MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

Huku kwetu Pwani hali hiyo tunaiita Schizophrenia

Nimekutana na haya maneno hapa chini....

Schizophrenia is a mental disorder characterized by disintegration of thought processes and of emotional responsiveness. It most commonly manifests itself as auditory hallucinations, paranoid or bizarre delusions, or disorganized speech and thinking, and it is accompanied by significant social or occupational dysfunction. The onset of symptoms typically occurs in young adulthood, with a global lifetime prevalence of about 0.3–0.7%.Diagnosis is based on observed behavior and the patient's reported experiences.

Source: Schizophrenia - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Hehehe kwa hiyo mapepo yamewaingia asilimia 30 ya vijana wa vijijini Brazil?!

Mimi sijui ila nilichosoma na kufahamu, huku uswahilini tunasema kuwa, "wana tabia mbaya" hadi wanaamua kubaka wanyama...tena hata kuku jamani!!
 
Mimi sijui ila nilichosoma na kufahamu, huku uswahilini tunasema kuwa, "wana tabia mbaya" hadi wanaamua kubaka wanyama...tena hata kuku jamani!!

Nami ni mmoja wa hao Waswahili. Hawana mapepo, staarehe zao tu zimewatuma hivyo
 
Acha tu mambo ya jinsia,

Kwanza huyo anayemwita Mungu ni nani??? Yule Rais wa nchi kubwa kubwa ambaye baba yake alizaliwa kwenye mazizi ya ng'ombe au mzee wa Mabwabwa!!!???

Hahahaha babu sasa unatupeleka kwenye mjadala wa mapunga sasa
 
Acha tu mambo ya jinsia,

Kwanza huyo anayemwita Mungu ni nani??? Yule Rais wa nchi kubwa kubwa ambaye baba yake alizaliwa kwenye mazizi ya ng'ombe au mzee wa Mabwabwa!!!???

Kwani Mungu anabadilika kutokana na anaemwita? :]
 
Okay let's leave maandiko aside.

Let's go with logic and science

1. God is loving to both females and males equally, why would He make females with demons?

2. Science talks about hysterics and depression. Are females prone to these then males?

Logic will take u from point A to B, imaginations will take you anywhere
 
Hivi hujui kwamba kuna watu hawana idea kabisa kama kuna Mungu?

Nawajua kuwa wapo tele.

Lakini nimeshangaa kuwa unamdefine Mungu kwa kuzingatia misimamo binafsi ya kimaisha ya wanaomzungumzia Mungu

Anyway, tuendelee na mapepo.
 
Nawajua kuwa wapo tele.

Lakini nimeshangaa kuwa unamdefine Mungu kwa kuzingatia misimamo binafsi ya kimaisha ya wanaomzungumzia Mungu

Anyway, tuendelee na mapepo.

Hapana Gee,

Nilitaka kuwastua wale wanaodhani kuwa kila mtu anaamini uwepo wa Mungu...Sina hakika wale wanaoamini kama Mungu yupo kama wana stratification criteria wanazotumia kumwelezea Mungu wao na kama zinabadilika kutegemeana na nyakati.

Kuhusu mapepo bwana nalo ni jambo tata sana!
 
Hebu tufafanulie kidogo

Though Albert Einstein alisema " Science without religion is lame and religion without science is blind" bado hapa tunazungumza kutoka background totauti kabisa.
  • Kuna mwanasayansi asiyeamini Mungu ana argument zake kutokana na uelewa wake.
  • Kuna mwamini Mungu anayeamini kuna majini/mashetani na kadhalika ambayo ni associated na damu na siku za mwanamke kiasi kwamba haruhusiwi hata kushiriki baadhi ya ibada aka NAJISI
  • Kuna wanaoamini Mungu ambao wanaamini kimtokacho mtu kinywani ndio kimtiacho najisi, mwanamke aliyetengwa kwa miaka 14 hadi kuja ponywa na Yesu/
Kwa hiyo ni watu watatu wenye arguments based of on background hatuwezi fikia muafaka kirahisi hivi. Ni kama kulinganisha utamu wa embe na nyama. Tunatakiwa kulinganisha nyama kwa nyama, embe kwa embe ndo muafaka utafikiwa.

Umeshawahi ona mijadala ya dini pale daraja la manzese? Huwa haina muafaka. Lasy week mijadala ya background tofauti imesababisha vurugu ambazo hata hazieleweki mwanzo na mwisho ulikwa nini.
 
Kongosho,
Sidhani kama mijadala ya JF huwa na kufikiana muafaka kikawaida. Tunachojaribu ni kuelezea misimamo tu ya kila upande (kwa ushahidi ikiwezekana) ili hayo magurupu matatu (au chini ya hapo au zaidi ya hapo kwa wakati mwengine) waweze kuelewa msimamo wa wengine.

Si lazima kwangu kuamini vitabu kuweza kuelewa kuwa watu wengine wanaamini mwanamke ana mapepo kwa sababu vitabu wanavyovifuata vimeandika hivyo.

Hii naamini itatusaidia kufungua wigo ya kufikiri na kuelewana ndani ya jamii.

Mwenye ushahidi wa kimaandiko ya kuwa wanawake wanamapepo naomba anipatie (japo kuwa mimi siamini hayo maandiko yake)
 
...2. Science talks about hysterics and depression. Are females prone to these then males?
Kwa sehemu kubwa hayo ambayo watu wengi wanaita (tunayaita) mapepo ni matatizo tu ya akili...sasa mara nyingi watu tukishindwa kuelezea tatizo fulani tunaishia kusema mapepo...na kama ni kitu kizuri tutasema miujiza (hata kama sio miujiza kwa maana yake hasa!).

Wataalamu wamegundua kuwa kuna tofauti ya namna ubongo wa mwanaume na mwanamke ulivyoumbwa (structured) na hivyo jinsia hizi mbili ku react kwa namna tofautii katika matukio au stimuli. Kwa jinsi ubongo wao ulivyoumbwa uwezekano wa wanawake kupata mood disorders (depression, anxiety etc) ni mkubwa zaidi kuliko wanaume.
 
Kwa sehemu kubwa hayo ambayo watu wengi wanaita (tunayaita) mapepo ni matatizo tu ya akili...sasa mara nyingi watu tukishindwa kushindwa kuelezea tatizo fulani tunaishia kusema mapepo kama ni kitu kizuri tutasema miujiza (hata kama sio miujiza kwa maana yake hasa!). Wataalamu wamegundua kuwa kuna tofauti ya namna ubongo wa mwanaume na mwanamke ulivyoumbwa (structured) na hivyo jinsia hizi mbili ku react kwa namna tofautii katika matukio au stimuli. Kwa jinsi ubongo wao ulivyoumbwa uwezekano wa wanawake kupata mood disorders (depression, anxiety etc) ni mkubwa zaidi kuliko wanaume.

Hapo umegonga bingo mkuu

Mantiki inyotumika kusema wanawake wana mapepo ni ile ile inapotokea ajali watu wakasema "kazi ya Mungu"

Hatujaribu kutafuta chanzo wala solutions, tunakimbilia kwenye supernaturals tu
 
Afadhali wewe mwenzangu unasubiri ushahidi wa kimaandiko.....mie nilidhani kuwa kuna watu wanatuletea empirical data zinazotokana na utafiti wa kisayansi...

Mbado kuona...Labda Teamo atatembelea search engines kadha wa kadha ili atusaidie!

Mimi ushahidi wa kisayansi wa kuwa wanawake wana mapepo zaidi nimeshaukatia tamaa, kwa hiyo nimebaki wa kiimani zaidi. Ila nao hata huo haujitokezi ukinipa shaka kuwa labda hawa watu wanazizulia tu hizi dini zao hazijasema hivyo
 
Sio kweli kwa kuwa hilo halijawahi kusemwa na mungu wakati wa uumbaji wa viumbe, nadhani hata wewe umezaliwa na mwanamke
 
Back
Top Bottom