Miradi ya wizara ya ardhi inavyochochea umaskini

....ilikuwa ni fagio la kinamna kwa ajili ya DC Kijana mpya? Mbona hatuoni kauli yoyote ya huyo DC?
 
Kwa wale wasioilewa hii issue hawawezi ku catch up kwa jinsi presentor alivyoileta. Tafadhali anaeijua vizuri ailete upya
 
Naona kama hii stori inaeleweka kidogo,lakini hujasema DC kijana kamgalagaza vipi Mh.Waziri na tofauti zao kimtazamo zilikuwaje! Nafikiri wewe ni mhanga wa kilichotokea Luguruni.Umetanguliza emotions zaidi wakati wa kuwakilisha mada kiasi kwamba mada ikapoteza mwelekeo.

Asante
 
mkuu Luguruni ipo Kibamba kama unaelekea Kibaha. Ni Manispaa ya Kinondoni. Wale mafisadi walivyomaliza kuwadhulumu wazaramo ardhi yao wakapata kiulaini viwanja 20000, ambavyo walijilimbakizia kwa kwenda mbele. Ndipo wakahamia huku kuanzisha kitu wanaita mji wa mfano wa kwanza hapa nchini. Fidia walilipa Shs 300 kwa sq mita wao wanauza shs 30000. Sasa wanehamia kigamboni. Kwembe ni eneo linalopakana na hicho kituo na mbele yake kidogo kitajengwa Chuo Kikuu cha Muhimbili. Ndo mafisadi wote wanataka kujilimikisha eneo hilo. Ishakuwa DECI ingine kwa waliotoa fedha zao



JK na kundi lake wana mauza uza sana kila siku wanakuja na mapya kisa ni umaarufu tu na kusema CCM oyee sasa wacha waumbuke .Kwembe kazeni buti
 
DC kijana hana jina?

As an old sage friend would have it...

The tawdry tabloidism taunts the tongue tied towards temper tantrums.

Colossal colloquism in a collision of continuously cantankerous conflicting codes.
 
Last edited:
Nawashukuru sana wana JF kwacomments zenu. Nilitegemea wengi wetu tunafuatilia migogoro ya ardhi inayoendelea hapa jijini kwa kuwa ninaamini wengi wetu tunamiliki viwanja ama mashamba hivyo sikuona umuhimu wa kueleza kila kitu kwakuwa ingekuwa ni makala badala ya habari.

Kama nilivyoeleza kukumbka kwa waziri ni pale alipotumia masaa matatu yeye mwenyewe na timu akimdanganya DC mpya kijana kuhusu mradi wa upimaji viwanja unaotekelezwa na wizara yake huko Kwembe. Awali eneo lililotengwa lilipangwa kupimwa viwanja 600 ka ajili ya watu 259 waliohamishwa Luguruni, 41 ambao watakumbuka na barabara na miundo mbinu na 300 waliokutwa hapo Kwembe ambao atakuwa incorporated kwenye huomradi kwa viwanja watakavyobaki navyo kupimwa nakupatiwa hati.

Uhuni ni pale wizara inapogeuka na kupima zaidi ya viwanja 1000 katika eno hilo. Ndio chanzo cha mgogoro wanakwembe kulamikia viwanja wanavyoachiwa kuwa ni vidogo sana. nadhani tunakumbuka recently ilibainika kuwa watumishi wa wizara ya ardhi wanahodhi idadi kubwa ya viwanja katika maeneo mbali mbali walipoendesha miradi ya upimaji viwanja.

Mwandishi wa Gazeti la Daily news la tarehe 21 machi 2009 aliripoti kshuhudia wapimaji wakipima viwanja kwa kutumia ramani ambyo mkurugenzi msaidizi wa upimaji wa wizara aliita ni feki na kuwataka wakachukua ramni ambayo ni sahihi kutoka kwenye gari. NDIO TULIPOFIKA HAPO JAMANI!!!

Hwezi kuamini kwamba viwanja watu waliokutwa Kwembe wanaichiwa viwanja vidogo sana kiai kwamba ukipata msiba ni lazima ufunge turubai barabarani kma Kariakoo. Mtu ulikuwa unamiliki ekari moja au mbili leo hii unaachiwa kiwanja ambapo gari lako moja tu haliwezi kunegotiate kuingia ukiuliza wanakijibu ukalaze gari ofisi ya CCM.

Haya mambo yametokea kweli ndio maana tunahabarishana ili kila mmoja hapa mjini ajue watakapofika katika maeno yenu. Mnaonidhihaki nina hakika iko siku mtatafuta hizi information watakapofika makwenu.

Tarifa zaidi soma makala katika gazeti la Fikra Endelevu Kwanza la Jumanne hii MIGOGORO YA ARDHI INACHOCHE UMASKINI
 
DC kijana hana jina?

As an old sage friend would have it...

The tawdry tabloidism taunts the tongue tied towards temper tantrums.

Colossal colloquism in a collision of continuously cantankerous conflicting codes.


...Or as Readers Digest would have written; 'Towards More Picturesque Speech'...!
 
Nawashukuru sana wana JF kwacomments zenu. Nilitegemea wengi wetu tunafuatilia migogoro ya ardhi inayoendelea hapa jijini kwa kuwa ninaamini wengi wetu tunamiliki viwanja ama mashamba hivyo sikuona umuhimu wa kueleza kila kitu kwakuwa ingekuwa ni makala badala ya habari.

Kama nilivyoeleza kukumbka kwa waziri ni pale alipotumia masaa matatu yeye mwenyewe na timu akimdanganya DC mpya kijana kuhusu mradi wa upimaji viwanja unaotekelezwa na wizara yake huko Kwembe. Awali eneo lililotengwa lilipangwa kupimwa viwanja 600 ka ajili ya watu 259 waliohamishwa Luguruni, 41 ambao watakumbuka na barabara na miundo mbinu na 300 waliokutwa hapo Kwembe ambao atakuwa incorporated kwenye huomradi kwa viwanja watakavyobaki navyo kupimwa nakupatiwa hati.

Uhuni ni pale wizara inapogeuka na kupima zaidi ya viwanja 1000 katika eno hilo. Ndio chanzo cha mgogoro wanakwembe kulamikia viwanja wanavyoachiwa kuwa ni vidogo sana. nadhani tunakumbuka recently ilibainika kuwa watumishi wa wizara ya ardhi wanahodhi idadi kubwa ya viwanja katika maeneo mbali mbali walipoendesha miradi ya upimaji viwanja.

Mwandishi wa Gazeti la Daily news la tarehe 21 machi 2009 aliripoti kshuhudia wapimaji wakipima viwanja kwa kutumia ramani ambyo mkurugenzi msaidizi wa upimaji wa wizara aliita ni feki na kuwataka wakachukua ramni ambayo ni sahihi kutoka kwenye gari. NDIO TULIPOFIKA HAPO JAMANI!!!

Hwezi kuamini kwamba viwanja watu waliokutwa Kwembe wanaichiwa viwanja vidogo sana kiai kwamba ukipata msiba ni lazima ufunge turubai barabarani kma Kariakoo. Mtu ulikuwa unamiliki ekari moja au mbili leo hii unaachiwa kiwanja ambapo gari lako moja tu haliwezi kunegotiate kuingia ukiuliza wanakijibu ukalaze gari ofisi ya CCM.

Haya mambo yametokea kweli ndio maana tunahabarishana ili kila mmoja hapa mjini ajue watakapofika katika maeno yenu. Mnaonidhihaki nina hakika iko siku mtatafuta hizi information watakapofika makwenu.

Tarifa zaidi soma makala katika gazeti la Fikra Endelevu Kwanza la Jumanne hii MIGOGORO YA ARDHI INACHOCHE UMASKINI


Mkuu, Tunakushukuru sana kwa ufafanuzi huu muhimu sana. Hata hivyo, bado kuna katatizo kadoogo. Unaposema kuwa 'Chiligati aumbuka mbele ya DC kijana, je baada ya Waziri huyo kutoa maelezo ya masaa matatu kumdanganya 'DC Mpya Kijana', kuna kauli yoyote iliyotolewa na DC Kijana kuonyesha kuwa hakubaliani na maelezo ya Waziri na hivyo Waziri huyo kuwa amejiumbua mbele ya DC kijana kwa maana ya kwamba pamoja na maelezo yote ya masaa matatu DC Mpja Kijana alisema hakubaliani na maneno ya Waziri??
Kama DC mpya Kijana hakusema lolote, unajuaje kama hakubaliani ama amekubaliana na maneno ya Mkuu wake wa Kazi??
Kama hakutoa kauli yoyote kwa nini tusiseme kuwa 'DC Mpya Kijana akubaliana na maelezo ya Chiligati'?? kwa maana ya kwamba kimya kinaweza kuwa na tafsiri nyingi??? Ni mawazo yangu tu mkuu, lakini ujumbe wako ni mwema na tunaushukuru.
 
Hii story haieleweki, mtunzi alihitaji kutulia kidogo sio kuandika ili mradi tu. Mambo mengi ameacha kichwani kwake, hapa ametudondoshea cheche tu......!
__________________
HUTAKIWI KUMEZESHWA KILA KITU VINGINE UNATAFUNA.....
 
Wacha wambandike picha ya ze utamu..............jama utamu uko wapi.....wahsenzi wanataka kutuzidi nguvu sie......
 
Mkuu unajua tena mtu mzima na timu yake wamekaa masaa matatu wanampotosha kijana. Basi kmati ya wananchi ilipoingia mtu mzima akatangaza kuwa mradi umekamilika na viwanja 700 tayari basi kamati ya wananchi ilimdondokea mtu mzima na akapata aibu kuwa anjaribu kushirikiana na watumishi wake kuvuruga sheria, kanuni na taratibu za upimaji viwanja. Jamni mmesahau ndi huyu huyu alipandisha mshahara wa wafanyakazi ndani ya wiki tu akashusha tena.

Kwa mujibu ya waliohudhuria kikao Kijana alibaki anashangaa jinsi mtu mzima anavyoweza kutumia madaraka yake na kushirikiana na watumnishi wake wa chini kupotosha ukweli. Lakini imekuwa welacome note nzuri kwa kuwa kaja Kinondnoni ambako ndio wajanja wote wapo. Kijana atakachokuwa amejifunza kuwa hakuna kumuamini mtu hata kwa umri wake kwanza wazee ndio mafisadi wakubwa.
 
28 APRILI 2009

Na Chrizant Kibogoyo

KUTOKANA na wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji na mitaa kushindwa kutumia sheria nzuri zilzizopo kulinda maslahi ya wananchi katika ardhi, Watanzania wanatakiwa kufuata nyayo za hayati Mwalimu Nyerere aliyetangaza hadharani kumuunga mkono na kisha kumpigia kura mgombe wa NCCR Ndg Paul Ndobo kwa ajili ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini mwaka 1995 na kumuacha mgombea wa CCM aliyekuwa na tuhuma za kufilisi ushirika.

Ikiwa hayati Mwalimu Nyerere muasisi wa TANU na baadaye CCM aliweza kutambua umuhimu wa kuweka maslahi ya nchi mbele kabla ya maslahi ya chama chake cha CCM kwa kuchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi kwa kuwa katoka CCM. Mwaka 2009 na 2010 Watanzania wanatakiwa kuamka na kutumia vyema haki zetu za kikatiba kuchagua timu ya viongozi ambao watakwenda kuweka maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya vyama na binafsi Bungeni.

Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 imeanda utaratibu muafaka na shirikishi kweli kweli wa kuingiza eneo katika MPANGO WA URASIMISHAJI MASLAHI YA WANANCHI KATIKA ARDHI. Ni kutokana na umakini wa sheria hii ndio maana watendaji wa Wizara ya Ardhi, Halmashauri za Wilaya na Miji wanaikwepa kwa kuwa hawatapata chochote na kupendelea kuwapoka wananchi ardhi zao kienyeji tu.

Hivyo suala la urasimishaji ardhi za wananchi ni lazima wananchi walifanye kuwa ajenda ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani kwa kuwauliza wagombea wanaotaka kurudi ni kwanini walishindwa kutumia sheira hii kurasimisha maslahi ya wananchi katika ardhi?

Ni kwanini walikaa kimya wakati Watendaji wa Wizara ya Ardhi, halmashauri za Miji na Wilaya walipokuwa wakikiuka Sheria za ardhi na kanuni za ulipaji fidia?

Sambamba na hilo ni lazima wananchi wawahoji viongozi wanaotaka kurudi ni kwanini walishindwa kusimamia utekelezaji ?

Ufuatao ni uzoefu wangu katika kushughulika na masuala ya fidia za ardhi kwa takribani miaka miwili. Mara tu baada ya wakazi 259 wa eneo la Luguruni kulipwa fidia tarehe 18 na 19 Desemba 2007, walilazimika kuacha shughuli zao za uzalishaji mali na kutumia kipindi cha miezi tisa hadi Septemba 2008 kutafuta haki ya kulipwa fidia kwa mujibu wa bei ya soko kama inavyoelekezwa na Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kwa kuendesha mikutano, kutafuta elimu ya sheria za ardhi, kukwaruzana na maafisa wa wizara na wapima ardhi, kufanya maandamano n.k.

Kwa nchi ambayo bado iko nyuma kimaendeleo hii ni dosari kubwa. Na baada ya kudhihirika kuwa wapo watendaji waliosababisha hali hiyo na Serikali kulazimika kuwaongezea wananchi fidia walistahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili liwe fundisho kwa watendaji wengine wa aina hiyo.

Lakini , hadi sasa watendaji bado wanatamba katika nyadhifa zao wakiendelea kuwakorofisha wananchi katika maeneo mengine na hivyo kuwalazimisha kuacha shughuli za uzalishaji mali ili kudai haki zao za kisheria.
Mhe John Chiligati mara tu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa wa waziri katika Wizara ya Ardhi, alilazimika kutembelea eneo la Luguruni, Kibamba tarehe 15 Machi 2008 kutatua mgogoro huo.

Kufuatia kushuhudia mwenyewe ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu alilazimika kuwaondoa kwenye mradi wathamini mali waliofanya uthamini wa mali za wakazi wa Luguruni kwa kutumia madaftari badala ya nyaraka halali za Serikali zijulikanazo kama VAL FORM 1 na 2 na kuleta timu mpya iliyoongozwa na ndg Mulokozi. Timu mpya ilifanya kazi nzuri ya kuwashirikisha kikamilifu waathrika 259 katika uthamini wa pili uliofanyika kati ya Mei na Agosti 2008. Wafidiwa walipatiwa haki ya kuorodhesha mali zao kwa usahihi katika form ijulikanayo kama VAL FORM Namba 1; wafidiwa walipatiwa fursa ya kutosha kuhakiki idadi na usahihi wa orodha ya mali zao kabla ya kuweka sahihi mbele ya kiongozi wa Mtaa na mthamini mali.

Hivyo kila msomaji wa makala hii, atakayehusika katika zoezi la kufanyiwa uthamini anatakiwa kudai haki ya kuorodhesha mali zake katika katika fomu hiyo kwa usahihi na akiridhika ndipo aweke sahihi yake mbele ya kiongozi wa eneo lake na si vinginevyo.
Kwa uzoefu wangu wathamini mali wengi hujifanya kuwa wana haraka kwa nia ya kumchanganya mwanachi.

Kila mara mwanachi anapaswa kukumbuka kuwa ardhi aliyonayoishikilia ina thamani kubwa na taasisi iliyomtuma mthamini mali ndio inataka ardhi hiyo hivyo masuala ya haraka hayapo kabisa.

Kwa mradi wa Luguruni katika uthamini mali wa awali, Wizara ya Ardhi ilikuwa imewalipa waathirika wa Luguruni kwa kiwango cha Shs 300 kwa Mita 1 ya Mraba ilihali tokea mwaka 2005 bei halisi ya viwanja katika eneo la Kibamba ilikuwa ni kati Shs Milioni 4 hadi 6 kwa kiwanja cha Mita 20 X 20 chenye Mita Mraba (20 X 20= 400); sawa na Shs 10,000/= hadi 15,000/= kwa Mita 1 Mraba ( 6,000,000/= ÷ 400 Mita Mraba= 15,000/=). Hivyo Wizara ya Ardhi ililipa fidia kwa kiwango cha kati ya 2-3% ya bei halisi ya ardhi eneo la Kibamba.

Kazi nzuri ya uthamini iliyofanywa na timu mpya ilingia dosari pale Waziri Chiligati aliposhindwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa tarehe 25 Mei 2008 katika ukumbi wa Urafiki alipokutana na waathrika hao na kuahidi kuwa mara tu baada ya wizara yake kukamilisha utafiti mpya wa bei za soko la ardhi na nyumba katika eneo la Kibamba ataitisha mkutano mwingine wa kujadili viwango vipya vitakavyotumika katika kuwalipa fidia. Badala yake Wizara ya Ardhi ilijiamulia kutumia kiwango kipya cha Shs 1,977/= kwa Mita 1 Mraba sawa na Shs 1,977 X Mita Mraba 400=Shs 790,800/= kwa kiwanja cha Mita 20 X 20.

Kutokana na Waziri Chligati kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuhakikisha wizara yake inafanya majadiliano na waathirika kuhusu viwango vitakavyotumika katika kuwalipa fidia.
Yeye binafsi na watendaji wa wizara yake walivunja Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu 3(1)f cha kinachosisitiza “kufanyika kwa mapatano pale maslahi ya ardhi waliyo nayo wananchi yanapoathriwa kwa namna yoyote ile”.

Kutokana na kuvunjwa kwa kifungu hicho wizara ya Ardhi ilifanikiwa kuwalipa waathirika wa Luguruni 13% tu ya bei halisi ya ardhi katika eneo la Kibamba.

Na hivyo fidia hiyo kutoweza kukidhi haja ya waathirika kujipatia viwanja mbadala vyenye hadhi kama ambavyo walikuwa navyo yaani kufikika kirahisi, kuwa jirani na huduma za kijamii kama vile umeme, maji, usafiri, shule, maduka, ajira n.k Upo ushahidi wa kimaandishi unaonyesha kuwa wengi wa waathrika wa Luguruni walilazimika kuchota fedha zaidi kutoka katika fedha walizofidiwa nyumba zao ili kumudu kununua viwanja mbadala kwa bei za soko za kati ya Shs Milioni 4 hadi 18. Huu ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, haki za makazi na haki zinginezo za waathrika hao 259.
Kutokana na ushirikishwaji kukosekana kabisa Wizara ya Ardhi ikajiamulia kupandisha kiwango cha fidia za nyumba kutoka kati ya Shs 100,000/= na 150.000/= hadi 250,000/= na 300,000/= kwa Mita 1 Mraba ya nyumba.

Kwa mujibu wa wakandarasi wa majengo, ili mwananchi aweze kujenga nyumba na kuikamilisha ikiwa na huduma zote muhimu ikiwemo umeme, maji, barabara n.k. kama zilivyokuwa nyumba nyingi zilizobolewa eneo la Luguruni atahitaji kiasi cha ya Shs 500,000/= hadi 650,000/= kwa Mita 1 Mraba kulingana na hadhi ya jengo husika.

Hivyo kutokana na waaathirika wa Luguruni kutoshirikishwa katika utafiti wa bei za soko walipunjwa kati ya Shs 250.000/= hadi 400,000/= kwa Mita 1 Mraba ya jengo.

Tukikumbuka kuwa pia waathrika hawa walilazimika kuchota fidia za nyumba ili kumudu kujipatia viwanja mbadala kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya, ni wazi kuwa wengi walishindwa kujirejeshea viwango vya makazi kama waliyo kuwa nayo hapo awali.

Sheria, kanuni na taratibu za fidia zinaelekeza ufanyike utafiti wa bei za soko katika eneo husika kabla ya zoezi la uthamini mali kuanza.

Kwa kuwa haiwezekani mtu kutoka mbali akamzidi mwejnyeji ktika kufahamu bei za ardhi, vifaa vya ujenzi na mazingira ya ujenzi katika eneo husika, ni muhimu wananchi wakadai kushirikishwa katika utafiti huo na kufanya majadiliano kuhusu viwango vitakavyotumika kuwalipa fidia ndipo wakubali kuingia katika zoezi la uthamini mali.

Kukubali kuingia kwenye zoezi la uthamini mali kabala ya viwango vya malipo havijatangazwa hadharani ni kosa lililowagharimu waathrika wa Luguruni kwa kukosa ufahamu.

Itaendelea Jumanne ijayo.

Chrizant Kibogoyo ni mwanaharakati wa masuala ya ardhi.

Anapatikana kwa simu 0787-125599/0719-126575

 
nasikia katibu mkuu hapo ardhi washamchoka na anatakiwa kufukuzwa kazi lakini wamemwonea huruma nasikia anaachiwa mpaka a retire...kwa heshima na sasa hivi anakomba ile mbaya...na mafaili yanendelea kuchomwa moto tuuu
 
yaani ana nguvu kweli kweli,waziri asipotulia anampati transfer. Mzee Pombe alitaka kuwasaidia Kibamba akamuundia wizara ya kitoweo.
 
Ama kweli serikali ya JK heshima hamna kabisa. Waziri wa Ardhi Mhe Chiligati Juzi Jumamosi 25 Aprili 2009 alitangaza kusimamisha uuzwaji wa viwanja huko Kwembe baada ya kukutana na Kamati ya wananchi hao ofisini kwa DC wa Kinondoni.

Lakini Katibu Mkuu kasema uuzwajji uendelee, hivi sasa wizara inajipanga kuanza kuuza viwanja hivyo wiki ijayo. Katibu Mkuu anatamba kuwa atamhusisha Waziri Chiliagti kama alivyofanya kwa mwenzie waziri Magufuli alipojitosa kutatua mgogoro wa Kibamba na kuokekana kutaka kuwatendea haki wakazi wa eneo la Luguruni.

Zipo taarifa kuwa Katibu Mkuu Ndg Sijaona anapata kiburi kutoka kwa Katibu Mkuu kiongozi Ndg Luhanjo, ambaye amekuwa na tabia ya kuwatumia watendaji kuvunja nguvu za mawaziri katika wizara wanazopangiwa. Mtakumbuka jinsi Ndg Severe aliyekuwa Mkurugenzi wa wanyamapori katika Wizara ya Maliasili alivyokuwa akipata protection kutoka kwa Ndg Luhanjo.

Katibu Mkuu sijaona amepania kuhakikisha anatengeneza fedha ktk uuzwaji wa viwanja vya Kwembe kwa sababu wakazi wa Luguruni walikoma kiasi cha wizara yake kulazimika kuwaongeza fidia kwa kiwango cha 85% ya malipo mpunjo waliyokuwa wamewalipa awali. Sambamba na hilo ilibidi timu nzima kutoka Wizarani waliotekeleza mradi huo watumie fedha nyingi kuzima makosa ya jinai yalioyokuwa yakiwakabili kutokana na kulipa watu hewa, viwanja vitupu kana kwamba kuna nyumba n.k na kufanya uthamini wa mali kwa kutumia counter books na badala ya nyaraka halali za Serikali zijulikanazo kama VAL FORM 1 & 2.

Kwa hakika Luguruni walikamatika ndio maana sasa wamepania kurudisha nusu hasara kutoka viwanja vya Kwembe na wakazi wa Kwembe wameapa hakuna mtu atakayeingia kwenye eneo lao kwa kuwa Waziri Chiligati alitamka mara tatu kusimamisha uuzwaji wa viwanja katika eno hilo mbele ya DC.

Kazi ipo nani zaidi kati ya Waziri na Katibu Mkuu. Watakaoliwa ni wananchi watakaotoa fedha zao kununua viwanja Kwembe.
 
Du mwanangu hiyo title na kiswahili humo ndani mbona naona kinyumenyume, what are you tryin' to say son?.....Fanya editing basi kimtindo and have some references.

Ni mtizamo tu.

Killuminati
 
Hivi sasa limezuka tatizo la wananchi kukimbilia kwa viongozi wa juu kabisa pindi yanapotokea matatizo hata yale madogo tu. Lakini kibaya zaidi hivi sasa ni Pinda na JK , nahisi hata Shein ingawa imekuwa ni nadra sana kusikia wananchi wakimtaka akawatatulie matatizo yao labda kutokana na upole wake. Ni kawaida kusikia wananchi wakidai kama haji Pinda / JK patachimbika hapa, Mtu atakaa akijiuliza je hii ni nini hasa?
Tukuchukulie mfano wa Kwembe Kati, Wakazi wa eneo hilo walikumbwa na matatizo ya watendaji wabovu wa Wizara ya Ardhi na tamaa zao walizoweka mbele. Wakazi hao walikimbilia kwa viongozi mbali mbali kuomba msaada bila ya suluhisho lolote la maana. Wananchi hao wanafahamu kuwa Ardhi ni msingi wa maendeleo. Hivyo kwa muda mrefu wametunza ardhi yao ili iweze kuwasidia kusukuma siku mbele hasa wakati huu ambapo kuna tatizo kubwa la ajira. Wengi wao wanajihusisha na kilimo cha msimu katika maeneo ya mabondeni yasiyofaa kwa ujenzi wa nyumba na majengo mengine, wakitumia maeneo yao kwa maendeleo endelevu.
Ghafla kulitokea miradi ya kujenga chuo Muhimbili, kujenga mji wa Luguruni, kujengwa kwa Chuo kikuu cha Mt. Joseph n.k. Hii ilipelekea mafisadi wa wizara ya ardhi kuanza kulimezea mate eneo hilo, na hivyo kuanza kupiga jalamba ili kulipora toka kwa wananchi, Hivi sasa wanatumia mbinu mbali mbali kufanikisha wizi huo.

Mbinu ya kwanza ilikuwa kuwatisha wananchi kuwa kuwa kuna mpango wa kutwaa maeneo yao kwa malipo ya shilingi 300,000/= kwa eka moja ama mtu akikataa basi eneo husika litatwaliwa na Raisi kwa manufaa ya umma. Baada ya madai haya wananchi wengi waliogopa na kuanza kuuza maeneo yao kwa bei ya kutupa, na hivyo kuwapa mwanya maofisa wa wizara ya Ardhi kutwaa maeneo hayo kwa manufaa yao kwa bei ya kutupa.
Baada ya hapo maofisa hawa walikuja na kuanza zoezi la uthamini huku bei ikiwa siyo ile waliyowatishia wananchi wakati ule. Hata hivyo walitumia mbinu mbali mbali kuwanyonya wananchi huku wakikiuka sheria na taratibu zote zilizowekwa na mamlaka husika.
Baadhi ya mambo ya wazi ni kama ifuatavyo:
1) Wametwaa eneo la Veterinary lililokaribu na shule ya Joha lililotengwa kwa ajili ya kuhamishia watu waliobomolewa Luguruni na kuwagawiana viwanja pale, viwanja hivi wamevipima kwa ujazo wa chini baadhi ya hivyo ni 70 x 70. wao wanadai eti ni makazi ya viongozi nao wameainishwa ikiwemo baadhi ya viongozi wenye heshima zao ambao hatuamini hata kidogo kuwa wanashiriki katika ubatili huu. Hii ndiyo sababu ya Ramani kufichwa kinyume na utaratibu ambapo ramani inatakiwa iwe wazi kwa muda wa miezi miwili kabla ya kuitumia. Lakini hadi sasa bado ramani hiyo ni siri ya Mama Mushi na wenzie.
2) Watu wengi wamelipwa chini ya kiwango ambapo wengi wamelipwa kidogo kupindukia na kupelekea kuwekwa kwa walipwaji hewa. Hapa mtu akikutwa na ekari moja yenye minazi ishirini, anadanganywa kuwa ataongezewa minazi hadi 40 hapa anapigwa changa la macho kwani kwenye ardhi anaandikiwa nusu eka na nusu nyingine anapewa mtu wa ardhi ama jamaa yake.
3) Maofisa wa wizara ya ardhi wamepima upande wa pili wa eneo la mradi la Luguruni na baadaye wanaviuza kwa watu tunaoporwa hapa kwembe kwa bei ya juu sana, ukikutwa na maendelezo yeyote yasiyokamilika waambiwa bomoa haraka ili wapime viwanja wakauze kwa bei ya kujipangia. Hii iangalie na kufanyiwa utafiti kwani haya siyo majungu bali kweli tupu, Ukikutwa na robo eka (30x50) unapewa chini ya shilingi milioni mbili, wengine wamepewa milioni moja Ukienda upande wa pili unaonyeshwa kiwanja nusu ya hicho (30x20) kwa bei kati ya Mil. 6 hadi 8.
4) Wamekuwa wakichagua nani aandikiwe eneo gani. Mzee mmoja alilazimishwa akachukue shilingi Millioni 21 naye akakataa akidai eneo hilo si lake naye hataki kufungwa. Haya yalielezwa mbele ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya, Masawe naye aliahidi kushughulikia ingawa hakufanya chochote kile.
5) Maeneo waliyonunua wakati wa vitisho kutohusishwa katika uporaji kwa madai kuwa watapima na kuuza wenyewe kwa bei watakayo hapo baadaye. ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI analo eneo kubwa karibu na kinapojengwa chuo cha Muhimbili ambalo analihodhi yeye na mama Mushi, Pamoja na eneo lingine kubwa katika mtaa wa Kibwegere ambalo nalo ni la mama Mushi, Haya hayahusiki ila yetu sisi wanyonge ndiyo yanatwaliwa kwa bei ya kutupa, huku tukinyimwa haki ya kupewa angalau kiwanja kimoja katika maeneo yetu yanayotwaliwa kwa madai kuwa hatujamalizia kujenga, hii ni kinyume cha kanuni na sheria. Waziri husika hataki kutolea tamko jambo hili . Kanza analo eneo kubwa karibu na maduka sita mtaa huu wa Kwembe kati ambalo halijausishwa na wizi huu.
6) Kutishia wananchi watoe pesa la sivyo maeneo yao yatafanya maeneo ya miundo mbinu kama barabara, na hivyo nyumba zao kuvunjwa. Wananchi wamelalamika katika vikao halali juu ya hili bila kutokea mtu wa kuwafuta machozi.
7) Waliwaeleza wananchi kuwa wale waliokuwa na majengo ambayo hayaisha wasubiri hadi pale michoro mipya itakapokuwa tayari. Lakini sasa wamewageuka wananchi wakisema wayabebe majengo yao ambayo hayajawa tayari wayapeleke porini, Huu ni uonevu ambao hautavumiliwa hata kidogo, kwani wote tunajenga pole pole kwa ukosefu wa pesa, kutugeuka na kuvunja maendelezo yetu bila malipo ni suala gumu sana linaloweza kuhatarisha amani.
8) Maeneo ya mabonde ambapo watu maskini walikuwa wakilima mbonga mboga wanadai watapewa watu wengine ili wayaendeleze ingawa hakuna viwanja hapo. Wanasikitisha eti kuna wawekezaji toka India wanataka lima pili pili kwa ajili ya kusafirisha nje, hili lilisemwa na Mama Bura mbele ya Massawe lakini pamoja na wananchi kuwazomea hakuna kauli dhabiti iliyotolewa hadi sasa kupinga uhuni huu. Hapa mtu atajiuliza hivi kwa nini aliyekutwa asiwezeshwe kufanya mradi huo. Eti kiwanja kilichopo karibu na hapo lazima apewe mwekezaji
9) Maofisa wa ardhi ambao wanalipana posho kubwa za "Special Duty" kila mmoja kati ya 80,000/= hadi 150,000/= kwa siku gharama zitakazobebwa na wakazi, na hii imepelekea wao kutomaliza kazi hii kwa muda mrefu ili siku ziwe nyingi. Kwa utaratibu wa sheria gharama za mradi zafahamika hivyo ziwekwe wazi tujue ni utaalamu gani hasa wanaoleta hadi walipwe mshahara wa mwalimu mmoja kwa mwezi wao walipwe kwa siku moja kama siyo wizi mtupu.
10) Kwa kulipana kiasi hiki kikubwa imepelekea watu wengi kuchukuliwa maeneo yao bila kulipwa kwani pesa imetumika kuwalipa hawa wahuni malipo hewa na sasa wanadai kuwa wenye maeneo watalipwa pindi wakimaliza kuuza viwanja, na wenye maeneo hawapewi kipaumbele.
11) Wamekuwa wakipita maeneo ya Kibamba na Luguruni wakinadi viwanja ambavyo tunavimiliki wakitumia ramani hewa, hivyo Kamati ya Wananchi ikitaka marekebisho wanagoma kwani wameishaahidiwa fedha. Wengine maeneo yetu yameuzwa tukiwapo bila aibu yeyote. Wanaoendesha uhuni huu ni Kanuti na Kamala ambao hata siku za jumapili wanakuwa site wakinadi viwanja vyao, bila aibu yeyote.
12) Mwananchi akikutwa ameishajenga nyumba hilo ni kosa kwani wanahakikisha anabakiwa na sehemu yenye nyumba tu na sehemu nyingine wanawapa wapendwa wao, hata kama kuna maendelezo mengine kama vyoo n.k tena bila kulipwa. Hii inatuletea umaskini wakutisha kwani pale tulipotumia kufugia kuku, ngombe na mifugo mingine wametwaa na kuwapa wapendwa wao sisi tukiachwa bila utetezi wowote ule. Hivi maisha bora ni kwa watu wa Wizara ya Ardhi tu ama ni kwa kila Mtanzania kama alivyotangaza mtukufu Raisi.
13) Wamekuwa wakibabaika kila mara katika kauli zao, Waziri amekuwa akidai kuwa watu wa Kwembe Kati wanapangwa wakati maofisa wa ardhi wanahaha kupora maeneo ya watu kwa ajili ya kuuza viwanja vya watu. Waziri aliyedai Kwembe kati watapimiwa naye kaingia mitini.
14) Wamekiuka taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa ili kuweza kufanya ufisadi wao, sasa wanadai eti eneo linalojulikana kama Kwembe Kati eti ni sehemu ya Luguruni wakati wao wanafahamu kuwa maeneo hayo ni tofauti kabisa.
15) Kwa kuwa kamati iliyoundwa Kihalali na ni kimbilio la Wananchi wanyonge hawataki kuisikia kwani wanataka wananchi wawafuate wao ili wawaombe hongo. Ikumbukwe sheria za ardhi namba 4 ya 1999 inatambua kamati hizi, lakini watu wa Wizara ya ardhi wanadai kuwa itawazuia kufanya usanii wao.
16) Waliwauzia wananchi waliohamishwa Luguruni viwanja walivyokuwa wameodhi na hivi sasa wanahaha kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya kulangua hapo baadae, wakitumia mbinu chafu zisizokubalika hata kidogo.. Kama kuvunja maendelezo ya watu na kudai hongo wazi wazi.
17) Wamekuwa wanadai wananchi waliofanya maendelezo ambayo hayajakamilika hongo ili eti yatambuliwe ukikataa unakiona cha moto kwani wanavamia na kudai yavunjwe mara moja.
Undumilakuwili wa viongozi
Baada ya kero zote hizi wananchi waliwakimbilia viongozi wao wakidhani kuwa watasikilizwa jambo ambalo halikuwa hivyo hata kidogo. Hii inatokana na kuwa mafisadi wa Wizara ya Ardhi wameishajua dawa yao. Nayo ni kuwaahidi viwanja, wakishafanya hivi viongozi hawa uwageuka wananchi mara moja na kuungana na mafisadi hawa kuwakomoa wananchi waliowachagua. Hawa viongozi kwa ahadi ya viwanja ni kama mbwa kwa chatu hawachomoki hata kidogo. Wakifika na kuwasikiliza wananchi ukweli wanauona mfano Ni kitu gain kinasababisha mwananchi mmoja aambiwe avunje endelezo lake ili apewe mwingine? Hapa jibu liko wazi lakini wakishaelezwa kuwa tukifanya hivyo wewe upati kiwanja hapa wanashindwa kuchukua maamuzi ya busara na kulegea kabisaaaa. Hii imepelekea wananchi kuanza kukimbilia kwa Waziri Mkuu, na Mheshimiwa Rais kwa matatizo madogo yaliyokuzwa kwani wana maamuzi yasiyoteteleka, na hivyo kuwafanya wawe na majukumu mengi isivyotakikana. Kwa Kwembe Kati mifano ya viongozi hao ni kama ifuatavyo:
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya
Alipoombwa kuingilia kati baada ya mambo kwenda mrama yeye aliingia pale kwa mbwembwe akionekana ni mtetezi wa wananchi, alifika akifuatana na maofisa wa TAKUKURU, na maofisa wengine. Alionyesha uelewa wake katika masuala ya Ardhi akibainisha wazi mapungufu mengi katika zoezi la Kwembe Kati. Aliahidi kuwa yote yatawekwa sawa.
Baada ya kuahaidiwa kiwanja aligeuka ghafla na kufanya mambo mengi ya ajabu, alianza kwa kudai kuwa watu wa ardhi ni kama baba akijamba wananchi wasihoji hivyo hata kama sheria zimekiukwa hakuna shida watu wavumilie. Aliendelea kutisha wananchi kuwa yeye ana uwezo wa kumweka ndani mtu saa 48. Lakini aliwacha watu hoi pale alipodai kuwa hata kama ujalipwa uache tu kwani utalipwa watakapouza viwanja watakavyopima. Mambo mengine ya ajabu ni pamoja na:
1) Alikimbiliwa tangu mwezi Septemba 2008 akiombwa msaada lakini yeye aliingia mitini pamoja na kupewa barua. Baada ya kuona wananchi wameungana kupinga ufisadi akaja bila kuitwa na kuanza kutugawa akidai atawasikiliza wenye nyumba tu na wale wengine watajiju.
2) Alipanga mamluki (wengi wao wakiwa madalali na vibaka) siku ya Idd El Haji (3-3-09) ili ionekane kuwa wananchi tumekubaliana na madai yao ya kupora ardhi yetu, ila kuna wakorofi wachache lakini janja yake iligunduliwa na wananchi baada ya siri kuvuja na hivyo kujikuta uso kwa uso na wananchi wenye mabango pale serikali ya mtaa, aliumbuka na kuondoka na waandishi wa habari aliowaita kufanya usaniii ule. Vile vile alitoa hongo ili habari hiyo isiandikwe magazetini, hapa waweza kupata ukweli toka kwa OCD wilaya ya Kipolisi ya Kimara aliyefika siku ile. Vile vile amekuwa akitumia mamluki hao hao kuwapeleka ktk ngazi mbali mbali za serikali ili ionekane kuwa taratibu zilifuatwa wakati si kweli, vibaraka wake twawajua akiwemo mtendaji na madalali
3) Aliandika barua kuwa tumekubali kuporwa maeneo yetu kuwapa watu "hewa" wa Kibamba na Luguruni. Baada ya wanakamati kukataa barua hiyo yeye alielekeza wasishirikishwe tena bali itumike mitutu ya Polisi katika zoezi husika.
4) Amekuwa akimdanganya Waziri husika kuwa mambo yapo sawa wakati hiyo yote si kweli kwani mabango aliyokutana nayo siku ya Idd yanaeleza ukweli halisi. Aliyachukua mabango yetu kuwa atayafikisha kwa waziri husika lakini hakuyafikisha sehemu husika kwani aliumbuka siku hiyo.
5) Amehongwa kiwanja na MAMA MUSHI ambaye amekuwa akilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu bila mafanikio, wala hatua zozote kuchukuliwa dhidi yake, alivuruga sana pale Luguruni bila kuchukuliwa hatua yeyote ile, huyu mama ni hatari kwani amekuwa akifanya vikao na Kijana wa Uru Kishumundu pale Rombo Green View kupanga jinsi ya kuwaumiza watu wanyonge.
Naibu Kamishna wa Ardhi ( Shewio)
Katika maofisa wote waliowahi kuhusika na mgogoro huu huyu ndiye aliyeonekana kuwa na afadhali kwani alisikiliza na kukubali masuala yote ya msingi. Akisistiza kuwa kiwanja cha mwananchi ambaye ajalipwa akitauzwa bali atapewa yeye mwenyewe naye alipie gharama za upimaji. Katika mkutano mmoja ambapo wananchi walikuwa na hasira kali yeye aliwakonga nyoyo wananchi kwa kueleza wazi wazi kuwa sheria lazima zifuatwe. Akifuatwa ofisini anasisitiza kuwa hakuna haja ya kumwondoa aliyeendeleza hata sehemu ndogo na kumkabidhi mtu mwingine eneo husika. Alishangiliwa pale aliposema lengo ni kuepuka Manzese nyingine hapa. Alidai kama kuna maendelezo yeyote yule aliyendeleza atapewa kipaumbele kwanza, akasema labda akatae kupewa kiwanja husika mwenyewe, alida kiwanja cha aina hiyo kitakuwa "reserved". Lakini baadaye nae ameonekana kulega lega katika msimamo wake.
Kamala, Kanuti / Mama Mushi / Mama Mmbaga
Hawa ndiyo maharamia ambao watu wa Kwembe Kati watawakumbuka kwa maisha yao yote. Mwanzoni waliwaongopea wananchi kuwa kiwanja cha ukubwa wa chini (high density) kitakuwa na ukubwa wa meta 35 x 35 na kuendelea na kudai kuwa tutapewa kila aina ya huduma za jamii. Kwa sasa ndiyo wanaoongoza kwa kutumia kila hila kupora wakazi hawa na kuendelea kuwatwisha jiwe zito la ufukara. Wanatumia ramani zisizo halali na kutumia maneno ya vitisho ili mradi wapore wananchi, usipokubali kuwaonga unajuta kuwafahamu kwani watakufanyia visa vya kila aina kama vile kupitisha barabara sebuleni kwako, kukupunja kiwanja hata kama kipo katika viwanja vya ujazo wa chini na kutenganisha choo chako na nyumba yako ili mradi ujute kwa kutowapa hongo. Kwao cha msingi ni kupata viwanja vya kuodhi ana kulangua na pesa nyingi ili walipwe posho kubwa kubwa walizojipangia. Baada ya zoezi la kwanza kwisha na kufanikiwa walirudia zoezi husika ili wapate viwanja vingi hasa vya mbele kwa ajili ya kuuza na kuwapa watu wao, lakini hii ndiyo iliyoamsha hamasa ya wananchi. Hili ni kundi la maharamia ambao wanaweza hatarisha usalama katika jamii. Wanawatumia madalali hivi sasa kunadi maeneo waliyoyatayarisha kwa ajili ya kupatia pesa kwani hivi sasa kama ulikuwa na eneo lako sehemu nzuri basi ujue atapewa mteule wao. Kati ya watu watakaojuta juu ya ujio wa maharamia hawa ni akina mama na wajane wanyonge ambao hatuna nguvu ya kupamba na maharamia hawa huku viongozi wetu wakiwa hawakotayari kutusaidia hata kidogo.
Katibu tarafa / Mtendaji wa Mtaa Mw/kiti mtaa / Baadhi yaWajumbe
Hawa wote wamehaidiwa ama viwanja ama posho za shilingi 5,000/= na hivyo kuwasaliti wananchi moja kwa moja bila aibu hata kidogo. Hawa wengi wao hawatafaidi lolote zaidi ya kupata pesa ya kuganga njaa na kuwatongoza wafanyakazi wa ndani na watoto wa shule basi.
Aliyekuwa mkuu wa Mkoa (Kandoro)
Huyu alifanya kila analoweza kuondoa kadhia kwa wananchi na kuagiza kuwa yule atakayekutwa apewe kipaumbele kwanza katika kugawa kiwanja, na wengine wapewe sehemu itakayobaki. Vile vile amesisitiza kuwa yeye ni mtu wa mungu hawezi kudhulumu watu maskini Alionyesha uadilifu wake na kumwogopa mungu, kwani mambo mengi ni suala la kumwogopa mungu tu. Haya aliyafanya kwa matendo siyo maneno watu wa Mwanza watanufaika na busara / kuridhika / uadilifu na ucha mungu wake.
Waziri wa Ardhi
Waziri wa Ardhi alifika Kwembe kufafanua juu ya ujio wa Mradi wa ujenzi wa chuo cha Muhimbili na kiwanda cha dawa pale. Wananchi walimuuliza juu ya utwaaji wa ardhi Kwembe Kati naye alikanusha na kusema kuwa wananchi wa kwembe kati tulieni hamtaporwa bali mtapimiwa viwanja vikubwa alidai kuwa pale tu miundombinu itakapopitia ndipo watapatwaa. Alishangaa ni kwa nini watu wanafanyiwa tathmini, bali maofisa wa ardhi walisema kuwa ni kwa ajili ya sehemu zile tu zitakazopitiwa na miundo mbinu pekee ndipo wanalipa.
Hatujui kama ni kuahidiwa kiwanja ama kuwa na kazi nyingi lakini naye ameonyesha dalili ya kuwahadaa wananchi kwani anadai atasimamia uuzwaji wa viwanja hivyo bila kubainisha wale waliopimiwa bila kupewa fidi itakuwaje, wataachiwa maeneo yao ama la.
Madai yake kuwa watapewa kipaumbele watu waliohamishwa Luguruni ni ya kutilia mashaka kwani wengine hawakuwa na majengo bali ardhi tupu, iweje wao wapewe kipaumbele bali wale walioko Kwembe Kati na hawajamalizia majengo yao wabomoe kama siyo kuleta mwanya wa watu hewa wa Luguruni??. Vile vile kuna watu ambao wamevamiwa na hivyo taarifa zake hazipo wizarani kwani hawakulipwa yeye amenyamaza kimya bila kutoa ufafanuzi.

Ameombwa iwekwe wazi kiwanja kimetokana na mlipwa yupi kwa namba ya uthamini ipi lakini amepuuza kwani madudu yalofanywa kwenye uthamini ni ya kutisha mno. Kuna uwezekano kuwa watu wengi wamenufaika na fungu hili ndo maana wanagwaya kuchukua hatua.
Katibu tarafa / Mtendaji wa Mtaa / Baadhi yaWajumbe
Hawa wote wamehaidiwa ama viwanja ama posho za shilingi 50,000/= na hivyo kuwasaliti wananchi moja kwa moja bila aibu hata kidogo. Hawa wengi wao hawatafaidi lolote zaidi ya kupata pesa ya kuganga njaa na kuwatongoza wafanyakazi wa ndani na watoto wa shule basi.
Kutokana na watendaji hawa wabovu kumepelekea kuendelea kufedheheshwa kwa serikali mbele ya wananchi wake, ambao wanatazamia kupata huduma safi kutoka kwa watumishi wa serikali badala ya kuombwa rushwa, kuporwa ardhi, kupunjwa malipo ya fidia kutokana na kuwepo vitendo vya malipo hewa, baadhi ya watu maeneo yao kutwaliwa bila kulipwa kwa madai kuwa watalipwa pindi viwanja vikiuzwa, na baadhi ya watu kuzidishiwa malipo isivyo halali. Utawala bora kama ilivyokusudiwa na Serikali yetu tukufu usiwe kwa kauli mbiu tu bali kwa vitendo na mlengwa awe ni huyu mtu wa chini anayekandamizwa na mafisadi hawa.
Hii ndiyo sababu wananchi wanakimbilia kwa Waziri Mkuu na Raisi hata kwa mambo ambayo Mkuu wa Wilaya angeweza kabisa kuyatatua kwa urahisi zaidi. Kama suala la kupima viwanja ambalo taratibu ziko wazi kuwa anayekutwa apewe kipaumbele kama hajapitiwa na miundo mbinu.
Vile vile kuhamishwa kwa kijana wa Uru Kishumundu baada ya kuongwa viwanja hivyo suala hili tayari lilikuwa limemshinda, kumefanya watu wadhanie kuwa JK kaliona hili na kumwondoa , na hivyo kuwaonea huruma huko aendako, mwenyezi mungu mwingi wa rehema awasaidie awape ushupavu wa kutambua na kukabiliana na hila zake.
Mkuu wa Wilaya aliyekuja asikubali kuongwa kiwanja hata kidogo. Ashirikiane na Serikali kuwanyanganya viwanja walivyopora kwenye mradi wa viwanja 20,000 ili wauziwe wanyonge, hakuna haja ya kumwita mkuu wa mkoa hapa. Kama mkuu wa wilaya atasimamia vizuri basi mambo yataenda vizuri..

Halima Songambele
Kwembe Kati
Kata ya Kibamba
 
habari ya hapo inasikitisha sana, mimi pia ni mdau wa eneo hilo, ndio tupo kwenye mapambano, kitu cha hatari sana kinachofanyika pale, kuiona ramani ya hapo ni issue , kwa kweli hapo ndio utajua kweli Tanzania hakuna serikali, maana wanakuja kupima viwanja wakiwa na askari wenye silaha za moto kama watu wako vitani.
 
habari ya hapo inasikitisha sana, mimi pia ni mdau wa eneo hilo, ndio tupo kwenye mapambano, kitu cha hatari sana kinachofanyika pale, kuiona ramani ya hapo ni issue , kwa kweli hapo ndio utajua kweli Tanzania hakuna serikali, maana wanakuja kupima viwanja wakiwa na askari wenye silaha za moto kama watu wako vitani.
Huo utulivu wanaosema uko Tanzania ni wa viongizi tu; lakini sisi watu wa chini tuko vitani kuanzia kuuawa ukiwa albino mpaka kuporwa ardhi yako na kupewe watu wenye fedha!! Hapa ndipo sisi wanyonge tunamkumbuka hayati JKN kwani angekuwa hai uharamia unaofanywa na serikali ya Kikwete usingekuwepo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom