Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

He he kuna kazi hapa sasa, tutaamini vipi huyu mama na mafisadi wengine lao sio moja dhidi ya kufuta ushahidi?

Icadon,

Kadri nilivyoona kwenye buzz line... Mama Muganda ana very low approval rating and significantly higher negative rating kulinganisha na Ballali. Sidhani kama hata yeye atapona kwenye hili la wizi BoT.
 
PEZZONOVANTE:

Mada nzuri lakini kama moderator usianze kutoka nje ya mistari. Point ni kuwa tunataka kujenga taifa hivyo wizi wa mali za umma lazima uchungu uwe kwa taifa.

Hili suala la mtu kuiba na kwenda kwao kujiosha kwa kutoa pilau, sadaka misikitini au makanisa na kuwafuraisha watu wa kwao haitatufikisha popote. Na hicho ndicho kinachofanyika sasa.
 
Hili suala la mtu kuiba na kwenda kwao kujiosha kwa kutoa pilau, sadaka misikitini au makanisa na kuwafuraisha watu wa kwao haitatufikisha popote. Na hicho ndicho kinachofanyika sasa.

Nani mbaya zaidi, mtoa pilau au mla pilau?
 
Inachekesha kumwona Mkapa akijiweka katika position ya u-underdog.... It is really funny!!!

URL: http://dailynews.habarileo.co.tz/home/index.php?id=4813

HARRIETH KIAMA in Masasi
Daily News; Tuesday,May 27, 2008 @08:29


RETIRED President Benjamin Mkapa has broken his silence over alleged abuse of power while in office, dismissing such allegations as false claims by people out to settle scores with him.

Addressing residents at his home village of Lupaso in Masasi district, Mtwara region, Mr Mkapa said over the weekend that those accusing him were the same people who came asking for favours from him during his tenure as president.

"Do not listen to their lies … there is no truth in the allegations but only hatred … mostly from people who thought I would have favoured -- but didn't," he said amid applause from the villagers.

Mr Mkapa made the address shortly after handing out various medical supplies for a health centre run by the Catholic Church at the village. He said that he was not wealthy -- as his detractors allege would have everyone believe -- and told people to ignore such malice.

The retired president has come under an ugly spotlight lately following allegations that he conducted private businesses while still at State House, citing the newly established Tanpower Company Limited that owns majority shares in the Kiwira Coal Mine in Mbeya region.

According to the allegations, Mr Mkapa formed the firm jointly with former Energy and Minerals minister Daniel Yona, expecting the firm would rake in some 140m/- in daily capacity charges from the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) once Kiwira started generating electricity.

There are also reports that he pushed for a 15-year extension of a contract on behalf of Messrs Tanzania International Containers Terminal Services (TICTS) before expiry of a previous contract – of ten years – that would have expired in 2010.

"I am not that financially well-off … although I know that you hear and read a lot about this … I live on my pension benefits from the government, as does my predecessor, (Mzee) Ali Hassan Mwinyi," Mr Mkapa told the gathering, stressing that he couldn't even afford the price of the equipment he was donating – because he wasn't that rich.

"I spent my family savings to transport the equipment from Canada to Dar es Salaam … the government helped me transport it to this village. Where would I get the money to buy such equipment?" he queried.

He also used the occasion to encourage the villagers to cultivate a culture of living healthy lives by building latrines, using them and checking their health status regularly.
 
Hassan Simba, Mtwara
Daily News; Tuesday,May 27, 2008 @00:02

RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amevunja ukimya kuhusu tetesi na tuhuma kwamba alikiuka misingi na kujikita katika biashara wakati akiwa madarakani kwa kusema madai hayo si ya kweli na kwamba wanaomtuhumu wana chuki dhidi yake.

Akihutubia mwishoni mwa wiki katika Kijiji alichozaliwa cha Lupaso, Wilaya ya Masasi, Mkapa alisema wanaomtuhumu wanamchukia kwa kutowapendelea wakati wa utawala wake. Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba kwa Kituo cha Afya kinachomilikiwa na Kanisa la Katoliki kijijini hapo, alisema;

"Msisikilize uongo huo kwa sababu hauna msingi wowote isipokuwa ni chuki …hasa inayotokana na watu ambao walifikiri nitawapendelea … sikuwapendelea," alisema Mkapa huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake waliohudhuria makabidhiano hayo.

Alisema kuwa yeye si tajiri na kwamba tuhuma hizo ni za uongo na hivyo kuwataka wananchi kuzipuuza kwa kuwa hazina msingi wowote wala chembe ya ukweli.

"Sina uwezo wa fedha ingawa najua mnasikia na kusoma mengi …naishi kwa pensheni yangu kutoka serikalini kutokana na kuwa kiongozi kwa miaka 10 ambayo hata Mzee Mwinyi anaishi hivyo maana sisi sote ni wastaafu. Huo (uvumi) ni uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo," alisema Mkapa na kuongeza;

"Mimi si tajiri, nimeomba msaada nimepewa…nimejinyima mimi na mke wangu ndiyo tukaweza kugharimia kusafirisha vifaa hivi kutoka Canada hadi Dar es Salaam, kutoka hapo hadi hapa vimesafirishwa na Serikali…..sikuwa na uwezo wa kununua vifaa kama hivi. Nitapata wapi fedha za kununua vifaa kama hivi," alisema Mkapa.

Katika hotuba yake hiyo Mkapa hakujibu tuhuma dhidi yake moja kwa moja na badala yake alirudiarudia kusema kwamba hakuna ukweli kuhusiana na yanayoelezwa dhidi yake.

Mkapa alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa kijijini kwake kujenga utamaduni wa kujali afya zao kwa kujenga vyoo na kuvitumia sambamba na kupima afya zao mara kwa mara.

"Tunapojenga nyumba basi tujenge na vyoo na misala….na si kujenga tu lakini pia tuvitumie. Hii ni kwa faida ya afya zetu maana ukicheza na afya unajitengenezea mazingira ya umasikini kwa kuwa hutaweza kushiriki vema katika shughuli za uzalishaji," alisema.

Kwa kipindi kirefu sasa Mkapa amekuwa akituhumiwa kwa kuendesha biashara akiwa Ikulu na hasa kuhusu umiliki wa Kampuni ya Tanpower inayomiliki hisa nyingi katika Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Kiwira mkoani Mbeya.

Imekuwa ikidaiwa kwamba Mkapa alishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona katika kununua hisa za Kiwira kwa matarajio kwamba umeme ungezalishwa kutoka hapo baada ya muda mfupi ujao na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lingelazimika kuwalipa takribani Sh milioni 140 kwa siku, hata bila umeme kuzalishwa.

Kupatikana kwa vifaa hivyo vilivyotolewa na Mkapa kutawezesha kituo hicho kutoa huduma bora zaidi na hivyo kuwanufaisha wananchi zaidi ya 43,000 wa vijiji tisa jirani ambao hadi siku za karibuni walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 34 hadi ilipo Hospitali ya Wilaya.

Akipokea msaada huo Askofu wa Kanisa hilo Jimbo la Masasi,Tunduru, Castro Msemwa, alimshukuru Mkapa kwa jitihada zake za kuwatafutia wafadhili waliowezesha kupatikana kwa vifaa hivyo na kumuomba aendelee kusaidia kwa vile Kanisa linatambua mchango wake.
 
Askofu Msemwa inampasa arudishe msaada huu kwa Mkapa maana alivyotenda ni kinyume na mafundisho ya kanisa katoliki.

Biblia haijatoa exceptions zozote kuhusiana na kupokea misaada from the third party through fisadi. Kuupokea msaada huu kutoka kwa Mkapa ni kujaribu kupingana na maandiko matakatifu.

Hata kama waumini ni watu maskini, biblia bado hairuhusu watumishi wa Mungu kurubuniwa kipesa na wenye dhambi. Kanisa katoliki (kumradhi) limejiwekea utaratibu kwa wenye dhambi kwenda kuungama dhambi zao. Mkapa, kama wakatoliki wengine, ana nafasi ya kwenda kuungama zambi ya kuwaongezea watanzania umaskini kwa kiasi kikubwa. Akishasamehewa dhambi zake na kuukana usemi kwamba yeye si mwizi, then kanisa litakuwa katika nafasi nzuri ya kuanza taratibu nyingine za kuupokea tena msaada huu.
 
... Mama Muganda ana very low approval rating and significantly higher negative rating kulinganisha na Ballali. Sidhani kama hata yeye atapona kwenye hili la wizi BoT.

M wa Kike, kama wazungu wanavyo sema "do not hold your breath over it."

Mama Muganda alisha kuwa cleared na Serikali.

Sasa utakaa chini mwenyewe ukiona ni nani ali m clear Mama Muganda!

Kutoka Bungeni. July 1st 2007

THE government yesterday dismissed as "false and fabricated," claims by the opposition camp that the wife of BoT governor Daudi Ballali, Anna Muganda, directed and owned shares in mining companies associated with the Central Bank.

The Minister for Energy and Minerals, Mr Nazir Karamagi, told the National Assembly here after question time, that the allegations in the House by the Deputy Leader of the Opposition, Dr Willbroad Slaa, had no iota of truth and were deliberately aimed at misleading the public...


(Habari Kamili: http://www.afronewz.com/Tanzania/tanzanian_government_opposition.html)
 
M wa Kike, kama wazungu wanavyo sema "do not hold your breath over it."

Mama Muganda alisha kuwa cleared na Serikali.

Sasa utakaa chini mwenyewe ukiona ni nani ali m clear Mama Muganda!

Kutoka Bungeni. July 1st 2007

THE government yesterday dismissed as "false and fabricated," claims by the opposition camp that the wife of BoT governor Daudi Ballali, Anna Muganda, directed and owned shares in mining companies associated with the Central Bank.

The Minister for Energy and Minerals, Mr Nazir Karamagi, told the National Assembly here after question time, that the allegations in the House by the Deputy Leader of the Opposition, Dr Willbroad Slaa, had no iota of truth and were deliberately aimed at misleading the public...


(Habari Kamili: http://www.afronewz.com/Tanzania/tanzanian_government_opposition.html)

Hawa si kawaida yao kukanusha na ku-clear watu?!

Unakumbuka walisema nini kuhusu Richmond na Buzwagi mwanzoni? Mafisadi wa ccm wanajua kukanusha kabla hawajakubali kwa siri kuwa wanahusika na kila umasikini wa watanzania.
 
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amekanusha matumizi mabaya ya ofisi yake na kuanzisha biashara akiwa madarakani....... alisema; “Msisikilize uongo huo kwa sababu hauna msingi wowote isipokuwa ni chuki …hasa inayotokana na watu ambao walifikiri nitawapendelea … sikuwapendelea,” alisema Mkapa huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake waliohudhuria makabidhiano hayo.

Kwa hiyo aliowapendelea hawawezi kumgeuka na kusema ukweli kwa umma???
 
Hmm.. wasn't Anna Muganda who introduced Ballali to Mkapa pale DC, jioni moja ya mwaka 1996?

This guy BWM has an addiction for ladies called "Anna". Yule Anna wa kwanza alimpora kutoka kwa mshkaji wake wa Makerere, Mramba, akabeba pamoja na mwanae! Halafu kuna yule Anna Rweyemamu, maarufu sana. Na huyu Anna Muganda, hamjahisi chochote? Na wengine wa jina hilo tuwatilie shaka pia? Kama udaku vile, lakini bongo naiogopa siku hizi, likisemwa jambo sipuuzii, wahenga waliposema "lisemwalo lipo" walisikia na kuona mengi kabla ya kufikia conclusion hiyo.
 
"Sina uwezo wa fedha ingawa najua mnasikia na kusoma mengi …naishi kwa pensheni yangu kutoka serikalini kutokana na kuwa kiongozi kwa miaka 10 ambayo hata Mzee Mwinyi anaishi hivyo maana sisi sote ni wastaafu. Huo (uvumi) ni uongo …uongo ….uongo ….uongo …uongo….uongo….uongo," alisema Mkapa.

Ha, ha, Haya Baba ila hukuwa na haja ya kurudi hili neno "Uongo" mara kibao maana tunaamini ONLY TIME WILL TELL. Na Mzee Mwinyi asiwe Egemeo lako Mkuu. STAND OUT FROM THE CROWD KIVYAKO MKUU.
 
Hmm.. wasn't Anna Muganda who introduced Ballali to Mkapa pale DC, jioni moja ya mwaka 1996?

Sishangai.

Muganda-Mkapa connection is deeper kuliko mizizi ya M-Buyu. Anna Muganda na Anna Mkapa ni marafiki wa kuchanjia. And this goes way back, before either one was Madam First lady or Madam Mrs. Governor. Hili niliambiwa na mtu anaemjua Anna Muganda kindugu. Na Mkapa mwenyewe amefanya kazi Foreign affairs na kaka yake Anna, Marehemu Bernard Muganda. Na dada yake mkubwa Anna, ni Mke wa kwanza wa Mzee Butiku, mtu ambae Mkapa would go thru kumuona mentor wake Nyerere, na baadae wakamfanyia campaign, kama Butiku alivyo lia majuzi kwamba Mkapa kawageukia Mbogo baada ya kumbeba kwenye ma Land Rover kwenye campaign trail across the country.

Kwa hiyo, the web of connection btn Mkapa and Ballali is unmistakable.
 
Mzee Mwinyi anaishi kwa pensheni yake nyumbani kwake na wanae na wajukuu, na hili linaonekana wazi ndio maana husikii watu wakihoji. Sasa huu ulinganisho anaolazimisha Mkapa kwa kigezo kimoja tu cha "ustaafu" kuwa yu kama Mzee Mwinyi ni sawa na kusema mbuzi na kunguru wako sawa kwa kuwa wote wana macho mawili au wana damu nyekundu! Lakini twajua wazi ya kuwa kunguru hafai kwa kitoweo wala hafugiki!
 
Haya Baba ila hukuwa na haja ya kurudi hili neno "Uongo" mara kibao maana tunaamini ONLY TIME WILL TELL

Time will not tell kama hajashitakiwa. Mahojiano mjini au kijijini hataya saidia lolote. Atarudia tena kusema "uongo" "uongo." Halafu atapotelea hospitali kabla time haija tell!

Tumeiona hii sinema na tunajua inavyo isha.

Wenye vidhibiti wamshitaki. Sasa hivi!

Hatutaki maelezo!
 
Time will not tell kama hajashitakiwa. Mahojiano mjini au kijijini hataya saidia lolote. Atarudia tena kusema "uongo" "uongo." Halafu atapotelea hospitali kabla time haija tell!

Tumeiona hii sinema na tunajua inavyo isha.

Wenye vidhibiti wamshitaki. Sasa hivi!

Hatutaki maelezo!

kwi kwi kwi...

yaani hapa imebidi nicheke kwenye hii ya kupotelea hospitalini...
 
Bubu,

Tume ya Madini imependekeza iundwe Tume ya Madini kuchunguza mgodi ulivyo milikishwa!

Tume ya Madini No.2 itashauri Mkurugenzi wa Mashitaki afanye tathmini kuona kama kuna kesi ya Kujibu!

DPP akimaliza tathmini yake tutahitaji Tume ya Katiba kuangalia, je, Mkapa anaweza kushitakiwa?

At that time, Kikwete yuko ngwe ya pili ya Awamu ya Nne, na Mkapa atakuwa "Mahutihuti" katika hospitali inayolipiwa - lakini isiyo julikana - na Serikali, au mtu yeyote isipokuwa Anna. The other one, sio Anna Muganda.

Ili kum locate Mkapa na hospitali aliko, tutahitaji Tume kuchunguza hili: Hundi za Serikali za kulipa bills za hospitali huwa zimeandikwa nani azikeshi, zimeandikiwa ziende hospitali gani, kama sio ya Prof. Maji Marefu?

Hiyo ndio script ya maonyesho ya Mchiriku wa Kikwete Administration!
...teh teh teh, kazi ipo!
 
Back
Top Bottom