Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Babu ataka kusema: I fundamentally disagree with you. You can't just disrespect your former president like that man! kama ni fisadi, mbona hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yake. Acheni ushabiki usiokuwa na maana vijana. Mkapa sio fisadi. Period.
 
....inawezekana mkapa alikuwa mzuri,na ninaamini alikuwa better kuliko mwinyi na sijui kwa speed hii ya Jk kama anaweza kumfikia mkapa kwa aliyoyafanya...tukubali mkapa alijenga barabara nyingi sana na kukusanya kodi vizuri ingawaje hizi kashfa za Meremeta,EPA...ila kikubwa ninachomlaumu mkapa ni wizi wa kura zanzibar na kuua wapemba,JK is just a hopeless guy...lakini lazima awajibike kwa upuuzi wa rushwa aliofanya kiwir na mikataba mibovu aliyotuingiza na hatutamwachia!
 
Kuhani...Why all the name-calling, homie?

Homeboy/homegirl, you kidding me?

Wewe ndio umeanza kutuita sisi wote tunaotofautiana na wewe hapa ni foolish!

Au naongopa?

Umesema sisi Watanzania ni foolish!

Sasa nani mwenye matusi hapa sisi au wewe?

Tena ni kwa sababu Wabongo wenzangu huwa hawajali jali statement za watu, lakini ungekuwa unaishi kwenye dunia ya wanao maindi maindi kauli ungejikuta unaomba msamaha hapa, trust me. Yani kuanzia leo ungeiona JF chungu kwa negative treatment ambayo ungeipata.

Ukiita watu majina kijumla jumla hivyo sio poa, na hakuna tusi baya kama kumwambia mtu pumbavu. Na ni afadhali useme 'wewe Kuhani pumbavu' kuliko utuambie kijumla jumla 'nyinyi nyote pumbavu.'

Wewe ndio umetuita sisi foolish, homie!
 
I suppose humu vijana wengi wamedata kwelikweli. Nevertheless, "If you judge, investigate." Acheni tabia ya kurukia mambo msiyoyajua.
 
Mkapa; jiwe linaloelekea kudharauliwa na Watanzania limekuwa jiwe la kimataifa

Na, Padri Kitambo Robert

Rais mstaafu Benjamin Mkapa ni Rais wa Awamu ya Tatu tangu Tanzania ipate uhuru, na ni rais ambaye aliingia Ikulu kupitia mfumo wa vyama vingi. Amekaa madarakani tangu Novemba 23, 1995 hadi Desemba 21, 2005. Hakuweka wazi kaulimbiu yake bali siku zote alisisitiza ukweli na uwazi, ametambulika kama mzee wa itikadi hii. Alitumia ukweli na uwazi ikiwa ni njia mojawapo ya kuleta maendeleo kwa Watanzania. ‘Che Mkapa’ amempisha Jakaya Kikwete, mwenye kaulimbiu ya ‘Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari mpya’ (naye ni baba wa dhana hii), ikiwa ni njia mojawapo ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.

Ni wazi katika kipindi chake cha uongozi, Mzee Mkapa ameikuta Tanzania ni nchi ambayo imetawaliwa na dhana ya ruksa iliyoanza kushamiri katika awamu ya pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi. Mfumo huu wa ruksa kwa upande mmoja, umetokana na nguvu za nchi za Magharibi zikiwa chini ya mfumo unaojulikana kama ‘Structural Adjacent Program’ ni Marekebisho ya uchumi yaliyoongozwa na mawazo ya Margreth Thatcher wa Uingereza na Ronald Regan wa Marekani. Kwa upande mwingine, taasisi za kimataifa zinazohusiana na masuala ya fedha, Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (IMF) nazo zilishinikiza nchi zinazoendelea kurekebisha njia za uzalishaji ikiwa katika harakati za kupiga vita umaskini na kuleta maendeleo. Marekebisho hayo yalilenga kufungua milango kwa ajili ya wawekezaji, kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za serikali kwa kuruhusu asasi zisizo za serikali kuingia katika shughuli zote za uzalishaji na soko la ajira, serikali kutojihusisha moja kwa moja na mambo mengi ya uendeshaji wa uchumi, bali serikali inabaki kuwa msimamizi tu.

Mzee Mwinyi alikumbana na haya mabadiliko na yeye kwa mtazamo wake na serikali ya wakati huo, waliyabariki na kuanza kutumika kwa jina la ruksa. Kwa Mtanzania aliyekuwepo wakati huo katika upevu na ukomavu wake kwenye masuala ya uchumi na siasa, alishuhudia mabadiliko mbalimbali, ikiwamo kuchangia huduma za jamii, mfano elimu na matibabu; kupunguzwa na kuachishwa kazi (redundancy), bei za bidhaa kupaa kila siku kunakosababishwa na shilingi yetu kushuka thamani kila siku, kufurika kwa bidhaa za nje kila kona ya Tanzania na mengine kadhaa wa kadhaa yaliyo pacha na haya.

Heshima ya kazi za serikali maofisini ilishuka, na kazi zingine zilianza kusahaulika na kukimbilia biashara. Kazi iliyodharaulika na wengi ni ualimu wa shule za msingi. Wengi walikimbia kazi hii na kukimbilia biashara kwani kazi ya ualimu ilionekana hailipi. Madhara makubwa yalikuwa ni kufubaa kwa uchumi, kudumaa kwa huduma muhimu za jamii. Hii yote imetokea katika awamu ya pili. Haijulikani ni mfumo wa kijamaa, kibepari au mrengo wa kiliberali ndio tulikuwa tunafuata.

Katika kipindi chake, Mkapa hakutofautiana sana na mzee Mwinyi katika kurekebisha mifumo mbalimbali ya kiuchumi. Lengo la Mkapa ilikuwa ni kujenga uchumi mkuu (macro-economy). Yeye alichofanya ni kubinafsisha mashirika ya umma kwa kufungua milango kwa wawekezaji kwa ridhaa ya soko huria.

Kwa upande mwingine alijitahidi sana kukusanya kodi kama yeye alivyosema; “Mwaka 2003/04, mwenendo wa mapato ya ndani ulikuwa wa kuridhisha, hasa mapato yatokanayo na kodi. Uboreshaji wa mfumo wa kodi umeleta ongezeko katika ukusanyaji wa mapato kufikia kiasi cha wastani wa shilingi 108 bilioni kwa mwezi katika 2004/04, ikilinganishwa na mapato ya ndani yalikuwa yanakusanywa, mwanzoni mwa miaka ya 1990, yalikuwa chini ya wastani wa sh 25 bilioni kwa mwezi…” (Mkapa: Hali ya Taifa, Septemba 25, 2004).

Usimamizi haukuishia kwenye kodi tu bali hata shughuli zingine za uchumi. Kutokana na juhudi hizi Tanzania ikasamehewa madeni na nchi nyingi za Magharibi kuongeza misaada kwa Tanzania.

Mkapa wakati anaingia madarakani hali halisi ya kiuchumi kwa macho ya wengi bila kuangalia kwenye mafaili ya makabidhiano yake na mzee Mwinyi hali halisi ya maisha ilionekana katika hali ya ‘u-ruksa-ruksa’, ndiyo iliyokuwa imetawala. Kwa mtazamo huu basi, hali ya kwanza ilikuwa ni kuitoa kama si kuibadilisha hali hii ya ‘u-ruksa-ruksa’ kuwa katika utaratibu unaoeleweka. Hivyo basi, kazi kubwa ilikuwa ni kurudisha heshima ya kazi katika ofisi za umma zilizokuwa zimejeruhiwa na mfumo wa ruksa. Hii iliwezekana, ninyi mnaofanya kazi katika ofisi za umma mliliona hili. Kazi ilipata heshima na watu walithamini kazi.

Mkapa kama binadamu wengine na kama viongozi wengine, kwanza hawezi akawa mkamilifu katika kutenda bila kosa, kuna yale ambayo alikosea kama binadamu, kwa kutodhamiria, kudhamiria na kushauriwa na watendaji wake. Ukizingatia kuwa uongozi ni kazi ya timu (leadership is a team work), na mbaya zaidi katika siasa kuna kitu kinachoitwa kuwajibika na kulindana kwa pamoja (collective responsibility).

Pili, Mkapa kama kiongozi hawezi akamridhisha kila mtu kadiri kila mmoja anavyofikiria na anavyotaka.

Tatu, hawezi akapendwa na wote na papo hapo hawezi akachukiwa na wote. Kwa mantiki hii basi, katika kipindi chake kuna mambo mengi mazuri tu ameyatenda ambayo Watanzania wengi tunayaona bila kutumia ‘microscope’ na wala haihitaji kwenda mpaka maktaba kupekua vitabu au kusubiri nchi za nje waseme kilichotendwa na Mkapa. Sidhani kwamba kipindi chake cha utawala kimefunikwa na upungufu tu, yaani hapakuwa na mazuri aliyotenda akishirikiana na viongozi wengine na wananchi pia katika kuleta maendeleo kwa Watanzania...
Soma makala yote hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/8/5/makala7.php
 
You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.

Foolish people.

Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!

Be smart people.


(a) Naona una usongo sana na kutoa utetezi wa nguvu kwa niaba ya mkapa na vile vile kutukana wote wale wasiokubaliana nawe. Nadhani topic hii umeisambaza sehemu nyingi kwani mimi niliona na kuijibu hapa kwa kukushauri ifuatavyo:

Hebu changanua kwa kina ulinganishe mabaya na mema ya Mkapa halafu utuambie uzito umelalia wapi. Utakapofanya mchanganuo wako jitahidi uwe kiona mbali, usiwe myopic wa kuangalia mambo mdogo madogo yenye upeo wa miaka miwili au mitatu huku ukiacha mambo yenye athari za miaka 30 na zaidi ijayo.

Hiyo conclusion yako kuwa

Cha msingi hapa ni kujua kuwa Mkapa sio Malaika bali mwandamu. na kama mwadamu, naye pia anahadawa na tamaa ya kuwa na maisha yaliyotulia. You know, financial security and all those things, kwa ki-inglish.

Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).

inaonyesha mambo mawili:

(a) Unajua kuwa Mkapa aliboronga ila unataka kutafutsa sababu za kuhalalisha makosa yake. Sasa kama unajua kuwa Mkapa siyo malaika kwa nini useme kuwa Mkapa ni mtu msafi? Kwa taarifa yako, hiyo tamaa yake ya kutafuta financial security kwa njia zisizo halali ndiyo inayomfanya awe fisadi. Kwa level yake kama rais wa nchi hakuwa na wasiwasi na maisha yake ya baada ya kustaafu kwa vile pensheni yake ni kubwa sana. Mzee Jumbe aliachiswa kazi (siyo kustaafu kwa mujibu wa katiba) takriban miaka ishirini na tano iliyopita lakini hadi leo anakula pensheni yake salama kama makamu wa rais mstaafu. Mkapa alitaka aishi kwa gharama ya kiasi gani hadi aogope hiyo financial insecurity ambayo ingemfika baada ya kustaafu?



(b) Na ili kusaidia kuondoa lawama kwa Mkapa, unadai kuwa anachafuliwa jina na utawala wa Kikwete. Nadhani hapa ndipo unapoonyesha jinsi gani ulivyo na mtazamo mfupi sana kuhusu watanzania. Kikwete mwenyewe amebanwa vya kutosha kutokana na madudu yaliyotokea kwenye utawala wake kama haya ya Richmond na EPA, lakini vile vile amekuwa anaulizwa yale yaliyoachwa na Mkapa kama manunuzi ya ndege ya rais, mikataba ya madini, Mgodi wa Kiwira, ITPL, na ANBEN LTD kuwa na makazi Ikulu huku nyumba hiyo ni mali ya umma na mengine mengi ikiwa ni pamoja na uuzwaji holela wa mashirika ya umma na nyumba za serikali (nadhani unajua lilitokea Kenya hivi majuzi tu kuhusiana na uuzwaji wa ile Hotel, lakini Mkapa alikuwa akilazimisha mashirika ya umma na nyumba za serikali wauziwe ndugu zake, k.m. mkataba wa uendeshaji wa TANESCO). Kwa bahati mbaya Kikwete amekuwa anamtetea sana Mkapa huyo lakini siku zao zitafika.

Kwa jumla madai haya yanathibitisha jambo moja ambalo tumeliongelea muda wote hapa kuwa utawala wa CCM wote ni mbovu. Uliharibiwa zaidi na Mkapa ambaye ndiye alijenga msingi mkubwa sana wa ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka.
 
bongotz....you have a point..

kuna kambo ambalo tokea tuhuma dhidi ya mkapa zianze kushika kasi hasa miezi sita ya mwanzo baada ya kikwete kuingia madarakani..tena bila ya kukemewa na rais..zilionesha wazi kuwa there was a big force behind those allegations....it was like ..now i am the president i want to show how it is done.......baada ya muda wa miezi sita kupita na kazi ikionekana wazi kuwa ngumu .....kuliko alivyotarajia..ndio alirusha taulo kwa mara ya kwanza kutetea mkapa aichafuliwe...pale MAJIMAJI STADIUM -SONGEA...hasa baada ya washauri kumwambia kuwa taifa lilikuwa linayumba na kama tuhuma zikiendelea zitahamia na kwake kwa kuwa nchi haiendi vema....baada ya hapo juhudi za kumchafua mkapa zimeendelea kwa lengo la ku divert attention ...hasa ya utendaji mdogo wa serikali ya awamu ya nne....siku hizi watu hawajadili kwa kina matatizo ya leo...tunapoteza muda mwingi "kufukua makaburi"....nashauri tujenge nchi kwa hoja za leo leo...haya masuala ya kina mkapa na wengine akiwemo pia kikwete na mtandao wake wa mafisadi ni bora yapelekwe mahakamani ......sheria ifuate mkondo ....

kuhusu usafi wa mkapa ........HAKUNA BINADAMU ALIYEKAMILIKA ....LAKINI SIONI AIBU [NA KILA MARA HILI HUSEMA]....KUSEMA KUWA KWENYE MIZANI UTENDAJI MZURI WA MKAPA UNASHINDA ..MAKOSA YAKE ALIYOYAFANYA........kuna wimbo unasema ".....bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu ..nanii angesimama ..nani angesimama ..nani angesimama mbele yakooooo.."

ila pia mkapa anao wajibu wa kuweka historia yake sawa..........
 
PM.. katika kashfa zote tunazozingumzia sasa hivi na ambazo zimeenda kuitikisa nchi ni zipi zimeanzia chini ya utawala wa Rais Kikwete miaka hii miwili na miezi saba hii? Labda hapo tunaweza kujua kama kweli kumshika shati Mkapa ni haki au tunamuonea?
 
Babu ataka kusema: I fundamentally disagree with you. You can't just disrespect your former president like that man! kama ni fisadi, mbona hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yake. Acheni ushabiki usiokuwa na maana vijana. Mkapa sio fisadi. Period.


Bongo Tz,

Mbona unajichanganya ? Si wewe ndio ulisema ya kuwa Mkapa alifanya Biashara alipokuwa ikulu na sasa unasema ya kuwa Mkapa sio fisadi ? Why are you contradicting yourself ?
 
jamani in the first place aliyefungua hii thread (bongo tz) nia yake ni nini hasa? and why now? tuseme anapima kina cha maji,au kuna mtu ndani ya serikali ya JK kamuudhi,au kashikishwa kitu kidogo na nonino au.........,muhimu kujua kabla ya kuendelea na huu mjadala tusije tukawa tunasaidia ku push ajenda ya watu wengine bila sisi kujua.
 
I suppose humu vijana wengi wamedata kwelikweli. Nevertheless, "If you judge, investigate." Acheni tabia ya kurukia mambo msiyoyajua.
mkuu sasa unachanganya kabisa, nani anarukia mambo kama si wewe... kumuita mkapa msafi wakatim kulamtu anajua si msafi na kumtetea kwa viinformation vyako hujigundui kuwa wewe ndo unarukia mambo...

kwa tuita sisi follish huoni kuwa unadandia gari la mkaa wakati umevaa suti nyupe.....

acha kujidhalilisha bana
 
Endeleeni kulinganisha tawala tatu za wezi: kipindi cha Mwinyi, kipindi cha Mkapa na kipindi cha Kikwete. Halafu mtapata jibu tu kwamba CCM ni Chama Cha Mafisadi, CCM ya Mapinduzi aliondoka nayo Nyerere! Halafu mtajua haja ya kubadili mfumo mzima. Mwizi gani kaiba zaidi jamani? Mwizi, ni mwizi tu. Hakuna mwizi wa kupewa nishani na mwizi wa kukamatwa. Wote stahili yao ni mahakamani tu!

Huyo Mwinyi na Chavda wake kwenye Kamati ya Ayombo Ayilla naye alikuwa na EPA zake

Huyo Mkapa ndio gwiji la EPA

Na kikwete naye ameingia na Richmond, ATCL na EPA yake ya ziada ya juzi juzi tu hapa.

Sasa chagueni, tunasuka au tunanyoa?

Hiyo ndio Chukua Chako Mapema(CCM).

Asanteni sana

Asha
 
Hivi wewe BongoTz unatoka Mirembe? Naomba ujinga wako huo na Nkapa wako uupeleke Masasi.Mtu wako yuko uchi wee wasema amevaa,je watu wengi wanaozungumzia umaaluni wake alioufanya nduguyo ni wajinga kiasi chako? mshauri afunue domo lake kadamnasi na apitie hoja baada ya hoja na si vinginevyo. unanifanya nitamani vita ianze leo ili watanzania tujikomboe na kurudisha mali zilizoporwa kutoka kwa manyang'auTZ
 
- na ni chini ya utawala wa Mkapa ndipo wizi mkubwa kabisa katika Benki Kuu umetokea!
- Ni chini ya Mkapa Usalama wa Taifa was compromised kwa kubadilisha sheria ya usalama na kuunda picha ya kitu kinachoitwa Usalama wa Taifa na hivyo kuruhusu wezi kuingia hadi jikoni kuiba huku picha hiyo ikiwa imesimama mlangoni!
- Ni chini ya Mkapa Sheria mbovu ya Madini ya 1998 imeandikwa ambayo ilifungua mlango kwa upotevu wa mabilioni ya shilingi katika sekta hii muhimu kwa uchumi.
- Ni chini ya Mkapa sheria mbili za fedha zenye mambo ya ajabu ziliandikwa 2001, 2004 ambazo pamoja na sheria nyingine ziligeuza tanzania kuwa kisima cha uchotaji wa fedha na kuzirusha nje.
- Ni chini ya Mkapa makampuni feki yaliyoundwa na kuchota fedha za umma ikiwemo Meremeta yalipoundwa na yeye mwenyewe akiwa ni mmoja wa watu waliojua nini kinaendelea!
- Ni chini ya Mkapa kwa mara ya kwanza Rais wetu alitumia nafasi yake kuingia kwenye ubia na taasisi iliyo chini na hivyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi - na hili si dogo, ni kubwa mno! Nchi nyingine rais anaondolewa na Bunge!
- Ni yeye aliyemteua Mwanasheria Mkuu mbovu kabisa katika historia ya Tanzania huru


Hitimisho:

Mkapa alifanya aliyoyafanya na katika aliyoyafanya aliyoyafanya kwa kuyafanya vibaya kabisa ni yale aliyoyafanya ambayo hataki kuyazungumzia kuwa aliyafanya!

Mkuu umesahau haya
- aliuza Nyumba za serikali kwa bei ya mbuzi
- alihalalisha rushwa kwa kutunga sheria ya takrima
- akauza mashirika yote.
Tusipomchiluba huyu tutakuwa hatujamtendea haki.
 
You know I posted this thread to test and see how smart or foolish Tanzanians really are, and most of you (indeed) have proved to be the latter.

Foolish people.

Acheni kukaririshwa mambo na inner circle wa Kikwete hapa!

Be smart people.

wanaJF mimi mgeni kidogo jamvini hivi tukiitana foolish humu siyo tusi? maana naona BongoTz ameamua makusudi kuchafua hali ya hewa hapa. Wakati muda mwingi tunatumia kujadili ufisadi ambao umekuwa orchestrated wakati wa BWM jamaa anakuja na masifa ya kumwaga kuhusu kiumbe yule yule kinara wa UFISADI. si vyema kuanzisha topic hapa ambazo zinatukumbusha machungu tuliyonayo dhidi BWM(Mr.Clean?).

Maslahi ya nchi hii yanatakiwa yaanze kwanza kabla ya maslahi yako binafsi! Hii si sifa aliyokuwa nayo BMW sasa atakuwaje mzuri leo?
 
Warioba; Tusiruhusu Kashfa zitugawe

Na Yahya Charahani

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameonya dhidi ya utamaduni wa kuchafuliana majina ulioibuka miongoni mwa jamii kwa kuwa utakapokomaa utasababisha wananchi kusahau mambo ya msingi na kusababisha vurugu. ....

Tag it:?

Ndugu yangu, hata Warioba analo lake - Mwananchi Gold! Amekuwa mpole sana kwenye vita ya ufisadi!

Huyo BongoTz is a fool in the real meaning of the word
 
PM.. katika kashfa zote tunazozingumzia sasa hivi na ambazo zimeenda kuitikisa nchi ni zipi zimeanzia chini ya utawala wa Rais Kikwete miaka hii miwili na miezi saba hii? Labda hapo tunaweza kujua kama kweli kumshika shati Mkapa ni haki au tunamuonea?

.......mkapa na kikwete [aliyeingizwa madarakani na pesa za kifisadi na mbinu chafu],wote mafisadi...angalau tunasema mkapa kajenga uchumi,tumefutiwa madeni na kadhalika....hatujui kikwete anatupeleka wapi...!

.....mimi naona kama vile saa zinakwenda ....kazi haziendi...tuache gumzo ....tumsaidie rais kikwete kwa kuwa kama PRESSURE GROUP...ili angalau asahihishe makosa na kuchagiza maendeleo sawa...na maisha bora!!!
 
Lakini pia katika viongozi tuliowahi kuwapata, ukimuacha Mwalimu, ni Mkapa peke yake aliyekuwa na ubavu wa kupinga kuendeshwa na nchi za Magharibi. Mwinyi alikuwa anajikojolea wahisani wakikohoa, Kikwete (sote tumeshuhudia) anacheza samba kila mara nchi za magharibi zikimuamuru afanye hivyo.

haya matusi yanakuonyesha ulivyo na akili pungufu na kama alivyosema Mwinyi majuzi, umesoma lakini hujaelimika kama mumeo Mkapa, maana kwa unavyoongea kama wewe si Anna Mkapa, basi ni nyumba ndogo yake
 
Last edited:
Hii mada tumeivamia kijazba kwa hiyo hatuwezi kuwa objective sana. Pengine ni kwa sababu mleta hoja naye kaleta hoja yake kijazba. Hata hivyo kuna hoja za msingi za kujadiliwa.

Kwanza nikanushe madai ya Bongo TZ na Philemon Mikael kwamba utawala wa Kikwete ndiyo ulioibua na unaendelea kuchochea moto kashfa za Mkapa. Hii ni hapana kwa sababu tunajua kwamba kwa mara ya kwanza kashfa za Mkapa ziliibuliwa kwa uwazi kabisa tarehe 15 Septemba 2007 na Dr Slaa pale Mwembe Yanga baada ya jina lake kuwa juu kabisa katika list ya aibu ya mafisadi. Na ni mtu mwehu pekee atakayekubaliana kwamba Dr Slaa walitumwa na akina JK kumwaga ile list.

Baada ya kusema hayo, nakubaliana na akina Bongo TZ kwa jambo moja, nalo ni kwamba utendaji wa Mkapa kama Rais ulikuwa bora kwa mbali sana kuliko JK. In fact ni aibu kulinganisha utendaji wa akina JK na Mkapa kwa sababu ni vitu viwili tofauti. It is simply unaffair and illogical to try to compare between a presidential president and a pretentious president.

Niseme pia kwamba ni ukweli kwamba Mkapa alifanya mambo makubwa ikiwemo kuirudisha nchi ianze kuonekana nchi na kuifanya serikali ionekane serikali. Ni ukweli pia kwamba Mkapa alitumia vibaya madaraka yake na hasa zoezi la ubinafsishaji kwa manufaa yake na jamaa zake badala ya nchi. Halafu kuna jambo moja ambalo apologists na critics wa Mkapa huwa hawalisemi, nalo ni kwamba Mkapa ni Rais aliyetumia madaraka yake na nguvu nyingi za dola kudhaifisha upinzani. Huyu ni mtu aliyedhamiria kuua kabisa upinzani kwa gharama yeyote ile.

Sasa swala la kujadili hapa ni: Je, mabaya ya Mkapa yanazidi na kufuta mazuri yake?

Lakini kusema kwamba Mkapa ni "clean, period" ni ulimbukeni wa hali ya juu. Vilevile, kusema kwamba Mkapa hakufanya chochote cha maana katika nchi yetu zaidi ya kuiba ni ulimbukeni na ujuha wa kutisha!
 
Warioba; Tusiruhusu Kashfa zitugawe

Na Yahya Charahani

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameonya dhidi ya utamaduni wa kuchafuliana majina ulioibuka miongoni mwa jamii kwa kuwa utakapokomaa utasababisha wananchi kusahau mambo ya msingi na kusababisha vurugu.

Akizungumza jana ofisini kwake Oysterbay, Dar es Salaam Jaji Warioba alisema, amestushwa na utamaduni huo ambao unaonekana kukomaa kiasi cha kumgusa mtu muhimu kama rais.

"Nimeulizwa maswali mengi baada ya kutoka 'orodha ya mafisadi', nimeipata, lakini ninachoweza kusema hakuna jipya katika orodha ile, zaidi ya kupakana matope, kwani orodha ile inafanana kabisa kimtiririko tuhuma zake na orodha mbili zilizopita,"alisema.

Alisema ameona yaliyoandikwa katika ile orodha inayoitwa 'list of shame' mengine yamemstua sana, nchi ikifikia kumtaja rais ni fisadi imefika mbali, na kwamba mtu hawezi kutoa tuhuma kama hizo mpaka awe na ushahidi mzito usioacha shaka.

Alisema rais ni alama ya taifa na kwa maana hiyo mtu anapomtaja rais kuwa fisadi na kisha akaendelea kujigamba kuzungumzia juu ya hilo hatimaye ina maana hakutakuwa na uongozi wa taifa, itakuwa ni hatari.

Alitoa mfano kama tuhuma za namna hiyo zinaendelea ina maana kuwa wananchi wanaweza kukosa imani na serikali yao suala ambalo ni hatari na halitakiwi kufumbiwa macho.

"Unapomtaja rais kama fisadi unakuwa na unataka kufanya wananchi wakose imani na serikali yao suala ambalo ni hatari, wananchi watakimbilia wapi kama wanayetaka kumkimbilia naye anachafuliwa," alisema.

Hivi karibuni Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Willibrod Slaa, aliwataja vigogo 11 wengi wao wakiwa katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Nne kwamba ni mafisadi waliohusika na ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.

Miongoni mwa waliotajwa na Dk Slaa akishirikiana na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu, ni makatibu wakuu wawili, mwanasheria pamoja na viongozi wengine waliokuwa katika serikali ya awamu ya tatu.

Dk Slaa aliwataja vigogo hao wiki iliyopita katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa vyama vya upinzani katika mikoa 11 ya Tanzania, ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwezi uliopita katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia tuhuma, Jaji Warioba alishangazwa hata Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kutajwa katika baadhi ya ripoti wakati rekodi yake inaonyesha kuwa kafanya mengi mazuri, lakini taarifa zinazotolewa zimelenga tu kumchafua.

Kwa muelekeo ulivyo sasa alisema, inaonekana kwamba kuna njama na jitihada za makusudi za kuchafua majina na kisha kusumbua utawala uliopo kukimbizana na hoja za ufisadi wakati mambo ya msingi yakiachwa bila kutekelezwa.

Alishangaa kwamba kila kukicha viongozi wanatishia kwenda mahakamani suala ambalo linaonyesha kuwa viongozi wanatumia muda huu kujibu tuhuma badala ya kushughulikia masuala ya maendeleo ya taifa.

"Sikatai Mkapa ni binadamu anaweza kuwa na mambo yake, lakini siyo kiasi cha kufuta rekodi yake. Hivi kweli mtu unaweza kweli kufuta rekodi ya Mkapa kwa utendaji wake uliowezesha kushusha inflation ya asilimia 30 alipoingia madarakani hadi tano wakati anaondoka, kisha ukatoa tuhuma za jumla jumla tu, hivi nadhani si sawa," alisema.

Aliorodhesha miongoni mwa mambo yaliyofanywa na Rais Mkapa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, elimu, uchumi miundombinu na vitu vingine.

Kwa mtazamo wake alisema kuwa, baada ya uchaguzi mambo ya msingi ambayo sasa yangekuwa yakishughulikiwa ni pamoja na uboreshaji wa kilimo, kukabiliana na tatizo la bei za umeme kuwa juu, mfumuko wa bei na vinginevyo, lakini badala ya kushughulika na hayo, suala lililowekwa mbele ni kuchunguza dosari za viongozi.

Hata hivyo aliitaka jamii kutoacha kupambana na viongozi wala rushwa iwapo kunakuwapo ushahidi wa msingi na uthibitisho usioacha shaka, lakini jamii hiyo hiyo isitumie mwanya huo kujineemesha kisiasa.

"Sisemi kwamba viongozi wala rushwa wasiandamwe la hasha, waandameni iwapo mna ushahidi wa kutosha na msiishie kuwataja tu songeni mbele zaidi kuhakikisha haki inatendeka," alisema.

Pia alisema ni muhimu vyombo vya habari na jamii vikasisitiza katika kuwapo utawala bora, lakini si kwa kiwango cha kusahau vipaumbele vingine katika jamii.

Alisema inavyoonekana kama kuna jitihada za makusudi za kuchengesha mambo ya msingi kwa jamii yasishughulikiwe, ili suala liwe ni moja tu kukimbizana na tuhuma ambazo zinatolewa na kisha kutofuatiliwa.

Hali hii anasema Warioba kuwa huenda ikasababisha muda si mrefu masuala yaliyolisumbua taifa kipindi kilichopita yakarudia tena kusumbua, sababu mwelekeo unaonekana ni kukimbizana na kujibu tuhuma.

"Wiki chache zilizopita nilikuwa Mara kwa shughuli za uchaguzi, nikasikia kwenye vyombo vya habari Mungai analalamika watu wanampaka matope eti mara wanamwita si raia, inashangaza sana, hivi kweli mtu kama Mungai anaweza kuhojiwa vitu vya ajabu kama hivi, tunakokwenda siko," alisema.

Aliwachekesha waandishi wa habari pale alipojibu swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi wa habari aliyetaka kujua kama alitumwa kutoa taarifa hiyo akajibu : "Sikutumwa na mtu, simo katika siasa, wala serikali mimi ni mtu huru hakuna mtu aliyenituma, nasema ninachokiamini."

Source: Mwananchi

Tag it:?

Huyo ni WARIOBA WA GAZETI LA MWANANCHI...AMA NI WARIOBA HUYO HAPO CHINI?

KATIKA kauli ambazo zitawashitua watawala, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema nchi ina viongozi dhaifu, umma unanyonywa, rushwa imeongezeka, wezi wa fedha za EPA waanikwe na Rais Msitaafu, Benjamin Mkapa akajibu tuhuma zake mahakamani.
Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, Warioba amesema kuna dalili ya kuwapo watu wakubwa nyuma ya kashfa ya fedha zilizopotea katika sakata la EPA na kwamba yaliyotokea ni wizi wa hali ya juu na baadhi wameghushi na kwamba hatua za kisheria ni lazima zichukue mkondo wake.


26.jpg

JAJI Warioba

“Niliyosoma hasa kutokana na taarifa ile ya Serikali, ukiisoma kwa makini unaona kuwa haukuwa ununuzi wa madeni, huo ulikuwa ni wizi wa fedha za umma,” anasema Jaji Warioba.
Anasema kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, baadhi ya madeni si madeni bali kuna watu wametumia ulaghai kuchukua madeni ambayo yamekwisha kulipwa na wao kufanya udanganyifu kuyadai.
“Wapo ambao wamefanya hivyo kwa kughushi. Sasa kuna makosa mawili hapo. Wizi na kughushi, ni makosa mazito, na kama nilivyosema wakati ule ilipotoka mara ya kwanza, ukiona makampuni ambayo yametajwa si makampuni makubwa na mengi yake yaliundwa kwa kazi hii tu,” alisema katika mahojiano ambayo sehemu yake ya kwanza imechapishwa katika kurasa za 12 na 13 za toleo hili.
Akionyesha kuwapo kwa watu wakubwa nyuma ya wizi wa fedha za EPA, Warioba anasema biashara ya kununua madeni inataka mtu mwenye fedha na mwenye ujuzi wa biashara hiyo lakini makampuni yaliyoorodheshwa na serikali mengi yanamilikiwa na watu wa kawaida kabisa wasio na uwezo huo.
“Kampuni hizi ni ndogo, watu wenye kampuni hizi wameandikwa watu wenye majina ya kawaida. Kwa mtu yeyote mwenye busara atajua hii ni hadaa tu. Wanaoshughulika hawakujiandika kwenye kampuni hizi, wamechukua watu wengine tu. Kwa hiyo, kuna kazi, kuna kazi ya kuwatafuta hawa wazito waliokuwa wanahusika. Na kama ni wazito na wameingia katika wizi wa mali ya Taifa na kughushi, suala hili ni zito kuliko tunavyoliona,” anasema na kuongeza;
“Mimi naamini kama kweli tunaishughulikia kwa nguvu zote, EPA ni kubwa kuliko Richmond, kuliko haya yaliyotokea. Kwa hiyo tutangojea matokeo. Na hapa kwa kuwa walau ushahidi wa kawaida upo, taarifa zinasema zile nyaraka zilizowezesha madeni hayo kununuliwa ni za kughushi, basi unaanzia hapo. Ukihakikisha kwamba ni za kughushi, kwamba haya madeni hayakuwapo, ukithibitisha kwamba hili deni halikuwapo sasa huyo aliyechukua fedha hizo alitumia wapi?”
Alisema akiwa kama raia mwema wa Tanzania anasubiri kwa makini kuona matokeo ya EPA, na kuongeza kwamba kama kweli nia ya kusafisha ipo, ni lazima waliofanya makosa wapatikane na kushughulikiwa na si wale waliotangulizwa.
“Mimi sijui utaratibu wanaotumia. Lakini kwa utaratibu wa kawaida, mimi nilikuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi, kwa suala hili la jinai unalishughulikia linakwenda mahakamani. Adhabu inatolewa pamoja na kurudisha hizo fedha, hilo ndilo nalitarajia,” anasema.
Anasema kwa kawaida hatua za kisheria ni lazima zichukuliwe na kwamba unapokwenda mahakamani unaweza kutumia sheria kurudisha fedha zilizoibwa hata ikibidi kufilisi wahusika.
Hivi karibuni timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia waliochukua fedha za EPA ilieleza wazi kwamba imekua ikipokea fedha kutoka kwa watuhumiwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kuepuka kupoteza fedha hizo huku wanaozirejesha wakiendelea kuwa siri.
Timu hiyo ya Rais inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema, na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea, wote wakisaidiwa na maofisa kutoka ofisi zao na kutoka asasi nyingine za umma.
Akizungumzia kitendo cha viongozi hao wa juu wa dola kufanya mazungumzo na watuhumiwa, Jaji Warioba anasema; “Kwamba hawa ndio kweli viongozi wa ngazi ya juu wa vyombo vya dola vinavyoshughulika na uhalifu wanafanya kazi hiyo. Imani yangu ni kwamba hawatapinda sheria. Wakipinda sheria tutakuwa tumeleta madhara makubwa sana kwa nchi hii. Kwa sababu wananchi lazima kwa upande wa sheria waamini ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ni lazima waamini ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, lazima waamini ofisi ya TAKUKURU.”
Warioba anasema watendaji hao wa dola wakipinda sheria, imani ya wananchi itapungua na hivyo ni jukumu lao ni kubwa, na kwamba yeye ana imani kwamba hawatapinda sheria.
Akizungumzia hali ya kisiasa ya nchi kutokana na kukwama kwa mambo mengi ikiwamo muafaka wa kisiasa Zanzibar na kuibuka kwa wimbi kubwa la tuhuma za ufisadi, Jaji Warioba anaonekana kutokua na imani na hali hiyo na anakiri kuwapo kwa udhaifu katika uongozi wa juu wa kitaifa.
“Kama nilivyosema, kila mtu ni kuzungumzia ufisadi, hata mafisadi wenyewe, maana ukiona wote hawa wanaozungumzia, huwezi kusema ni watu safi, pamoja na vyombo vya habari, navyo haviwezi kujisifu. Wengine wanaoandika juu ya ufisadi ndio hao hao waliokuwa wakichukua fedha za hawa, wanawaandika kuwa ni wazuri wakati wa uchaguzi. Walikuwa wakiwapamba. Kwa hiyo kuna wengine ni unafiki tu, ama ni ufisadi na wenyewe,” anasema.
Warioba anapongeza juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari na wabunge katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini anaonya vita hiyo isitumike kufunika madhambi yaw engine ama kuwaumiza baadhi yao.
“Sina hakika kama wote wamezinduka hivi. Jana walikuwa wanasema hakuna rushwa, hakuna ufisadi. Leo ndiyo wako msitari wa mbele wanatafuta mafisadi na ukiangalia zaidi ni viongozi. Na hasa wabunge ndio wanaongoza vita hii. Ni vizuri Bunge liongoze lakini je, tunawaamini wote? Kwamba nia yao hasa ni kumaliza ufisadi au kuna sababu nyingine?
“Ikifika mahali tuwaulize hawa ambao sasa wanaonekana wana uchungu sana na ufisadi. Mwaka 2005 tuliona yaliyotokea. Hivi ni wangapi ambao wako safi? Mwananchi akimwuliza mbunge wake, na hii inawezekana kwa zaidi ya nusu ya wabunge, kwamba mbona wewe ulikuja na fedha nyingi sana kwenye uchaguzi na wewe si tajiri, ulizipata wapi?” anahoji Jaji Warioba.
Anasema wamo wengi ambao ni sehemu ya uongozi, na hivyo isije tokea mapambano ndani ya uongozi yakageuzwa kuwa ni vita ya kweli kumaliza ufisadi.
“Mimi nataka niwe na uhakika tukifika mwaka 2010 tuweze kuchagua viongozi safi, tusipate viongozi ambao katika mchakato wa uchaguzi watakwenda na takrima kwa sababu kama wanakwenda na takrima wamezipata fedha hizo kwa ufisadi,” anasema.
Akizungumzia muafaka kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Jaji Wariona anasema tatizo kubwa ni mgawanyiko katika uongozi. Anasema wapo ambao hawataki muafaka wanaona njia ni kusema tupate maoni ya wananchi wakitarajia kwamba wananchi watakataa.

Kuhusu wanaotishia kurejea kwenye Afro Shirazi Party (ASP) kuliko kuingia katika Muafaka na CUF, Warioba anasema hivyo ni vitisho visivyo na maana katika mazingira ya sasa kwani hata wakiachwa hawana uwezo huo na kwamba tatizo kubwa ni udhaifu wa viongozi.
“Zaidi wanaosema warudi ASP ni watu wa Zanzibar, lakini nadhani pia kuna udhaifu katika viongozi Bara. Wakiisha kusikia madai hayo ya ASP, wanasema jamani waachieni mambo yao! Lakini haya si mambo yao, ni mambo ya nchi. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, likitokea tatizo Zanzibar ni tatizo la Tanzania. Hawa wanaosema waachieni haya ni mambo yao ni viongozi dhaifu,” anasema na kuongeza;
“Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa. Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaumu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana. Manufaa ya Taifa sasa hivi ni kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Lolote linalohitajika kumaliza mpasuko huo ni vizuri viongozi wakachukua uamuzi, utakuwa ni mgumu lakini ni wajibu wao kuchukua uamuzi.”
Pamoja na kuonekana kukwepa kumshutumu Rais Mstaafu Mkapa, Jaji Warioba anasema kinga waliyonayo viongozi akiwamo rais ni ya kisiasa tu, na hivyo kwake yeye suala la kinga ya kisheria si tatizo bali ukweli na uhakika wa tuhuma zinazomgusa kiongozi husika na kwamba ni mahakama inayoweza kutoa uamuzi wa haki.
“Nimeona wanaandika na nimeona mjadala mkubwa tu unaolenga kwenye immunity. Mimi nafikiri suala hilo si la msingi kwa sasa hivi. Na mjadala unalenga kwamba aseme, naona si la msingi. Kwa sababu hatutaki kwamba huyu awe tried na vyombo vya habari. Maana hapa naona kama ni trial kwenye vyombo vya habari.
“Waseme ni kosa gani, amefanya kwa msingi wa sheria gani, sasa waendelee. Sasa mengi wanayosema ni ya kisiasa. Yakisemwa ya kisiasa unataka mtu awajibike kisiasa. Kama ni kosa la jinai, waseme amevunja wapi sheria, lakini kusema kweli mimi sioni kwa vyombo vya habari kusema yote haya na wanachotaka ni kwamba ajitetee, ajitetee wao ndio wamekuwa Mahakama?” anahoji Jaji Warioba ambaye amewahi kufanya kazi kwa karibu na Mkapa.
Warioba anasema vyombo vya habari vinataka kuwa Mahakama na akashauri kwamba kama kuna kosa alilofanya Mkapa ni vyema wakasubiri afikishwe mahakamani ambako atakuwa na nafasi ya kujitetea na kueleza upande wake.
“Immunity nasema sasa hivi siyo issue. Sema kosa lililotendeka. Anashitakiwa lakini wanasema hatuwezi kuendelea kwa sababu kuna immunity. Bila kusema kosa huwezi kufika kwenye immunity. Huwezi kuanza na immunity bila kuwa na kosa, kwa hiyo mimi sitaki kujiingiza katika mjadala wa immunity. Hii ni ya kisiasa tu,” anasema.
 
Back
Top Bottom