Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Yaaani kujiuzulu wadhifa au kuvuliwa Presidential Immunity, then mahakamani! Ooh boy it is coming tena very soon!


I see hii ikitokea nitajua CCM imezaliwa upya na nitaandika a special pursuasive article ya kumjengea imani JK. By now naendelea kuamini kwamba JK is the most incompetent leader our country has ever had.

Bila hawa watu kufikishwa mahakamani ili ukweli ujulikane, haya mengine yataendelea kuwa ni ngonjera. Na kusema kweli serikali inatukosea na inawakosea sana hawa watu wanaotuhumiwa kwa kutowafikisha mahakamani au angalau kuunda tume ya kuwachunguza kwa tuhuma ambazo zimezagaa mitaani.

Nchi yetu inaanza kuelekea kwenye utawala wa rule of the jungle; watu wanahukumiwa kwenye vijiwe na kwenye internet cafe kama vile hatuna vyombo vya sheria. I hate kuona Rais aliyeongoza nchi for ten years na, pamoja na matatizo yake, akafanya mambo mengi tu kwa nchi yake kuzomewa mtaani kwa kuitwa jambazi. Lakini wananchi wafanyeje kama serikali yao imekaa tu wakati tuhuma zimetolewa?
 
Mkapa Hata Akilonga tusitegemee lolote jipya labda ni machache sana atasema ambayo yanaweza kushitua umma na sidhani kama hiyo itawezekana na kama itawezekana basi na yeye ataenda kutibiwa nje ya nchi kama wenzake wote walivyowahi kwenda kutibiwa na kurudishwa Na Majeneza Yao Nchini au kuchomwa huko huko kama Balali .

1 ) Je na yeye anapenda kufuata mkondo wa mwenzake ? Jibu analo mwenyewe

2 ) Kama akiamua kufuata mkondo huo , nchi itakuwa katika hali gani ? Yeye mwenyewe na wenzake ndio wanajua .

Lililo wazi ni kwamba Lowassa na mwenzake chenge wameshaenda UK kutoa ushahidi wao katika SFO nchini kule , inawezekana Mkapa anataka kujichomoa katika suala hili kwa kujisafisha hapa tanzania kabla hiyo ripoti ya SFO haijatoka rasmi kwa sababi inaweza kutoka wakati wowote kuanzia mwezi ujao .

Pia kuna suala la mradi wake wa Kiwira , kama mnavyojua watu hawalipwi kule kiwandani watu wanataga kugoma na habari zinazosambaa inasemekana wameshaanza kubadilisha majina na vitu vingine kuhusu umiliki wa mradi huo wa kiwira , inawezekana mpaka ijumaa MKapa na mwenzake daniel atakuwa wameshajitoa na hisa zao katika Kiwira .

Kuna mradi wa madini katika Williamson , Mradi huu maokola majogo , mkapa na wengine wengi wanahusika , kuna mzungu mmoja anafanya kazi Regent Tanzania Limited anajua mengi Jinsi maokola Majogo alivyohongwa mpaka kutoa mradi huo kwa bei chee sijui kama mkapa atakuwa na lolote jipya hapa

Ni hayo tu kwa leo
 
Mkapa Hata Akilonga tusitegemee lolote jipya labda ni machache sana atasema ambayo yanaweza kushitua umma na sidhani kama hiyo itawezekana na kama itawezekana basi na yeye ataenda kutibiwa nje ya nchi kama wenzake wote walivyowahi kwenda kutibiwa na kurudishwa Na Majeneza Yao Nchini au kuchomwa huko huko kama Balali .

1 ) Je na yeye anapenda kufuata mkondo wa mwenzake ? Jibu analo mwenyewe

2 ) Kama akiamua kufuata mkondo huo , nchi itakuwa katika hali gani ? Yeye mwenyewe na wenzake ndio wanajua .

Lililo wazi ni kwamba Lowassa na mwenzake chenge wameshaenda UK kutoa ushahidi wao katika SFO nchini kule , inawezekana Mkapa anataka kujichomoa katika suala hili kwa kujisafisha hapa tanzania kabla hiyo ripoti ya SFO haijatoka rasmi kwa sababi inaweza kutoka wakati wowote kuanzia mwezi ujao .

Pia kuna suala la mradi wake wa Kiwira , kama mnavyojua watu hawalipwi kule kiwandani watu wanataga kugoma na habari zinazosambaa inasemekana wameshaanza kubadilisha majina na vitu vingine kuhusu umiliki wa mradi huo wa kiwira , inawezekana mpaka ijumaa MKapa na mwenzake daniel atakuwa wameshajitoa na hisa zao katika Kiwira .

Kuna mradi wa madini katika Williamson , Mradi huu maokola majogo , mkapa na wengine wengi wanahusika , kuna mzungu mmoja anafanya kazi Regent Tanzania Limited anajua mengi Jinsi maokola Majogo alivyohongwa mpaka kutoa mradi huo kwa bei chee sijui kama mkapa atakuwa na lolote jipya hapa

Ni hayo tu kwa leo
 
Mimi nachoomba wakuu ni kwa familia ya Balali kutoa report yote kwa wanamapinduzi wetu.. Dr. Slaa au Zitto na nakala iende kwa rais mwenyewe..
Hiyo report isomwe bungeni wazi kwa wawakilishi wetu wote ambao watakuwa na nguvu ya kufungua mashtaka dhidi ya Mkapa....Inawezekana kabisa...

Mkandara,

Familia ya Ballali itoe ripoti kwa manufaa ya nani?

Manufaa yetu sisi yanapingana na ya familia ya Ballali.

Familia ya Ballali haiwezi kushirikiana na chombo chochote cha dola katika namna itakayohatarisha usalama wa Mkapa. Hawa ni wamoja hawa. Kuna matundiko kwenye thread moja ya Ballali humu inaelezea uhusiano wa karibu baina ya familia ya Ballali na Mkapa. Kiufupi, Anna Muganda na Anna Mkapa ni marafiki wa damu. Na ndio mwanzo wa kupeana vyeo baina ya hizi familia.

Kwa hiyo kusema familia ya Ballali itoe ripoti ni ku assume kwamba na wao wana nia kama yetu, ya kuona Mkapa anapelekwa mbele ya haki. Hawana!
 
Is Mkapa really a mere government pensioner?

-Questions still abound over his failure to address the real issues at hand

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

VARIOUS political commentators have reacted strongly to former president Benjamin Mkapa’s attempt to depict himself as a mere pensioner surviving on government retirement benefits � at a public rally in his home village in Masasi District, Mtwara Region over the weekend.

It was the ex-president’s first and much-awaited formal public response to serious allegations of corruption and abuse of office that have shadowed him for approximately one full year now.

But according to the commentators, Mkapa failed to adequately explain to Tanzanians why he chose to conduct private business dealings while still at State House, or his dubious involvement in the private ownership of the formerly state-run Kiwira coal mine.

Mkapa is said to have left several questions unanswered as he blamed the allegations against him mainly on ’’disgruntled’’ individuals with a personal grudge against him - apparently because he refused to favour them during his 10-year presidency from 1995 to 2005.

The ex-president was quoted as telling the public rally in his Lupaso home village: ’’Don’t listen to their lies...there is no truth in the allegations, but only hatred, mostly from people who thought I would favour them (in my administration) - but didn’t.’’

He added: ’’I am not financially well-off...I live on my government pension, just like my predecessor, (Ali Hassan) Mwinyi.’’

He made no mention of his controversial ownership of the Kiwira coal mine, or his business dealings from Ikulu from 1999 - when he set up a private company called ANBEM Limited with then first lady Anna Mkapa - until his retirement at the end of 2005.

Contacted for comment by THISDAY yesterday, the Vunjo Member of Parliament on a ruling CCM party ticket, Alloyce Kimaro (CCM) - who raised the allegations of graft and abuse of office against Mkapa in the National Assembly for the first time only last month - criticized the former president for failing to directly address the accusations.

’’Mkapa should respond to these serious allegations before MPs and journalists, instead of merely making public statements from his home village. After all, he was the president of Tanzania � not just of his village,’’ said Kimaro.

The MP said he believed the ex-president still hasn’t addressed the real issue at hand, but simply made a propaganda speech in dismissing the allegations wholesale.

Asked if he had any personal vendetta against Mkapa and whether or not he had ever asked for any favours from the former president, Kimaro remarked: ’’First of all, I don’t think he (Mkapa) even knows me personally�and I certainly never asked for any favours from him.’’

Kimaro said what drove him to speak out in parliament against Mkapa’s dubious involvement in the privatization and ownership of the Kiwira coal mine, was his desire to defend the interests of Tanzanians.

He challenged the ex-president to respond properly and in a proper public forum to the burning questions regarding his private business dealings at Ikulu, and involvement in the ownership of the Kiwira coal mine based in Mbeya Region.

Likewise, Karatu Member of Parliament Dr Wilbrod Slaa, from the opposition CHADEMA party, was scathingly critical of the weekend remarks by the retired president, insisting that he still has some serious explaining to do to Tanzanians.

’’Mkapa should tell us if he really did call himself an entrepreneur, start and operate a private business company from inside the State House premises? Did he pay office rent to Ikulu for this private company?’’ Slaa queried.

The opposition legislator also challenged the ex-president to publicly declare his current assets so that Tanzanians can make a comparison of his wealth from the time he first entered State House in 1995 to when he completed his second and final term in 2005.

Investigations by THISDAY have already established that Mr and Mrs Mkapa registered ANBEM Limited in 1999 while still at State House, and operated the firm for personal financial gain from inside the official Ikulu walls.

Three years after starting the company, the State House couple applied for and received a hefty loan of $500,000 (approx. 630m/-) from the National Bank of Commerce (NBC) Limited, which came on the heels of a heated national debate over the April 2000 privatization of the previously state-owned bank.

The NBC privatization was fiercely opposed by, amongst others, the Father of the Nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, until his death in 1999. A good number of MPs from both sides of the political divide � ruling and opposition parties - were also strongly against the deal, arguing that the once-giant national institution was being sold off far too cheaply.

The privatization of the then NBC (1997) Ltd still went ahead as scheduled with the formation of NBC Ltd in April 2000 and acquisition by South Africa’s ABSA Group of 70 per cent of the bank’s shares - for a reported total price of just 15bn/-.

Records also show that Mkapa, as sitting president, was always a vocal supporter of the privatization process which resulted in the bank being taken over by ABSA Group, whose direct association with NBC actually began in August 1999 when the South African firm effectively started managing the bank at the request of the government of the day.

Further investigations by THISDAY have also established that in December 2002 - five months after securing the NBC Ltd loan � ANBEM Ltd landed another big credit-line in the form of a 250m/- loan granted by CRDB Bank Limited.

The revelations about the then president and first lady doing business from Ikulu followed reports by THISDAY that the Mkapa family owns an office building in Dar es Salaam, where a new bank with some big-name local businessmen on the shareholders list was to be located.

Situated right next to Mr and Mrs Mkapa’s official residence after retirement, the two-storey building is currently the official headquarters of Bank M (Tanzania) Limited.

Records show that ANBEM Ltd bought the building, registered under certificate of title number 6809 at Number 8 Ocean Road in the city’s upmarket Sea View area, from a company called Tanzania Building Works in 2002.

THISDAY has also learnt that the former president has recently moved into a luxurious beachfront house in the Masaki neighbourhood of Dar es Salaam, and also owns more expensive property elsewhere.
 
Mkapa achokoza nyuki

Na Muhibu Said
Mwananchi

WATU wa kada mbalimbali jijini Dar es Salaam jana waligeuka kama nyuki waliochokozwa baada ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kujaribu kujisafisha tuhuma zinazomkabili, huku wengi wakiwa hawaridhiki na utetezi wake na kumtaka ajibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili moja baada ya nyingine.

Watu hao, wakiwamo wanasiasa, wabunge na wanasheria, kwa nyakati tofauti, pia wamemtaka Mkapa kutokwenda kujisafisha kijijini, badala yake azungumze na waandishi wa habari ili apate kuulizwa maswali na kuzitolea ufafanuzi tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema Mkapa hapaswi kwenda kuwaeleza wanakijiji kuhusu ufisadi anaotuhumiwa kuufanya wakati wa utawala wake, kwani hawawezi kumhoji, badala yake wataishia kumpigia makofi kwa vile aliwapelekea msaada wa vifaa vya zahanati.

Alisema anachotakiwa kufanya ni kuzungumza na waandishi wa habari ili ajibu tuhuma hizo kwa vile zina vielelezo na Watanzania waweze kumwelewa.

"Hizi ni tuhuma nzito, alipaswa kuzijibu akizungumza na waandishi wa habari. Na badala ya kuzieleza kwamba ni uongo, tuhuma hizi zimetolewa na vielelezo. Na ni nyingi," alisisitiza Profesa Lipumba.

Alisema tuhuma ya kwanza nzito, ambayo Mkapa anapaswa kuijibu, ni ile inayohusu kuanzisha kampuni ANBEN mwaka 1999 ambapo anadaiwa kuwa alikopa dola nusu milioni kutoka benki wakati huo akiwa rais na akiwa Ikulu na akaweza kuzirejesha katika kipindi cha mwaka mmoja.

Lipumba alisema kitendo cha mtu kuanzisha kampuni akiwa kama rais, ni ukiukwaji wa maadili ya uongozi, kwani kwa kawaida viongozi hata wakiwa na makampuni, huwa wanamweka mtu mwingine anayeendesha kusudi pasiwe na migongano ya masilahi.

"Hilo hajalijibu. Kwamba, ilikuwaje akaanzisha kampuni mwaka 1999 na akakopa nusu milioni na akawa mfanyabiashara bora kweli kuweza kuzirudisha fedha hizo katika kipindi cha mwaka mmoja. Si rahisi kukopa dola nusu milioni ambazo ni zaidi ya Sh milioni 500 na kuweza kuzirejesha na kulipa riba kwenye benki. Hilo la kwanza," alisema Lipumba.

Lipumba alisema shutuma nyingine nzito ambazo Mkapa anatakiwa azijibu ni zile zinazohusiana na rada ambazo zimethibitishwa na Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza ambayo imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya Kampuni ya BAE System iliyoiuzia Tanzania rada hiyo mwaka 2002.

Alisema mwaka 1995, kulikuwa na jaribio la kuiuza rada hiyo na kwamba, ili serikali iinunue, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitakiwa iweke dhahabu iliyonayo kama dhamana ya kununulia ili kama serikali itashindwa kulipa, dhahabu hiyo iende kwa muuzaji.

Lipumba alisema jaribio hilo lilikakataliwa na mradi huo wa kununua rada ukafa, lakini ulikuja kufufuliwa baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kufariki dunia.

Alisema pamoja na mradi huo kufufuliwa, SFO imeeleza kwamba, wakala Shailesh Vithlani aliyesimamia ununuzi wa rada hiyo, amelipwa rushwa ya dola 12 milioni na Kampuni ya BAE, zikawekwa kwenye akaunti nchini Uswisi.

"Mimi binafsi nilikuwa nikipiga kelele kwamba, hii rada ina kila harufu ya rushwa. Serikali ikapinga, ikasema ni utaratibu mzuri kabisa, hauna matatizo. Leo hii tunafahamishwa kwamba, kulikuwa na rushwa ya dola milioni 12," alisema Lipumba.

Alisema wakati ununuzi wa rada hiyo unafanyika, ripoti ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Mambo ya Anga (ICAO) ilitoa taarifa kwamba, rada ambayo inakidhi mahitaji ya Tanzania inaweza kupatikana kwa dola 5 milioni, lakini serikali ya Tanzania ikaenda kununua rada ya dola 40 milioni, huku wakala aliyesimamia ununuzi huo, akiwekewa dola 12 milioni.

Alisema wakala huyo ndiye ambaye alikuwa wakala wa kununua ndege ya rais iliyogharimu zaidi ya dola 40 milioni ambayo pia yeye (Lipumba) aliipigia kelele kwamba haihitajiki, kwa vile ni gharama kubwa, lakini Mkapa wakati huo akasema kwamba, ni muhimu.

Alisema wakala huyo pia alishiriki katika ununuzi wa magari na helikopta za jeshi na kwamba, mambo yote hayo yalitokea katika kipindi cha Mkapa, licha ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Maendeleo, Claire Short wa Uingereza kupinga katika Bunge la nchi hiyo kwamba, rada hiyo isinunuliwe na serikali ya Tanzania kwa vile ina kila harufu ya rushwa, ingawa akazidiwa nguvu na Waziri Mkuu wake, Tony Blair.

"Kwa hiyo kuna suala la rada anapaswa atujulishe, imekuwaje wakati sisi tulikuwa tunamweleza kwamba, ununuzi wa rada, una kila harufu ya rushwa na sasa imethibitishwa kwamba, Shailesh Vithlani alilipwa dola 12 milioni. Je, yeye alipatiwa chochote katika hili? Swali hilo atujibu," alisema Lipumba.

Alisema tuhuma nyingine, inahusu suala la ununuzi wa mgodi wa Makaa ya Kiwira ambapo taarifa zinaeleza kwamba, Mkapa na jamaa zake wa familia pamoja na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Yona walianzisha kampuni ya TanPower Resources Limited iliyonunua mgodi huo kwa bei poa ya Sh milioni 700, lakini wamelipa Sh milioni 70.

Alisema kutokana na hali hiyo, Mbunge wa Vunjo (CCM), Aloyce Kimaro alilieleza suala hilo Bungeni.

"Sasa Mheshimiwa Aloyce Kimaro ana chuki gani binafsi dhidi ya Mkapa, ama Mheshimiwa Mkapa alimnyima nini Kimaro, mpaka sasa Kimaro amelieleza hili na kwamba, katika mkataba huu kuna Capital Payment ambapo kila siku tunalipa Sh milioni 146 kama Capital Charge. Hilo anapaswa kulieleza," alisema Lipumba.

Alisema kashfa nyingine, ni ufisadi wa Sh 133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje katika BoT ambazo alisema benki hiyo isingeweza kutoa malipo kwenye makampuni husika 130 bila serikali kuwa na taarifa.

"Pana kashfa nyingine ambazo bado hazijafanyiwa uchunguzi, kama gharama za majengo ya ofisi za BoT", alisema.

Alisema Mkapa alipoanza kutawala, alitangaza mali zake, lakini alipoondoka madarakani hadi sasa hajasema ameondoka akiwa na mali kiasi gani.

"Laiti Mwalimu angelikuwa hai baada ya shutuma zote hizi, nadhani angejilaumu sana kwamba amedanganywa vibaya na mwanafunzi wake aliyemsimamia na kumpigia debe mpaka kuwa rais," alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa alisema yeye ni kati ya waliomtuhumu Mkapa hadharani kwa rekodi na kwa hiyo hajawahi na kamwe hatoajiriwa na serikali.

Hivyo, Dk Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu alisema anachotakiwa kukifanya Mkapa ni kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili na kwamba, hawatahitaji kusikia kutoka kwake jambo la pensheni ambalo hajaulizwa.

"Brela (Kitengo cha serikali cha Kusajili Makampuni) inaonyesha yeye (Mkapa) na mkewe, walianzisha kampuni yenye S.L.P 15 Luthuli Street akiwa Ikulu. Kwa maana alikuwa mjasiriamali akiwa Ikulu. Tunataka kujua mtu huyo ni yeye au la. Na pia alilipa pango ya jengo la Ikulu shilingi ngapi kwa kuitumia Ikulu kufanya biashara?" alisema Dk Slaa.

Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro alimtaka Mkapa kujibu hoja na kwamba, maelezo aliyoyatoa Bungeni kuhusu Mkapa namna alivyonunua mgodi wa Kiwira bila kufuata utaratibu, alifanya hivyo kwa vile zama hizi ni za ukweli na uwazi.

"Hajajibu hoja. Wabunge wangetaka kusikia hayo yanayosemwa dhidi yake. Tunataka yasiendelee kutokea, pia serikali ibadilike, bunge libadilike na viongozi wa ngazi zote wabadilike, watumikie wananchi, siyo wananchi wawatumikie," alisema Kimaro.

Kimaro alisema ataendelea kusema ukweli kwani fitina kwake ni mwiko na Mkapa ndiye muasisi wa kauli mbiu ya uwazi na ukweli.

Naye Hussein Issa anaripoti kuwa, Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Cyriaws Kamugisha, alisema iwapo Mkapa atapatikana na hatia ya kuhusika na tuhuma za ufisadi, anatakiwa afikishwe kizimbani kwani, sheria ni msumeno.

Alisema ikiwa rais aliyeko madarakani akiwa na kosa la madai, anatakiwa ashitakiwe na kuhoji iweje aliyemaliza muda wake asishitakiwe ikiwa ana kosa la kujibu?

Tuhuma za kununua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira (KMCL) ulioko wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya , zililipuka mwanzoni mwa mwaka huu.

Kufuatia tuhuma hizo, hadhi ya Mkapa ambaye aliingia madarakani akiwa safi na kujulikana 'Mr Clean' inazidi kuporomoka miongoni wananchi mbalimbali, ambao wanaamini kuwa alitumia vibaya wadhifa wake kujipatia mali kinyume na maadili ya uongozi.

Juzi Mkapa alikaririwa na vyombo vya habari, akisema watu wanaomtuhumu wamefanya hivyo kwa vile aliwanyima vyeo wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 10 na kwamba watu wote wanaomuita fisadi ni wa kupuuzwa kwa kuwa wana chuki binafsi naye.

Mkapa alikuwa akiwahutubia wanakijiji wa Lupaso wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa uongozi wa kituo cha afya kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki kijijini hapo.
 
Msishangae Mkapa akazimia gafla, maswali yaliyoko mbele yake hawezi kupata majibu haraka haraka ni maswali ya kumpeleka segerea tu.
 
Athari za kutokushughulikiwa kwa Mkapa kwa CCM zinapimika. CCM is to act now before it is too late!
 
Hizo ni tuhuma nzito kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi. Hao wapinzani wasije kuambiwa wana wivu wa kike tena.
 
Mkapa Hata Akilonga tusitegemee lolote jipya labda ni machache sana atasema ambayo yanaweza kushitua umma na sidhani kama hiyo itawezekana na kama itawezekana basi na yeye ataenda kutibiwa nje ya nchi kama wenzake wote walivyowahi kwenda kutibiwa na kurudishwa Na Majeneza Yao Nchini au kuchomwa huko huko kama Balali .

1 ) Je na yeye anapenda kufuata mkondo wa mwenzake ? Jibu analo mwenyewe

2 ) Kama akiamua kufuata mkondo huo , nchi itakuwa katika hali gani ? Yeye mwenyewe na wenzake ndio wanajua .

Lililo wazi ni kwamba Lowassa na mwenzake chenge wameshaenda UK kutoa ushahidi wao katika SFO nchini kule , inawezekana Mkapa anataka kujichomoa katika suala hili kwa kujisafisha hapa tanzania kabla hiyo ripoti ya SFO haijatoka rasmi kwa sababi inaweza kutoka wakati wowote kuanzia mwezi ujao .

Pia kuna suala la mradi wake wa Kiwira , kama mnavyojua watu hawalipwi kule kiwandani watu wanataga kugoma na habari zinazosambaa inasemekana wameshaanza kubadilisha majina na vitu vingine kuhusu umiliki wa mradi huo wa kiwira , inawezekana mpaka ijumaa MKapa na mwenzake daniel atakuwa wameshajitoa na hisa zao katika Kiwira .

Kuna mradi wa madini katika Williamson , Mradi huu maokola majogo , mkapa na wengine wengi wanahusika , kuna mzungu mmoja anafanya kazi Regent Tanzania Limited anajua mengi Jinsi maokola Majogo alivyohongwa mpaka kutoa mradi huo kwa bei chee sijui kama mkapa atakuwa na lolote jipya hapa

Ni hayo tu kwa leo
Mkapa huna huruma "nguo yenyewe ni ndogo mnagawana hadi mnatuacha tu uchi" Serikali yako ilikuwa na kauli mbiu "UKWELI NA UWAZI" mbona ulifanya mambo mengi kwa siri? Mfano ulijimilikisha mgodi wa KIWIRA kule Mbeya?
 
...maswali yaliyoko mbele yake hawezi kupata majibu haraka haraka ni maswali ya kumpeleka segerea tu.

Kakindomaster,

Mkapa hawezi kwenda Segerea kwa maswali. Inabidi sisi tuwe na majibu.

Tatizo, Kakindomaster, ni kwamba ukisoma kwa makini hiyo article, unaona itakuwa vigumu mno kumfikisha Mkapa Segerea kwa sababu inaonekana kina Lipumba wana maswali kuliko majibu. Anauliza hapa ilikuwaje, na pale ikawa vipi, fulani alipewa 10% kununua ndege yako na rada, na wewe ulipewa? Uliwezaje kupata faida haraka haraka kwenye biashara yako? Hakuna mahali Lipumba anasema, definitively, umefanya lile na hili na lile.

Kwa maneno mengine, Mkapa ali operate katika mazingira yanayonuka rushwa. Kama hakukuwa na rushwa basi mazingira yanayozua maswali: kama hukula rushwa tueleze hapa ilikuwaje. Japo mimi binafsi naamini Mkapa hakuwa msafi hata kidogo, naanza kusikitika kwamba labda kweli hatuna vidhibiti hapa, labda huyu Mzee hakuacha fingerprints. I mean, kwenye hiyo article Lipumba ame present kesi ya Mkapa very clearly na kwa ustadi na ufundi, lakini unaisoma huku unatafuta, specifically what do they know that he did, and you hardly see that. Unasikitika kwamba labda tuna maswali kuliko majibu kwenye kesi ya Mkapa.

Wenye kesi ya nguvu wampeleke mahakamani. Hatutaki atoe maelezo ukumbi wa MAELEZO, mjini wala vijijini.
 
Bwanaee,
Yaani sasa hivi wabongo ni Mkapa, Mkapa! Miaka 10 ya JK itaisha baadae tutaanza JK, JK, JK! Tuache unafiki mengine yanayosemwa ukijipa nafasi kidogo tu yakufikiri utaona ni upuuzi! Ben, hatafanywa chochote kwani tuhumazingine ni za kitoto tu, eti alianzisha biashara Ikulu, Hivi mnajua JK"Original" (Mwalimu) alikuwa na shamba la Karanga alipokuwa rais na alikuwa na vibarua! pia hizo karanga alikuwa hali mwenyewe alikuwa nanauza! Hiyo haikuwa biashara?

Hebu tutumie nguvu zetu kuiambia serikali hii ya JK "Chipolopolo" iache mzaha na maisha yetu kwa kuruhusu bei za bidhaa kupanda kila kukicha huku vpato vyetu vikiwa palepale! Kama uchumi unawashinda kiasi hiki hii ni KASHFA KUBWA INAYO WAPOTEZEA KABISA SIFA YA KUONGOZA NCHI,chi za wenzetu kungekuwa na maandamano kila siku.
Tusisubiri hadi waondoke madarakani.
 
Kwahiyo Kanisa bado linapokea misaada kutoka kwa Mkapa pamoja na scandals zote alizonazo?

Sioni sababu ya msingi itakayolizuia kanisa lisipokee sadaka ya Mr.Clean.
Mr.Clean hakuitwa ka kanisa kutoa sadaka.

Mafundisho ya Dini niliyopewa primary school yaliwahi toa maelezo yanayokingana na matendo yanayofanywa na kanisa leo hii.

Pole sana ulipata mafunzo ukiwa primary?

Vilevile, biblia inakemea waziwazi uungaji mkono wa mambo ya dizaini hii.

Biblia unayoitumia wewe ni ipi?na mstari upi?Kuwa makini,unajua hata Gadafi ana bible yake feki.

Ama kweli njaa mbaya.... Duh!!!!!
Hakuna kanisa lenye njaa,unayozungumza hapa.Lamda huko kwako kuna njaa,inayopozwa kwa vijisenti.


Kanisa Katoliki lilitakiwa kuonyesha mfano mzuri kwa kukataa msaada kutoka kwa muumini fisadi anayefahamika kuwaongezea umaskini Wadanganyika kwa kiasi kikubwa;

Pumba achaaaaaaaaa.

Nitawaheshimu viongozi wa kanisa waliopokea msaada huu wakija tangaza siku za karibuni kwamba wametafakari na kuona kwamba walipokea kimakosa msaada huo ambao unaenda kinyume na mafundisho ya Biblia.

Hakuna kiongozi au muumini mwene shida ya kuheshimiwa na wewe.
 
mkapa umekwisha ! lichaa ya mkapa mafisadi wafuatao ambao ni ndugu zake lzima watujibu vema tuhuma zao

1. peter samsom maro, mtoto wa kufikia wa mkapa, alimaliza advanced diploma in buiding economics from ardhi imstitute, katika mazingira ya kutatanisha, alibakizwa pale kama tutorial assisitant licha ya kuwa alifaulu kwa kiwango kidogo, wakati huo babake wa kufikia akiwa waziri wa elimu ya juu. niaka michache baadaye alipewa ulaji wa kuwa mkurugenzi mkuu wa simu 2000, kampuni iliyoundwa kuuza mali za iliyokuwa TTCL, HUYU ALIJIUZIA NYUMBA NA mali nyingine za ttcl karibu kila mahali.isitoshe akmwuzia na mama yake nyumba kibao

2.0 joe maro, huyu alikuwa bank kuu, baadaye kiaina ndo akaunda lile genge la waporaji walioitwa netgroup solutions yeye akiwa local partiner, ufisadi wake unajulikana sana hapa jf
 
I cant resisit admiring those who believe kuwa Mkapa hatafanywa lolote.He will be dealt with.
Finally Watanzania inabidi tu-adopt moto ya Adidas...IMPOSSIBLE IS NOTHING!

Mkapa ataundiwa tume kama ile ya Richmond kwa ajili ya kuhojiwa tu.Na habari za ndani zinasema kuwa mkakati huo umeshaanza ukiongozwa na mkongwe mmoja wa CCM kwa kukusanya signature za wabunge ili avuliwe hio immunity.Then kutoka hapo ndio itakuwa ni juu ya public opinion.Kwa hio jamani,lets be a little patient.
 
Kakindomaster,

Mkapa hawezi kwenda Segerea kwa maswali. Inabidi sisi tuwe na majibu.

Tatizo, Kakindomaster, ni kwamba ukisoma kwa makini hiyo article, unaona itakuwa vigumu mno kumfikisha Mkapa Segerea kwa sababu inaonekana kina Lipumba wana maswali kuliko majibu. Anauliza hapa ilikuwaje, na pale ikawa vipi, fulani alipewa 10% kununua ndege yako na rada, na wewe ulipewa? Uliwezaje kupata faida haraka haraka kwenye biashara yako? Hakuna mahali Lipumba anasema, definitively, umefanya lile na hili na lile.

Kwa maneno mengine, Mkapa ali operate katika mazingira yanayonuka rushwa. Kama hakukuwa na rushwa basi mazingira yanayozua maswali: kama hukula rushwa tueleze hapa ilikuwaje. Japo mimi binafsi naamini Mkapa hakuwa msafi hata kidogo, naanza kusikitika kwamba labda kweli hatuna vidhibiti hapa, labda huyu Mzee hakuacha fingerprints. I mean, kwenye hiyo article Lipumba ame present kesi ya Mkapa very clearly na kwa ustadi na ufundi, lakini unaisoma huku unatafuta, specifically what do they know that he did, and you hardly see that. Unasikitika kwamba labda tuna maswali kuliko majibu kwenye kesi ya Mkapa.

Wenye kesi ya nguvu wampeleke mahakamani. Hatutaki atoe maelezo ukumbi wa MAELEZO, mjini wala vijijini.

Kuhani Mkuu,

Nimependa hiyo kwenye bold. Hiyo case ya mkapa itabidi iwe na a live streaming show hapa JF..... i cant wait!
 
Back
Top Bottom