MJADALA: Je, ni kwa namna gani YouTube humlipa mmiliki wa account?

srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
3,792
2,998
1587400059593.png

MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU MADA HII
Habari ndugu zangi ,
Kama kichwa kinavyouliza hapo , ningependa kujua ni kwa namna gani kupata subscribers wengi na viewers wengi kwenye you tube , kunaweza kukunufaisha mmiliki...

Tafadhali kama kuna mwenye majibu , ushuhuda, uzoefu au elimu yoyote kwenye hili anijuze na mchanganuo mzima.

Natanguliza shukran zangu za dhati kabisa.
---
Wakuu, naomba msaada nimesumbuka na hili swali muda sasa. Hivi msanii anapoweka video YOUTUBE anipigia promo hili watu waitazame hivi anapataga faida gani?

Je, huwa anaingiza pesa?? kama anaingiza ni kwa jinsi gani?

Je, kama anaingiza nini kinaonesha kuwa anastahili kulipwa?

Je, kama analipwa analipwa na nani na kwa jinsi gani?

Kama zinamuinguzia hela kupitia Viewers je ni idadi gani inahitajika au wanamcalculateje?
WAKUU NAOMBA MSAADA KWA WANAO FAHAMU.
---
Habari ndugu zangu mimi Nina channel ya YouTube lakini ninahitaji masaada mnielekeze au mnifundishe jinsi channel yangu kuwa online. Natanguliza shukurani

BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU
Ipo hivi, Pesa zinalipwa huko youtube kwa sababu ya matangazo, Narudia tena "MATANGAZO", mimi, wewe na makampuni makubwa iwapo tuna huduma au bidhaa tunazotaka zitangazwe tunaweza kutangaza kupitia Youtube ili bidhaa zetu zijulikane na watumiaji wa youtube.

Tukipeleka Tangazo letu youtube, Itabidi youtube tumlipe ili tangazo letu liwafikie watumiaji wa youtube.

Youtube yeye kama yeye ni kampuni tu inayoturuhusu kupandisha video, Video zinazowekwa youtube sio za youtube bali ni za wasanii, waandishi wahabari, n.k youtube hawezi kufanya chochote kwenye hizo video.

Sasa youtube tunapompa fedha atutangazie biashara zetu mimi na wewe kwa watumiaji wa youtube ina maana ya kwamba watumiaji wayaone matangazo hayo wanapotizama video za youtube

Youtube hawezi kuweka tu tangazo kwenye video za watu, Inabidi aombe ruksa ya kufanya hicho kitu kwa wasanii kama kina Diamond platnumz.

Sasa tuchukulie kwamba ndio youtube na diamond wanongea, mawasiliano yapo hivi (ni mfano tu, Diamond katumika kama mfano):,

Youtube: " Bwana diamond, kuna kampuni inaitwa jamiiforums wametengeneza app yao, wametupa tangazo lao tuwatangazie youtube liwafikie watanzania, sasa bwana Diamond tunaomba ruksa yako tuweke tangazo la jamiiforums liwe linaonekana kabla video yako haijaanza kucheza ama pembezoni, We unasemaje?"

Daimond: "Sawa, nimekuelewa Bwana youtube, matanmgazo yao nikiyaruhusu yaonekane kwenye video zangu basi itabidi na mimi mnilipe kiasi kadhaa kwenye hio pesa mliopewa,"

Youtube: "Ondoa shaka, wala usihofu kijana, wewe utachukua asilimia 55 na mimi ntabaki na asilimia 45, kwa hio kama jamiiforums walitulipa kwa kigezo cha elf 5 kwa kila watu elf 1 wataoliona tangazo wakicheki video yako wewe utachukua 2,750 na sisi tutabaki na 2,250"

Basi ndio mkataba huo unaanza kutekelezwa hapo ndipo unapoendaga kutazama video za wasanii huko youtube unakumbana na aina ya matangazo yale ambayo yanaanza kucheza kabla video uliyotaka kuicheki haijaanza na kuna kitufe cha kuruka tangazo (skip ad) ama aina nyingine ni matangazo yale ambayo yanakuaga pembeni mwa video, n.k

Jambo lingine ni kwamba watu wanaotaka kutangaziwa biashara zao kwa youtube huwa wanaseti kabisa tangazo lao liwafikie watu wa tanzania ama nchi flani, sisi watazamaji wa bongo tunayaonaga matangazo mengi ya kina vidacom ama tigo, Nao wenye biashara marekani huwa wamelenga watazamaji wa huko na ulaya.

Sasa endapo video za msanii zikitazamwa Marekani, Ulaya, Canada, n.k basi msanii anaweza kulipwa hata elfu 10 akipata views elf 1 kutoka majuu, hii ni kwasababu makampuni ya huko yanayotaka kutangaziwa biashara yana ni makubwa na pesa nyingi tu, wanaweza kulipa hata elf 20 kwa views elf 1 youtube wakachukua elf 9 msanii akabaki na elf 11, views za wabongo elf 1 msanii anaweza akabaki hata na buku tu kwasababu tangazo tutaloliona mimi na wewe tukiwa hapo buza litakua labda ni la kampuni ya ufugaji wa kuku ambayo bado ni changa
---
Kuna Aina Nyingi Za Kuingiza Pesa Kupitia YouTube Channel.

1. Google Adsense
- Hii Ni Program Ya Google Wenyewe, Wana Kitengo Chao Cha Matangazo Kinaitwa Google Adwords (Hata Wewe Kama Una Biashara Yako Unaweza Kutangaza Pia),

Kwahiyo Wafanyabiashara Wanapotangaza Kupitia Hiyo Program, Hayo Matangazo Unaweza Kuyafanya Yakawa Yanaonekana Kwenye YouTube Channel Yako Kupitia Setting (Utaona Kuna Kisehemu Kimeandikwa Monetize Your Account).

2. Direct Ads
- Hata Inatokea Kama Channel Yako Imekuwa Maarufu Sana ( Eg Diamond Platnumz & AyoTv ) Na Inatazamwa Na Watu Wengi Zaidi, So Makampuni Yanaweza Kutangazwa Kupitia Channel Yako Directly, Mfano. VodaCom Wanatangaza Directly Kwenye AyoTV Na Diamond Alipata Direct Ad Kutoka Kwa Dr Mwaka

3. Affiliate Marketing
- Hii Mara Nyingi Ni Kwa Wale Ambao Hutengeza Tutorials, Unaweza Kufundisha Watu Kufanya Make Up, Then Ukawapa Direct Link Ya Amazon Ya Hizo Bidhaa Unazotumia, Wakizinunua Unapata Commission

N.B.Hakikisha Video Ni Zako Na Ni Quality, Na Si Za Ubaguzi Au Ngono
---
Kwa kifupi unachotaka ni views na "engagement".
Makampuni wanawalipa Youtube (Google) kuweka matangazo yao youtube na kila mtu akiangalia tangazo wakati yupo kwenye video yako basi na wewe unapewa vijisenti.

Ni vigumu sana kujua utapata kiasi gani maana inategemea mambo mengi sana, aina ya tangazo, alipo mwangaliaji etc. Pia anapo click tangazo unapata kiasi fulani.

Mtu anapofungua video yako na kuiangalia kwa angalau sekunde 30 hiyo ni view ila sio kila view itakupatia hela maana sio kila mara wanaonyesha tangazo.

Kuna hizi calculator online zinakupa kadirio la mapato kutokana na views
Estimated Youtube Money Calculator (By Social Blade)

Ushauri wa kawaida ni kufocus kwenye niche (sekta) moja kwenye channel yako ya youtube so kama ni games basi kila siku iwe games au vitu vinavyohusiana ili watu wajiunge na channel yako na wawe wanaangalia video kila unapotoa.

Jihadhari na kubandika kazi za watu za aina yoyote maana hii ina penalty zake ikiwemo kufungiwa account. Kumbuka kuwa hata game ni kazi za watu na watengeneza game wakikumind wanakubania.

Nisengependa kuweka channel yangu humu ila inadeal na mambo ya technolojia.
---
Wasanii au mtu yoyote mwenye channel iliyothibitishwa na Youtube anaweza kuingiza kipato kupitia matangazo yanayowekwa katika video mfano wa matangazo hayo ni matangazo ya video(Skippable Ads) ambayo huanza kuonekana kabla ya video husika kuanza kucheza pia kuna matangazo ya graphics(overlay) ambayo hutokea ndani ya video huwa yanaonekana zaidi chini ya video na mengine huonekana nje ya video pembeni.

Matangazo haya huwa yanatolewa kupitia mfumo wa matangazo kwenye mitandao unaojulikana kama adsense ambao unamilikiwa na google na hela inayopatikana kupitia haya matangazo hugawanywa kwa asilimia kati ya Youtube na mtu anayemiliki channel ya Youtube inayodisplay matangazo hayo mfano msanii au mtu yoyote anayemiliki channel ya youtube na malipo hufanyika kupitia Western Union,Cheque au Wire Transfer kwenda kwenye account ya Bank.

Watu wengi wamekuwa wakitumia vibaya mfumo huu kwa kupakia video zinazohamasisha ngono, mauaji, ubaguzi au kuiba na kupakia video amabazo hawazimiliki jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Youtube na matokeo yake huwa ni channel yako kufungiwa au kupelekwa mahakamani.
---
biashara ya mtandaoni ni kama biashara ya mziki au filamu, unatoa movie watu wasipoipenda movie itafeli lakini wakiipenda utapata hela ya kutosha, hivyo mapato ya movie yanategemea na jinsi itakavyopendwa inaweza kuwa shilingi 100 au milioni au bilioni au trilioni.

same kwenye youtube unaweza publish video wakaangalia watu 100 tu na usipate faida yoyote, then mwengine akaeka video ikaenda viral mamilioni ya watu wakaiangalia akapata mamilioni ya hela.

hivyo kama una uhakika una idea ukieka tu video watu kibao wataziangalia, usisite fanya hii biashara itakulipa. ila kama huna hata idea unategemea video za wenzako copy and paste wala usihangaike fanya tu biashara nyengine
---
Mtandao wa Youtube unajulikana kuwalipa watu kutokana na views za video zao. Kitu kigumu kwa wanao-upload video zao pale youtube ni kujua kama zitapata views za kutosha.

Ni kweli kuwa unaweza kulipa watu wawe wanafungua video yako mara nyingi ili kuongeza views, na vile vile kuna robots za kutumika kufungua video yako hata kama haingaliwi lakini hizi hukwama mara nyingi kutokana na security ya youtube. Sasa swali linarudi pale pale, kuwa ni nini kinachotakiwa kwa video kutazamwa sana. Jibu lake lina sehemu tatu:

(1) Sehemu ya kwanza ni maudhui ya video yenyewe. Video za Muziki ndizo hufunguliwa sana kwa sababu ni fupi, halafu binadamu wote hupenda muziki.

(2) Sehemu ya pili ni wigo wake ( yaani reach). Video inayofikia watu wenye background mbalimbali hupata views nyingi sana kuliko video inayofikia watu wa aina fulani tu.

(3) Sehemu ya tatu, ambayo inaweza kuwa na uhusiano wa karibu na hiyo sehemu ya pili hapo juu ni kuhusu umaarufu wa mtoa video na promotion ya video yenyewe. Mtu anayetoa video akiwa mtu maarufu mwenye wafuasi wengi akitangaza kuwa ametoa video yake, basi wafuasi wake karibu wote watakuwa wa kwanza kuiangalia hata kama ni mbaya. Sasa iwapo mtu huyo ana wafuasi milioni 20, ni wazi kuwa video hiyo inaweza kupata views milioni kumi kwa siku moja tu hata kama siyo nzuri.

Nimejaribu kuangalia kwa makini hizi video tatu ambazo zina views bilioni tatu na zaidi nikashindwa kabisa kujua ni vigezo gani vilivyotumika kuvuta watazamaji namna hiyo zaidi ya content ya muziki wenyewe.

Video ya kwanzaVideo hii ina zaidi ya views 3.4 billions katika muda wa miezi sita tu. Video hii imepigiwa mitaani kwa kawaida tu, ila ina muzuki mzito sana ambao nadhani ndio unaovuta watazamaji. Ni kweli kuwa inapata advantage kubwa sana ya kupendwa na watu wote wanaouzungumza spanish lakini nadhani content ya muziki wake ndiyo inayovuta watazamaji. Hakuna cha mavazi au video effects hapo.

Video ya piliVideo hii ina zaidi ya views 3.0 billions katika miwili iliyopita. Video hii ina muziki wa nguvu sana ambao nadhani ndio unaovutia watazamaji kuliko hata majina ya waimbaji wenyewe. Kibaya ni kuwa Muziki huo unajitokeza kwa muda mfupi sana na kutoweka, kwa hiyo mtazamaji anajikuta akirudia rudia. Characters wote katika muziki huu wamevaa mavazi ya kawaida tu kama ilivyo kwenye mitaa ya miji mbalimbali ya Marekani na wala muziki haukutumia video effects zozote.

Video ya tatu niVideo hii ina karibu ya views 3.0 billions katika miaka mitano iliyopita. Huyu jamaa Psy hakuwa anajulikana kabisa duniani kabla ya kutoa video hiyo, lakini video yake ilikuwa maarufu sana duniani kote. Amevaa na kutumia mazingira ya kawaida ya jijini Seol na hata video effects alizotumia ni minimal sana. Utaona kuwa hapa kilichovuta watazamaji ni creativity zake katika mziki wenyewe na katika uchezaji wake.

Outlook hiyo fupi inaonyesha kuwa video za muziki hazivuti watazamaji kwa sababu ya video effects au mavazi ya characters bali uzito wa muziki ulio embedded kwenye video zenyewe. Music producers wa kitanzania wanatakiwa kufanya kazi za ziada kupaisha video za wanamuziki wetu kuliko kutumia njia za mkatomkato kama inavoendelea sasa

---
youtube ni mtandao ambao unakuwezesha kuweka video yako mtandaoni ili watu waweze kujua kipaji chako kua na channeli yako mwenyewe youtube sio jambo la msingi sana

kwani cha msingi unatakiwa kuifanya channeli yako ikuingizie pesa.kupata p[esa youtube ni jambo rahisi sana unachotakiwa tu ni kukubalika kwa watu kama uanataka kuanzisha

channeli yako youtube kwa lengo la kupata pes basi hapa ndio penyewe keanza kabisa unahitaji uwe na wazo je wazo gani?

ni aina gani ya video utakazo kua unaposti hilo ndilo wazo la msingi kwanza.ktk mawazo ni wewe mwenyewe na ubongo wako kisha baada ya hapo unachoa takiwa unatakiwa uwenagoogle account.

tembelea www.gooogle.com/signin ilikujisajili ukishapata gmail accont yako basi nenda youtube mojakwa moja kupitia www.youtube.com/signup ukisha jiunga na account ya youtube kinacho fuata ni kwenda

hapa www.youtube.com/upload na utaweza kupost video zako na kama ukifanya vizuri basi unaweza ukapata pesa kupitia matangazo kama google adsense.

Kama hujaelewa comment namba yako nikucheki.
---
Kunga YouTube channel na AdSense n hatua ya kwanza lakini kupata pesa ile inayoitwa mkwanja in hatua nyingine

YouTube wana TOS nyingi kuamzia ubora WA video na content ya video husika

Unaweza kuwa na video 100 lakin suitable for ads n 10 tu.

Pili copy videos aisee hapo utakuwa unapoteza muda wako kwani utapewa banning ya maisha

NB. Kama utaka kucopy plz usicopy video za wanamuziki.

Ili channel yao iweze kutrend fast hakikisha unatunia metadata vizuri( title, description na tags)

Kuanzia trh20 February ili uwe eligible na monetizations ni lazma uwe na subscribers 1000 na watching hours 4000.
Na siotena 10000 views
 
Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,333
1,908
Mimi wananilipa kwa electronic transfer moja kwa moja kwenye account yangu. Kutegemea na nchi uliyopo wanasupport check, EFT, Western Union etc.
 
srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
3,792
2,998
Mimi wananilipa kwa electronic transfer moja kwa moja kwenye account yangu. Kutegemea na nchi uliyopo wanasupport check, EFT, Western Union etc.
Na mchanganuo wake ndio upoje? Na wewe ni channel yako gani wanayokulipia? Unaweza nipatia link tafadhali nikaiona!?
 
BOB OS

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,392
6,636
wanalipa kutokana na views,advertisement(Pay-per-click (PPC),
ila ninavyojua ili uweze kulipwa lazima umonetize account yako kwanza,content zako ziwe original(video unazoweka,miziki,yote isiwe na copyright)
ikiwa na copyright nyingine zinafutwa,au earning zinakwenda kwa mwenye original content
..1000views=1.30$
 
Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,333
1,908
Na mchanganuo wake ndio upoje? Na wewe ni channel yako gani wanayokulipia? Unaweza nipatia link tafadhali nikaiona!?

Kwa kifupi unachotaka ni views na "engagement".
Makampuni wanawalipa Youtube (Google) kuweka matangazo yao youtube na kila mtu akiangalia tangazo wakati yupo kwenye video yako basi na wewe unapewa vijisenti.

Ni vigumu sana kujua utapata kiasi gani maana inategemea mambo mengi sana, aina ya tangazo, alipo mwangaliaji etc. Pia anapo click tangazo unapata kiasi fulani.

Mtu anapofungua video yako na kuiangalia kwa angalau sekunde 30 hiyo ni view ila sio kila view itakupatia hela maana sio kila mara wanaonyesha tangazo.

Kuna hizi calculator online zinakupa kadirio la mapato kutokana na views
Estimated Youtube Money Calculator (By Social Blade)

Ushauri wa kawaida ni kufocus kwenye niche (sekta) moja kwenye channel yako ya youtube so kama ni games basi kila siku iwe games au vitu vinavyohusiana ili watu wajiunge na channel yako na wawe wanaangalia video kila unapotoa.

Jihadhari na kubandika kazi za watu za aina yoyote maana hii ina penalty zake ikiwemo kufungiwa account. Kumbuka kuwa hata game ni kazi za watu na watengeneza game wakikumind wanakubania.

Nisengependa kuweka channel yangu humu ila inadeal na mambo ya technolojia.
 
Kadada

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
202
203
Na nikitaka kuweka muziki au video yangu Youtube ili kuiuza kwa viewers. Steps ni zipi
 
gambalakobe

Member
Jul 1, 2015
55
73
Wakuu, naomba msaada nimesumbuka na hili swali muda sasa. Hivi msanii anapoweka video YOUTUBE anipigia promo hili watu waitazame hivi anapataga faida gani?

Je, huwa anaingiza pesa?? kama anaingiza ni kwa jinsi gani?

Je, kama anaingiza nini kinaonesha kuwa anastahili kulipwa?

Je, kama analipwa analipwa na nani na kwa jinsi gani?

Kama zinamuinguzia hela kupitia Viewers je ni idadi gani inahitajika au wanamcalculateje?
WAKUU NAOMBA MSAADA KWA WANAO FAHAMU.
 
JAY BLACK

Member
Jun 15, 2016
12
12
Wasanii au mtu yoyote mwenye channel iliyothibitishwa na Youtube anaweza kuingiza kipato kupitia matangazo yanayowekwa katika video mfano wa matangazo hayo ni matangazo ya video(Skippable Ads) ambayo huanza kuonekana kabla ya video husika kuanza kucheza pia kuna matangazo ya graphics(overlay) ambayo hutokea ndani ya video huwa yanaonekana zaidi chini ya video na mengine huonekana nje ya video pembeni.

Matangazo haya huwa yanatolewa kupitia mfumo wa matangazo kwenye mitandao unaojulikana kama adsense ambao unamilikiwa na google na hela inayopatikana kupitia haya matangazo hugawanywa kwa asilimia kati ya Youtube na mtu anayemiliki channel ya Youtube inayodisplay matangazo hayo mfano msanii au mtu yoyote anayemiliki channel ya youtube na malipo hufanyika kupitia Western Union,Cheque au Wire Transfer kwenda kwenye account ya Bank.

Watu wengi wamekuwa wakitumia vibaya mfumo huu kwa kupakia video zinazohamasisha ngono, mauaji, ubaguzi au kuiba na kupakia video amabazo hawazimiliki jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Youtube na matokeo yake huwa ni channel yako kufungiwa au kupelekwa mahakamani.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,618
33,830
Kuna Aina Nyingi Za Kuingiza Pesa Kupitia YouTube Channel.

1. Google Adsense
- Hii Ni Program Ya Google Wenyewe, Wana Kitengo Chao Cha Matangazo Kinaitwa Google Adwords (Hata Wewe Kama Una Biashara Yako Unaweza Kutangaza Pia), Kwahiyo Wafanyabiashara Wanapotangaza Kupitia Hiyo Program, Hayo Matangazo Unaweza Kuyafanya Yakawa Yanaonekana Kwenye YouTube Channel Yako Kupitia Setting (Utaona Kuna Kisehemu Kimeandikwa Monetize Your Account).

2.Direct Ads
- Hata Inatokea Kama Channel Yako Imekuwa Maarufu Sana ( Eg Diamond Platnumz & AyoTv ) Na Inatazamwa Na Watu Wengi Zaidi, So Makampuni Yanaweza Kutangazwa Kupitia Channel Yako Directly, Mfano. VodaCom Wanatangaza Directly Kwenye AyoTV Na Diamond Alipata Direct Ad Kutoka Kwa Dr Mwaka.

3.Affiliate Marketing
- Hii Mara Nyingi Ni Kwa Wale Ambao Hutengeza Tutorials, Unaweza Kufundisha Watu Kufanya Make Up, Then Ukawapa Direct Link Ya Amazon Ya Hizo Bidhaa Unazotumia, Wakizinunua Unapata Commission.

N.B: Hakikisha Video Ni Zako Na Ni Quality, Na Si Za Ubaguzi Au Ngono
 
martini enock

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
633
269
Labda nami niulize ni jinsi gani wasanii wanavyoweka miziki yao YouTube maana huwa kuna kitu napenda nikiweke you tube
 
AjayTv1

New Member
Apr 30, 2017
1
1
Wapendwa naomba kujua juu ya mitandao ulipwaji wake na faida zake mfano kama youtube nk ukilinganisha na biashara zisizo za mtandaoni.

Kichuguu,
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom