Tukio hili linanikumbusha kisa cha mwanake aliyetuhumiwa kuwa mzinzi katika biblia... Yule mwanamke alipopelekwa mbele ya Bwana Yesu wale jamaa wakiwa na mawe mkononi wakasema bwana mkubwa Musa aliagiza watu kama hawa wapigwe mawe, wewe una maoni gani?
Bwana mkubwa akawajibu asiye na doa awe wa kwanza kurusha jiwe. Mwandishi anaelezea kuwa jamaa walianza kudondosha mawe kuanzia wadogo mpaka wakubwa na kuondoka...
Nikiangalia katika hao waliojitokeza na watakao jitokeza ambao kuna fununu kuwa wana mpango wa kujitokeza sijaona ambaye hana dosari hasa ikizingatiwa kuwa wote ni binadamu, hakuna Malaika kati yao.
Mtazamo wangu huko namna hii; kama yupo kiongozi anayeweza kusababisha au kutoa mchango uchumi wa nchi yetu kukua katika kiwango ambacho huduma za msingi kama elimu, afya, makaazi na lishe zikapatikana kiasi cha kutosha huyo kiongozi atakua anatufaa bila kujari anatokea kutoka katika chama gani cha kisiasa.
katika suala la kumpata kiongozi wa namna hiyo tusimtafute kama vile tunacheza kamali maana mwisho wa siku ni majuto. Na vitu kama ushabiki na upenzi vinapaswa kuwekwa pembeni kama siyo mbali. Na hisia kama huruma ndiyo viwekwe mbali kabisaaaa.
Mimi nina imani kiongozi wa namna hiyo yupo ila anaweza hasijitokeze kwa sababu ya kuona uzito wa jukumu lenyewe la nafasi ya urais. Aina ya kiongozi huyo sisi ndio tunatakiwa tumfuate na kumsihii awe kiongozi wetu kwa sababu tuna imani kuwa yeye anaona sisi wengine kama siyo tuna chongo basi ni vipofu kabisaaa.
Ninasistiza tena hapo inatupasa kumchagua kiongozi anayeona. Tukimchagua kiongozi kipofu atatupeleka shimoni bila shaka.
Tuchague kiongozi anayethamani utu wa watu. Tusichague kiongozi anayependa sana mali kuliko watu. Tuchague kiongozi ambaye anatambua kuwa hapa duniani siyo makaazi yake ya kudumu anafanya kupita hivyo anaona haina haja ya kujilimbikizia mali binafsi sana kama walivyokuwa akina Mobutu Seseko kuku Wazabanga....
Kiongozi ambaye yupo tayari kupika majungu na fitina ila awe kiongozi huyo hatatufaa. Kwani ni lazima uwe rais? Hakuna kazi nyingine za kufanya?
Kiongozi anayetaka kazi ya urasi aje na mipango yake ya sasa, kesho na kesho kutwa. Tuiingalia sasa, kesho na kesho kutwa tunaiona ikibadirika sasa. Mipango ambayo akituelezea tushawishike kuwa inatekelezeka. Ntarudi tena baadaye....