Tujadili viumbe walioumbwa kwa moto na upepo ambapo humo tunapata Malaika, majini, vibwengo, shetani wana maumbo au hadaa zetu tu?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Habari wakuu.

Leo nimeona nilete kwenu hii hoja kwa mfumo wa swali. Kama nililivyoliweka hapo kwenye heading kuhusu taswira au umbo lionekanalo kwa macho pale inavyowezekana, hawa viumbe ambao tunaaminishwa kupitia imani zetu kwamba wameumbwa kwa moto na upepo wanabeba taswira gani?

Upepo sote tunaufehemu kwamba hauna umbo linaloonekana bali tunauona ukileta matokeo ambayo ni kutikisa ama kuhamisha vitu vinavyoonekana pale unapovipitia. Pia moto tunauona kwa macho ingawa tunasema hauna umbo maalumu wala haushikiki bali nao unapimwa kwa matokeo unayoyaacha kwa mguso ama kuvipitia.

Viumbe ninavyoviongelea, havijawahi kuwa dhahiri kwenye macho yetu kwenye ukawaida wa maisha yetu. Lakini tumekuwa katika kuamini na kujenga taswira ya namna muonekano wa viumbo hivyo vinavyotawala ulimwengu usioonekana. Ingawa kwenye kujenga taswira hizo tumeshuhudia itikadi za nyeupe ni utukufu na nyeusi ni uovu na laana ikipewa kipaumbele.

Kabla sijaendelea, napenda kuuliza jukwaa. KUNA AWAYE YEYOTE AMESHAWAHI KUONA MALAIKA AMA MAJINI? Je unaweza kushare nasi nini ulichoona? (Mimi nimewahi kuona majini na viumbe wengine) lakini kwa kuwa naandika uzi huu napenda kupata ushuhuda wa kutoka kwa wasomaji wengine. Kwenye uzi huu mbeleni nitachangia nini nilichokiona.

Tuendelee sasa.
Ufunuo wa Yohana 4: 6 anaelezea uwepo wa Wenye UHAI wanne. je ni kina nani hao na kama kuna ufafanuzi wa umbo lao ukoje?

Je, tunawezaje kumtofautisha Malaika kutoka kwa Kerubi? Tunamtambuaje Kerubi akiwa amesimama na Serafi? Je jini tunalitofautishaje na mapepo? Shetani na majini wana tofauti gani? Kama jini na mapepo na mashetani wanaweza kukaa ndani ya mtu, je malaika na jamii zao wanaweza pia kukaa ndani ya mtu?

Je viumbe hao wapo au ni illusions zetu wanadamu? Narejea taswira zilizochorwa na akina Michellangelo, Da Vinci, Raphael na wengine enzi za rennainsance?

Karibuni tukate maneno
 
Wazee 24
220px-The_Four_and_Twenty_Elders_(William_Blake).jpg
 
Majini ni ya kiislamu

Mapepo ni ya kikristo

Kuhusu aina za malaika, Kuna nadharia mbalimbali, ila ninachojua wanapangwa kulingana na ukaribu wao na kiti cha enzi....

Mapepo yanaweza kuvaa mtu, kuna ushahidi kwenye bibilia.
Hakuna mahali malaika amemvaa mtu kwahiyo tutahitimisha hawawezi.

Hivi viumbe ni hadithi kwasababu, utaviona endapo unaamini kwenye uwepo wao.

Utasikia sana wakristo wakisema wameona malaika, hutowasikia waislamu.

Wazungu watasema wamemuona bigfoot, watz watasema wameona kibwengo.

Nimekosa neno la kiswahili hili jambo linaitwa indoctrination.
 
Hakuna mapepo ya kikristo!
Kristo yupo kinyume na Shetani na ndugu zake wote wakiwemo mapepo na majini.

Malaika hamvai mtu lakini anaweza kutokea watu na kuwapa ujumbe sanasana kwenye ndoto.
 
Hakuna mapepo ya kikristo!
Kristo yupo kinyume na Shetani na ndugu zake wote wakiwemo mapepo na majini.

Malaika hamvai mtu lakini anaweza kutokea watu na kuwapa ujumbe sanasana kwenye ndoto.
Namaanisha yaani mapepo yanatajwa kwenye bibilia tu

Majini yanatajwa kwenye Quran tu

Na hili ni tatizo kubwa wakristo wamechanganya mafile hamna adui yao aliyetajwa kwenye bibilia kwa jna la 'jini'

jini ni adui wa waislamu tu wanawaita 'jinn' kama sikosei

hivyo vingine umepatia
 
biblia gani haijataja majini?...majini ndo mapepo ndo mashetani hakuna jini mwema hata mu1 kwa mjibu wa biblia na wote hao ni malaika walioasi mbiguni......na kiongozi wao mkuu ni ibilisi yaan shetani...ambaye hapo kabla alikuwa lucifer ....biblia inamsema kuwa alikuwa mzuri kupita wote miongoni mwa walioumbwa ......video za siku hzi zinamtoa ana mapembe tena mwafrica daah....afu kisha yesu yule actor mlevi wa italy wanamtoa mzungu wakiamini ni Yesu kabisaa...... kwa mujibu wa quruani tukufu inasema kuna majini wabaya na wazuri...na ya kwamba majini mazur yanaswali tena yalisikia adhana yakasema tumesikia adhana ya ajabu ya mnyaaz ...daah mauzauza sjui nimeandika utumbo gan.
 
Attachments

  • Screenshot_20240318-120428_Biblia.jpg
    Screenshot_20240318-120428_Biblia.jpg
    523.9 KB · Views: 12
  • Screenshot_20240318-120545_Biblia.jpg
    Screenshot_20240318-120545_Biblia.jpg
    527.3 KB · Views: 7
biblia gani haijataja majini?...majini ndo mapepo ndo mashetani hakuna jini mwema hata mu1 kwa mjibu wa biblia na wote hao ni malaika walioasi mbiguni......na kiongozi wao mkuu ni ibilisi yaan shetani...ambaye hapo kabla alikuwa lucifer ....biblia inamsema kuwa alikuwa mzuri kupita wote miongoni mwa walioumbwa ......video za siku hzi zinamtoa ana mapembe tena mwafrica daah....afu kisha yesu yule actor mlevi wa italy wanamtoa mzungu wakiamini ni Yesu kabisaa...... kwa mujibu wa quruani tukufu inasema kuna majini wabaya na wazuri...na ya kwamba majini mazur yanaswali tena yalisikia adhana yakasema tumesikia adhana ya ajabu ya mnyaaz ...daah mauzauza sjui nimeandika utumbo gan.
eti Lucifer muafrika😂

kuna utata kwenye neno 'jini'

ukisoma bibilia za kiingereza zinatumia maneno 'demons' na 'devils'

hilo neno 'jini' limetolewa kwenye lugha ya kiarabu, kutokana na neno 'jinn'/'djinn'

kwahiyo nakubaliana na wewe, ila kwa sharti kwamba hilo neno lina utata
 
Namaanisha yaani mapepo yanatajwa kwenye bibilia tu

Majini yanatajwa kwenye Quran tu

Na hili ni tatizo kubwa wakristo wamechanganya mafile hamna adui yao aliyetajwa kwenye bibilia kwa jna la 'jini'

jini ni adui wa waislamu tu wanawaita 'jinn' kama sikosei

hivyo vingine umepatia
Waislam marafiki zao ni majini na ndio maana wanayabembeleza,
Adui hachekewi
 
Well.... onaa;

Jibu fupi: Jini, malaika, pepo, mzimu au kibwengo huonekana katika sura inayolingana na itikadi na tabia yake kuu yaani 'personality'. (Full stop). Na maranyingine taswira hutokana na mtu binafsi anavyoichukulia tabia fulani ipojepoje kimuonekano🤔

Haiya twende sawa: kama ambavyo wanyama huchukua maumbo na sura kulingana na tabia zao kuu basi vivyo hivyo na roho za viumbe huchukua tabia zao kuu.

Sie wanabaiolojia, tukiona mnyama amekenua na meno yake mengi ni bapa, tunajua huyu anakula na kusaga majani. Na tukimuona ana meno yamechongoka basi tunajua anakula na kurarua nyama.

Na kwa sie wanabaiolojia tunaokubaliana na Lamark tunasema: mnyama huyo alianza kwa kuwa na tabia husika (mfano kupenda kula nyama sana) na mwishowe sura umbo lake limekuwa na ukali husika.

Muda mwingine wadudu hutumia mbinu ya kuvaa sura za wanyama wakali ili nao pia waogopwe maana kipepeo akionesha urembo kama macho ya bundi, wawindaji wake watamuogopa kwa kuhisi naye pia ni mkali kama bundi.

Sasa mabadiliko ya kibaiolojia huchukua miaka miiiiiigi sana, mamilioni kuweza kutokeza sura husika. Na kwa wanadamu huchukua miaka kadhaa; Lakini kiroho inaweza kuwa hapohapo 'instantly' mfano jini mpole akikasirika hapohapo anabadilika kutoka barafu na 'ac' na anakuwa moto na 'fireplace'. Na ukimuomba msamaha anabadilika ghafla yaani kulingana na tabia inayo'trendi' muda huo.

Mfano mtu akianza leo tabia ya ukali, itachukua si chini ya miezi sita kumiliki ndita. Na kila atakayemuona 'instantly' atajua kuwa ni mkali. Vivyo hivyo mwenye kuanza tabia ya kutabasamu au kufyonza (dharau) itachukua muda kabla hajaanza kuvaa sura ya tabia yake..

Kwa wanadamu kubadilika, ushahidi wa jambo hili ni wanandoa wanaofanana baada ya muda. Sababu kuu ni wao kuanza kuigana tabia zao hivyo mwishoni wanavaa sura zenye muelekeo mmoja. 'Hence' kuanza kufanana sura na maumbo🤗.

Haiya turudi sasa kwenye hao walioumbwa kwa upepo, sijui moto. Niseme tu viumbe ambao sisi huhusiana nao kiroho zaidi:

Hawa viumbe huwa na hisi yaani 'feel' inayoendana na tabia ya msingi ya roho zao;
-Kama kiumbe ni mkali 'sura-hisia' yake itakuwa labda na rangi nyekundu-njano hivi kuendana endana na moto.
-Kama kiumbe huyo ni mpole basi utakapo'interact' naye utamuona sura-hisi yake kiupande wa rangi kuendana na ubuluu, nyeupe na hata nyeusi flani tulivu hivi(kwa maana ya kijivu kijivu).

Hiyo mifano miwili imeongelea rangi, lakini unaweza kuweka sifa yoyote ile kulingana na tabia kuu na tena (here is the catch). Umbile mida mwingine litaendana na wewe binafsi rohoni mwako unavyoamini sura/umbile fulani lina maana gani.

Mfano anayeamini kuwa aliyeridhika anakuwa na mwili mdogo. Basi atamuona jini/pepo/mzimu mwenye tabia ya kuridhika kuwa na umbo dogo lakini kama mtu huyo anaamini kiwa mwenye umbo dogo ni yle asiyeridhika(hana shukurani) basi jini/mzimu/pepo huyohuyo yeye atamuona kuwa na mwili mnene kiasi. It is personal, it is sometimes a subjective experience.

Kwa hiyo hao viumbe huonekana kwa tabia zao kuu.
1. Anayependa kuelekeza kwa amri utamuona atafanana na taswira ya jemedari unayoijua.
2. Muongo muongo atafanana na taswira ya muongo ulonayo rohoni.
3. Anayependa kutishia watu basi atatokea na taswira ya kutisha iliyopo kichwani kwako.

Jini mzuri ataonekana katika sura ya dragon huko China, wakati huohuo jini mbaya ataonekana kwa sura ya Dragon huko Marekani
 
eti Lucifer muafrika😂

kuna utata kwenye neno 'jini'

ukisoma bibilia za kiingereza zinatumia maneno 'demons' na 'devils'

hilo neno 'jini' limetolewa kwenye lugha ya kiarabu, kutokana na neno 'jinn'/'djinn'

kwahiyo nakubaliana na wewe, ila kwa sharti kwamba hilo neno lina utata
Mkuu
Ingawa naona wengi wa wachangiaji wamejitahidi kuelezea uelewa wao na hakika wameishia kutaja nasaba ama aina za hao viumbe wasioonekana ingawa tunajulishwa kwamba wapo.

Hebu tujiulize kidogo ama tutafakari kwa nukta chache. Watu wengi tumeshuhudia baadhi ya matukio yanayoitwa kupandisha majini. Kuna jina wanalitumia kwa mtu ambaye anasadikika kuwa ana majini, anaitwa KITI. Na tumeona ama kusikia kuhusu matukio haya na kwa walioshuhudia kwa macho (nikiwemo mimi) wanaweza kuthibitisha kuwa hali fulani isiyo ya kawaida inamkumba mtu ambaye hajawahi kuwa na historia ya tatizo la akili wala ufahamu, na mtu huyo anazungumza maneno ambayo watu wengi husema ni jini ama majini yaliyomkalia mtu huyo ndiyo yanazungumza. Imetukia wakati mwingine jini ndani ya mtu linawasiliana nawe mwenye ufahamu kamili na kukuelezea matukio hususan mabaya uliyoyafanya wakati uliopita... kama vile uzinzi, wizi na kadhalika...

Hali hii tunaiitaje na nini kinatuthibitishia kuwa huyo mtu ana majini na hayo majini yapoje haswa?
 
Faith is the practice of training the mind to ignore facts, evidences and logic. Hakuna ushaidi ya kuwepo kwa viumbe hivyo. Ni ubongo wako tu ukichanganywa au kiuchanganyikiwa ndo utafikiri hao viumbe wapo.
Absolutely true
 
Majini ni ya kiislamu

Mapepo ni ya kikristo

Kuhusu aina za malaika, Kuna nadharia mbalimbali, ila ninachojua wanapangwa kulingana na ukaribu wao na kiti cha enzi....

Mapepo yanaweza kuvaa mtu, kuna ushahidi kwenye bibilia.
Hakuna mahali malaika amemvaa mtu kwahiyo tutahitimisha hawawezi.

Hivi viumbe ni hadithi kwasababu, utaviona endapo unaamini kwenye uwepo wao.

Utasikia sana wakristo wakisema wameona malaika, hutowasikia waislamu.

Wazungu watasema wamemuona bigfoot, watz watasema wameona kibwengo.

Nimekosa neno la kiswahili hili jambo linaitwa indoctrination.
Hili Jibu lako ligongolewe Msumari na liwekwe sebuleni kabisa kama pambo..
🤝🤝🤝👏👏👏👏
 
Back
Top Bottom