mkuu Luguruni ipo Kibamba kama unaelekea Kibaha. Ni Manispaa ya Kinondoni. Wale mafisadi walivyomaliza kuwadhulumu wazaramo ardhi yao wakapata kiulaini viwanja 20000, ambavyo walijilimbakizia kwa kwenda mbele. Ndipo wakahamia huku kuanzisha kitu wanaita mji wa mfano wa kwanza hapa nchini. Fidia walilipa Shs 300 kwa sq mita wao wanauza shs 30000. Sasa wanehamia kigamboni. Kwembe ni eneo linalopakana na hicho kituo na mbele yake kidogo kitajengwa Chuo Kikuu cha Muhimbili. Ndo mafisadi wote wanataka kujilimikisha eneo hilo. Ishakuwa DECI ingine kwa waliotoa fedha zao
DC kijana hana jina?
As an old sage friend would have it...
The tawdry tabloidism taunts the tongue tied towards temper tantrums.
Colossal colloquism in a collision of continuously cantankerous conflicting codes.
Nawashukuru sana wana JF kwacomments zenu. Nilitegemea wengi wetu tunafuatilia migogoro ya ardhi inayoendelea hapa jijini kwa kuwa ninaamini wengi wetu tunamiliki viwanja ama mashamba hivyo sikuona umuhimu wa kueleza kila kitu kwakuwa ingekuwa ni makala badala ya habari.
Kama nilivyoeleza kukumbka kwa waziri ni pale alipotumia masaa matatu yeye mwenyewe na timu akimdanganya DC mpya kijana kuhusu mradi wa upimaji viwanja unaotekelezwa na wizara yake huko Kwembe. Awali eneo lililotengwa lilipangwa kupimwa viwanja 600 ka ajili ya watu 259 waliohamishwa Luguruni, 41 ambao watakumbuka na barabara na miundo mbinu na 300 waliokutwa hapo Kwembe ambao atakuwa incorporated kwenye huomradi kwa viwanja watakavyobaki navyo kupimwa nakupatiwa hati.
Uhuni ni pale wizara inapogeuka na kupima zaidi ya viwanja 1000 katika eno hilo. Ndio chanzo cha mgogoro wanakwembe kulamikia viwanja wanavyoachiwa kuwa ni vidogo sana. nadhani tunakumbuka recently ilibainika kuwa watumishi wa wizara ya ardhi wanahodhi idadi kubwa ya viwanja katika maeneo mbali mbali walipoendesha miradi ya upimaji viwanja.
Mwandishi wa Gazeti la Daily news la tarehe 21 machi 2009 aliripoti kshuhudia wapimaji wakipima viwanja kwa kutumia ramani ambyo mkurugenzi msaidizi wa upimaji wa wizara aliita ni feki na kuwataka wakachukua ramni ambayo ni sahihi kutoka kwenye gari. NDIO TULIPOFIKA HAPO JAMANI!!!
Hwezi kuamini kwamba viwanja watu waliokutwa Kwembe wanaichiwa viwanja vidogo sana kiai kwamba ukipata msiba ni lazima ufunge turubai barabarani kma Kariakoo. Mtu ulikuwa unamiliki ekari moja au mbili leo hii unaachiwa kiwanja ambapo gari lako moja tu haliwezi kunegotiate kuingia ukiuliza wanakijibu ukalaze gari ofisi ya CCM.
Haya mambo yametokea kweli ndio maana tunahabarishana ili kila mmoja hapa mjini ajue watakapofika katika maeno yenu. Mnaonidhihaki nina hakika iko siku mtatafuta hizi information watakapofika makwenu.
Tarifa zaidi soma makala katika gazeti la Fikra Endelevu Kwanza la Jumanne hii MIGOGORO YA ARDHI INACHOCHE UMASKINI
Huo utulivu wanaosema uko Tanzania ni wa viongizi tu; lakini sisi watu wa chini tuko vitani kuanzia kuuawa ukiwa albino mpaka kuporwa ardhi yako na kupewe watu wenye fedha!! Hapa ndipo sisi wanyonge tunamkumbuka hayati JKN kwani angekuwa hai uharamia unaofanywa na serikali ya Kikwete usingekuwepo.habari ya hapo inasikitisha sana, mimi pia ni mdau wa eneo hilo, ndio tupo kwenye mapambano, kitu cha hatari sana kinachofanyika pale, kuiona ramani ya hapo ni issue , kwa kweli hapo ndio utajua kweli Tanzania hakuna serikali, maana wanakuja kupima viwanja wakiwa na askari wenye silaha za moto kama watu wako vitani.