Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Tatizo liko wapi katika kulaumu iwapo yeye mwenyew alishindwa kusifia kile alichokikuta. Umri wa mchangiaji unadetermine kile anachokisifia. Iwapo mchangiaji hajui vipi Tanzania ilivyokuwa kiabla ya kuingia Mwinyi tutegemee nini? Hana kitu cha kufananisha kati ya utawala wa Mkapa na uliomtangulia. Ama kwa utawala wa Kikwete na tusubiri baada ya miaka 10 kwani huyo Mkapa tunamuhesabu kwa aliyofanya miaka kumi. La kukumbusha tu ni kuwa lawama alianza yeye Mkapa kwa aliyemtangulia na wala hakufanya nusu ya yanayolalamikiwa sasa, kwa hivyo wacha tumrejeshee fimbo aliyoitumia kwa mwenziwe.
Katufanyia mabaya na tutamtaja kwa hayo aliyotufanyia.
 
Tunafahamu kuwa Mkapa ni ndugu yako wa Damu, Lakini hatuko personal hapa, Tunajariku kuelewesha kuwa Mabaya alaiyoyafanya Mzee wako.

Pili usipokiri sasa utapata shida katika maisha yako ya kisiasa mbeleni.

Wewe Nicolus Baba mkwe wako ndiye attorney wa serikali kule kiwira sio, Mzee Mbuna hayo yote tunajua, Ila we are giving you more Time Kutubu kabra hujaanza kulaaiwa na watanzania wanaolala njaa.

Mwongozo wa JF ama imekaa vipi?
 
Hii mada tumeivamia kijazba kwa hiyo hatuwezi kuwa objective sana. Pengine ni kwa sababu mleta hoja naye kaleta hoja yake kijazba. Hata hivyo kuna hoja za msingi za kujadiliwa.

Kwanza nikanushe madai ya Bongo TZ na Philemon Mikael kwamba utawala wa Kikwete ndiyo ulioibua na unaendelea kuchochea moto kashfa za Mkapa. Hii ni hapana kwa sababu tunajua kwamba kwa mara ya kwanza kashfa za Mkapa ziliibuliwa kwa uwazi kabisa tarehe 15 Septemba 2007 na Dr Slaa pale Mwembe Yanga baada ya jina lake kuwa juu kabisa katika list ya aibu ya mafisadi. Na ni mtu mwehu pekee atakayekubaliana kwamba Dr Slaa walitumwa na akina JK kumwaga ile list.

Baada ya kusema hayo, nakubaliana na akina Bongo TZ kwa jambo moja, nalo ni kwamba utendaji wa Mkapa kama Rais ulikuwa bora kwa mbali sana kuliko JK. In fact ni aibu kulinganisha utendaji wa akina JK na Mkapa kwa sababu ni vitu viwili tofauti. It is simply unaffair and illogical to try to compare between a presidential president and a pretentious president.

Niseme pia kwamba ni ukweli kwamba Mkapa alifanya mambo makubwa ikiwemo kuirudisha nchi ianze kuonekana nchi na kuifanya serikali ionekane serikali. Ni ukweli pia kwamba Mkapa alitumia vibaya madaraka yake na hasa zoezi la ubinafsishaji kwa manufaa yake na jamaa zake badala ya nchi. Halafu kuna jambo moja ambalo apologists na critics wa Mkapa huwa hawalisemi, nalo ni kwamba Mkapa ni Rais aliyetumia madaraka yake na nguvu nyingi za dola kudhaifisha upinzani. Huyu ni mtu aliyedhamiria kuua kabisa upinzani kwa gharama yeyote ile.

Sasa swala la kujadili hapa ni: Je, mabaya ya Mkapa yanazidi na kufuta mazuri yake?

Lakini kusema kwamba Mkapa ni "clean, period" ni ulimbukeni wa hali ya juu. Vilevile, kusema kwamba Mkapa hakufanya chochote cha maana katika nchi yetu zaidi ya kuiba ni ulimbukeni na ujuha wa kutisha!

Kitila,

President hatakiwi kushukiwa kwa chochote kile .... either ni mbaya au mzuri ... hawezi kuwa vyote!!! Apologists wa mkapa wanatumia macroeconomic performance ya Mkapa ......na kusema siii malaika....yaani anaweza kuiba ila tuakasahau kwa kuwa alistabilize economy..... For what??? Let's be serious. Any allegation ya matumizi mabaya ya madaraka IS A MORTAL SIN! Hata kama angekuwa aliiachia nchi hii Mabilioni, .... kuiba ni kuiba tuuuu. THIS IS A SHAMED PRESIDENT, KASAFISHENI UCHAFU MWINGINE!!!!
 
Babu ataka kusema: I fundamentally disagree with you. You can't just disrespect your former president like that man! kama ni fisadi,mbona hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yake . Acheni ushabiki usiokuwa na maana vijana. Mkapa sio fisadi. Period.

Kutokana na matusi yako nilijaribu kukwepa kuchangia hapa lakini imebidi niingie kukujibu swali lako "mbona hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yake?" JIBU analindwa na inner circle ya Kikwete, kama kikwete ataruhusu haki kutendeka kuna kila ushahidi BEN ataozea Jela! Period.
 
Tatizo liko wapi katika kulaumu iwapo yeye mwenyew alishindwa kusifia kile alichokikuta. Umri wa mchangiaji unadetermine kile anachokisifia. Iwapo mchangiaji hajui vipi Tanzania ilivyokuwa kiabla ya kuingia Mwinyi tutegemee nini? Hana kitu cha kufananisha kati ya utawala wa Mkapa na uliomtangulia. Ama kwa utawala wa Kikwete na tusubiri baada ya miaka 10 kwani huyo Mkapa tunamuhesabu kwa aliyofanya miaka kumi. La kukumbusha tu ni kuwa lawama alianza yeye Mkapa kwa aliyemtangulia na wala hakufanya nusu ya yanayolalamikiwa sasa, kwa hivyo wacha tumrejeshee fimbo aliyoitumia kwa mwenziwe.
Katufanyia mabaya na tutamtaja kwa hayo aliyotufanyia.

Rais akitoka madarakani, ndo inakuwa muafaka kumjadili na ku-sum-up performance yake. Baada ya Mz. Ruksa kustaafu, ilionekana alikuwa rais dhaifu kiutendaji... Makosa ya kiutendaji hayoooo kibao yanaonekana. Lakini ya Mh. Mkapa si ya kiutendajiiii, ni ya JINAI....
 
Mheshimiwa BongoTz katuletea topic hii ya “Mkapa ni mtu safi. Period” kwa sababu hata yeye mwenyewe BongoTZ haamini kwamba Mkapa ni msafi au la, kwa hiyo anataka tujadili lipatikane jibu!

Tunayoyaona kwamba ni 'Mazuri ' yaliyofanywa katika awamu yoyote ya uongozi ndio wajibu sahihi wa viongozi wahusika. Tunapoyataja mazuri yaliyofanywa, ni sawa na kusema kwamba Rais ama kiongozi muhusika ametimiza wajibu wake ipasavyo kwa maslahi ya wananchi waliompa uongozi na kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Yanapotendeka mambo ‘mabaya’ ambayo yanaonekana kulididimiza Taifa makusudi, ama yana maslahi binafsi ya kiongozi ama maslahi ya watu wachache, ni kwamba kiongozi hakutelekeza wajibu wake ipasavyo, amekwenda kinyume na wajibu wake kwa wananchi waliompa cheo hicho. Katumia cheo kwa maslahi yake au ya wachache, ama kaliangamiza taifa kwa kutumia cheo alichopewa.

Wananchi wala hawalazimiki kumsifu kiongozi yeyote kwa mazuri; ni wajibu wa kiongozi huyo kufanya hivyo kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa kuwa mipango yote ya Serikali inapaswa iwe kwa manufaa ya wananchi wote. Wananchi wanayo haki na ni wajibu wao kutaka wapate maelezo kuhusu yale ambayo wanaona kiongozi waliyempa dhamana ya uongozi anatenda maovu ama Serikali yake inatenda kinyume.

Uongozi makini hujiwekea utaratibu wa kutathmini mambo yanavyokwenda, hubaini na kukiri makosa na hujaribu kusahihisha makosa yaliyojitokeza. Uongozi usiokubali makosa ya dhahiri, na unaojaribu kuyatetea makosa ama kuyafunika kwamba hayakutendeka, uongozi huo hauwatendei haki wananchi na taifa kwa ujumla.

Kama ilivyojitokeza kwa watu wengi akiwemo Bongo Tz, uongozi wa Mwalimu Nyerere unaonekana tofauti; unasifiwa na ni dhahiri utaendelea kufisiwa hata na vizazi vijavyo. Si kwamba Mwalimu hakutenda makosa katika uongozi wake, bali ni kwa sababu alitenda makosa yale ndani ya nia njema ya kutekeleza wajibu wake kwa wananchi waliompa uongozi na si kwa maslahi binafsi ama ya wachache.

Mwaka mmoja tu baada ya nchi kupata Uhuru, bila ya kupigiwa kelele Mwalimu alibaini makosa yaliyojitokeza ndani ya uongozi wake na akayatangaza kwenye mikutano ya hadhara. Ushahidi umo katika kijitabu alichotoa mwaka 1962 cha ‘TUJISAHIHISHE’ akiwataka viongozi wa Serikali yake na Chama cha TANU, na wananchi kwa ujumla watambue makosa yaliyojitokeza ndani ya mwaka mmoja wa kujitawala na kuyasahihisha. Mwalimu aliendelea na mtindo huo wa kutathmini na kujikosoa. Tathmini ya mwaka 1977 katika Miaka Kumi Baada ya Azimio la Arusha ni mfano mwingine. Pia, hotuba zake nyingi ikiwemo ile ya Miaka mitano ya Serikali ya CCM ni mfano wa Rais kujikosoa, kuikosoa Serikali na hata kuwakosoa wananchi kwa nia njema ya kutaka wapate maendeleo.

Mwaka mmoja baada ya kuanza kwa uongozi wa Awamu ya Tatu (1996) Mwalimu aliwahi kusema: “…Fikra nzito hazifi kwa urahisi, zinabaki zikikera, na kila jamii ya binadamu katika historia inajipalia makaa kwa kuzipuuza….”

Na katika ‘TUJISAHIHISHE’, Mwalimu Nyerere anasema hivi: “Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo laki kwa sabatu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa

Mahasimu wa CCM, Zitto Kabwe, Dk. Slaa, Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba na wengine wamekuwa tayari kukubali “Ukweli” na kuelezea hadharani kwamba kuna viongozi waliwapuuza wananchi wakajaribu kupiga teke jiwe kwa kudhani ni dongo! Wapinzani wanakiri na kuuthamini hadharani uongozi wa Mwalimu uliojali na kutetea maslahi ya wananchi ambao ni mfano wa kuigwa. Lakini, viongozi wa Serikali na CCM wanatafuta kila mbinu kuwaficha wananchi ukweli. Wanapata na kigugumizi kikali kutaja hadharani na kujivunia jina la Muasisi wa Chama chao - Wanapuuza Ukweli!
 
Hii mada tumeivamia kijazba kwa hiyo hatuwezi kuwa objective sana. Pengine ni kwa sababu mleta hoja naye kaleta hoja yake kijazba. Hata hivyo kuna hoja za msingi za kujadiliwa.

Kwanza nikanushe madai ya Bongo TZ na Philemon Mikael kwamba utawala wa Kikwete ndiyo ulioibua na unaendelea kuchochea moto kashfa za Mkapa. Hii ni hapana kwa sababu tunajua kwamba kwa mara ya kwanza kashfa za Mkapa ziliibuliwa kwa uwazi kabisa tarehe 15 Septemba 2007 na Dr Slaa pale Mwembe Yanga baada ya jina lake kuwa juu kabisa katika list ya aibu ya mafisadi. Na ni mtu mwehu pekee atakayekubaliana kwamba Dr Slaa walitumwa na akina JK kumwaga ile list.

Baada ya kusema hayo, nakubaliana na akina Bongo TZ kwa jambo moja, nalo ni kwamba utendaji wa Mkapa kama Rais ulikuwa bora kwa mbali sana kuliko JK. In fact ni aibu kulinganisha utendaji wa akina JK na Mkapa kwa sababu ni vitu viwili tofauti. It is simply unaffair and illogical to try to compare between a presidential president and a pretentious president.

Niseme pia kwamba ni ukweli kwamba Mkapa alifanya mambo makubwa ikiwemo kuirudisha nchi ianze kuonekana nchi na kuifanya serikali ionekane serikali. Ni ukweli pia kwamba Mkapa alitumia vibaya madaraka yake na hasa zoezi la ubinafsishaji kwa manufaa yake na jamaa zake badala ya nchi. Halafu kuna jambo moja ambalo apologists na critics wa Mkapa huwa hawalisemi, nalo ni kwamba Mkapa ni Rais aliyetumia madaraka yake na nguvu nyingi za dola kudhaifisha upinzani. Huyu ni mtu aliyedhamiria kuua kabisa upinzani kwa gharama yeyote ile.

Sasa swala la kujadili hapa ni: Je, mabaya ya Mkapa yanazidi na kufuta mazuri yake?

Lakini kusema kwamba Mkapa ni "clean, period" ni ulimbukeni wa hali ya juu. Vilevile, kusema kwamba Mkapa hakufanya chochote cha maana katika nchi yetu zaidi ya kuiba ni ulimbukeni na ujuha wa kutisha!

Kitila
mkuu wewe kwangu mimi naona una aproach tatizo logically na huna mambo ya kiitikadi .

thx
 
Jamani,

Mimi nashangaa wale waopinga hoja ya kuhoji vitendo vilivyofanywa na viongozi wetu wakiwa madarakani au kwa walio madarakani.

Kwa taarifa yako, mtu anapoamua kugombea uongozi inaaanisha kwamba uhuru wako na mambo yako (personal affairs) umeyaweka hadharani, kwa maana unaruhusu wananchi kukuhoji kwa lolote lile kuhusu wewe, liwe baya au zuri.

Swala la kwamba mkapa ni msafi au si msafi ni swala la public opinion, kwani mengi aliyoyafanya tumeyaona na kuyasikia.

Hili swala la kumtetea ua kujaribu kuficha/kusafisha yale maovu aliyoyafanya sio sahihi, kwani hakuna aliyemtuma kwenda kugombea uraisi, so he must bear the consequences of being a public leader.

Naomba niwashauri pia wale wanaogombea uongozi mbalimbali kwamba, unapoingia kwenye uongozi wa jamii lazma ukubaliane na matakwa yanayoendana na nafasi hizo kwa mfano kukubali kuhojiwa kila kitu kuhusiana na wewe, baya au zuri.

Its difficult to claim individual/confidential/personal affairs at the helm of public affair leadership otherwise better remain a normal citizen
 
hii Mada Tumeivamia Kijazba Kwa Hiyo Hatuwezi Kuwa Objective Sana. Pengine Ni Kwa Sababu Mleta Hoja Naye Kaleta Hoja Yake Kijazba. Hata Hivyo Kuna Hoja Za Msingi Za Kujadiliwa.

Kwanza Nikanushe Madai Ya Bongo Tz Na Philemon Mikael Kwamba Utawala Wa Kikwete Ndiyo Ulioibua Na Unaendelea Kuchochea Moto Kashfa Za Mkapa. Hii Ni Hapana Kwa Sababu Tunajua Kwamba Kwa Mara Ya Kwanza Kashfa Za Mkapa Ziliibuliwa Kwa Uwazi Kabisa Tarehe 15 Septemba 2007 Na Dr Slaa Pale Mwembe Yanga Baada Ya Jina Lake Kuwa Juu Kabisa Katika List Ya Aibu Ya Mafisadi. Na Ni Mtu Mwehu Pekee Atakayekubaliana Kwamba Dr Slaa Walitumwa Na Akina Jk Kumwaga Ile List.

Baada Ya Kusema Hayo, Nakubaliana Na Akina Bongo Tz Kwa Jambo Moja, Nalo Ni Kwamba Utendaji Wa Mkapa Kama Rais Ulikuwa Bora Kwa Mbali Sana Kuliko Jk. In Fact Ni Aibu Kulinganisha Utendaji Wa Akina Jk Na Mkapa Kwa Sababu Ni Vitu Viwili Tofauti. It Is Simply Unaffair And Illogical To Try To Compare Between A Presidential President And A Pretentious President.

Niseme Pia Kwamba Ni Ukweli Kwamba Mkapa Alifanya Mambo Makubwa Ikiwemo Kuirudisha Nchi Ianze Kuonekana Nchi Na Kuifanya Serikali Ionekane Serikali. Ni Ukweli Pia Kwamba Mkapa Alitumia Vibaya Madaraka Yake Na Hasa Zoezi La Ubinafsishaji Kwa Manufaa Yake Na Jamaa Zake Badala Ya Nchi. Halafu Kuna Jambo Moja Ambalo Apologists Na Critics Wa Mkapa Huwa Hawalisemi, Nalo Ni Kwamba Mkapa Ni Rais Aliyetumia Madaraka Yake Na Nguvu Nyingi Za Dola Kudhaifisha Upinzani. Huyu Ni Mtu Aliyedhamiria Kuua Kabisa Upinzani Kwa Gharama Yeyote Ile.

Sasa Swala La Kujadili Hapa Ni: Je, Mabaya Ya Mkapa Yanazidi Na Kufuta Mazuri Yake?

Lakini Kusema Kwamba Mkapa Ni "clean, Period" Ni Ulimbukeni Wa Hali Ya Juu. Vilevile, Kusema Kwamba Mkapa Hakufanya Chochote Cha Maana Katika Nchi Yetu Zaidi Ya Kuiba Ni Ulimbukeni Na Ujuha Wa Kutisha!

....kitila Mkumbo Una Akili Sana ...wala Haikuwa Ajabu Pale Ulipopewa Nafasi Ya Kufanya Kazi Pale Udsm ..mara Tu Baada Ya Ku Graduate....

Nafikiri Umetoa Mwelekeo Wa Namna Tunavyotakiwa Kuyachambua Mambo Hapa Jf.........maana Wengi Hapa Wanapenda Tu Kusema ...mkapa Hakufanya Kitu!!!....au Mkapa Sio Fisadi !!!

Naomba Wachambuzi Mfuate Msingi Alioleta Kitila Ili Hii Mada Ichambuliwe Kitaaluma Zaidi.....naomba Kuwasikia Wachambuzi Maarufi ..kama Rev Kishoka ,kichuguu,fmes,....na Wengine.....woote!!
 
Sasa swala la kujadili hapa ni: Je, mabaya ya Mkapa yanazidi na kufuta mazuri yake?

Mabaya ya Mkapa yanafuta kabisa mazuri mengi aliyoyafanya,

1. Kiongozi safi ni yule ambaye akiwa kwenye power, anajaribu kwanza kuheshimu sheria ambayo in the process anaishia kudumisha utawala na maisha ya haki, kwenye hili ni zero kwa Mkapa.

2. Kazi ya pili ya kiongozi safi inatakiwa kuliongoza taifa kwenye kujikwamua na tabia ya utegemezi wa wafadhili, yaaani hata kama hawezi kulitoa kabisa basi kama lilikuwa linapata 40% ya bajeti toka wafadhili, basi aliache likiwa linategemea 20% au 0%, aliimarisha uchumi lakini hili pia hakuweza.

3. Kuhamasisha Participation ya wananchi kwa siasa ya taifa lao, hili alishindwa kabisaa kwa sababu under him ndio tumeona matajiri wakikiteka chama CCM, na aliondoa kabisa tabia ya kufuata katiba za CCM, sasa zikawa zake yeye, ni mtu aliyekuwa hapendi kuheshimu sheria kwa hiyo hata katiba ya CCM kwake ilikuwa ni bure, na hakuheshimu chama chochote cha siasa nchini, ndio maana nilikwaruzana naye sana kwenye mkutano mmoja kwa sababu nilimuambia kuwa ni unafiki mkubwa kwake kwenda US kukutana na viongozi wa vyama vyote vyote vya siasa huko yaani watawala na wapinzani, lakini akagoma kukutana na upinzani wa Tanzania, wakati huo alikuwa na tabia ya kukataa kukutana na upinzani bongo.

4. Maisha bora kwa wananchi, alijitahidi kidogo kwenye hili, uchumi pia alijitahidi sana, uwajibilkaji kwa viongozi pia alijitahidi sana, kama sio tamaa zake mwishoni, angeweza kuwa the best ever, kuna wakati nikiwa BCS niliamini hivyo mpaka yalipoanza kutoka machafu yake, Ninasubiri siku yeye na mzee wa Mbeya, watakapopanda kizimbani, maana they destroyed our nation, hawa watu wawili tu,

Kumlinganisha yeye Mkapa na utawala wa sasa ni mapema mno, siwezi kwenda huko bado ingawa dalili sio nzuri sana kwa utawala wa sasa, ambao nao pia unahitaji kupongezwa kwa kuheshimu demokrasia, na uwazi, ingawa ndio hivyo kiduchu kiduchu, lakini sio sawa na Mkapa.
 
Kuna mengi yamesemwa/andikwa kuhusu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa: "Oh, mkapa ni fisadi," "Mkapa alitumia madaraka ya Urais vibaya," "Mkapa ajitete mbele ya umma," "Blah... blah... blah..."

Lakini ukweli ni kwamba: ni Mzee Ben, na sio Mzee ruksa, wala this Kikwete guy, ambaye ameifanyia nchi hii mema na mazuri. Ikumbukwe kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, Mkapa alipokea nchi iliyokuwa katika hali mbaya kupindukia.

Rushwa ilikuwa imekithiri. Pato la taifa lilikuwa chini. Ukwepaji kodi ulikuwa katika kiwango cha kuogofya. Na miundo mbinu ilikuwa imechoka kupindukia.

Ni chini ya utawala wa mzee Ben ndipo watanzania kwa mara ya kwanza tulipoanza kuona sera ya taifa kuhusu uchumi ikipewa kipaumbele. Miundo mbinu ikiboreshwa. Pato la taifa likikua. Na kamba dhidi ya vita ya rushwa ikikazwa.

Lakini pia katika viongozi tuliowahi kuwapata, ukimuacha Mwalimu, ni Mkapa peke yake aliyekuwa na ubavu wa kupinga kuendeshwa na nchi za Magharibi. Mwinyi alikuwa anajikojolea wahisani wakikohoa, Kikwete (sote tumeshuhudia) anacheza samba kila mara nchi za magharibi zikimuamuru afanye hivyo.

Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ktk kipindi cha miaka 10 akiwa ikulu: (1) mikataba mibaya hususani madini (ambayo hata hivyo ni mwanasheria mkuu ndiye anapaswa kulaumiwa);(2) kumuachia mke wake a—dictate badhi ya shughuli za kiserikali ( one of his weakness). (3) kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...

Cha msingi hapa ni kujua kuwa Mkapa sio Malaika bali mwandamu. na kama mwadamu, naye pia anahadawa na tamaa ya kuwa na maisha yaliyotulia. You know, financial security and all those things, kwa ki-inglish.

Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).

Ukumbuke na Ndani ya Uongozi wa Mkapa ndio Baba wa Taifa alifariki dunia, sina mengi ya kuongezea
 
Mkuu Bongo, Mwinyi ni rais mstaafu kama alivyo Mkapa, umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini TUHUMA za ufisadi zinatolewa nyingi sana dhidi ya Mkapa kuliko Mwinyi?
 
Hitimisho: BongoTz is quite likely Ben's publicity secretary
Keep trying
 
Mabaya ya Mkapa yanafuta kabisa mazuri mengi aliyoyafanya,

1. Kiongozi safi ni yule ambaye akiwa kwenye power, anajaribu kwanza kuheshimu sheria ambayo in the process anaishia kudumisha utawala na maisha ya haki, kwenye hili ni zero kwa Mkapa.

2. Kazi ya pili ya kiongozi safi inatakiwa kuliongoza taifa kwenye kujikwamua na tabia ya utegemezi wa wafadhili, yaaani hata kama hawezi kulitoa kabisa basi kama lilikuwa linapata 40% ya bajeti toka wafadhili, basi aliache likiwa linategemea 20% au 0%, aliimarisha uchumi lakini hili pia hakuweza.

3. Kuhamasisha Participation ya wananchi kwa siasa ya taifa lao, hili alishindwa kabisaa kwa sababu under him ndio tumeona matajiri wakikiteka chama CCM, na aliondoa kabisa tabia ya kufuata katiba za CCM, sasa zikawa zake yeye, ni mtu aliyekuwa hapendi kuheshimu sheria kwa hiyo hata katiba ya CCM kwake ilikuwa ni bure, na hakuheshimu chama chochote cha siasa nchini, ndio maana nilikwaruzana naye sana kwenye mkutano mmoja kwa sababu nilimuambia kuwa ni unafiki mkubwa kwake kwenda US kukutana na viongozi wa vyama vyote vyote vya siasa huko yaani watawala na wapinzani, lakini akagoma kukutana na upinzani wa Tanzania, wakati huo alikuwa na tabia ya kukataa kukutana na upinzani bongo.

4. Maisha bora kwa wananchi, alijitahidi kidogo kwenye hili, uchumi pia alijitahidi sana, uwajibilkaji kwa viongozi pia alijitahidi sana, kama sio tamaa zake mwishoni, angeweza kuwa the best ever, kuna wakati nikiwa BCS niliamini hivyo mpaka yalipoanza kutoka machafu yake, Ninasubiri siku yeye na mzee wa Mbeya, watakapopanda kizimbani, maana they destroyed our nation, hawa watu wawili tu,

Kumlinganisha yeye Mkapa na utawala wa sasa ni mapema mno, siwezi kwenda huko bado ingawa dalili sio nzuri sana kwa utawala wa sasa, ambao nao pia unahitaji kupongezwa kwa kuheshimu demokrasia, na uwazi, ingawa ndio hivyo kiduchu kiduchu, lakini sio sawa na Mkapa.

Thanks a lot FMES. Ni mazuri gani aliyoyafanya Mkapa na kuwanufaisha Watanzania wakati alipokuwa madarakani? Mimi kwa maoni yangu hakuna lolote alilolifanya ambalo lilileta neema yoyote kwa Watanzania walio wengi. Kama lipo liwekwe hapa hadharani ili tulichambue kwa mapana na marefu.

Msilete takwimu za IMF na WB za uchumi wa Tanzania kukua kati ya asilimia 5 mpaka 7 wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 10. Maana uchumi ukikua kwa kiwango hicho basi ni rahisi Wananchi wenyewe kutamka kwamba wanaona mabadiliko mazuri katika maisha yao ya kila siku maana ajira huongezeka, mishahara huongezeka na hivyo kuongeza purchasing power ya wananchi wa nchi hiyo. Hili halikutokea katika miaka 10 ya Mkapa kuwa madarakani.

Kuhusu jazba hakuna jazba yoyote hayo yaliyoandikwa na wengi ni ya ukweli kabisa hakuna lolote liliongezewa chumvi na kuyajadili si kuonyesha jazba, bali ndiyo ukweli wa mambo.
 
BongoTz,
Mkuu nitakwenda na wewe kwa kituo pamoja na kwamba hukujibu swali langu...
Nakuomba pia rudia kufanya Utafiti wa haya uliyoandika..
Mkandara, at least wewe una-think big kidogo. Analysis yako ina make sense kiasi. Ila kumbuka kuwa mashiraka hayo unayodai kuwa Mkapa aliya-uza kwa bei ya njugu kujinufaisa, yalikuwa yanatia serikali hasara (huu sio ujamaa mkuu). So, ni bora kuyauza kwa bei nafuu kwa makaburu (watu wapate ajira, kodi ikusanywe) kuliko kuyaacha yakiwa jumba la maonyesho.
Plus, bear in mind that in today's global economy you can't just be a protectionist. You will suffocate your economy. It's all about economic interconnnections with the rest of the word. It's globalization.
Globalization is here to stay whether we like it or not, people.
I have to concede, though, kwamba we jumped to this globalization thing so unprepared (naamnisha utawala wa Mkapa), ila tusimshikie bango Mzee Ben kupita kiasi wananchi. let's learn from our mistakes, and move on.
Majibu sahihi ni kwamba hakuna mashrika yaliyokuwa yakileta hasara isipokuwa palikuwa hakuna uzalishaji.. Huwezi kuendelea kutengeneza nguo kama huna Pamba, pamba haiwezi kulimwa kama wananchi hawana pembejeo na mboleo...sababu ni nyingi sana na nadhani unaelewa kwamba maendeleo hayawezi kuja kwa kutazama kitu kimoja kuna mnyororo mrefu wa kutegemeana..
Hivyo mashirika alouza Mkapa sio tu yalikuwa muhimu ktk dunia hii ya viwanda (Utandawazi) bali ndio chombo pekee kinachoweza kumtoa maskini ktk lindi hilo..Utalima hadi lini ikiwa huna viwanda..
Kisha umezungumzia habari za Globalization, mkuu labda umeshindwa kuelewa maelezo yangu hapo juu kwamba ni ktk awamu ya Mwinyi tulipoingia UJamaa na NYERERE mwenyewe alikuwa mbele ya tamko hilo ktk hotuba mapema mwaka !984. Na utekelezaji ulianza rasmi July 1984, mimi binafsi nilirudi Tanzania toka Sweden baada ya kuzamia huko....Kwa hiyo sii kweli kwamba Globalization ni mfumo ambao haukukubalika Tanzania, kumbuka tu kwamba Urusi wenyewe chini ya Gobachev tayari walisha tambua umuhimu wa Globalization kiuchumi..
Kwa hiyo ni ktk Utekelezaji wa mfumo huu wa Globalization ndipo tunaweza kutoa hukumu ya uendeshaji serikali wa Mkapa. Na sio kweli kabisa kuwa Mkapa alielewa Globalization kuliko Nyerere au Mwinyi..
Tulivihitaji viwanda na mashirika hayo iwe hata yailileta hasara kwani hasara haipatikani kutokana na kiwanda isipokuwa ni makosa ya uendeshaji wa biashara yenyewe (management)....Mkuu kweli unaamini Breweries, Sigara, Ufi, nakadhalika Simu na kadhalika vilileta hasara nchini?..au kulikuwa na sababu nyingine za kiuongozi?

Tatizo letu sisi Watanzania siku zote ni pale tunapoona kwamba ukiwekesha fedha zako ktk mradi fulani basini lazima faida ipatikane kesho yake (Ulanguzi)...Mkuu haiendi hivyo na ndio maana utaona siku zote sisi hutafuta sababu nje ya sisi wenyewe. Mtu anauza daladala yake kwa sababu haileti faida yaani kosa ni la Daladala badala ya kujitazama yeye mwenyewe pengine kuna makosa anayoyafanya ili apate kujirekebisha..

Tazama mfano mdogo wa Bakhresa, alipoanzisha Azam ilimchukua zaidi ya miaka 5 kuanza kuona faida ya biashara hiyo (nafahamu hili) kwa sababu ya gharama ya mitambo na msingi wa biashara hiyo lakini baada ya miaka 20 leo hii ni mmoja kati ya matajiri wakubwa Tanzania. Sasa kama angekuwa akifikiria kama nyie yaani kuitazama faida iliyokuwa ikiingia katika miaka 10 ya mwanzo, bila shaka angeuza mitambo yote na kurudi kushona viatu..Lakini kwa sababu Bakhresa ni mfanya biashara alifahamu kuwa gharama za uendeshaji sii hoja ikiwa soko lipo.. siku zote soko ndio kiamsho cha biashara na sio kutazama faida. Pengine kilichotukwamisha kilikuwa ni standard au muundo (fashion) wa mali zetu ndio ulitakiwa kurekebishwa badala ya kosa kuwa viwanda na mashirika.
Lakini maamuzi ya Mkapa yalikuwa kuuza viwanda, kairudisha nchi kushona viatu mtaani tukiagiza sole na kiwi toka nje hali kilichotakiwa ni kubadilisha mfumo wa uendeshaji biashara yenyewe toka mali ya Taifa na kufungua soko la DSE ambapo wananchi wangeweza kununua share zao....Tulihitaji viwanda hivyo hata kama havikuleta faida mwanzoni..Wadanganyika wakasahau kwamba viwanda hivyo vilijengwa kwa mikopo na fedha zilitakiwa kulipwa kabla hujahesabu faida....

Kwa hiyo mkuu tusipoteze muda zaidi wewe nambie Mkapa alifanya nini muhimu ambacho wewe umefikia kumpa pongezi zote hizo!...Ikiwa utasema miundombinu nakuomba uitaje hiyo Miundombinu unayozungumzia!...kifupi rudi nyuma usome maelezo yangu ya awali kisha nipe jibu..
 
Hebu tujiulize kidogo je tulisamehewa madeni sababu ya Mkapa? Je uchumi ulitengemaa kwa sababu ya Mkapa? Hii si kweli hata kidogo na nimojawapo ya vitu ambavyo watu wengi wanataka kumpa sifa Mkapa kwacho.

a. Kampeni ya kufutiwa madeni Tanzania ilikuwa ni msukumo wa watu kama Nyerere na Taasisi za kimataifa ikiwemo Oxfam na Jubilee 2000. Ni wao ndio walitia mshinikizo mkubwa kuelekea ufutwaji wa madeni duniani. Hivyo si Tanzania tu iliyonufaika bali nchi nyingi za dunia ya tatu. Si juhudi za Mkapa. Kwenye suala la kufutiwa madeni heshima kubwa na shukrani bado inamuoendea baba wa TAifa ambaye alishiriki katika kampeni hiyo na aliyekuwa na ujasiri wa kuwaambia IMF na WB kuwa 'madeni tuliyonayo ni makubwa mno kiasi kwamba hayalipiki, yafuteni tuanze upya" Mkapa hakuwa na clout hiyo.

Baada ya kuanza kutufiwa madeni, ni wao wakubwa IMF, US, Paris Club, WB ndio walioingiia kati na kusema ni sera gani za kiuchumi tufuate na ni wao ambao wametoa maelekezo mengi ya kufine tune sera zetu za kiuchumi (angalia mawasiliano kati ya Daniel Yona na WB/IMF).

Kiufupi ni kuwa Mkapa alivuna asichopanda na ni pale alipogundua kuwa madeni yamesamehewa, na kuna fedha nyingi iko nchini ndipo na yeye akajigeuza kuwa mjasiriamali wa ghafla!

Mkapa ataingia katika historia kama kiongozi aliyepoteza heshima na hadhi ya Mtanzania na ambaye alifungulia malango ya ufisadi nchini yeye mwenyewe na familia yake wakiwa wa kwanza kuingia ndani. Kwa hilo hatasamehewa na siku moja atakuwa ni Rais wa Kwanza wa Tanzania kuvuliwa kinga ya Urais na kusimamishwa kizimbani.
 
Mkuu Bongo, Mwinyi ni rais mstaafu kama alivyo Mkapa, umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini TUHUMA za ufisadi zinatolewa nyingi sana dhidi ya Mkapa kuliko Mwinyi?

Watu tunaamua nini na nani asulubiwe .Sio kwa misingi ya haki bali kwa misingi ya manufaa binafsi.

Kwani Mrema alimshika nani Live akisafirisha Madini kwenda nje??

Kufanya Biashara si kosa kosa ni Mazingira na wakati unaanzisha biashara Pia kuoa mwanamke si kosa, kosa ni yale mazingira na wakati Mwinyi akiwa ikulu alitumia ikulu kujichukulia kimwana kisichana kama mke kikiwa sekondari pale Jangwani.

Lakini hayo akifanya mwalimu wa sekondari utasikia kelele akizubaa miaka 30 jela.
 
Thanks a lot FMES. Ni mazuri gani aliyoyafanya Mkapa na kuwanufaisha Watanzania wakati alipokuwa madarakani? Mimi kwa maoni yangu hakuna lolote alilolifanya ambalo lilileta neema yoyote kwa Watanzania walio wengi. Kama lipo liwekwe hapa hadharani ili tulichambue kwa mapana na marefu.

Msilete takwimu za IMF na WB za uchumi wa Tanzania kukua kati ya asilimia 5 mpaka 7 wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 10. Maana uchumi ukikua kwa kiwango hicho basi ni rahisi Wananchi wenyewe kutamka kwamba wanaona mabadiliko mazuri katika maisha yao ya kila siku maana ajira huongezeka, mishahara huongezeka na hivyo kuongeza purchasing power ya wananchi wa nchi hiyo. Hili halikutokea katika miaka 10 ya Mkapa kuwa madarakani.

Kuhusu jazba hakuna jazba yoyote hayo yaliyoandikwa na wengi ni ya ukweli kabisa hakuna lolote liliongezewa chumvi na kuyajadili si kuonyesha jazba, bali ndiyo ukweli wa mambo.

Ni vigumu kuyaona mazuri ya Mkapa kama tayari una conclusion

Maisha Bora ni ELIMU bila elimu hakuna kitu ,kama unataka kuona mazuri ya Ben kaulize wafanyakazi wa Serikali kati ya miaka 1990-1996 hasa walimu wa shule za misingi.

Wafanya kazi waliacha kazi nakuamua kuwa wafanya biashara, walikua hawalipwi mishahara hasa walimu ,kupata mshahara napo mpaka achape mguu kwenda wilayani maili zaidi ya 50.

Wanafunzi wa msingi kipindi hiki waliingia asubuhi na kutoka jioni bila masomo hakuna walimu.

kipindi hiki walimu walimaliza chuo bila kuajiliwa mpaka miaka 1998 ndio wamepata ajila.

Kushuka kwa Elimu ya UDSM na elimu kwa ujumla ni consequences zinazotokana na miaka hii 1990-1996.

Kipindi hiki kilikua ni kushinda kwenda sekondari wilaya nzima wanaoenda secondari baadhi ya wilaya walikua hawafiki hata wanafunzi 100.

Serikali ilikosa nidhamu ,serikali ilikosa mwelekeo
Rais wa nchi alikua SHEMEJI yani mtani wa wanafunzi.

Mkapa kashika serikali iliyokua ni VIRTUAL serikali .Mwinyi hakuna alichofanya zaidi ya RUKSA yani bidhaa kutapakaa kutoka nchi za nje.

Najua wengi tunampenda Mwinyi kwa sababu tu ktk kipindi chake ndio tuliona Video na films za akina RAMBO ,VANDAME, LANJITI nk

Kila binadamu ana mabaya yake lakini mazuri aliyofanya ni makubwa zaidi ya kiwira .

Mwinyi aliua makampuni yote na viwanda karibu vyote vya umma

MWAtex,mutex,kagera sugar vyote vilikua ni makazi ya NGUCHIRO na si kwamba kulikua na mashine ndani yani hata machine zilikua zinang'olewa na kuuzwa.
Sasa Mkapa kubinafsisha hayo makapi imekua nogwa?? Kampuni zipi zilikua hai wakati mkapa aniingia madarakani kama sio sigara na bia ?

Kwanza hizo masalia ya viwanda hata angevigawa bure kwa watanzania wachache sana wangevichukua na kuviendeleza zaidi ya AZAM,Mengi na Gachuma.

Kumbe cha kuangalia hapa si bei gani kilizwa bali Serikali inaingiza ,mapato na bado nchi inazalisha bidhaa zake.

Tungeyakumbatia hayo maviwanda kwa kudemand mahela mengi na yakakosa watu wa kuyaendeleza serikali ingelikua wapi? ingetegemea sijui nini??
 
Ni vigumu kuyaona mazuri ya Mkapa kama tayari una conclusion

Maisha Bora ni ELIMU bila elimu hakuna kitu ,kama unataka kuona mazuri ya Ben kaulize wafanyakazi wa Serikali kati ya miaka 1990-1996 hasa walimu wa shule za misingi.

Wafanya kazi waliacha kazi nakuamua kuwa wafanya biashara, walikua hawalipwi mishahara hasa walimu ,kupata mshahara napo mpaka achape mguu kwenda wilayani maili zaidi ya 50.

Wanafunzi wa msingi kipindi hiki waliingia asubuhi na kutoka jioni bila masomo hakuna walimu.

kipindi hiki walimu walimaliza chuo bila kuajiliwa mpaka miaka 1998 ndio wamepata ajila.

Kushuka kwa Elimu ya UDSM na elimu kwa ujumla ni consequences zinazotokana na miaka hii 1990-1996.

Kipindi hiki kilikua ni kushinda kwenda sekondari wilaya nzima wanaoenda secondari baadhi ya wilaya walikua hawafiki hata wanafunzi 100.

Serikali ilikosa nidhamu ,serikali ilikosa mwelekeo
Rais wa nchi alikua SHEMEJI yani mtani wa wanafunzi.

Mkapa kashika serikali iliyokua ni VIRTUAL serikali .Mwinyi hakuna alichofanya zaidi ya RUKSA yani bidhaa kutapakaa kutoka nchi za nje.

Najua wengi tunampenda Mwinyi kwa sababu tu ktk kipindi chake ndio tuliona Video na films za akina RAMBO ,VANDAME, LANJITI nk

Kila binadamu ana mabaya yake lakini mazuri aliyofanya ni makubwa zaidi ya kiwira .

Kuna msemo wa Kiswahili kuwa kizuri kinajiuza... Kama kuna mazuri aliyoyafanya Mkapa yatakuwa self evident. Tusingekuwa na haja ya kuyajadilia hapa.
 
Ni vigumu kuyaona mazuri ya Mkapa kama tayari una conclusion

Maisha Bora ni ELIMU bila elimu hakuna kitu ,kama unataka kuona mazuri ya Ben kaulize wafanyakazi wa Serikali kati ya miaka 1990-1996 hasa walimu wa shule za misingi.

Wafanya kazi waliacha kazi nakuamua kuwa wafanya biashara, walikua hawalipwi mishahara hasa walimu ,kupata mshahara napo mpaka achape mguu kwenda wilayani maili zaidi ya 50.

Wanafunzi wa msingi kipindi hiki waliingia asubuhi na kutoka jioni bila masomo hakuna walimu.

kipindi hiki walimu walimaliza chuo bila kuajiliwa mpaka miaka 1998 ndio wamepata ajila.

Kushuka kwa Elimu ya UDSM na elimu kwa ujumla ni consequences zinazotokana na miaka hii 1990-1996.

Kipindi hiki kilikua ni kushinda kwenda sekondari wilaya nzima wanaoenda secondari baadhi ya wilaya walikua hawafiki hata wanafunzi 100.

Serikali ilikosa nidhamu ,serikali ilikosa mwelekeo
Rais wa nchi alikua SHEMEJI yani mtani wa wanafunzi.

Mkapa kashika serikali iliyokua ni VIRTUAL serikali .Mwinyi hakuna alichofanya zaidi ya RUKSA yani bidhaa kutapakaa kutoka nchi za nje.

Najua wengi tunampenda Mwinyi kwa sababu tu ktk kipindi chake ndio tuliona Video na films za akina RAMBO ,VANDAME, LANJITI nk

Kila binadamu ana mabaya yake lakini mazuri aliyofanya ni makubwa zaidi ya kiwira .

Sina haja ya kwenda kumuuliza yoyote kuhusiana na 'mazuri' ya Mkapa. Hao wafanyakazi unaowataja wamejaa tele hapa JF na sijasikia hata siku moja wakimtetea fisadi Mkapa. Wewe unayemtetea labda ulinufaika kwa namna moja au nyingine na ufisadi wa Mkapa, lakini Watanzania walio wengi hawakunufaika na chochote.

Nimeuliza mazuri aliyoyafanya fisadi Mkapa ni yepi? Je, yanaweza kuwekwa hapa? 😕
Ooh! Kamuulize huyu kamuulize yule! Nyerere ameng'atuka miaka 23 iliyopita pamoja na kuwa alikuwa na makosa yake lakini leo hii ukiuliza Watanzania wengi mazuri aliyoyafanya Nyerere basi hawatapata kigugumizi na kukwambia labda nenda kawaulize watu wa Butiama au wale waliokuwa Ikulu wakati alipokuwa madarakani. Toka kona moja ya nchi mpaka kona nyingine ya nchi Nyerere mazuri yake hayajifichi pamoja na kuwa mengine hayakuwa na mafanikio makubwa kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake kama kupigwa vita na mataifa ya magharibi kwa kufuata siasa za ujamaa na pia kupanda kwa bei kubwa ya mafuta duniani mwaka 1973, vita dhidi ya nduli Idi Amini 1979, na ukame mkubwa ulioikumba Tanzania mwaka 1975.

Sasa uliza matatizo ya Mkapa yote yamesababishwa na wizi na ufisadi wake na sera ambazo zilitowa upendeleo dhahiri kwa wageni wachukuaji badala ya Watanzania.

Kwa Watanzania wengi Mkapa ni fisadi tu na wengi tungependa afikishwe Mahakamani kushtakiwa dhidi ya wizi alioufanya na hatimaye kufilisiwa. Sheria za nchi ni lazima ziwabane wote bila upendeleo wowote wa kujali wana utajiri mkubwa kiasi gani au walikuwa na wadhifa mkubwa kiasi gani ndani ya chama au serikali.
 
Back
Top Bottom