Migogoro ya Ardhi haiishi sababu wafanyakazi wengi wa wizara ni watoto wa vigogo, hakuna wa kuwagusa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Unaweza ukajiuliza kwanini migogoro ya ardhi inaongezeka kila siku na hakuna mtumishi wa serikali anayekamatwa wala kuchukuliwa hatua. Ukweli ni kwamba wizara hii na Idara zake wamegawana watoto wa viongozi wa chama na serikali.

Lakini pia watumishi wa wizara hii kwa uelewa ni weupe sana, ni wizara ya watu waliofeli. Mtumishi wa masijala ya ardhi anayetunza kumbukumbu hana uelewa wowote kuhusu sheria ya ardhi. Watendaji wengi wanachofanya ofisini nikunyofoa taarifa za mtu A na kuweka za mtu B.

Swali lakujiuliza wanaotoa ajira hawawezi kuona kama kuna shida? Mgogoro wa ardhi unatatuliwa vipi na waziri wakati kuna makamishna na viongozi wengine hadi kwenye halmashauri?

Waziri alikoroma anaambiwa nenda polepole usimpotezee mwanangu kazi, nenda pole pole usimpotezee mpenzi wangu kazi nk, nadhani ikifika wakati watumishi wa umma wakawa adhabu yao kubwa ni kumfuta kazi anayekosea na kuajiri mwingine itasaidia sana kuondoa uzembe serikalini. Lakini je wazazi wa hawa vigogo wa ardhi watakubali? Nani wakumfunga paka kengele?

Siku tukiajiri wananchi migogoro itaisha ila tukiendelea kupeana kazi kwa sababu tu baba alifanya kazi ardhi migogoro hizi zitaongezeka na kurithiwa siku kwa siku.
 
Back
Top Bottom