Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,915
....kitila Mkumbo Una Akili Sana ...wala Haikuwa Ajabu Pale Ulipopewa Nafasi Ya Kufanya Kazi Pale Udsm ..mara Tu Baada Ya Ku Graduate....
Nafikiri Umetoa Mwelekeo Wa Namna Tunavyotakiwa Kuyachambua Mambo Hapa Jf.........maana Wengi Hapa Wanapenda Tu Kusema ...mkapa Hakufanya Kitu!!!....au Mkapa Sio Fisadi !!!
Naomba Wachambuzi Mfuate Msingi Alioleta Kitila Ili Hii Mada Ichambuliwe Kitaaluma Zaidi.....naomba Kuwasikia Wachambuzi Maarufi ..kama Rev Kishoka ,kichuguu,fmes,....na Wengine.....woote!!
phillemon mikael,
Mimi si maarufu lakini nakumbuka siku Mkapa amewaita waandishi wa habari na kueleza nia yake ya kutaka kugombea Uraisi, alizungukwa na watu wawili. Kwa upande moja alikuwapo Waziri Mkuu mstaafu, Judge Sinde Waryoba na upande wa pili alikuwepo aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa wakati huo wa Habari Corporation, Jenerali Ulimwengu. Nakumbuka Watanzania wengi, pamoja na kutoridhika na utendaji wa CCM, tulikuwa na kila sababu ya kuwa na "HOPE" especially baada ya utawala wa Ali Hasan Mwinyi. Na kilichowaongezea matumaini wananchi wengi ni kule kuungwa mkono na Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere. Hata hivyo kuna wachache kati yetu tuliojiuliza mara mbili hivi huyu Mkapa anatokea wapi na sifa zipi zinamfanya awe chaguo bora. Wenzetu walio ughaibuni na hasa nchi ya Marekani alikowahi kuwa balozi walitueleza jinsi alivyojumuika nao kwenye shughuli mbalimbali. Sifa zilianza kutafutwa ili aweze kuuzika na moja tu ilipatikana, hakuwa na kashfa iliyojulikana. Iweje hii iwe sifa pekee na itoshe kumkabidhi any Tom, Dick na Harry jukumu la kuongoza nchi - kosa namba moja.
Nakumbuka pia siku alipokutana na waandishi wa habari, kwa mara ya kwanza na ya mwisho, baada tu ya kuchaguliwa kuwa Rais. Ubabe aliouonyesha siku hiyo did not befit mtu aliyewahi kuwa balozi wa nyumba kumi leave alone balozi wa nchi. Tabia hii ilitosha kabisa kuwasha taa nyekundu of what was in store for us lakini kama kawaida ya Watanzania tulifunikwa na wingu la uCCM ambalo liko tayari kuita koleo kijiko. Rais huchaguliwa na kuapishwa kuwa ataitetea na atailinda katiba ya nchi ambayo kimsingi ni kulinda haki za wananchi wake. Katika mwaka wake wa kwanza tu Mkapa alivunja katiba kwa kukatisha maisha ya wananchi waliokuwa wanadai haki huko Pemba. Pia alishindwa kuwalinda wananchi waliokuwa wakishangilia ushindi wa Mbunge wao wa Temeke na kusababisha wengine wapate vilema vya maisha.
Madhambi mengine yamekwishatajwa lakini kuna mawili zaidi. Moja, katika kipindi chake mkewe alinunua jengo lililokuwa likitumika kama tawi la benki NBC kwa njia ambayo kwa nchi zenye sheria, hutafsiriwa kama fraudulent. Pili, katika utawala wa Mkapa, pamoja na kuigeuza Ikulu sehemu ya biashara, hasara ambayo nchi iliipata kutokana moto mkubwa uliounguza sehemu muhimu ya Ikulu bado haijulikani.
Hitimisho: Kujaribu kumtetea Mkapa kwa kutaja mazuri aliyoyafanya (ambayo ni wajibu wake) na kulinganisha na mabaya (ambayo si wajibu wake) ni ujuha usio mfano.Watu wamefungwa na wengine kunyongwa kwa sababu kuna siku walienda kinyume cha wajibu wao licha ya waliyotenda awali. Mabaya aliyofanya Mkapa akiwa Rais wa Tanzania hayasameheki.