KigaKoyo
JF-Expert Member
- Nov 14, 2019
- 273
- 1,926
Ladies and gentlemen, its me again. The creater of stories like “How I met my wife” na “Cheaters: the series”.
Nakuleteeni Goodness of fit. A story of love, blackmail, betrayal and politics. Pamoja na kua moderators wamekua wananyofoa nyuzi lakini naona mwaka huu wamelegeza kidogo na kutoa uhuru. Nawaomba kama wakiona kitu kinaenda sivyo wawasiliane na mwandishi ili aweze kuedit badala ya kuufuta.
So hii story itahusu maisha. Nimejaribu kuwaza katika jamii yetu mstari wa maadili uko wapi? Wengi wamekua wanapewa labels kama Malaya, wadangaji, mhuni, fisadi, muuaji lakin hao wanaoita wenzao hayo majina ukiwafuatilia maisha yao wanayaishi hayo wanayoyakemea japo kimya kimya. Na kwa wale wanaoitwa hivyo sometimes wanafanya hayo kwa sababu mbalimbali kama vile mapenzi yao kwa familia zao, wapenzi wao, imani zao au nchi yao.
Kwa wale wataalam wa statistics, goodness of fit ni mstari unaojaribu kuonesha wastani wa viwango katika population. Sasa ni kwa kiwango gani watu wanatoka katika huo mstari? je hao tunaodhani wanaishi katikati ya mstari huo wa goodness of fit, ki uhalisia wanauishi? Ni idea tu so ntakua naandika mojakwamoja kwa hiyo mtanisamehe kama ntakua nachapia.
I am sorry uwezo wangu ni one episode per week. Ikitokea nimepata fursa ntakua naweka surprise episodes katikati ya wiki.
Endelea..........
Episode 1: That man Tom
Siku hiyo nlikua nimechoka kinyama, unajua ile kuchoka hata kufungua kope za macho unaona uvivu eeh? yeah, that kind of tiredness. Nlijikuta nimejilaza tu kwenye kochi langu pekee lililokua hapa sebuleni. Ndani ya dera, simu mkononi ingawa hata sikua nampigia mtu bt just kuperuz page za social media.
Ilikua mida ya saa mbili hivi usiku, leo ilikua siku ndefu kweli, si mnajua shughuri za kuhama makazi zinavyochoshaga? Mvurugano na wasafirisha mizigo, kuzinguana na malipo ya wapandishaji na washushaji, kupotea potea kidogo na nini, full kuchoka yani.
Sikua hata nimepata nafasi ya kula cha jioni, so nikajiambia ngoja nipumzike kama nusu saa then nitaamka nitafute msosi,…. Loh! Nlikua najidanganya mwenyewe kumbe. Nimekuja stuka saa tano na robo usiku, of course sikujua muda wakati huo, mawazo yangu itakua between saa mbili na nusu na saa tatu, kumbe daah, nimepitiliza kinoma noma.
Nikajikokota hadi chumbani, nikavua dela nlilokua nimevaa, nikavaa zangu track suit, raba na kofia, vyote chapa Adidas. Sexy was my look, hahaha. Nikatoka. Ukimya uliokua nje ndo ulifanya nipate wasiwasi kidogo. Unajua ingawa giza ni lile lile, ila usiku wa saa mbili ni tofauti kabisa na usiku wasaa tano. Ukiniuliza tofauti yake wala hata sijui. Ila hisia ziliniambia kabisa em cheki saa kabla hujafika mbali.
Oh Oh…. Nlishtuka kwa sauti, na hiyo ndo hua namna yangu ya kushtuka, siitagi mamaa, wala kumtaja mtume, mi huwa ni short and clear ‘OH OH’. Nikawa nimesimama sasa najishauri niendelee na safari yangu ya kusaka chipsi mayai au nigeuze. Nikisema nigeuze ina maana ndo nalala njaa hivyo, maana leo ndo kwanza nlikua nimehamia makazi haya mapya, sina gesi, vyombo bado vipo kwenye mabox, na kiukweli hata kama hivyo nlivyovitaja ningekua navyo, nisingeweza kupika chochote maana hakukua hata na chochote cha kupikwa kiliwe.
Hii compound nilipohamia ilikua na three houses. Kuna hii nliyochukua mimi ambayo kwa muonekano ilikua ndo ndogo kuliko nyenzake mbili. Yaani ilikua na chumba kimoja na sebule. Ni self-contained ndiyo, ila jiko ndo uamue wewe, upikie sebuleni au chumbani. Lakini hata size ya vyumba ilikua ni ndogo hata kwa muonekano tu.
Nyumba zote tatu zilikua zimepangwa katika muundo wa herufi Z, yaani yangu ipo katikati, imeangaliana na moja iliyoko juu, na kuna nyingine kwa chini ambayo zimepeana mgongo kimshazari. Compound nzima ilizungukwa na ukuta mrefu ambao haukutoa nafasi wa nje kuona ndani wala sisi wa ndani kuona nje.
Shida moja ni kuwa, the compound ilikua mbali kidogo na mji. Hivyo pilikapilika za biashara na mizunguko ya watu vinaisha mapema sana. Na kwa ugeni wangu ingekua ni ngumu kuanza kuzurura alone kutafuta kijiwe cha baa ambapo wanaweza kuwa na msosi muda huu. Tofauti na nchi nyingine ambapo unaingia tu kwenye app ya simu unaagiza unachotaka, bongo ukiwa na njaa either upike au utoke. Na kama mjuavyo wasomaji, kwa msichana mrembo kama mimi, no, kwa msichana yeyote yule (maana wanaume hawaangalii sura sku hizi, as long as tundu unalo), Unless uwe unafahamu unapoenda, kwa kuuliza uliza tu watu usiowajua, utajikuta unabakwa.
So nikaona sina jinsi Zaidi ya kurudi ndani. Nikafunga mlango nikatafuta walau maji ya kunywa nilidanganye tumbo ili nisinzie, nikakuta chupa ya maji ya Kilimanjaro ambayo kimsingi yalikua yamebaki chini ya robo. Nikayagigida yoteee, then fasta nikavua nlichokua nimevaa, nikabaki na kichupi changu cheusi, nikaingia ndani ya duvet.
Kwani usingizi ulikuja sasa…… muda nao hata hauendi. Yaani harakati zote hizi nikajua itakua ishafika hata saa sita, kucheki muda bado saa tano na dakika kadhaa tu. Njaa nayo utadhani imeambiwa iongeze speed. Wakati mwingine hua nafikiri hii kitu inaitwa njaa ni just a state of mind hahaha, how comes inajua huyu mtu hana msosi ndani, maana kwa muumo huu hii njaa imeamua kunitesa kabisa.
Yaani, leo nisipodanja sijui. Ilipofika saa sita na robo, uzalendo ukanishinda. Nikavaa tena zile track suit, raba na kofia, nkatoka. Heri kufa kwa kubakwa walau watu watakusoma kwenye gazeti wakuonee huruma, kuliko kufa na njaa, watu watakutukana kwenye msiba wako. Kufika geti la kutoka nje moyo ukasita. Kubakwa kwa kweli hapana, yaani lidudu linipenye kabisa huko ndani pakiwa pakavu, tena machakani, gizani, no way. nikaanza kurudi tena, machozi yananilengalenga sasa.
Nilipofika usawa wa mlango wangu, kwa mbali nikawa nasikia movement kwenye nyumba ya jirani, either mtu anaflash toilet, au anaoga au anaosha vyombo, maana ni maji nayasikia yakitiririka. Nikasubiri hadi sauti ya maji ikatike, nikagonga mlango.
Wakati nashusha mizigo ile jioni, nliona mdada anaingia hapa. So nlijua atakuepo ndani, na naeza mueleza shida yangu akanisaidia. Wanawake huwa tuna huruma bana.
Ngo, ngo,ngo…. Nikagonga then nikasubiri. Nikaona kimya. Uoga wa kugonga tena ukanifanya nianze kuondoka. Bt ile nafika mlangoni kwangu, nikasikia mlango wa jirani unafunguliwa. Kwa matumaini makubwa ya kupata hata mkate nikarudi mlangoni kwa jirani nikiwa nimeandaa na tabasamu lile la kuomba kitu kwa mtu ambaye ndo mnakutana kwa mara ya pili tu, na mara ya kwanza mlipoonana hukumsalimia. Kufungua mlango nakutana na mwanaume, dah. Tabasamu nliloandaa likafutika ghafla, matumaini ya msosi yakapotea. Naanzaje kumuomba mkaka msosi?
“Mambo?”, akaniuliza kwa sauti kavu kama ya dada Halima wa viti maalum. Nilimjibu huku naona aibu. Kwanza alikua nusu uchi tuseme. Maana alikua kifua wazi na kipensi kifupi ambacho kinaweza tafsirika kama boxer tu “Poa…….., samahani, unaweza kuwa na namba ya dereva bodaboda anayewezakuwa macho muda huu anilitee hata chipsi?”, nlijikuta namuuliza huku macho nimeyaelekeza down. “Mhhhhhh…. Mtaa huu wanawahigi sana kulala hawa vijana, bt kuna mmoja mitaa ya Philips huwa anachelewa kulala, nipe dakika moja nimcheki”, alinijibu huku akiingia ndani kuchukua simu.
Nikapata wasaa wa kumcheki fresh sasa, he was good looking. Yaani kama nnavyopendaga… kaka ambaye kama ni mazoezi sio yale ya kupitiliza. Sipendagi wale misuli imevimba vimba kila sehemu kama viazi mbatata. Napenda mwanaume asiwe tipwatipwa sawa ila sio baunsa sasa, katikati pale, mmenipata eeh?. Yani awe soft kidogo bana, sio mkavu kama harmorapa, yani hata nikiwa napapasa kalio wakati unanila isiwe kama nashika jiwe, hahahah.
Baada ya dkk chache jirani akageuza. “sorry sistaa, jamaa hapokei simu, itakua naye kalala”. Alivyoniita hiyo sistaa, nikajua huyu ni chalii wa chuga, “usjali kaka yangu, siko vibaya kiviile, thanks sana kwa msaada”. “usjali” alijibu huku akifunga mlango.
Nimekaa kitandani usingizi hauji. Nikaona labda nipoteze maumivu kwa kuangalia movie. Nikafungua laptop yangu, nikaanza kucheki upya series ya ‘The Throne’, Ingawa nshaiona ila sikua tayari kuangalia movie mpya usiku huu, unaeza kuta inascenes za kutisha nikalazimika kwenda kumgongea mkaka wa watu kwa mara ya pili. Na ndugu msomaji nadhani unajua nikienda mara ya pili kitakachonikuta.
Movie ikiwa katikati nikasikia mlango kama unagongwa…. Ngo, ngo, ngo, nikawa kama sielewei, ni huu mlango wangu unagongwa au wa jirani, Ngo, ngo, ngo…. It was my door for sure. Kwanza nikaogopa. Nani anagonga usiku huu?, sikuitikia. Nlivyojiuliza ndo nikahisi pengine ni yule jirani, labda amempata bodaboda aliyekua hapokei simu, “ni mimi jirani” sauti yake ikanitoa wasiwasi zaidi, nikafungua kwa matumaini ya kupata solution ya hii njaa.
“Hey sorry kwa usumbufu, vipi ushapata mtu wa kukuletea msosi?”.. aliuliza huku akionekana pia hana mpango wa kuingia ndani. ‘hapana kaka yangu”, “okay subiri robo saa hivi”.
Nikamshukuru pale, maana najua atakua kapata mtu wa kumletea chips. Nikaingia ndani, nikachukua laptop yangu from bedroom, nikakaa kwenye sofa langu kusubiri chips huku nacheki movie. Baada kama ya dkk 20 hivi, nikasikia mlango umegongwa kidogo alafu kabla hata sijaitikia ukafunguliwa. kaka wa watu alikua kabeba sahani mkono mmoja, mkono mwingine umebeba glass ya juice. Nikainuka fasta kumpokea. “Thank you jamani”, nlimwambia huku nakiweka kwenye meza. “usjali bana, I hope unakulaga pilau”……. Alinijibu huku akitabasamu. “Yaani kwa njaa nliyonayo hata ungeleta nyoka ningekula aisee”, alijikuta anacheka kwa jibu langu.
nikakaa ila nikamkaribisha pia akae hata kidogo. Aisee kuna pilau tamu alafu kuna pilau tamu unayokutana nayo ukiwa na njaa ya kufa mtu…. That shit was delicious. “Naitwa Tom”, alijitambulisha huku akikaa pia pembeni yangu. “Mi Neema” nlijitambulisha pia huku nikitafuna mnofu mkubwa wa nyama ya mbuzi. “mgeni kabisa hapa Arusha? Au umehama mtaa tu”, aliniuliza huku macho yakikodolea movie pia. “Miezi mitatu imepita since nimekuja Arusha, ila nlikua naishi kwa rafiki yangu Sanawari”, nikamjibu huku naendelea kuinjoi pilau. Tukapiga stori kadhaa pale hadi namaliza kula.
Nimemaliza kula nikachukua sahani nikapeleka kwenye sinki. Nikarudi nikawa Napata juice ambayo kwa ladha ilikua ni mchanganyiko wa parachichi na passion. Akilini nlijua kabisa huyu jirani hawezi kuwa ameandaa this kind of msosi, nikakumbuka mchana nliona mdada anaingia pale kwake. Kutomuona yule dada muda huu kukanipa idea kuwa alikuja kuliwa tu akasepa, na itakua kabla ya kusepa alimuandalia boy wake misosi ambayo kwa bahati mbaya imeishia tumboni mwangu, yani kumbe a man can cheat you in so many ways.
“asante sana kaka yangu kwa chakula, leo sjui ningelala aje, nlikua na njaa ya hatari”, nlimwambia huku nikimalizia tone la mwisho wa ile juice. “usjali Neema, I’m glad nimeweza saidia, nlivokuona nlijua kabisa utakua unanjaa ya hatari, kama jirani sikua na namna zaidi ya kusaidia maana nlikua na chakula ambacho mdogo wangu alipika mchana”,
“Oh…….”, hiyo oh ilivonitoka nikajistukia inaeza sababisha yale mawazo yangu ya mwanzo yakawa revealed. “dada yako huishi nae hapa?” nikaendelea kwa kuuliza swali ambalo kimsingi halikua na maana. “No anasoma hapo chuo cha ufundi so anakaa hostel za chuo, bt mara nyingi weekends anakuja” alijibu huku akikodolea zaidi movie.
Tom alionekana yuko so taken na hiyo movie. Mi usingizi ndo ulikua umenijaa, kumfukuza siwezi, hata ungekua wewe ndugu msomaji, unamfukuzaje mtu aliyekusaidia msosi. Nlichofanya kwa kuwa yeye alikua amekaa kwenye stuli, mi nikajilaza pale kwenye sofa kama naangalia movie vile, bt lengo langu nlale palepale, akimaliza kucheki atagundua nimelala then asepe zake.
Nimekuja stuka saa nne asubuhi. Huwa nimeset alarm ya kuniamsha saa 12 na nusu asubuhi, lakini sijui hata ni kwa namna gani niliizima alarm ya simu ilivyoita muda huo. Niliamka pale kitandani kivivu na kwenda bathroom. Ni kama vile sikua nakumbuka vyema matukio ya siku iliyotangulia. Ile naoga ndo nikakumbuka sasa. Wait a minute!!!, jana nlilala kwenye sofa, how come nimeamkia kitandani.
Yani nlivokummbuka hii kitu nikamaliza kuoga fasta fasta zaidi ya siku nyingine, maana kwa kawaida mi hueza kaa bafuni saa zima, maji tu yakinimwagikia, I enjoy taking shower, like a lot. Basi nikajikausha maji pale nikaenda sebuleni, eti nachungulia kwanza isijekua Tom bado yupo hahaha. Nlivohakikisha safe ndo nikaenda sitting room, nikacheki laptop nikakuta imezimwa na kufungwa fresh mezani. Inamaana jamaa alinibeba kunileta bed usiku…. Ikabidi niwaze nlikua nimevaaje nliposinzia na nimeamkaje leo. Nikashusha pumzi ya ahueni, maana nlisinzia na dera na nimeamka nalo.
I didn’t know what to think of Tom, to be honest, sikutaka kabisa kufikiria abt any man. The last man to give my heart and body to, ended up to be an asshole. (ila haya matusi kwa Kiswahili nisingeweza yaandika mazee, eti asshole duh). The guy was called Danny. I loved than man, for real yani, nikaanza hadi kufikiria watoto wetu watafananaje. Unajua nlimpenda Danny hadi nikawa tayari kugive up all my dreams and ambitions.
Kampuni ninayofanya kazi ni kampuni ya mawasiliano ya simu. Niliajiriwaga mara tu baada ya kumaliza chuo, nashukuru Mungu jitihada zangu za kazi zimenipandisha hadi kuwa marketing manager wa zone hii ya kaskazini. Malengo yangu ni kupanda hadi kuwa CEO, yeah, why not, am still young and I work hard kwa kweli. Kila ninapopelekwa naleta matokeo chanya, jitihada zangu zimepandisha kampuni yangu hadi kuwa namba mbili nchini, kutoka kwenye namba sita huko chini. So mapenzi yangu kwa Danny nlikua radhi nipige chini vyote hivi kwa ajili yake, yani niwe mama wa nyumbani, ilibaki yeye tu kusema su!!
Nilikua kwenye mahusiano na Danny kwa miaka miwili mizima, imagine. Then ghafla tu kama mshumaa, yakazima. Yani wanaume. Muda wote yupo na mm kumbe ni mume wa mtu. Yani, siku najua I swear I tried to commit suicide. Namshukuru Mungu maana maumivu yaliisha, kilichobaki labda ni ile hali ya kutojiamini. Pamoja na uzuri nlionao, lakini naona kama vile sitakaa nimvutie mwanaume serious wa kunioa, hua nahisi kama vile ntaishia kuwa mlezi wa wana vilee. Wakati huo mdogo wangu Rehema aliolewa mapema kabisa, baada tu ya kumaliza chuo. Nimebaki nungayembe nahakaika, gadammit!!!
Nimekaa mle ndani nikiwa na plan ya kutoka mida ya saa tano, ili nikapate Brunch alafu pia nipitie mazagazaga ya kuniwezesha kupika. Saa tatu na nusu nasikia hodi tena. This time wala sikuwa na shaka, atakua tu Tom, mkaka jirani. Na kweli baada ya kumfungulia nikakuta ni yeye. What he brought kilifanya moyo wangu uyeyuke. The guy brought chapati, supu na thermos ambayo nliona kabisa imebeba maziwa (maana kuna vitone vilikua vinaonekana kwenye kifuniko chake), vyote akiwa ameviweka kwenye kibao. Nikajaribu kumpokea, akanikatalia kwa kichwa kwa akiogopa kuwa ntasababisha ajali, basi akavibalance fresh akatembea kama ananyata, mi nimemshikia mlango asijigonge, akaingia, akaviweka pale mezani.
Jamani, this gesture was too much. Sema nlijizuia tu, ila nlitamani nikamhug kwa shukrani. “jamani Tom, you shouldn’t”, Tom akatabasam kasha akasema, “enjoy jirani, huduma kama hizi unapewa siku ya kwanza tu ukihamia, baada ya hapo usitarajie huduma za aina hii”. Uzuri wa Tom, aliyafanya haya yote na ukimuangalia usoni unaona kabisa huyu hafanyi kwa kutarajia kitu, he is doing it kwa nia ya kusaidia kwa dhati, no hidden agenda. Kwa mara ya pili nikatamani nimkumbatie. Yani vitu vinavyotutekaga wadada mpaka hua najiuliza sjui tumerogwa, imagine…. Eti supu na chapatti vinaniyeyusha moyo.
Nakumbuka that day baada ya breakfast, tulikaa tunacheki tu series ya jana yake, alionekana kuipenda kinoma. Mi nlishaiona bt sikuonesha kama naijua ili nisimkatishe mood yake. “Tom I have to go to town kununua some things…” nlimwambia nikijiandaa kunyanyuka pale nilipo. “hata mm ntaenda town baadae, unaoneje tukapika cha mchana kwanza then tutoke wote kwenye saa kumi…”, well sikua na haraka sana ya kwenda huko town, lakini pia Tom amenipa kampani sana tangu jana, nisingeweza kumkatalia. So tukahamia home kwake ili tukapike.
His house was well organized. Too organized for a man of course, nikajua itakua yule mdogo wake anakujaga marakwamara. Tukawa tumekubaliana tupike chips mayai. Nlichofanya nikamwambia anioneshe tu where everything is at ili nipike mwenyewe. Na kwa kweli sikumlet down. Alinisifia chakula kitam alivoonja tu kijiko kimoja.
Mpaka kufika muda wa kutoka hiyo saa kumi tulikua tumeshazoeana utafikiri ni ndugu. Nishajua anabiashara zake Dodoma ambazo anajaribu kuzi establish. Ila kwa Arusha anabiashara za maduka ya vifaa vya nyumbani mawili, sakina na Moshono. Kwa namna anavyoongea anaonekana kabisa ana vision alafu deep down anaonekana kama ana ule ubinadam ambao ni nadra sana kuuona karne hii.
Wakati wa kutoka nikapiga zangu tshirt na skirt flani ya jeans (mi sio mtu wa suruali sana mchana) then tukaingia kwenye gari yake tukasepa. Well, ilikua kama a date, maana hatukuishia kufanya shopping ya mazaga ya kupika, tulienda kupata dinner maeneo ya milestone, mbuzi choma moja matata sana, then akanipeleka standup comedy flani pale Golden Crest hotel. I really enjoyed. Na kilichofanya ni injoi zaidi nadhani ni ile hali ya kutohisi labda jamaa ananitaka, nlikua free kabisa yani, sikufungwa na mawazo hayo negative.
Njia nzima wakati tunarudi tukawa tunakumbushana vituko vya Mr Beneficial alivyovitoa kwenye ile standup comedy, basi tunacheka wenyewe, utadhani tumejuana kitambo. Mpaka tunaingia kwenye compound yetu, nlikua nimeinjoi mno kwa kweli. Akanisaidia kushusha mizigo yangu kwenye gari, akaiweka yale maeneo nlikua nimepanga niwe napikia. Mi nikawa pale mlangoni, a little bit tipsy, maana nlishusha glasses kadhaa za wine pale Golden Crest.
Wakati anatoka Tom si akawa anapita pale mlangoni, mlango ni mdogo so obviosly tukagusana kiaina, alivo hajielewi eti akapita tu, kabisa akaniacha nimesimama tu mlangoni, ikanidi nimuite, “hey……..” akasimama na kunigeukia, alikua ashaenda umbali mrefu amekaribia kabisa mlango wa kuingia kwake, haya kumuita nimemuita, namwambia nn sasa hahahah, then kwa aibu aibu za kike nikajikuta namwambia, “Thanks for today………. And yesterday……….. oh, and this morning too”, Tom akatabasam pale, “my pleasure” then akafungua mlango wake akaingia kwake. Shit!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
I know me ndugu wasomaji, ingawa hata akili yangu ilikua haijagundua bado, lakini nlikua radhi Tom alale na mm that day. Mawazo haya yakaanza nifanya nijihisi kama kamalaya flani hivi, ntafikiriaje like this, mimi Neema, nliyelelewa kwenye familia ya kichungaji naanzaje kufikiria kuliwa na mtu nliyeonana nae just masaa machache tu yamepita. Nikaenda kuoga, nlipomaliza nikavaa zangu night dress nikazama bed.
Cha ajabu pamoja na kujizodoa, bado mawazo yangu ya kijinga yakawa yanazunguka. What if Tom ameoa?, nlipowaza haya nikakumbuka yule shwaini Danny basi nikaishia kujiaminisha almost all men are the same, so I shouldn’t trust any of them, Tom included.
Kesho yake ilikua ni jumatatu, kwa sisi waajiriwa ilipaswa tuamke mapema kwenda kutimiza majukum ya mwajiri. So nlikua nimeamka mapema, kama kawaida, mda mrefu bafuni nikiimba kwa sauti ya chini huku maji ya moto yakinitiririkia mwilini. Baada ya kujiweka safi, I had my simple breakfast, coffee and eggs kasha nikatoka.
Ile nafunga mlango, namuona Tom akifungua mlango wake. “Ndo unaenda job Ney?”, “yap, si unajua kazi zetu waajiriwa”, “naelewa, let me drive you, maana nataka nikapitie vijiwe vyangu nione kama kila kitu kipo sawa”, well, it was kind of him kuoffer lift, na kwa namna nlivyo muangalia hakua anaenda kwenye biashara zake wala nini, alionekana ndo kwanza ameamka. Bt sikutaka kumshushua, kwa kua amesema anatoka pia, mi sikua na namna zaidi ya kukubali.Njia nzima stori, Tom was funny kiasi chake, na pia alikua muongeaji, which was perfect kwangu maana mi ni mkimya kiaina. Safari ikawa fupi kwa stori zake za kufurahisha.
Weekend njema...
Kiga