A-Z Jinsi ya kupata pesa kupitia chaneli ya YouTube

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Je, wajua kwamba waweza jipatia pesa nyingi sana kupitia Youtube? Labda unajiuliza ni jinsi gani jambo hili linawezekana! Leo nakupa maujanja kuhusu mchongo huu. Video nyingi ambazo hua unazitazama YouTube ni chanzo kikubwa sana cha pesa kwa wanaopost video hizo, yawezekana hujawahi kuujua ukweli huu. Ni rahisi sana kujiingizia pesa kwa kupitia Youtube endapo ukifahamu kiundani kuhusu jambo hili.
>MAMBO MUHIMU YA KUYAFANYA ILI KUJIPATIA PESA NI HAYA HAPA.
1.UNATAKIWA KUWA NA YOUTUBE CHANNEL YA KWAKO. YouTube channel ni nini? Hii ni akaunti yako binafsi ya YouTube ambayo utakuwa ukiitumia kupost videos, jinsi ya kuifungua ni rahisi sana kwanza ingia YouTube kisha bonyeza SIGN IN hiyo link ipo upande wa kulia juu kisha ingiza E -mail yako ambayo utakuwa unaitumia na namba ya password yako.

Ita load kisha itafungua ukurasa mpya katika huo ukurasa bonyeza MY CHANNEL upande wa kushoto.
Baada ya hapo yatakuja maelezo yanayotaka ukamilishe kutengeneza channel yako, kisha tayari utakuwa umetengeneza channel ya kwako.

2.KUPATA MATANGAZO KATIKA CHANNEL YAKO KUTOKA GOOGLE ADSENSE. Kumbuka kwamba pesa unazopata kupitia YouTube ni kutokana na matangazo hayo ambayo utatumiwa kutoka Google (automatically), matangazo hayo yatakuwa yakionekana katika video zako utakazokuwa ukizipost lakini ili kupata matangazo hayo utatakiwa kukidhi vigezo ambavyo ni;-
Lazima channel yako iwe imetumika kwa miezi isiyopungua mitatu.
Lazima channel yako iwe na views wasiopungua 1000 kwa hiyo miezi mitatu.
Lazima channel yako iwe na subscribers wasiopungua 100.

Lazima uwe na Account ya Google Adsense. (Kwaajili ya kulipwa pesa utakazoingiza na kujua kiasi ulichoingiza ).
Endapo umekidhi viwango na vigezo hivyo ili kupata matangazo ndani ya channel yako Bonyeza SETTING kisha bonyeza ADVANCED SETTING kisha weka alama ya kwenye maneno ADVERTISEMENTS kisha upande wa kushoto bonyeza status and features kisha bonyeza Enable kwenye Monetization wataleta masharti yao kisha bonyeza Start kuonyesha umekubali masharti yao.

Kisha weka alama ya kwenye vibox vitatu vitakavyotokea kisha bonyeza Create. Google wataingia kwenye account yako kuona kweli umekidhi vigezo vya pale juu baada ya masaa 4 utaanza kupokea matangazo kwenye video zako nawe utaanza kuingiza pesa hapo hapo kupitia watu wanaoangalia video unazopost kwani watakuwa wanaona pia matangazo hayo, jinsi watu wanavyotazama zaidi video zako ndivyo unavyojiingizia pesa zaidi.

USHAURI WANGU KWAKO

Baada ya kutengeneza account yako ya YouTube anza kuapload video na kuzipost ili kukidhi vigezo vya kupata matangazo yaani views 1000 na Subscribers 100 pia uwe mbunifu kwenye video zako ili kuwavutia watazamaji wa YouTube.

ANGALIZO

Katika video unazopost epuka kupost video zenye HAKI MILIKI (COPYRIGHT) kwani wamiliki wa video hizo wakitoa malalamiko yao Google kwamba unapost video zao bila idhini yao account yako itapewa onyo kali na inawezekana hutapokea tena matangazo kwa hiyo hutaingiza pesa tena.

Mfano wa video zenye hati miliki ni video za Diamond Platnumz , Vanessa Mdee na wengineo wengi pia epuka kuingia YouTube na kuangalia video zako ili kujiongezea views kwa kutumia simu au Laptop uliyotengenezea account yako ya YouTube kwani Google wakigundua pia utapewa onyo kali.
HIVYO UKITAKA KUJIONGEZEA VIEWS TUMIA SIMU AU LAPTOP ZA WENGINE.
 
Shukran kwa elimu.

Nimejatibu fuata process nimeona kama sijakupata. Mi nna 624 Subscribers pia views 1000 nishazipita shida kwenye kuunganisha.

Kwenye app wanadai uwe na 1000 subscribers pia uwe na masaa 4000 ambayo ushatizamwa Youtube.

Naomba kueleweshwa zaidi ukute nimekaa na pesa hapa na sielewi.

Youtube yangu: https://youtube.com/@tinnvibez
 
Back
Top Bottom