Miradi ya wizara ya ardhi inavyochochea umaskini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miradi ya wizara ya ardhi inavyochochea umaskini

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Jatropha, Apr 9, 2009.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Wana JF,

  Hivi mna habari hapa nchini kuna utwaaji ardhi za wananchi kiholela (land redistribution) ukihamisha high value land kutoka kwa wanyonge na maskini kwenda kwa viongozi, matajiri na jamaa zao.

  Kibaya zaidi mpango huo unasimamiwa na viongozi waandamizi wa chama tawala waliopewa nyadhifa nyeti kama za uwaziri katika Wizara ya Ardhi.

  Fidia wananchi wanazostahili kwa mujibu wa sheria kwa ardhi yao inayotwaliwa inageuka EPA ya uchaguzi wa 2009 na 2010.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,570
  Likes Received: 18,537
  Trophy Points: 280
  Fafanua zaidi ni maeneo gani, wamiliki halali ni kina ni kina nani na viongozi hao ni wapi ili tukusaidie.
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  tazama hii habari ya yaliotokea na yanaendelea kutokea Kigamboni, Bunju, Mabwe Pande na kwingineko

  WIZARA YA ARDHI INAWAFANYA WANYONGE KUWA MASKINI ZAIDI.

  Mwaka 2009 umewadia, na hivi karibuni tutaanza kusikia tambo za wanansiasa mbali mbali wakijinadi kwa wananchi ili waweze kupigiwa kura katika chaguzi zijazo za serikali za Mitaa na hatimaye uchaguzi mkuu mwakani.

  Moja ya silaha za wanasiasa katika kipindi hiki ni Sera za vyama vyao ambazo wamezibuni ili kuwaletea wananchi maendeleo; na ndizo ambazo watakuwa wakizinadi ili kupata ridhaa ya wananchi katika maeneo husika kuongoza ili watekeleza sera walizozinadi na hatimaye wananchi wapate maendeleo. Kama wananchi watapata maendeleo au la, hilo hubaki kitendawili.

  Ni katika kipindi hiki ambacho utasikia wanasiasa wa kambi moja wakiwaambia wenzao wa kambi ingine kuwa hawana Sera. Ni kauli hizi ndio zimenifanya nijiulize kunatofauti gani kati ya wanansiasa wasiokuwa na sera na wale wenye sera laikini wakishachaguliwa na kushika hatamu za uongozi hawatekelezi sera walizozinadi kwa wananchi?

  Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ilitolewa na Ofisi ya waziri Mkuu mwaka 2004. katika suala la Ardhi Sera hiyo inatamka bayana kuwa "Serikali itatumia ardhi kama njia ya kuwawezesha wananchi wake kushiriki kikamilifu kiuchumi. Lengo ni kusaidia wananchi watumie ardhi waliyo nayo ama kwa kujipatia hisa katika shughuli za uwekezaji huo au pato lenye kuwanufaisha kushiriki kikamilifu jkatika shughuli zingine za kiuchumi". Mkakati wa utekelezaji wa tamko hilo ibara ya 4.9.3.(ii), "Kutoa ardhi kwa wawekezaji wakubwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi.Pale ambapo itabidi Wananchi wahamishwe ili kuwapisha wawekezaji wakubwa. Serikali itawasidia utaalamu wa kuingia katika makubaliano muafaka na wawekezaji kwa nia ya kuwanufaisha".

  Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ilitolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2004 ni moja mihimili iliyotumika kutunga Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005; mathalani katika Ibara ya 48 ya Ilani ya CCM ya 2005 inatamka kuwa "utekelezaji wa dhati wa Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi itatuepusha na balaa la kuwa na jamii ambayo ina matajiri wachache walionacho na wananchi wengi wasio nacho".

  Katika miaka ya hivi karibuni limekuwepo ongezeko kubwa la migogoro ya ardhi kati ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wananchi. Wananchi wakipinga viwango vidogo vya fidia wanayolipwa ili kupisha miradi mbali mbali ya maendeleo inayopendekezwa na Wizara ya Ardhi. Kibaya zaidi Wizara ya Ardhi inatumia kutokuelewa kwa wananchi kuhusu thamani halisi ya ardhi na nyumba zao kukiuka kwa makusudi Sheria za Ardhi namba 4 & 5 za mwaka 1999 zinazotamka bayana kuwa "fidia itakuwa ni kwa bei ya soko"; na pia zinaelekeza utaratibu wa kufikia bei ya soko "kuwa itakuwa ni kwa kulinganisha na mauzo ya hivi karibuni ya ardhi au nyumba katika eneo husika".

  Madhumuni ya Wizara ya Ardhi kukiuka Sheria za Ardhi ni kujipatia faida kubwa ya zaidi ya 1000% (asilimia 1000) kwa kuuza ardhi ilizozipoka kutoka mikononi mwa wananchi wanyonge, ilihali wananchi wanaohamishwa kwa malipo ya fidia hafifu wakishindwa kujirejeshea viwango vya makazi na maisha waliyokuwa nayo awali kabla ya kuhamishwa kwao. Wengi wao hushindwa kujijengea nyumba bora kama walizokuwa nazo, kujirejeshea huduma za umeme, maji, barabara, ajira n.k na hivyo kurudisha nyuma jitihada za kufikia malengo ya milenia.

  Tuchukue mfano wa mradi wa mji wa mfano wa Luguruni ulioanza kutekelezwa na Wizara ya Ardhi Januari mwaka 2007. Tokea mwaka 2005 viwanja katika eneo la Kata ya Kibamba vilikuwa vikiuzwa kwa bei ya Shs Milioni 6 (6,000,000/=) kwa kiwanja cha Mita 20 X 20. Kiwanja cha Mita 20 X 20 kina Mita mraba 20 X 20= 400. Ukikokotoa utagundua kuwa ardhi katika Kata ya Kibamba inauzwa kwa bei ya Shs 15,000/= kwa Mita 1 Mraba tokea mwaka 2005. Cha kushangaza Wizara ya Ardhi na pasipo utu wala ubinadamu Mwezi Desemba 2007 iliwalipa fidia wakazi 259 wa eneo la Luguruni walitakiwa kuhama kupisha mradi huo Shs 300 tu kwa Mita 1 Mraba; sawa na Shs 120,000/= kwa kiwanja cha Mita 20 X 20. Iliwabidi wananchi walioathriwa na mradi huo kuikaba koo Wizara ya Ardhi ndipo wakalazimika ikapandisha kiwango hicho kufikia Shs 1977/= tu kwa Mita 1 Mraba, sawa na fidia ya Shs 790,800/= kwa kiwanja cha Mita 20 X 20.

  Kwa upande wa fidia za nyumba, awali fidia zilipwa kwa kiwango cha kati ya Shs 100,000/= na 150.000/= na baadye kupandishwa kufikia 250,000/= kwa Mita 1 Mraba ya nyumba. Kwa mujibu wa wakandarasi wa majengo bei halisi ili nyumba iweze kukamilika kikamilifu ikiwa na huduma zote muhimu ikiwemo umeme, maji, barabara n.k. ni katia ya Shs 500,000/= hadi 650,000/= kwa Mita 1 Mraba ya jengo kulingana na hadhi ya jengo husika. Ndugu msomaji utabaini kuwa kutokana na mchakato wa fidia kutokuwa shirikishi wafidiwa wa Luguruni walipunjwa kati ya Shs 250.000/= hadi 400,000/= kwa Mita 1 Mraba ya jengo. Tukikumbuka kuwa pia waathrika hawa walilazimika kuchota fidia za nyumba ili kumudu kununue viwanja mbadala kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya kwa bei ya Shs Milioni 6 hadi 8, ni wazi kuwa wengi walishindwa kujirejeshea viwango vya makazi kama waliyo kuwa nayo hapo awali.

  Mara tu baada ya kukamilisha kuwahamisha wananchi kutoka eneo hilo, Wizara ya Ardhi ilitangaza tenda kuuza mapori hayo (pasipo uendelezaji wowote). Nyaraka za tenda zinagharimu Shs 300,000/= na bei ya Mita 1 Mraba ni Shs 30,000/=. Mnunuzi yoyote anayetuma ombi chini ya kiwango hicho hukataliwa kwa kutofikia bei iliyopangwa. Kutokana na bei hiyo, Wizara ya Ardhi inauza kiwanja 20 X 20 chenye Mita Mraba 400 kwa Shs Milioni 12, ilihali yenyewe ilimfidia mwananchi Shs 790,800/= tu; na hivyo kujipatia faida ya asilimia 1500 (1500%).

  Katika hali inayothibitisha kuwa maadili ya kitaifa yameporomoka kwa kiwango cha kutisha sana. Taasisi ya Serikali inabuni mpango wa kujipatia faida kubwa sana kiasi hicho kwa kuwanyonya wananchi kwa kukiuka sheria zilizopo kwa makusudi. Katika lengo hili hilo la kujipatia faida kubwa zaidi Wizara ya Ardhi imewavamia wananchi wa eneo la Kwembe walioko jirani na kituo cha mji wa wa Luguruni na kupima viwanja vidogo vidogo ndani ya ua wa makazi yao. Makaro ya maji machafu, matanki ya maji, nyumba za watumishi, mabanda n.k vimemegwa na kuingizwa katika viwanja vipya vilivyotengenezwa kwa ajili ya kuuzwa pasipo kujali hawa binadamu wataishi vipi kuanzia sasa. Wakazi waliokuwa wakipakana na barabara ardhi zao zimemegwa kwa mbele kutengeneza viwanja vya kibiashara kwa ajili ya kuuzwa kwa faida kubwa. Haki za kibanadamu wala utu havijaliwi kabisa, kinachozingatiwa ni idadi ya viwanja vinavyoweza kuzalishwa ili Wizara ya Ardhi iweze kutengeneza fedha zaidi kutokana na mauzo ya viwanja hivyo.

  Wakati haya yakitendwa na taasisi ya kiserikali, Sera za uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutumia ardhi zilizonadiwa kwa wananchi mwaka 2005 ziko wapi? Je wanaopaswa kutekeleza sera hizi wako wapi? Hawaoni yanayotendeka; tena wengine ni viongozi waandamizi katika chama tawala. Ni nini kinwafanya wakae kimya kuhusu hali hii ya kinyonyaji? Wanaopaswa kusimamia utekelezaji wa sera hizi wako wapi? Ina maana hawasikii malalamiko ya wananchi katika maeneo yao na katika vyombo vya habari? Kama huu ndio mwendo wenyewe ni afadhali ya kukosa sera kuliko kuwa na sera za kuwadanganyia wananchi na kisha kushindwa kuzitekeleza.
   
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Leo Waziri wa Ardhi ameumbuka mbele ya DC mpya wa Kinondoni baada ya kugundulika kuwa yote waliyosema Waziri na timu inayohusika Kwembe sio ya kweli hata kidogo. Mhe alikuwa amechepuka kutoka katika kikao cha bunge kule Dodoma kuja kuiongezea nguvu timu yake ili ifanikiwe kuanza zoezi la ugawaji (kuuza) viwanja. Kama kawaida timu ya Wizara ilimpika DC huyu kijana kwa zaidi ya saa tatu ikiwa ni pamoja na kuipachika majina kamati ya wananchi kuwa wakorofi na wanatumiwa na vyama vya siasa. Baada ya kikao kuanza Mhe aliwashukuru sana wanakamati kwa ushirikiano na kutangaza kuwa viwanja 730 vilikuwa tayari vimeshapimwa na vitaanza kugawiwa wakati wowote, na vingine 450 vilikuwa vinaendelea kupimwa. jina la mradi ni MRADI WA UPIMAJI VIWANJA 600 KWEMBE KATI. Baada ya hizo porojo kamati ilimtaka Mhe awape shukrani watumishi wa wizara ma polisi walioshirikishwa ktk upimaji huo. Wajumbe wa kamati walimshukia waziri mbele ya DC kijana kuhusu uozo na rushwa vilivyofanyika kiasi cha yeye mwenyewd kukubali kutangaza kuwa hakuna hata mtu mmoja asiyekuwa muathirika wa kuhamishwa kupisha mji wa mfano wa Luguruni na wakazi waliopo ktk eneo hilo ndio tu wanaostahili viwanja Kwembe Kati. Changamoto iliyobaki ni kuhakikisha eneo lililotengwa linatoa viwanja 600 kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo. Kazi ambayo tunaamini DC kijana ataiweza. Poleni sana mlioliwa fedha kwa ahadi kuwa mtapata viwanja Kwembe. Kama ukombozi wa wanyonge uliwezekana Luguruni. Na sasa Kwembe. Naamini hata Kigamboni na kwingineko itawezekana. Dawa pekee ni kuacha kuamini porojo za huyu Mhe Waziri
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu huko Kwembe na Luguruni ni maeneo gani hayo?
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mkuu Luguruni ipo Kibamba kama unaelekea Kibaha. Ni Manispaa ya Kinondoni. Wale mafisadi walivyomaliza kuwadhulumu wazaramo ardhi yao wakapata kiulaini viwanja 20000, ambavyo walijilimbakizia kwa kwenda mbele. Ndipo wakahamia huku kuanzisha kitu wanaita mji wa mfano wa kwanza hapa nchini. Fidia walilipa Shs 300 kwa sq mita wao wanauza shs 30000. Sasa wanehamia kigamboni. Kwembe ni eneo linalopakana na hicho kituo na mbele yake kidogo kitajengwa Chuo Kikuu cha Muhimbili. Ndo mafisadi wote wanataka kujilimikisha eneo hilo. Ishakuwa DECI ingine kwa waliotoa fedha zao
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Naomba nieleweshe hapo tena Mkuu, Kwembe ipo Kigamboni au Kibaha...umesema kituo, unaamaanisha kituo kipi?

  Ahsante
   
 8. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndani ya kinondoni kama unaelekea kibaha
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Stori haieleweki
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,006
  Trophy Points: 280
  KWEMBE HIPO KATA YA KIBAMBA, WILAYA YA KINONDONI, KUNA WILAYA MPYA AMBAYO INAANZISHWA ENEO HILO, NA KUNA PLAN NZURI SANA YA MJI MPYA AMBAO UMEBATIZWA NI MJI WA MFANO TANZANIA, 2004 ILICHUKULIWA PICHA YA NDEGE (AERIAL PHOTO YA ENEO LOTE) NA PLAN YA HUO MJI IKADESIGNIWA KUWA NA FACILITIES ZOTE AMBAZO ZINAPATIKANA CITY CENTER, ACTUAL PLAN NI NZURI SANA KUTAKUWA NA 8WAYS ROADS, LARGEST AND MODERN BUS TERMINAL, NI MJI AMBAO UTAKUWA UKO MODERN SANA NI MAENEO HAYO AMBAKO UNIVERSITY OF MUHIMBILI INAPOJENGWA. NA KAZI HIZO ZA SURVEY NA COMPENSATION IKO FUNDED NA DONORS (EU?) TATIZO KUBWA LILILOPO NI KWAMBA HAYO MAENEO YALIKUWA NI MASHAMBA SASA KILICHOKUWA KINAFANYIKA MAFISADI WALISHAONA HIYO PLAN NA WANAJUA WAPI NI POTENTIAL( COMMERCIAL AREAS), KINACHOFANYIKA NI DHURUMA KUBWA KWA WENYE MASHAMBA, KAMA ALIVYOSEMA MSEMAJI WA KWANZA KWA WATU WA KAWAIDA WANAKULIPA 300KWA Sqr M, lakini cha ajabu wakishakulipa wao wanavitangaza hivyo viwanja kwa bei ya 30000kwa SqM, tatizo zoezi linafanyika kiubabe sana survey inafanywa chini ya police wenye silaha za moto
  nadhani hoja ya muweka hii post alikuwa anataka kuwaeleza wana JF kuwa mkuu mpya wa wilaya analijua hilo na sasa amelikomalia hilo suala bila kuwa na ubabaishaji wa aina yoyote
   
 11. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  Hii story haieleweki, mtunzi alihitaji kutulia kidogo sio kuandika ili mradi tu. Mambo mengi ameacha kichwani kwake, hapa ametudondoshea cheche tu......!
   
 12. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #12
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Jatropha

  Hongereni. Vipi mahakama iliamuaje kuhusu zuio?

  Kuna masuala mbalimbali ya kuyatafakari katika hili hali: JJ: Ardhi na Maendeleo ya mgeni njoo mwenyeji akonde!

  Songeni mbele mpaka kieleweke

  JJ
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160

  Mahakama ndani!...wakuu mbona hii mada haieleweki? Hongera ya nini, na nani?
   
  Last edited by a moderator: Apr 26, 2009
 14. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Niliona ninyamaze kwanza halafu niirudie mara kumi kumi hivi lakini kila nikirudia ndio nazidi kuona maluweluwe ni kadhani labda ni huu uzee maana wakati mwingine huusingizia. Weye jathropas bila shaka umeshapata muda wakuihakiki stori yako rudi uielezee upya.
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Apr 26, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  DC kijana haya bwana
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nawashukuru wana JF. Habari kamili ipo kwenye Habari Mchanganyiko Title UPORAJI WA ARDHI na Siasa Title SIRI KUU YA KUUZA KIGAMBONI HII HAPA. Fuatilia makala ya MIRADI YA WIZARA YA ARDHI INACHOCHEA UMASKINI ktk gazeti la Fikra Endelevu kila Jnne. Ni kweki ktk kutafu ta haki wanakwembe walienda mahakamani lakini bado hawajapata stop order. Nakushukuru Kituko kwa ufafanuzi wako mzuri. Baada ya Luguruni na Kwembe Wizara itahamia Kigamboni, Pugu Kajiungeni, Bunju. Mji Mwewa. Kongowe nk. Kama tuliweza kuwabana wakaongeza Fidia Luguruni na sasa hivi tunavyowabana Kwembe hivyo wakazi wa maeneo hayo wajitayarishe kupambana HAKI HAIPATIKANI HIVI HIVI UTWALIWA
   
 17. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  Bro bado chenga tu! Una matatizo gani lakini??? Tuliza mawazo kabla ya kuandika. Unapotuandikia kitu hapa lengo lake lazima kitu hicho kijitosheleze ili tunufaike na kile unachotaka kitufikie, vinginevyo usichangie just toa thanks kwa wenzako inatosha. Pia epuka jabza wakati wa kuandika......!
   
 18. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  reporter jipange vizuri story yako haieleweki ni kama magazeti ya dar leo na alasiri, vichwa vikubwa content mbovu
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ..mkuu umetaja kigamboni?? mbona nasikia kizunguzungu?
  enewei wazee wa kigamboni wanawangoja kwa mikono miwili....
  Mnakumbuka zile nyumba mbili za serikali pale maeneo ya vict kuelekea moroko?? hivi kuna mtu anaishi mule au bado ni mahame since mid eighties?...

  Halafu wana JF hamjasoma alama za nyakati? uchaguzi unakaribia na watatoa wapi hela za kampeni? ebo!!
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2009
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  point ni kwamba eneo lililotakiwa kupimwa viwanja 600 vishapimwa 730 na 450 vinaendelea kupimwa na waziri hastuki?
   
Loading...