1. Tuliambiwa huko nyuma kuwa Lowassa, hawezekaniki anajua siri nyingi za rais hawezi kumtosa, halafu ni mshikaji wake sana, mimi nikasema hivi muungwana alienda kuiona nyumba ya mtoto wa Lowassa saa za usiku, hakwenda kule bila sababu, the next thing mkulu akatemwa,
Muungwana, akakutana na wabunge wote waliomtwanga Lowassa bungeni kwa siri na kuwapa ahsante, na pia kuwapa barua nzito inayowakataza viongozi wote wa juu wa serikali na ccm, kuwatisha wabunge wakati wakismama kidete bungeni, hii ilikuwa ni baada ya viongozi hao kulalamika kwa muungwana kuwa kuna wabunge wa ccm wanaoshirikiana na wabunge wa upinzani,
2. Tukaambiwa Chenge, ana siri nyingi sana za muungwana na hela za wauza unga alizopewa nao kwenye kampeni za urais, kwa hiyo hawezi kumgusa kabisa, boy! tumejionea Chenge akiadhirika. Karamagi, Msabaha.
3. Now here comes Mkapa, tayari tumeshaanza kuambiwa yale yale kuwa hawezi kuguswa, nilitabiri siku nyingi sana kuwa kuna siku muungwana atamtema tena kiroho mbaya sana Mkapa, wanaosema eti hakuna ushahidi naomba mteme mate chini maana kuna ushahidi wa kutosha kwamba hata siku Mkapa alipokuwa anakwenda Uwanja Wa Taifa kukabidhi urais, alisaini hela nyingi sana kuchukuliwa huko BOT, kuna ushahidi wa kutosha wa viongozi wote waliopewa special "viinua mgongo" dakika za mwisho na Mkapa kutoka BOT, kuna ushahidi wa kutosha jinsi alivyoitumia Wizara ya Miundo Mbinu kujitajirisha, kuna ushahidi wa kutosha jinsi alivyomtumia Mramba kujitajirisha,
I mean ushahidi upo tena wa kutosha sana kisheria na analijua sana hilo, na anajua sana kuwa kuna wabunge wanao huo ushahidi, siku ile Kimaro alipoongea haikuwa bure tu, kulikuwa na sababu nzito sana nyuma yake, Mkapa is going down tena sio mbali, mkewe analijua sana hilo na tayari ameshanza kuchekesha mbele ya wenziwe, mapesa mengi sana yalitumika kujaribu kuwanyamzisha wabunge ile siku ya kipigo cha Lowassa, tunaambiwa kuwa billions of our money zilimwagwa kwa wabunge ili waikatae ile ripoti, inasemekana kuwa haijawahi kutokea maana kuna wabunge waliopewa mpaka shillingi millioni 10 to 20, na kwamba Mkapa alikuwa pia anahusika na hizi kutolewa kwa hizi hela, kwa sababu alijua Lowassa akitolewa, basi next wataishia mlangoni kwake, ninasema hivi haoo wanakuja,
na sisi wananchi tunakuja, kuanzia kikao kijacho cha bajeti kutakuwa na moto ambao Mkapa hatauweza, it is only a matter of time kabla mvua haijamuangukia, he is done! Ni kweli Tanzania nchi yangu ina matatizo mengi sana ya uongozi, lakini this one Mkapa hawezi pona hata afanye nini he is next on line!
Unajua hakuna watu wanaojua kusoma upepo wa siasa za nchi kama Wahindi, sasa hawakubali tena deal yoyote toka Lowassa apigwe chini, unafikri wameona nini hao? Viongozi wengi wanaopitia hapa JF wanasema kuwa tunaonekana kutokumbuka kauli ya muungwana kuwa hana ubia na mtu yoyote kwenye urais wake, na pia wanasema kuwa inaonekana kuwa hatujui kuwa ile siku ya interview ya Lowassa kwenye ITV baada ya kutemwa, ilikatishwa na yeye muungwana na kwamba alishawapa warning walinzi wake na uwt kwa ujumla kuwa hataki kumuona huyo mkulu karibu yake bila sababu maalum, meaning kwamba sasa hivi ni rahisi kwangu mimi na wewe kumuona muungwana kuliko Lowassa kumuona muungwana!