Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Niaamini kuwa wakati ukifika, hatakuwa na ujanja, tulisema siku nyingi sana huko nyum akuwa huyu Mkapa, sio a good politician ila ni a good messenger tu na kuandika English safi, that is all kwa sababu angekuwa na akili ya siasa aisngefanya aliyoyafanya akiwa rais, na kuacha ushahidi kila kona,

Kama yeye mwizi kweli na mwanasiasa, kilichomshinda kwenda kuiba hela za kutoka majuu na kukatia huko huko ni kipi? Sasa hivi kinga yake ya Presidential Immunity, ni suala la wabunge tu kuiondoa kwa kura 2/3 basi ameenda na maji, rais hawezi kuizuia maana hata rais mwenyewe sasa hivi hana hamu na bunge tena,

Toka atoke kwenye urais, ndio basi hana mtu hata mmoja aliyebaki kwenye power wa kusema atamsimamia, alimtegemea sana Lumbanga, lakini not only kwamba alitemwa bali pia na yeye anahusika na kesi ya Mahalu, maana alishiriki pia, na hata Mkapa yumo kule so far kesi haijamuendeea vibaya Mahalu, ambaye ameapa in private kuwa yakimfika shingoni atawasema wote aliokula nao,

Kuna wanaotuambia kuwa Mkapa ni mzuri wa kuongea atawashinda wote kwa hoja, damn! ninakumbuka baada tu ya kupata urais 1996, nilipambana naye kwenye mkutano mmoja wa wabongo, nikamtwanga na hoja mpaka akakatisha mkutano kwa hasira na kukataa hata dinner aliyokuwa ametayarishiwa na balozi pale, kesho yake kidogo amle yule balozi kwa kuniruhusu kuhudhuria ule mkutano huku akiwa anajua kuwa mimi ni mpinzani, na toka siku ile ikawa kila anapokwenda ule mji ilikuwa ninatumiwa ujumbe mzito na idara kuwa nisiende kwenye mikutano yake, au nikienda nisiulize maswali tena, ikiwa ni amri toka kwake mwenyewe,

wallahi siku itakapofika nitawaomba serikali wanipe nile naye sahani moja, huyu ni panja tu, yaani mwizi mimi wanipatie huyo tuone kama ana hoja kweli!
 
Mtanzania you got my attention here.. huku kutwangana risasi kunafanywa na nani, kwaweza kufanywa na nani, au kufanywe na nani ili kupunguza ufisadi?

Mwanakijiji,

Sijawahi hata kuua paka, lakini kwenye hili kama hawa jamaa watahukumiwa kisheria na bunduki ikatayarishwa niko tayari kuifyatua pale uwanja wa taifa kwi kwi kwi kwi!!!

Tumezidi kunyanyaswa na watu wachache wenye tamaa za ajabu.

Wewe ukisoma mafao ya Mkapa, kweli alikuwa anahitaji kuiba? Linganisha na mafao ya Bush au Blair, Mkapa anawapita wenzake kwa mbali.
 
main.jpg


By: THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

FORMER President Benjamin Mkapa is already guaranteed a comfortable life after retirement, courtesy of taxpayers’ money, according to legislation that he himself assented to while at State House.

The current Political Service Retirement Benefits Act, passed by the National Assembly in 2000, spells out a generous package of retirement perks for the former president, including an annual pension granted monthly of a sum equal to 80 per cent of the salary of incumbent President Jakaya Kikwete.

On top of that, Mkapa also now gets a monthly maintenance allowance also equal to 80 per cent of Kikwete’s current salary.

Furthermore, after leaving public office, he was entitled to receive a gratuity of a sum equal to 50 per cent of the total sum received by himself as salaries during his entire ten-year tenure as head of state from 1995.

Mkapa also received a winding-up allowance of a sum equal to the amount that would be received as salary in 24 months by incumbent President Kikwete.

Apart from this financial windfall, the legislation also allows the ex-president to continue using diplomatic passports for himself and his wife, plus the use of the VIP lounge at all airports.

He was also given a health insurance policy that covers medical treatment within Tanzania, plus the services of two motor vehicles to be provided by the government, and two drivers.

Also included in Mkapa’s handsome retirement benefits package is a fully-furnished house of not less than four bedrooms, two of which shall be self-contained, with a furnished office and servants’ quarters.

The specific legislation also guarantees ’’all necessary security and other protection services to himself and his immediate family.’’

Courtesy of taxpayers’ money, the former president also gets one of each of the following: Personal assistant, personal secretary, office attendant, personal cook, laundry man, domestic servant, and gardener.

And if he is requested to travel outside Tanzania on official (Kikwete) government business, only first class travel is appropriate for Mkapa, with the state also obliged to foot travel expenses for his spouse and two assistants.

Overall, the perks listed in the legislation in question basically ensured that the ex-president would be well taken care of by the state for the rest of his life, after retirement in 2005.

But still, Mkapa stands accused of aggressively seeking to acquire even more personal wealth during his tenure as president, regardless of the huge pension cheque he knew he would receive after leaving public office.

Records show that the legislation in question was assented hardly a year after Mkapa and former first lady Anna Mkapa started their own private business company, ANBEM Limited, and operated it from within the Ikulu premises.

ANBEM Ltd dealings included obtaining loans totalling 750m/- from the National Bank of Commerce (NBC) and CRDB Bank, some of this money reportedly being used to buy a two-storey building in Dar es Salaam’s upmarket Sea View area, which has now been rented to Bank (M) Tanzania Limited.

It has also been established that Mkapa, while still president, joined forces in 2004 with his then energy and minerals minister, Daniel Yona, to form another private company, Tanpower Resources Limited, with various members of their immediate families.

Both Mkapa and Yona were then heavily involved in the privatization of the formerly state-owned Kiwira coal mine in Mbeya Region, ensuring that this lucrative national asset was cheaply sold to the Tanpower Resources company in 2005.

Meanwhile, the Chairman of the opposition Civic United Front (CUF) Party, Prof. Ibrahim Lipumba, has joined the chorus of strong public criticism against Mkapa.

Speaking at a meeting of the Editors’ Forum in Dar es Salaam yesterday, Lipumba described Mkapa as a wolf in sheep’s clothing.

He charged that Mkapa who retired in 2005 was not the same man as the ’Mr Clean’ who entered State House for the first time in 1995.

The CUF leader said it was somewhat surprising to see Mkapa apparently grieving deeply the death of the Father of the Nation, Mwalimu Julius Nyerere, in 1999 - the same year that he started his own private company at State House.

’’It would seem that immediately after Mwalimu’s death, Mkapa began abusing public office by conducting his private business affairs at State House,’’ said Lipumba.

He cited apparently corruption-tainted deals under the Mkapa administration as including the 70bn/- military radar transaction, and equally dubious purchases of military vehicles, helicopters and the presidential jet - all done through controversial middleman Shailesh Vithlani.

Various political commentators have roundly dismissed Mkapa’s weekend attempt to respond for the first time to the widespread allegations of corruption and abuse of office that have hounded him for a full year now, with the general consensus being that he failed completely to address the real issues at hand.
 
Jamani nisaidieni.
Sheria ya maadili inakataza mtu kufungua kampuni akiwa Ikulu au inakataza Kufanya biashara ukiwa Ikulu.
What if Ben an mama walifungua kampuni halafu kamuni ikawa floated?
Kwa kuwa hatujaona file la Kampuni hiyo twatumia vigezo gani kumhukumu moja kwa moja?
Isijetokea siku akasema tukamwambia basi usiseme tena
 
Moderator naomba uiunganishe hii thread na ile nyingine kwani tofauti yake ni Heading, mwingine katumia ya kiingereza na mwingine katumia ya kiswahili lakini contex ni moja!
 
Hawa watu watakufa vibaya jamani.... wanakula mapaka basi, hiyo 80% si ni sawa tu na mshahara wa JK tuu,
 
The ex President is heartless! What can be done to make him pay for the crimes he has commited?

How can we develop our nation when there are criminals of this sort?
1.Stealing from the people without mercy.

2.Killing the people(Pemba killings) and getting away with it!
3.Grabbing Kiwira and stealing from BOT..(EPA)

And probably many more crimes we don't know....

Where are the smart lawyers to make him pay?
 
Moderator naomba uiunganishe hii thread na ile nyingine kwani tofauti yake ni Heading, mwingine katumia ya kiingereza na mwingine katumia ya kiswahili lakini contex ni moja!
Shukrani kigarama... Credit to you!
 
Kuna watu walikasirika pale Mkapa alipokosa ile tuzo ya Rais bora mstaafu iliyotolewa kipindi cha nyuma kidogo na mfanyabiashara mmoja hivi maarufu wa kiafrika (details sikumbuki vizuri). Nadhani wengi tulikuwa tunaamini jamaa alikuwa "msafi". Sio msafi kihivyo, lakini alionekana angalau msafi kidogo. Kipindi kile labda niseme upinzani ulikuwa haujakomaa au watu walikuwa waoga au Mkapa alikuwa anawaziba midomo wapinzani sijui nisemeje, lakini mambo haya ya ufisadi wa hili jamaa yalikuwa hayazungumzwi sana kipindi akiwa madarakani. Wengi hatukujua haya yote. Labda niseme jamaa alikuwa mkali. Alikuwa anajua kuongea kwa kukaripia tofauti na JK. Zile speech zake za mwisho wa mwezi zilikuwa ni za vitisho tu utadhani anaongoza nchi ya kikomunisti. Naona hili lilipelekea wengi kushindwa kuhoji au kupiga kelele kuhusu ufisadi wa huyu jamaa.
 

wabunge wawili wa ccm wamemjibu makapa leo magazeti yote yana hiy kumkoma nyani, yaani wabunge Anne Malecela na Kimaro, yaani mkapa hanan ujanja maana hii ndio hasa tunaita kumkoma nyani, arudishe Kiwira sasa ndio the mantra, mengine tutayaangalia baadaye,

Hakuna mwenye tatizo na pension yake, lakini hawezi kutufanya wabongo wote kuwa ni waginjwa wa akili kama yeye, mbona hakusema kuhusu Kiwira? Aliuziwa na wanaomchukia au kumuonea wivu? The guy is a thug period ndio maan kule kwenye MO watu walishangaa anatafuta nini mtu aliyekuwa akiiba akiwa Ikulu ya wananchi,

Time is up sasa, sasa hivi nikisikia kuwa ana mkutano mahali nitajimwaga nimpe part II ya ile ya 1996, mpaka akakatisha mkutano na kufoka sana, huwa halina hata hoja zaidi ya kufura tu, arudishe mali zetu wananchi kwanza!
 
Nkapa atapata taabu sana kwani ni rais wa kwanza Tanzania na Afrika ya mashariki baada ya kustaafu klwake watu wanataka kumwona akiwa mahakamani.

Moi wa kenya alikuwa Prof.wa siasa na aliserve hii trial sasa huyu sijui alikuwa nani na je ataweza kuzuia upepo wa kumtaka mbele ya koti?

Historia ilijengwa tarehe 15 September we are still moving and one day we willl be there......
 
Kuna watu walikasirika pale Mkapa alipokosa ile tuzo ya Rais bora mstaafu iliyotolewa kipindi cha nyuma kidogo na mfanyabiashara mmoja hivi maarufu wa kiafrika (details sikumbuki vizuri).

Jamaa anaitwa Mo Ibrahim. Website yake ni hii:
 
Pensheni hii mzee?

2008-05-29 16:33:55
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Kauli ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Benjamin William Mkapa kuwa yeye si mtu mwenye mapesa mengi na kwamba hivi sasa anaishi kwa kutegemea pensheni yake ya kuwa kiongozi mstaafu imezua mjadala zaidi ambapo sasa anatakiwa aueleze umma kama mali yote anayodaiwa kujilimbikizia wakati akiwa madarakani imetokana na pensheni anayolipwa sasa.

Wakizungumza na Alasiri leo asubuhi, baadhi ya wanasiasa wamesema hivi sasa, Mkapa anatakiwa atoe ufafanuzi wa kina kuhusiana na tuhuma za kujilimbikizia mali na familia yake, ikiwa ni pamoja na kueleza kama kweli mali zote anazodaiwa kuwa nazo sasa zimetokana na maisha yake ya kutegemea pensheni kama alivyowaeleza wanakijiji wa nyumbani kwao Lupaso kule Masasi, mkoani Mtwara.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, amesema Mkapa anapaswa kujibu hoja ya kukiuka maadili ya uongozi wakati akiwa Ikulu badala ya kutoa visingizio na kujipunguzia heshima yake kwa jamii na hasa kuhusiana na madai haya ya kujilimbikizia mali akiwa ikulu.

Amesema Watanzania wanajua kuwa anapewa pensheni yake na Serikali kwa vile ipo kwa mujibu wa sheria, lakini pia anapaswa kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu, jambo ambalo halikubaliki kwa kiongozi wa umma na tena halihusiani na pensheni yake hiyo.

Amesema Mkapa awathibitishie kwa nyaraka wananchi kama madai ya yeye na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wake Bw. Daniel Yona kupitia kampuni yao ya TANPOWER kumiliki mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ni ya uongo.

Pia Dk. Slaa amesema njia sahihi ya Bw. Mkapa kujisafisha ni kutangaza mali zake hadharani ili wananchi wajue kuwa majumba kibao yanayoelezwa kuwa anayamiliki Jijini Dar es Salaam na kule Lushoto mkoani Tanga ni uongo.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Cho Kikuu cha Dar es Salaam na aliyekuwa mgombea urais mwaka 2005 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Edmund Sengondo Mvungi amesema anachotakiwa kukifanya Bw. Mkapa ni kujitokeza hadharani na kuwaeleza wananchi ukweli juu ya tuhuma zinazomkabili.

Amesema madai ya kuwa wanaomsema wanamchukia, hayana msingi wowote na kuwa hakuna mtu anayemchukia.

``Mimi binafsi napenda Bw. Mkapa aishi maisha mazuri, siwezi kumchukia wala kujikomba kwake, wala sikuwahi kumuomba kazi... lakini yanapokuja masuala ya msingi kama haya anayotuhumiwa, anapaswa kuyajibu na sio kudai kuwa anachukiwa,`` akasema.

Akasema Bw. Mkapa anatakiwa awathibitishie wananchi kama madai ya yeye (Mkapa) kumiliki shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 5,000 kule Mtibwa mkoani Morogoro ni ya uongo au yametokana na hayo malipo ya pensheni.

Dk. Mvungi pia akasema Bw. Mkapa awaambie wananchi kuwa majengo ya ghorofa linalotumika kama hoteli pale Ilala Jijini ambayo mkewe anadaiwa kumilikishwa wakati wa urais wake , pia yanatokana na pensheni yake.

Kama hiyo haitoshi, Dk. Mvungi amemtaka Bw. Mkapa kutamka hadharani kama madai ya kuwa mmoja wa wamiliki wa benki moja maarufu Jijini yanatokana na pensheni yake.

``Wananchi wanayo haki ya kikatiba kumhoji Mkapa, asidhani kuwa wanamchukia. Hivyo njia sahihi ni yeye kusimama hadharani kuwajibu wananchi kwa kile wanachohoji,`` akasisitiza Dk. Mvungi.

Aidha, jana Dk. Mvungi alimtaka Mkapa aeleze pia kuhusu madai kuwa yeye na familia yake wamejilimbikia ekari kadhaa za mashamba kule Bagamoyo mkoani Pwani.

Akiwa kijijini kwao Lupaso hivi karibuni, Mkapa alisema yote yanayosema ni uongo kwani yeye, hivi sasa anaishi kwa kutegemea pensheni yake kama alivyo mtangulizi wake, Rais wa awamu ya pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi.

SOURCE: Alasiri
 
Back
Top Bottom