Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

which includes you, me and mkapa!

Mwanakijiji nafikiri umeji include kwa kigezo cha kwamba labda wewe kama mwananchi wa kawaida umesaidia kubaki kwake madarakani kwa kumpigia kura ama kwa njia nyinginezo...Kwa maana kuwa wananchi nao wameshiriki kuwaweka madarakani.

Ila naomba tusisahahu INFLUENCE ALIYOKUWA NAYO MWALIMU NA AMBAYO BADO ANAYO NDANI YA FIKRA ZA WENGI WETU.

Upande wa Mkapa ni wa kulaumu kwani yeye ndiye tuliyempa mdhamana wa Taifa letu na yeye akaliuza na the rest kugawana na wenzake.

Hata hivyo kwangu binafsi mtu wa kulaumu ni MWALIMU MWENYEWE...Pamoja na wale waliokubali kuwa MAPANDIKIZI kwenye uchaguzi ule wa 1995.

Tena nafikiri alikuwa na BIFU NA WACHAGGA KWANI ALIPOKUJA MOSHI KUMNADI MKAPA ALIZOMEWA!

Alikuwa na Picha ya Mkapa na akainyanyuwa juu na kusema TAKA MSITAKE HUYU NDIYE RAIS WENU AJAYE!

Watu walipiga ukunga na kuzomea kwani walikuwa wameshachoshwa na UFISADI!

Yeye kama baba wa Taifa ni wazi kilimuudhi na kilimkuna sana kwani yalishamtokea kama hayo kipindi cha nyuma wakati wa harakati za Uhuru na pia mara baada ya uhuru.

Ukiwa na mawazo mazuri na Taifa halafu ukawa na nia iliyojificha matokeo yake ni UNAFIKI na hakuna UKWELI bali PROPAGANDA na HUKU utendaji ukiwa ni HAKUNA!

Hivyo basi Baba wa Taifa, Marando, Lamwai, Kaburu na wengineo...Ni watu watakaoingia kwenye Historia kwani waliyakumbatia mawazo ya A SINGLE PERSON(MWALIMU) Na kuwa eliminite wananchi walikokuwa wameunganishwa na mpmbano wa kishujaa wa MREMA NA UJUMBE WAKE KWA WALALAHOI!

HAKIKA MREMA NI SHUJAA!

Sasa tunataka Haki...Na Haki ni SHERIA...Tunataka kuona kuwa huu unakuwa ni MWISHO WA HAYA YOTE!

Na kuwa ni MWANZO WA MAENDELEO YANAYOTOKANA NA UHURU WA KWELI.
 
mag3

Ubovu ni Taifa lisilotaka kwenda mbele ,nitaifa linalofanya mambo yaliyopita na kuyaleta wakati ambapo panatakiwa tuangalie mambo ya mbele zaidi.

ni taifa watu wake wanaopenda kutobadirika na kuenda na world of digital na kupendelea zaidi analog world.

Ndio utasikia pande zote mbili yani upinzani na utawala Mwl aliendesha mambo hivi chama chake yani TAA/TANU alichangiwa.

Hayo yalikua mazuri na mwafaka kwa wakati huo si kwamba mazuri na mwafaka kwa wakati huo ndiyo yatakua mazuri na mwafaka kwa wakati huu.Fundamentally mazuri ya TAA/TANU ukiyachukua inabidi yawe processed na sio kuchukua kama yalivyo.

Nikuulize swali
Hapa JF ni maada ngapi zinazojadili jinsi ya kutengeneza ajira TZ?? Na kuendeleza ELimu kwa misingi bora??
Kama sio Siasa zenye masilahi ya walengwa wachache.
 
Mkamapa hapo juu umemjibu nani?
Maana kama ulikuwa una analyze point uliyoitoa before bado sioni uhusiano wa wewe kuquote hiyo posting yako kwani maelezo ni yale yale na wala hakuna counter arguments ama hata further information or even analyisis.
 
Mkamap,

Mfano wako mzuri sana mkuu tena hapo nakupa pongezi..
Na ndio maana nimesema umeshindwa kuona wanachozungumza wana JF..
Alichofanya Mkapa ni kuwaozesha wale wajukuu kwa watu wenye fedha kisha ule mtaji akauweka benki na kutangaza maendeleo.. hao wajukuu ambao walikuwa miaka 8, 9 na 10..
Na kila naposoma maandishi yako yananipa hisia kwamba hata wewe ungefanya hivyo hivyo kwa sababu kusubiri mtoto wa miaka 8 apate elimu ya msingi, sekondary kisha sijui chuo kikuu loooh sii utakuwa umesha kufa?... kwa hiyo solution ni kuwaozesha mapema kabla hujafa..mnachotazama ni maisha yenu nyie vizee sio ya kizazi kijacho!..
Ndicho alichofanya Mkapa ktk maendeleo ya Tanzania... period!

Tatizo usipofanya hivyo ni kwamba hata siku 10 za kusubiri hazitafika

Maana wote watakua wameteketea kwa njaa.Sasa sijui utakua unasubiri nani??
Chakula hakuna walia njaa wajukuu kelele njaa wewe unashamba baada kumpa mkulima alime akupe mazao wajifanya bahiri .
Mali ya bahiri yaliwa na mchwa
 
Mkamapa hapo juu umemjibu nani?
Maana kama ulikuwa una alnalyze point uliuoitoa before bado sioni uhusiano wa wewe kuquote hiyo posting yako kwani maelezo ni yale yale na wala hakuna counter arguments ama hata further information or even analyisis.

Mag3

anajifanya teknolojia ya mzungu anaijua sana.
 
"Mkapa is the best president.Ila kosa lake tu nikuongoza Taifa bovu kama Tanzania." I couldn't agree more with you (Mkamap).

I know it's understandably hard for some of you to accept the assertion that Mkapa is one the finest presindets we ever produced; and that the problem is not him rather the bad supporting casts he had (mawaziri, wakurugezi n.k)--that Mkapa alone could not have possibly (magically if you will) in any way whatsoever undone/correct the wrongs and errors of colonial institutions, ujamaa policies, Mwinyi's economy, stupid, dysfuctional perfomance of the government/ immense corruption within ten years time frame. Let's be realistic here people.

Yes, I understand why you are angry for me defending Mkapa. But for those of you who have had a chance of reading my previous articles/threads, you must know well that I ain't not trying to be scarstic here. I'm trying to be objective. And that's why, if you carefully read my thread, you'll find out that I do also aknowledge the errors and wrongs done by Mr.Cean.

The point is: (if I can paraphrase William Tuf), failure to accord credit to anyone for what he may have done is a great weakness in any man

Yes, Mkapa amefanya mabaya, nakubaliana na nyie. Ila let's give the man his due credit where possible, and stop dragging the man's legacy into the mad by buying into all these Kikwete's inner circle-smear-campains ocherstrated to divert people's attention form pressuring his administration to perfom better.

Tanzania deserve better.
 
Kwahiyo basi mimi nafikiri wananchi wabovu na mkapa na kikwete mbovu mbovu wakae chini waulizane maswali mabovu mabovu kuhusu MEREMETA MBOVU?

Au nyie mwaonaje ndugu zangu!

Madhali tushakubaliana sisi sote ni WABOVU..Basi sioni ni kwanini tusikae chini sisi na UBOVU WETU NA TUJIBIANE MASWALI KIU BOVU UBOVU!
Shida IKWAPI?
 
Mkamap an point jmush1. Tatizo ni kwamba, Tanzania ni mbovu. Wasomi wetu wengi ambao wamekulia, soma na kuzeekea Tanzania (ambao hawajatoka nje ya nchi) wamechangia sana kuliangusha taifa letu. Angalia wewe mwenyewe: hivi kweli utanetemea tutoe vichwa vizuri vya wachumi na ma-injinia pale UDSM ambao wataifanya tanzania iweze kushindana vizuri kwehe global economy? No, hapana. Tatizo ni kwamba mind set ya watanzania wengi bado iko kwenye cold war na siasa za vijiji vya ujama na kusubiri serikali iwafanyie kila kitu.
 
Nyie watu msitufanye sisi ni mazezeta...Itakuwa vipi mkiri kuwa ni kweli wananchi hawakuandaliwa na RHUKSA NA WHITE PAPER za MWINYI NA MKAPA...Halafu at the same time MGEUKE NA KUSEMA WANANCHI NI WABOVU?

Yani kumbe PLAN YENU YA KUJISAFISHA NI KUTUKANDAMIZA WANANCHI KWA KUSEMA SISI NI WABOVU?

Hizo ndio story MKAPA ANAPIGA NA WENZAKE AKIWA PRIVATE WAKINYONYA MVINYO NA KUJISIKIA RAHA HUKU MAMILIONI WAKIFA NJAA?

Ebu acheni Utani...Mnasema wananchi ni WABOVU?

AMA NI NAMNA YA KUJIANDAA KUTUMIA JESHI NA POLISI KUWADHIBITI KWA VIGEZO KUWA WAO NI WABOVU?

NO WAY!
 
Tanzania sio mbovu ila wabovu ni watanzania

Ndio MAANA NASEMA KUWA ...KAMA KWELI TUNGEWEZA KUJUWA NI NANI YUKO BEHIND HII IDENTITY...Na kugunduwa labda ni MKAPA...BASI WATANZANIA NDIYO WANGETAKIWA WAMWONYESHE UBOVU WAO!

AMA KWELI ZIS IS ZE OBVIOUS MKAPAZ MAP.

NB:Ni kweli Tanzania siyo mbovu...Tanzania itakuwa vipi mbovu na ina MFUTA HUKO MTWARA ALIKO MKAPA NA INA MAGOLD YA KUMWAGA HUKO MARA ALIKO WANGWE?
 
mkapa alikuwa raisi bomu kuliko, na hata mtu atumie chlorite kusafisha, bado atakuwa mchafu.
katika watu waliopata mteremko katika kuongoza tanzania yetu ni mkapa, maana aliona makosa ya waliomtangulia, i.e mwl na ruksa, hivyo yeye kurudia makosa hayo hakueleweki kwa mtu mwenye akili timamu, labda huyo mtu awe punguani. kuhusu financial security ikumbukwe kwamba mafao ya viongozi yaliongezwa marudufu kufikia 80% ya mshahara wa current president etc, hivyo hakuhitaji kufuja mali au kuingia mikataba mibovu.
labda tuchukulie kauli ya Mzee ruksa kwamba kuna watu waliosoma lakini hakuelimika au alikuwa just limbukeni wa madaraka na mashai kwa jumla
 
Nyie mnaosema wananchi ni WABOVU NAOMBA MLETE TAKWIMU ZA WATOTO WANAOENDA SHULE NA PIA TULINGANISHE KATI YA BAJETI YA MASHANGINGI VS ILE YA ELIMU!
Yani hata hapo MLIMANI PENYEWE MAJI HAKUNA HALAFU MNASEMA WANANCHI NI WABOVU?
 
Watanzania ni wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk

Leo hii ukianzisha biashara ya kuuza manyoya ya kuku wakaona unaendelea wengi watakuja kujipanga ulipo na wao wataanza kuuza mnyoya ya kuku natena wakilalama wewe mwanzirishi unawanyima wateja.

Hapa JF kuna wasomi wazuri ,hapa Jf kuna watu wenye uwezo kifedha lakini badala ya kujadili mambo ya kuinua wananchi pamebaki jukwaa la siasa tena lisilo na masilahi kwa taifa zaidi ya wanasiasa wachache .

Leo hii nilitegemea JF kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ na Tena wahadhili watapatikana humu na tena kwenda kuingia ubia Na Serikali/Bodi ya mikopo ya kwamba wanafunzi watakaosajiriwa walipiwe fee na ili kurahisisha uendeshaji.Hilo hakuna

Lakini akiamua kufanya hivyo JK utasikia wanafiki conflict of interest.Kufanya hatutaki akifanya mwingine confilict of interest kwa hiyo nani afanye sasa?? Kazi tunapiga siasa zenye maslahi manono kwa wachache.

Serikali haiwezi kutuletea maisha bora ,maisha bora yataletwa na watanzania wachapakazi,wasio wanafiki na wenye upeo mpana.
 
Watanzania ni wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk

Leo hii ukianzisha biashara ya kuuza manyoya ya kuku wakaona unaendelea wengi watakujika kujipanga ulipo na wao wataanza kuuza mnyoya ya kuku natena wakilalama wewe mwanzirishi unawanyima wateja.

Hapa JF kuna wasomi wazuri ,hapa Jf kuna watu wenye uwezo kifedha lakini badala ya kujadili mambo ya kuinua wananchi pamebaki jukwaa la siasa tena lisilo na masilahi kwa taifa zaidi ya wanasiasa wachache .

Leo hii nilitegemea JF kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ na Tena wahadhili watapatikana humu na tena kwenda kuingia ubia Na Serikali/Bodi ya mikopo ya kwamba wanafunzi watakaosajiriwa walipiwe fee na ili kurahisisha uendeshaji.Hilo hakuna

Lakini akiamua kufanya hivyo JK utasikia wanafiki conflict of interest.Kufanya hatutaki akifanya mwingine confilict of interest kwa hiyo nani afanye sasa?? Kazi tunapiga siasa za zenye maslahi manono kwa wachache.

Serikali haiwezi kutuletea maisha bora ,maisha bora yataletwa na watanzania wachapakazi,wasio wanafiki na wenye upeo mpana.

OK Lets assume the self described MR CLEAN IS SOMEWHAT CLEAN..THEN WHATS NEXT?

Kwasababu to be honest with you wananchi hao hao wabovu wana maswali ya kumtoa kijasho chembamba kama si kumpa presha pale watakapoanza kuuhoji huo u CLEAN WAKE NA UBOVU WAO WANANCHI NA NI NINI HASWA KILICHOSABABISHA UBOVU WAO HUO WA BARABARA, ELIMU, MAJI SAFI, MADAWA NA HOSPITALI...NA HATA UBOVU WA VYAKULA NA OTHER CONSUMER'S GOODS!

SASA NANI MBOVU?
 
Mtaalamu_wake,

Mkuu binafsi nakubaliana na maelezo ya Mkamap na nadhani ndicho alichokuwa akisema MgonjwaUkimwi, lakini issue hapa ni UONGOZI wa Mkapa kama rais. Wananchi wote sio marais wanaoweza kujenga hoja ya Utawala kuwa questioned..Nini chimbuko la umaskini wetu ni uongozi Mbaya kwani Uongozi mzuri humtoa mtu ktk ubaya wa hali za wananchi na kuwa nzuri. Ni ubaya huo anaozungumzia Mkamap ambao Mkapa alityakiwa kuuona na kuunyoosha kama angekuwa kiongozi mzuri.. laa sivyo alikuwa akiongoza kitu gani kundi la malaika!

Wananchi wote pamoja na sisi wenyewe tuna makosa yetu kama raia, wananchi na tunaweza kulinganisha makosa yetu kwa kizazi kama wananchi lakini sio Watawala. Swala hapa ni Watawala mkuu!
Sote tunafahamu jinsi Ujamaa ulivyotugandisha kimaendeleo. Lakini ajabu ni kwamba hadi leo hii ndugu zetu wanashindwa kutafuta riziki zao isipokuwa kwa kusubiri misaada toka nje. Ni hali ambayo imejengwa na mifumo ya kitaifa.
Ebu jiulize, imekuwaje wananchi karibu wote kwa asilimia isiyopungua 60 kutegemea msaada toka kwa msamalia fulani hali ni mfumo huo huo unatumika ktk kuiendesha NCHI yetu..Tazama jinsi tunavyoabudu misaada ya IMF.
Taifa letu nitegemezi la misaada na raia wake ni tegemezi la misaada vile vile tofauti na wakati ule wa Ujamaa..Je, kila lawama zenu kwa hawa wananchi mbona mnashindwa kuziona kitaifa na kudai kwamba bila misaada tutakwama lakini hao ndugu zetu wanaodai misaada toka kwa ndugu zao mnawaona wao wazermbe!.. Je hivi kweli ukikata misaada nyumbani watu watakufa njaa? sidhani ila yawezekana ikawa ni msukumo mzuri wa wao kuanza kutafuta riziki zao vizuri, hivyo hivyo kitaifa..
Binafsi naamini kabisa kwamba kinachoendelea kitaifa ndicho kinachotafsirika kwa wananchi...Wamarekani walivyo ni sawa kabisa na mwenendo wa Taifa lao! Waarabu wanaishi kama tawala zao zilivyo, Wahiondi na hata wachina wote maendeleo yao yanatokana na tabia za maisha yao kutokana na kile kilichotangulia...
Mfumo wa serikali ndio humkunja samaki akingali mbichi..
 
Nataka wanijibu swali...Bara bara mbovu, shule mbovu, hospitali mbovu na madawa na vyakula vibovu...Nani mbovu aliyesababisha hayo?

Kati ya wabovu viongozi na wabovu wananchi wabovu wanaoathrika kwa UBOVU WA HUDUMA ZA JAMII...Nani yuko responsible na mali za TAIFA?
Na NANI MBOVU?

USIMAMIZI MBOVU WA MALI ZA TAIFA NI WA NANI?

Mkamap na wenzako naomba jibu tafadhali.
 
Watanzania ni wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk

Leo hii ukianzisha biashara ya kuuza manyoya ya kuku wakaona unaendelea wengi watakuja kujipanga ulipo na wao wataanza kuuza mnyoya ya kuku natena wakilalama wewe mwanzirishi unawanyima wateja.

Hapa JF kuna wasomi wazuri ,hapa Jf kuna watu wenye uwezo kifedha lakini badala ya kujadili mambo ya kuinua wananchi pamebaki jukwaa la siasa tena lisilo na masilahi kwa taifa zaidi ya wanasiasa wachache .

Leo hii nilitegemea JF kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ na Tena wahadhili watapatikana humu na tena kwenda kuingia ubia Na Serikali/Bodi ya mikopo ya kwamba wanafunzi watakaosajiriwa walipiwe fee na ili kurahisisha uendeshaji.Hilo hakuna

Lakini akiamua kufanya hivyo JK utasikia wanafiki conflict of interest.Kufanya hatutaki akifanya mwingine confilict of interest kwa hiyo nani afanye sasa?? Kazi tunapiga siasa zenye maslahi manono kwa wachache.

Serikali haiwezi kutuletea maisha bora ,maisha bora yataletwa na watanzania wachapakazi,wasio wanafiki na wenye upeo mpana.

Je wewe umejiweka kwenye kundi gani? kundi la wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk?

Umeanzisha maada ngapi za kujadili mambo ya kuinua wananchi humu JF?

Sio lazima watu wengine waanzishe maada za kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ kwani wewe pia unaweza kuanzisha halafu wengine wakakuunga mkono.

Ama kweli nyani haoni ......!
 
Mtaalamu_wake,

Mkuu binafsi nakubaliana na maelezo ya Mkamap na nadhani ndicho alichokuwa akisema MgonjwaUkimwi, lakini issue hapa ni UONGOZI wa Mkapa kama rais. Wananchi wote sio marais wanaoweza kujenga hoja ya Utawala kuwa questioned..Nini chimbuko la umaskini wetu ni uongozi Mbaya kwani Uongozi mzuri humtoa mtu ktk ubaya wa hali za wananchi na kuwa nzuri. Ni ubaya huo anaozungumzia Mkamap ambao Mkapa alityakiwa kuuona na kuunyoosha kama angekuwa kiongozi mzuri.. laa sivyo alikuwa akiongoza kitu gani kundi la malaika!

Wananchi wote pamoja na sisi wenyewe tuna makosa yetu kama raia, wananchi na tunaweza kulinganisha makosa yetu kwa kizazi kama wananchi lakini sio Watawala. Swala hapa ni Watawala mkuu!
Sote tunafahamu jinsi Ujamaa ulivyotugandisha kimaendeleo. Lakini ajabu ni kwamba hadi leo hii ndugu zetu wanashindwa kutafuta riziki zao isipokuwa kwa kusubiri misaada toka nje. Ni hali ambayo imejengwa na mifumo ya kitaifa.
Ebu jiulize, imekuwaje wananchi karibu wote kwa asilimia isiyopungua 60 kutegemea msaada toka kwa msamalia fulani hali ni mfumo huo huo unatumika ktk kuiendesha NCHI yetu..Tazama jinsi tunavyoabudu misaada ya IMF.
Taifa letu nitegemezi la misaada na raia wake ni tegemezi la misaada vile vile tofauti na wakati ule wa Ujamaa..Je, kila lawama zenu kwa hawa wananchi mbona mnashindwa kuziona kitaifa na kudai kwamba bila misaada tutakwama lakini hao ndugu zetu wanaodai misaada toka kwa ndugu zao mnawaona wao wazermbe!.. Je hivi kweli ukikata misaada nyumbani watu watakufa njaa? sidhani ila yawezekana ikawa ni msukumo mzuri wa wao kuanza kutafuta riziki zao vizuri, hivyo hivyo kitaifa..
Binafsi naamini kabisa kwamba kinachoendelea kitaifa ndicho kinachotafsirika kwa wananchi...Wamarekani walivyo ni sawa kabisa na mwenendo wa Taifa lao! Waarabu wanaishi kama tawala zao zilivyo, Wahiondi na hata wachina wote maendeleo yao yanatokana na tabia za maisha yao kutokana na kile kilichotangulia...
Mfumo wa serikali ndio humkunja samaki akingali mbichi..

Watanzania wazembe ,wavivu ,wanafiki.

Kwa macho yangu nimeona mateja,waulaji,wamachinga wakikamatwa pale Dar na kupelekwa pwani wakigawiwa mashamba ya bure walime badala yake walikimbia na kumwita Dikiteta aliyepwapeleka.

Najua walichotaka ni kupewa pesa na sio shamba na hata hivyo pesa wangezipiga mvinyo na matanuz.

Najua walitaka ma trekta wapewe bure lakini hata wangeyafilisi na kuuza vifaa kama yalivyofilisiwa RTC,viwanda kuwa nyumba za Nguchiro.
Kwa uzembe wetu wa kufikiri tuko lazi kusema maisha bora yanaletwa na serikali ama kiongozi wakati sisi tunachapa siasa vijiweni
 
Mkamap,
Mkuu umeshasema wala unga, njoo huku uwaone hao wala unga wanapewa kila kitu toka nyumba posho kubwa kuliko mishahara ya baadhi ya watu lakini hadi leo hii hali zao ndio kama hivyo....
Na kuwapa wala unga mashamba ni moja ya UONGOZI mbaya! kiongozi mzuri hata siku moja humpi shamba mtumia bwibwi... huyu anatakiwa kupelekwa hospital kupata matibabu!..
 
Je wewe umejiweka kwenye kundi gani? kundi la wanafiki ,wavivu wa kufikiri ,waoga wakuchukua risk?

Umeanzisha maada ngapi za kujadili mambo ya kuinua wananchi humu JF?

Sio lazima watu wengine waanzishe maada za kujadili jinsi ya kuchangisha michango na kutafuta wabia ili tukajenge vyuo vikuu TZ kwani wewe pia unaweza kuanzisha halafu wengine wakakuunga mkono.

Ama kweli nyani haoni ......!

Tatizo unajifanya kwa makusudi kutoelewa.
Kuna sehemu nimesema ninyi ?? ama nimesema watanzania??
 
Back
Top Bottom