza mali alizokuwa akizimiliki ikiwemo nyumba jijini Dar es Salaam na huko Masasi pamoja na shamba, lakini alipoondoka madarakani, mwaka 2005, hakuweka bayana alichokuwa anamiliki, ikiwemo kampuni yake ya Anben.

Akizungumzia hoja ya Simba kulifananisha suala hilo na nguvu zilizotoa msukumo Chiluba kushtakiwa kwa ufisadi kabla ya mahakama kumkuta hana hatia, alisema kuwa, kiongozi huyo wa zamani wa Zambia alibainika kuwa hana hatia baada ya kupandishwa kizimbani, hivyo waziri hawezi kulisemea hilo kabla Mkapa naye hajafanyiwa hivyo.

"Kitu kilichosema Chiluba hana hatia ni mahakama pekee. Sioni kuwa hapa kuna shinikizo lolote kutoka nje kwani ni nchi hizo hizo zilizoshirikiana na Mkapa. Kwa mfano rada, Uingereza inaweza kujivua kweli suala hilo?" alihoji.

Alisema kinachopaswa kufanywa na serikali hivi sasa ni kutaja nchi zile zinazoshinikiza kushtakiwa Mkapa kupitia vyombo vya habari, badala ya kutoa kauli zisizo na mashiko.

Juzi, Waziri Simba alisema Mkapa hashitakiki kwa kuwa ana kinga na serikali haina mpango wa kumshitaki kwa kuwa mataifa ya nje yamekuwa yakivitumia vyombo vya habari kushinikiza jambo hilo kama walivyofanya nchini Zambia kwa rais wa zamani ya nchi hiyo, Chiluba.

Kauli hiyo ya Waziri Simba imekuwa ni muendelezo wa viongozi wa serikali kutokuwa tayari kuona Mkapa akipandishwa kizimbani kwa tuhuma zinazomkabili.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Bunge lililopita la bajeti alisema kuwa, Mkapa alikuwa kiongozi safi, lakini baadhi ya wabunge wa CCM na viongozi wa kambi ya upinzani waliibuka na kutaka kiongozi huyo mstaafu ajisafishe mwenyewe badala ya kusafishwa.

Tuhuma za kujimilikisha Kiwira pamoja na washirika wake, tena kwa bei chee ya sh milioni 700 badala ya gharama halisi ya bilioni nne, kupitia Kampuni ya Tanpower Resources Limited, ni moja ya kashfa inayosimamiwa na watu wenye hoja kwamba Mkapa si mtu safi. Hata hivyo, katika kikao kilichopita cha Bunge la bajeti, serikali iliuchukua mgodi huo unaodaiwa kulipiwa asilimia 10 ya manunuzi yote kwa maelezo kuwa, mwekezaji anatafutwa ili aweze kuuendesha.
 
Jamani Mkapa akasimame kwenye mahakama zipi?? hizi hizi za Tanzania na maprosecutor ni hawa tuwajuao????? kazi kweli..
 
Mkapa : Ulijimilikisha mgodi au la? swali la pili: Unajua nini kuhusu ununuzi wa rada?Swali la tatu Ulijua nini kuhusiana na EPA? swali la nne : Ndege yako ulinunua bei gani?
 
Hatuna system nzuri, huwa naona ujinga wakati mwingine kuzungumzia ishu za RAIS MSTAAFU, HUKU RAIS ALIYEKO MADARAKANI HAWEZI KUMFANYA KITU, BAYA ZAIDI MKAPA NDIYO KAMWEKA JK!MUULIZENI JK MLIYEMPA KURA!!

Kuuliza maswali ya kiwira, migodi, ni dalili za jamii isiyoweza kufanya lolote, ni kama mbwa anayebweka, ukitaka kuokota jiwe anakimbia.

Tatizo si Mkapa, tatizo ni sisi wenyewe, tatizo ni system, tatizo hatuna utamaduni unaojulikana, hatuna namna ya kuwaonya viongozi, Tatizo hili ni la ujamaa zaidi(tumerithi-zidumu fikra), we need to know the foundations of our country, ikiwezekana tuweke underpinning.

Kelele za MKAPA KILA SIKU MWAKA WA TANO SASA, sidhani kama zinasaidia, siyo mkapa viongozi wooote, ikiwemo na sisi tukifika pale je kitu gani kinamzuia mtu asiibe.Moral? , kuipenda nchi? ubinadamu?

Condom zipo,binadamu wapo, ukimwi, hupo, hatari ya ukimwi inajulikana, lakini wapi! watu if ingekuwa the only means ya kuondokana na tatizo ni kuruhusu uondolewe hamu??

Kama hatutaweza kumwondolea madaraka makubwa rais, kama hatutamprotect kutoshtakiwa, kama hatutachagua viongozi based on their performance, kama tutarubunika na kuwatandikia mazuria viongozi walafi, kama hatutakuwa na migawanyiko juu ya maslahi ya taifa, kama hatutazuia rushwa toka ngazi ya mesenja, then leo tusingelia hivi

we need to rediscuss the foundation of our country from the days of yore

NYAKATI ZA NYERERE ZIMESHAPITA, NYAKATI ZA RAIS NDIYO KILA KITU, NYAKATI ZA YEYE KUWAHAMISHA MAFISADI TOKA SHIRIKA MOJA KWENDA LINGINE, NYKATI ZA RAIS KUTOSHAURIKA NA KULAMBWA MIGUU!!! NYAKATI ZA KUWATETEMEKEA VIONGOZI WETU, NYAKATI ZA KIONGOZI KUWA MTUMWA NA SIO BOSS, ZILE TABIA TULIZORITHISHWA, TUZIANGALIE TENA. NYAKATI ZA KUPAKA RANGI MATOFALI YA SHULE WAKATI KIONGOZI ANAKUJA, NYAKATI ZA KUTENGENEZA BARABARA UJIO WA RAIS, HIZI ZOOOTE ZINAASHIRIA RAIS NI MUNGU MTU, BILA KUONDOA HILI WINGU, TUNABWEKA SAANA.

JK inajulikana amecheza dirty deals nyingi, yet tukampa urais kwa silimia 80% kesho JK ikajulikana kaiba, tutalalamika kwa nani?

Mkapa ameleta mpasuko wa watu, leo Mkapa anapendwa sana kila kona pamoja na ubaya tunaoujua, ndio kuna watanzania wamezoea kuliwa na kuonewa, kuna wasiojua morals, kuna wenye kuishi kwenye dunia ya afadhali huyu.

Wizi ni wizi hata kama anayekuibia anakupenda sana, hatuna utamaduni wa kuwafanya viongozi wetu waogope kuiba mali ya umma kama binadamu wote walivyo na tabia ya kutowaza kufanya mapenzi na wazazi wao!!! tukifika hapa ndio tunashuhudia nchi za wenzetu ukiwa na tuhuma tu unaachia ngazi, ukibambwa tu na mke wa mtu, huna uongozi, sio mpaka ushauriwe kama Chenge la! wewe mwenyewe unaona umefanya kosa kubwa sana, zile nyakati tukiziondoa, tumepona!

Kama hatuna tabia hii, Mkapa angepata wapi? kama Mkapa asingeiba tungejua lini tuna matatizo haya, kuwa hatuna system nzuri, taifa ndio kwanza linakua, tungalie mbele tuzuie yasitokee tena, ILA IKIWA NI WATU TU WA KULALAMIKA BILA KUFANYA JITIHADA ZA KUZUIA LISITOKEEE TENA, JE CHENGE AU ROSTAM AKIWA RAIS??, HAWA TUNAWAJUA JE TUSIOWAJUA??
 
naona nkapa marafiki zake wote wamemkimbiam kuiba aliiba nao sasa wana muona tambara bovu, kweli laana ya watu aliowaibia , ina msumbua mkapa sasa, maana iddi simba ameomba radhi kwa kupitisha mikataba ya madini, mramba anasema alex stewart ni ikulu, hata ile kauli ya cc, kwamba watu au wana ccm wasi mseme nkapa naona haina nguvu tena.
 
Ni kwa sababu wanajua kwamba uchafu wake umekithiri na wao walifaidika na uchafu huo, ndio maana wanabwatuka ili yasijewafika na wao wakati wa kusugua uchafu huo kuutoa.

Chumvi ikishaoza itiwe nini ili ikolee?

Leka
 
Hatuna system nzuri, huwa naona ujinga wakati mwingine kuzungumzia ishu za RAIS MSTAAFU, HUKU RAIS ALIYEKO MADARAKANI HAWEZI KUMFANYA KITU, BAYA ZAIDI MKAPA NDIYO KAMWEKA JK!MUULIZENI JK MLIYEMPA KURA!!

Kuuliza maswali ya kiwira, migodi, ni dalili za jamii isiyoweza kufanya lolote, ni kama mbwa anayebweka, ukitaka kuokota jiwe anakimbia.

Tatizo si Mkapa, tatizo ni sisi wenyewe, tatizo ni system, tatizo hatuna utamaduni unaojulikana, hatuna namna ya kuwaonya viongozi, Tatizo hili ni la ujamaa zaidi(tumerithi-zidumu fikra), we need to know the foundations of our country, ikiwezekana tuweke underpinning.

Kelele za MKAPA KILA SIKU MWAKA WA TANO SASA, sidhani kama zinasaidia, siyo mkapa viongozi wooote, ikiwemo na sisi tukifika pale je kitu gani kinamzuia mtu asiibe.Moral? , kuipenda nchi? ubinadamu?

Condom zipo,binadamu wapo, ukimwi, hupo, hatari ya ukimwi inajulikana, lakini wapi! watu if ingekuwa the only means ya kuondokana na tatizo ni kuruhusu uondolewe hamu??

Kama hatutaweza kumwondolea madaraka makubwa rais, kama hatutamprotect kutoshtakiwa, kama hatutachagua viongozi based on their performance, kama tutarubunika na kuwatandikia mazuria viongozi walafi, kama hatutakuwa na migawanyiko juu ya maslahi ya taifa, kama hatutazuia rushwa toka ngazi ya mesenja, then leo tusingelia hivi

we need to rediscuss the foundation of our country from the days of yore

NYAKATI ZA NYERERE ZIMESHAPITA, NYAKATI ZA RAIS NDIYO KILA KITU, NYAKATI ZA YEYE KUWAHAMISHA MAFISADI TOKA SHIRIKA MOJA KWENDA LINGINE, NYKATI ZA RAIS KUTOSHAURIKA NA KULAMBWA MIGUU!!! NYAKATI ZA KUWATETEMEKEA VIONGOZI WETU, NYAKATI ZA KIONGOZI KUWA MTUMWA NA SIO BOSS, ZILE TABIA TULIZORITHISHWA, TUZIANGALIE TENA. NYAKATI ZA KUPAKA RANGI MATOFALI YA SHULE WAKATI KIONGOZI ANAKUJA, NYAKATI ZA KUTENGENEZA BARABARA UJIO WA RAIS, HIZI ZOOOTE ZINAASHIRIA RAIS NI MUNGU MTU, BILA KUONDOA HILI WINGU, TUNABWEKA SAANA.

JK inajulikana amecheza dirty deals nyingi, yet tukampa urais kwa silimia 80% kesho JK ikajulikana kaiba, tutalalamika kwa nani?

Mkapa ameleta mpasuko wa watu, leo Mkapa anapendwa sana kila kona pamoja na ubaya tunaoujua, ndio kuna watanzania wamezoea kuliwa na kuonewa, kuna wasiojua morals, kuna wenye kuishi kwenye dunia ya afadhali huyu.

Wizi ni wizi hata kama anayekuibia anakupenda sana, hatuna utamaduni wa kuwafanya viongozi wetu waogope kuiba mali ya umma kama binadamu wote walivyo na tabia ya kutowaza kufanya mapenzi na wazazi wao!!! tukifika hapa ndio tunashuhudia nchi za wenzetu ukiwa na tuhuma tu unaachia ngazi, ukibambwa tu na mke wa mtu, huna uongozi, sio mpaka ushauriwe kama Chenge la! wewe mwenyewe unaona umefanya kosa kubwa sana, zile nyakati tukiziondoa, tumepona!

Kama hatuna tabia hii, Mkapa angepata wapi? kama Mkapa asingeiba tungejua lini tuna matatizo haya, kuwa hatuna system nzuri, taifa ndio kwanza linakua, tungalie mbele tuzuie yasitokee tena, ILA IKIWA NI WATU TU WA KULALAMIKA BILA KUFANYA JITIHADA ZA KUZUIA LISITOKEEE TENA, JE CHENGE AU ROSTAM AKIWA RAIS??, HAWA TUNAWAJUA JE TUSIOWAJUA??

mapinduz ndio the only solution kwa nchi hii
 
Jamani Mkapa akasimame kwenye mahakama zipi?? hizi hizi za Tanzania na maprosecutor ni hawa tuwajuao????? kazi kweli..
Itakuwa kichekesho. Kwanza haiwezekani kwa sababu zifuatazo
1. Walioko madarakani kwa sasa wengi aliwaweka yeye.
2. Alikuwa kiongozi mkuu wa serikali hivyo anajuwa kashfa ya kila mmoja.
3. Kashfa zake zinawahusu walioko madarakani pia, hivyo kumshitaki ni sawa na mtu kujishitaki mwenyewe.
4. Anajuwana na wengi wenye fedha nyingi, hakuna atakayeweza kushindana na fedha hizo.
5. Wanasheria wakubwa wengi ni maswahiba wake, hawawezi kumtupa, watamtetea mpaka mwisho. Usitegemee Mkono na Lamwai kama watamtosa. Mkono ana kashfa na Lamwai si mnakumbuka jinsi alivyotolewa UDSM na kunyang'anywa leseni ya uadvoketi..??? sidhani kama atapenda kurudia hali ile.
 
Ni kwa sababu wanajua kwamba uchafu wake umekithiri na wao walifaidika na uchafu huo, ndio maana wanabwatuka ili yasijewafika na wao wakati wa kusugua uchafu huo kuutoa.

Chumvi ikishaoza itiwe nini ili ikolee?

Leka

Chumvi ikisha aribika, haifai kitu, ila niya kutupwa jalalani,lakini huyu tumtupe wapi maana hata jalala ni safi kuliko yeye.
 
Prof Baregu naye ameanza kuleta wivu wa kike sasa.Nani atampeleka Mkapa mahakamani?
Jk siyo mpuuzi kiasi hicho kwa sababu anajitambua na yeye kuwa siku aki-step down yanaweza kumkuta makubwa.
 
Back
Top Bottom