DOKEZO Rais Samia tupia jicho Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam, unahujumiwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Dr.

JF-Expert Member
Jan 2, 2014
217
193
Kwanza Kabisa nikupongeze kwa kazi nzuri unayofanya ya kuwaletea Maendeleo wananchi wako wewe Binafsi Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan bila kujali ni kwa kiasi gani unaangushwa na baadhi ya wasaidizi wako. Sasa sikia haya na uyafanyie kazi.

Miezi kadhaa iliyopita Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndugu Jerry Slaa (Mbunge) kupitia vyombo vya habari alipiga Marufuku vikao vya CMT (Council Management Team) katika Halmashauri zote nchini bila kutoa utaratibu mbadala kwa madai kuwa anakomesha ujenzi holela wa vituo vya Mafuta (inashamgaza sana).

Matokeo ya zuio hilo ni kuwa kazi za Uaandaaji wa Michoro ya Mipango miji, Mabadiliko ya michoro ya Mipango miji, Mabadiliko ya Matumizi ya Ardhi, upimaji Ardhi na utoaji hati umesimama au kusua sua hasa katika Mkoa wa Dar es Salaam. Hii ni kwa sababu ili upimaji Ardhi ufanyike na hati zitolewe lazima michoro ya Mipango miji iandaliwe lakini kwa sasa haiwezi kuandaliwa maana vikao vya CMT huko Halmashauri vimepigwa Marufuku kinyume na utaratibu bila kuleta utaratibu mbadala.

Matokeo yake ni kuwa makazi holela yanaendelea kushika kasi huku wawekezaji na wananchi wakipata usumbufu mkubwa pale wanapoenda Halmashauri au Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam na kushindwa kupimiwa Ardhi, kupewa vibali vya ujenzi au kubadilishia Matumizi ya Ardhi zao kisa Waziri amekataza (inasikitisha sana).

Kutokana na kadhia hii watumishi wa Ardhi Idara ya Mipango miji Halmashauri na Kanda ya Dar er Salaam ni kama hawana kazi ya kufanya maana kazi ambazo wangefanya hazipo wanashinda wamelala, wanajiondokea Mapema au hawafiki kazini kabisa (Ndio Maana nasema UNAHUJUMIWA).

Ili kujiridhisha na ninachokisema tuma vijana wako kimya kimya waende Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam wafuatilie Idara ya Mipango Miji wameidhinisha michoro mingapi kabla na baada ya tamko hilo la Waziri utagundua jambo.

Mwisho kabisa aisee inaumiza sana unapokuta wazee watu wazima, walemavu na vikongwe wakitezeka kupata huduma kwenye Jengo la Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam lenye Ghorofa 9 na halina lifti, lifti ni mbovu mwaka wa tatu Sasa. Huyo Waziri Salaam Kuna siku nilimsikia akisema hadharani alikataa rushwa ya Bilioni 3 (japo najua ni uongo), Bora angechukua hiyo hela atengeneze lift wananchi wako wanateseka sana. Na umosefu huu wa lifti inachangia utoro kazini.

MAPENDEKEZO: Mosi; Waziri Slaa alete mbadala wa katazo lake haraka iwezekanavyo, au abatilishe katazo lake kama hakujiandaa.

Pili:Jengeni lift kwenye Jengo la Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam na tuma watu wachunguze Nini kinapelekea lift kuharibika miaka 3 bila kutengeneza au kununuliwa mpya.

Tatu na Mwisho: Endelea kufuatillia nyendo za huyu Waziri wa Ardhi kijana Jerry Slaa ujiridhishe kama kweli anatenda kazi kuwaletea Maendeleo watanzania au anafanya kinyume chake Maana haiingii akilini Vita yake na matajiri wa Vituo vya Mafuta iathiri mwananchi wa kawaida. Unahujumiwa.

Asante sana, nakutakia utekelezaji mwema.
 
Aisee kupata huduma ardhi ni janga lingine. Unaweza kusota wiki 2 bila majibu ya kueleweka
 
Kwanza Kabisa Nikupongeze Kwa kazi nzuri unayofanya ya kuwaletea Maendeleo wananchi wako wewe Binafsi Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan bila kujali ni Kwa kiasi gani unaangushwa na baadhi ya wasaidizi wako. Sasa sikia haya na uyafanyie kazi.

Miezi kadhaa iliyopita Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndugu Jerry Slaa (Mbunge) kupitia vyombo vya habari alipiga Marufuku vikao vya CMT (Council Management Team) katika Halmashauri zote nchini bila kutoa utaratibu mbadala Kwa madai kuwa anakomesha ujenzi holela wa vituo vya Mafuta (Inashamgaza sana).

Matokeo ya zuio hilo ni Kuwa kazi za Uaandaaji wa Michoro ya Mipango miji,Mabadiliko ya michoro ya Mipango miji,Mabadiliko ya Matumizi ya Ardhi,upimaji Ardhi na utoaji hati umesimama au kusua sua hasa katika Mkoa wa Dar es Salaam. Hii ni Kwa sababu ili upimaji Ardhi ufanyike na hati zitolewe lazima michoro ya Mipango miji iandaliwe lakini Kwa Sasa haiwezi kuandaliwa Maana vikao vya CMT huko Halmashauri vimepigwa Marufuku kinyume na utaratibu bila kuleta utaratibu mbadala.

Matokeo yake ni Kuwa Makazi holela yanaendelea kushika Kasi huku wawekezaji na wananchi wakipata usumbufu mkubwa pale wanapoenda Halmashauri au Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam na kushindwa kupimiwa Ardhi, kupewa vibali vya ujenzi au kubadilishia Matumizi ya Ardhi zao kisa Waziri amekataza ( Inasikitisha sana).

Kutokana na kadhia hii watumishi wa Ardhi Idara ya Mipango miji Halmashauri na Kanda ya Dar er Salaam ni kama Hawana kazi ya kufanya Maana kazi amabzo wangefanya hazipo wanashinda wamelala, wanajiondokea Mapema au hawafiki kazini kabisa (Ndio Maana nasema UNAHUJUMIWA).

Ili kujiridhisha na ninachokisema tuma vijana wako kimya kimya waende Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam wafuatilie Idara ya Mipango Miji wameidhinisha michoro mingapi kabla na baada ya tamko hilo la Waziri utagundua jambo.

Mwisho kabisa aisee inaumiza sana unapokuta wazee watu wazima, walemavu na vikongwe wakitezeka kupata huduma kwenye Jengo la Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam lenye Ghorofa 9 na halina lifti, lifti ni mbovu mwaka wa tatu Sasa. Huyo Waziri Salaam Kuna siku nilimsikia akisema hadharani alikataa rushwa ya Bilioni 3 (japo najua ni uongo), Bora angechukua hiyo hela atengeneze lift wananchi wako wanateseka sana. Na umosefu huu wa lifti inachangia utoro kazini.

MAPENDEKEZO: Mosi; Waziri Slaa alete mbadala wa katazo lake haraka iwezekanavyo, au abatilishe katazo lake kama hakujiandaa.

Pili:Jengeni lift kwenye Jengo la Wizara ya Ardhi Kanda ya Dar es Salaam na tuma watu wachunguze Nini kinapelekea lift kuharibika miaka 3 bila kutengeneza au kununuliwa mpya.

Tatu na Mwisho: Endelea kufuatillia nyendo za huyu Waziri wa Ardhi kijana Jerry Slaa ujiridhishe kama kweli anatenda kazi kuwaletea Maendeleo watanzania au anafanya kinyume chake Maana haiingii akilini Vita yake na matajiri wa Vituo vya Mafuta iathiri mwananchi wa kawaida. Unahujumiwa

Asante sana, nakutakia utekelezaji mwema.
Kuna ubadilishaji mwingine wa matumizi ya maeneo ya wazi ndio yenye shida.
Haya mengine sio mbaya. Mfano karibu ya Shule ya Mugabe kupelekea simu 2000 pale kwenye Kona , mtu kapewa pale , Kesho au kesho kuitwa tunataka kuongeza lane itakuwa shida. Maeneo mengi ya Mwenge Kijijini kulikuwa na maeneo ya wazi , Barabara Pana, mifereji, Leo hii watu wameweka gereji ,Nyumba na kadhalika
 
Back
Top Bottom