Waraka wa wazi kwa Waziri wa Ardhi Jerry Silaa

Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,799
4,196
Natanguliza salamu za dhati kwako Mh. Waziri

Pili, niwasalimu waatalamu wa Ardhi nchi nzima wanao kusaidia kufikia azma ya majukumu yako ulio aminiwa na Taifa kuyasimamia na kuyaongoza.

Waraka huu ni mahususi kwa taaluma ya mipangomiji ambayo ni moja ya nyenzo muhimu katika kutekeleza majukum yako Mh. Waziri.

Mh. Waziri; siku chache zilizopita umekuwa ukifanya ziara maeneo mbalimbali kwa lengo la kutatua migogoro na kuona namna bora ya kuisimamia sekta hii nyeti ya ardhi kuiepusha na migogoro

Mh. Waziri; moja ya ziara yako imegusia sana kuhusu ujenzi au uwepo wa vituo vya mafuta katika miji hususan Dar es salaam.

Mh. Waziri; mara kadhaa nimeshuhudia maelekezo yako yakielekeza hatua mbalimbali zichukuliwe ndani ya sekta ya mipangomiji. Moja ya hatua ulio elekeza ni kumsimamisha kazi Mkurugenzi anaesimamia mipangomiji na maendeleo ya makazi ngazi ya wizara. Hoja yako iliyokusuma kufanya hivyo ni kuhusu waraka unaotumika katika kuidhinisha ujenzi wa vituo vya mafuta jambo ambalo siku chache zilizopita lilijitokeza Katika maeneo ya Mikocheni na bado lawama zako na hatua unazozichukua umezielekeza katika kitengo cha mipangomiji manispaa ya Kinondoni

Mh. Waziri; sina shaka na weredi wako katika medani za kisheria pamoja na utashi wako binafsi katika kufuatilia mambo ya kijamii

Mh. Waziri; kwa wataalamu wa mipangomiji Kinondoni umewakaripia kwa kusema kwamba hawawashiriki Wenye ardhi yao ambao kwa maelezo yako watu hao ni Waheshimiwa madiwani.

Mh. Waziri; naomba nikukumbushe kwamba kwa mujibu wa sheria ya Ardhi No. 4 (1999) ikisomeka pamoja na marekebisho yake inaeleza bayana kwamba Ardhi ya Tanzania ina milikiwa na wananchi na Rais ni mdhamana wa hilo. Hata hivyo pamoja na kwamba ardhi inamilikiwa na wananchi lakin hawana idhini ya kuitumia moja kwa moja bila kibali cha mdhamana ambaye ni Rais, na kibali hicho cha matumizi hutolewa na mamlaka za upangaji zilizo kasimishiwa wadhifa huo kwa niaba ya Rais

Mh. Waziri moja ya kaul yako umeeleza kwamba wataalamu wasiamue kupanga matumizi ya ardhi bila kuwahusisha madiwani na ukaenda mbali ukasema. Naomba kunukuu ......."waacheni Wakae Waheshimiwa Madiwani waamue wenyewe kupanga mji wao au kuharibu mji wao...."

Mh. Waziri; kauli hii inakwenda kuididimiza taaluma ya upangajimiji, miji yetu imeharibika kutokana na ardhi kuamuliwa na wanasiasa wasio na weredi na masuala ya ardhi hususan katka kupangilia matumizi na kukidhi haja ya watumiaji ardhi.
Ni wazi kwamba kwa kauli hiyo ni sawa na kusema hakuna haja ya kuwepo wataalamu na badala yake wakae wawakilishi wa wananchi wajipangie wenyewe mahitaji ya matumizi katika ardhi yao jambo ambalo linakwenda kuharibu mionekano ya miji yetu, inakwenda kudidimiza mipangilio ya miji lakin pia sura ya nchi inakwenda kusiginwa kupitia kaul hii.

Mh. Waziri; nipende pia kukupa taarifa kwamba sekta ya ardhi tangu mwaka 2016 imeandamwa na matamko tofauti ya viongozi waandamizi, matamko ambayo yameleta shida kubwa sana katika usimamizi wa maendelezo ya makazi nchini

Moja ya shida hizo ni kuwa na muundo mbovu wa maamuzi na kiutendaji katika idara zote za Ardhi na maendeleo ya makazi, watumishi wa idara hizo pia kuandamwa na mazingira magumu kiutendaji na kupekelea kukosa moral ya kazi.

Mh. Waziri; kwa hakika kabisa bila kuwa na muundo bora wa utendaji katika wizara yako, unayo isimamia madudu yataongezeka, maamuzi ya kiutendaji katika Halmashauri yatafubaa, kwa sasa ni jambo la kawaida kuikuta ofisi ya aradhi haina umeme wala printer au photocopy machine, ofisi za ardhi hazina hata kabati au shelf la kutunzia kumbukumbu watumishi hawana bajet ya kutekeleza majukum yao

Mh. Waziri; watangulizi wako katika wizara yako kuna jambo walilifanya huenda ni kwa nia njema lakin linahitaji maboresho makubwa sana, mambo hayo ni muundo, utoaji wa matamko kwa njia ya Waraka, maelekezo yasio tekelezeka.

Mh. Waziri; nilikusikusikia ukisema kwamba watumishi wa ardhi wakatae maelekezo ya Waziri wao kwa kuwa si alie waajiri, unasahau kwamba kwa sasa watumishi hao hawapo tena TAMISEM bali unao hapo ofisin kwako na muajiri ni Katibu mkuu wako maana yake chombo cha kinidhamu ambacho ni muajiri ni Waziri, mtumishi anawezaje kukataa maelekezo ya waziri au kuhoji maelekezo ya mwajiri wake??

Mh. Waziri; nia yako ni njema sana katika kuisimamia wizara pamoja na kuiratibu ili ikupe matokeo utakayo lakin bila kuondoa changamoto za kimuundo ya mikocheni utayakuta maeneo mengi nchini. Wataalamu wa mipangomiji si sehem ya CMT hawaingii katika kamati tendaji huu mfumo utaumiza hii sekta

Mh. Waziri; kwa heshima kubwa sana nikusihi kufanya marekebisho ya kimuundo katika wizara yako. Punguza urasimu katika idara hizi na buni mfumo tendaji utakao saidia kuratibu matumizi ya ardhi ili hayo ya Mikocheni yasijitokeze tena, migogoro ya utumiaji ardhi ipungue na kila Mtanzania apate stahiki sahihi ya kutumia Ardhi ya nchi yake.

Mh. Waziri; mimi nikiwa kama Mtanzania na mwenye kuipenda sekta ya ardhi naomba nikushauri yafuatayo;-

1. Boresha mfumo kimuundo wa wizara yako

2. Ondoa kauli ya kuwaachia madiwani kupanga au kuharibu mji wao

3. Peleka wataalam wa mipangomiji ngazi ya kata kusaidia kudhibiti ukuaji holela wa miji na makazi

4. Unda tume ikusaidie kuchunguza chanzo cha ujenzi holela wa vituo vya mafuta na katika muda ambao tume itakuwa kazin sitisheni utoaji wa vibal vipya na majibu ya tume yalete mapendekezo ya namna bora ya kujenga vituo vya mafuta mijin

5. Tengeneza kamati shauri katika ofisi yako itumie kama chombo chako cha kiintelijensia, kamati hiyo iwe na wataalam wa ardhi pekee yaani mipangomiji, Afisa ardhi, Mpima ardhi na mthamini mali na ardhi. Kamati hii iwe na watu wenye wered wa hali ya juu sana na wanao weza kukueleza ukwel bila kujal ni uchungu au utamu wake

6. Ikikupendeza simamisha kwanza ziara zako na kutana na wataalam wa ardhi wakueleze changamoto zao kiutendaji pamoja na wadau wengine ili kwa pamoja mtoke na njia mahususi ya kushughulikia migogoro ya ardhi na udhibiti wa maendelezo ya ardhi nchini

Mh. Waziri; nikuombe radhi pale nilipo tumia neno lisilo kuvutia machoni mwako lakin kwa sababu ile ile ya nia njema ya kutekeleza Ilani ya CCM na kudumisha maelekezo ya Rais wetu mpendwa ya kuitaka sekta hii iwe na mchango katika maendeleo ya Taifa letu

Wasalam
Na
Ismal Chingwele
(Dip.CE, Bsc. URP, Msc. PPM, Msc. CEM)
Land Development Consultant-East Africa
 
Hakuna sehemu kwenye sheria ya ardhi inasema madiwani ndiyo wapangaji wa ardhi. Sheria ipo wazi mpango wa matumizi ya ardhi inatakiwa iwe shirikishi na maamuzi yote yafanywe na Mkutano Mkuu wa Kijiji Kwa sheria ya ardhi number 5 ya mwaka 1999.

Na mijini ardhi inatakiwa igaiwe na kamishna wa ardhi Kwa mujibu wa sheria number 4 ya ardhi ya mwaka 1999 kwakutoa hati miliki kufuata taratibu zilizowekwa.

Mipango yote kuhusu ardhi inatakiwa iwe shirikishi lakini ipitishwe na baraza la madiwani. Madiwani wanatoka wapi?

Hakuna sehemu diwani anatajwa kuhusika na mipango ya ardhi ila nchi hii tumezoea kuvunja sheria na wala hatujui mipaka yetu inaishia wapi.
 
Namba 6 ni sahihi kabisa, namba 5 siiafiki Kwa sababu tume nyingi zimeundwa lakini hazijaleta nafuu yoyote.
 
Hakuna sehemu kwenye sheria ya ardhi inasema madiwani ndiyo wapangaji wa ardhi. Sheria ipo wazi mpango wa matumizi ya ardhi inatakiwa iwe shirikishi na maamuzi yote yafanywe na Mkutano Mkuu wa Kijiji Kwa sheria ya ardhi number 5 ya mwaka 1999. Na mijini ardhi inatakiwa igaiwe na kamishna wa ardhi Kwa mujibu wa sheria number 4 ya ardhi ya mwaka 1999 kwakutoa hati miliki kufuata taratibu zilizowekwa. Mipango yote kuhusu ardhi inatakiwa iwe shirikishi lakini ipitishwe na baraza la madiwani. Madiwani wanatoka wapi? Hakuna sehemu diwani anatajwa kuhusika na mipango ya ardhi ila nchi hii tumezoea kuvunja sheria na wala hatujui mipaka yetu inaishia wapi.
Nilikuwa nimekaa nikasimama baada ya kusoma hoja Yako ili niweze kuiunga mkono Kwa 100%.

Eti madiwani waachiwe wapange miji haijalisha wataharibu au vinginevyo.

Slaa Jerry n bomu linalosubiri kulipuka, ni suala muda tu.
 
Namba 6 ni sahihi kabisa, namba 5 siiafiki Kwa sababu tume nyingi zimeundwa lakini hazijaleta nafuu yoyote.
Shida washauri wake hawajulikani na hakuna wa kumlaumu anapoenda chaka na matamko yasiyo na tija...au yanayopingana na miongozo inayotoka chini ya uratibu wa ofisi yake.

Labda tukiwajua washauri wake tutakuwa tumemjua mchawi au Jini wa sekta ya Ardhi. Huoni kama tukijua chanzo cha ushauri wake ni hatua moja kuelekea stabilization?!
 
Nilikuwa nimekaa nikasimama baada ya kusoma hoja Yako ili niweze kuiunga mkono Kwa 100%.

Eti madiwani waachiwe wapange miji haijalisha wataharibu au vinginevyo.

Slaa Jerry n bomu linalosubiri kulipuka, ni suala muda tu.
Ukifuatilia uchafuzi mwingine kwenye Idara ya Ardhi ni zao la wanasiasa..na ndio Mh. Anataka awakabidhi zoezi la kuamua matumizi ya ardhi kinyume na sheria za nchi, zinazohimiza ushirikishwaji na demokrasia katika mchakato wa kupanga matumizi.
 
Tume ni wizi na ufisidi wa Mali za umma
Lazima Mh. Anashauriwa, tutafanyaje kuhakikisha hapokei ushauri wa kimchongo?! Wenye kelemea maslahi binafsi?! Nadhani kuwa na Timu tunayoijua inaweza kuwa mwanzo mzuri.
 
Ushauri murua kabisa.

Kama Serikali inaajiri maafisa maendeleo Kila kata,Afisa Afya Kila kata. Sasa kwanini wasiajiri ma Afisa mipango miji na wapima Kila kata Ili kudhibiti ukuaji holela wa miji!

Pia ningeshauri Kila palipo na Makao makuu ya kata basi iandaliwe GN na patangazwe kama ni "Planning area" Ili kudhibiti ukuaji holela wa Center za Kata ambazo baadaye inategemewa kuwa miji midogo na miji.

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Kutakuwa na sababu..
Na natamani kujua. Hili unalosema ni swala la wazi kabisa. Ila nashindwa kujua kwann kwa wanasiasa linaonekana kama alien knowledge?!

Playing dumb inawafaidisha nini?!

Miji inapoharibika inawafaidisha nini?!

Maana ni ngumu kuamini kuwa hili swala sio intentional! Tbh
 
Nilikuwa nimekaa nikasimama baada ya kusoma hoja Yako ili niweze kuiunga mkono Kwa 100%.

Eti madiwani waachiwe wapange miji haijalisha wataharibu au vinginevyo.

Slaa Jerry n bomu linalosubiri kulipuka, ni suala muda tu.
Inashangaza sana mwanasheria asiyejua sheria ya ardhi inataka nini
 
Ni kweli hafahamu au ni kwa namna fulani hii ni loophole yenye manufaa kwao?! Maana kuongoza mbumbumbu Kuna namna yake.

Msaada kwa Mwanasheria atusaidie kujua namna ya kushughulika na wapotoshaji kupitia matamko. Lazima kuwe na namna... maana wanasiasa they are out of control.

Inabidi tuanze kuwawajibisha.
 
Natanguliza salamu za dhati kwako Mh. Waziri

Pili, niwasalimu waatalamu wa Ardhi nchi nzima wanao kusaidia kufikia azma ya majukumu yako ulio aminiwa na Taifa kuyasimamia na kuyaongoza.

Waraka huu ni mahususi kwa taaluma ya mipangomiji ambayo ni moja ya nyenzo muhimu katika kutekeleza majukum yako Mh. Waziri.

Mh. Waziri; siku chache zilizopita umekuwa ukifanya ziara maeneo mbalimbali kwa lengo la kutatua migogoro na kuona namna bora ya kuisimamia sekta hii nyeti ya ardhi kuiepusha na migogoro

Mh. Waziri; moja ya ziara yako imegusia sana kuhusu ujenzi au uwepo wa vituo vya mafuta katika miji hususan Dar es salaam.

Mh. Waziri; mara kadhaa nimeshuhudia maelekezo yako yakielekeza hatua mbalimbali zichukuliwe ndani ya sekta ya mipangomiji. Moja ya hatua ulio elekeza ni kumsimamisha kazi Mkurugenzi anaesimamia mipangomiji na maendeleo ya makazi ngazi ya wizara. Hoja yako iliyokusuma kufanya hivyo ni kuhusu waraka unaotumika katika kuidhinisha ujenzi wa vituo vya mafuta jambo ambalo siku chache zilizopita lilijitokeza Katika maeneo ya Mikocheni na bado lawama zako na hatua unazozichukua umezielekeza katika kitengo cha mipangomiji manispaa ya Kinondoni

Mh. Waziri; sina shaka na weredi wako katika medani za kisheria pamoja na utashi wako binafsi katika kufuatilia mambo ya kijamii

Mh. Waziri; kwa wataalamu wa mipangomiji Kinondoni umewakaripia kwa kusema kwamba hawawashiriki Wenye ardhi yao ambao kwa maelezo yako watu hao ni Waheshimiwa madiwani.

Mh. Waziri; naomba nikukumbushe kwamba kwa mujibu wa sheria ya Ardhi No. 4 (1999) ikisomeka pamoja na marekebisho yake inaeleza bayana kwamba Ardhi ya Tanzania ina milikiwa na wananchi na Rais ni mdhamana wa hilo. Hata hivyo pamoja na kwamba ardhi inamilikiwa na wananchi lakin hawana idhini ya kuitumia moja kwa moja bila kibali cha mdhamana ambaye ni Rais, na kibali hicho cha matumizi hutolewa na mamlaka za upangaji zilizo kasimishiwa wadhifa huo kwa niaba ya Rais

Mh. Waziri moja ya kaul yako umeeleza kwamba wataalamu wasiamue kupanga matumizi ya ardhi bila kuwahusisha madiwani na ukaenda mbali ukasema. Naomba kunukuu ......."waacheni Wakae Waheshimiwa Madiwani waamue wenyewe kupanga mji wao au kuharibu mji wao...."

Mh. Waziri; kauli hii inakwenda kuididimiza taaluma ya upangajimiji, miji yetu imeharibika kutokana na ardhi kuamuliwa na wanasiasa wasio na weredi na masuala ya ardhi hususan katka kupangilia matumizi na kukidhi haja ya watumiaji ardhi.
Ni wazi kwamba kwa kauli hiyo ni sawa na kusema hakuna haja ya kuwepo wataalamu na badala yake wakae wawakilishi wa wananchi wajipangie wenyewe mahitaji ya matumizi katika ardhi yao jambo ambalo linakwenda kuharibu mionekano ya miji yetu, inakwenda kudidimiza mipangilio ya miji lakin pia sura ya nchi inakwenda kusiginwa kupitia kaul hii.

Mh. Waziri; nipende pia kukupa taarifa kwamba sekta ya ardhi tangu mwaka 2016 imeandamwa na matamko tofauti ya viongozi waandamizi, matamko ambayo yameleta shida kubwa sana katika usimamizi wa maendelezo ya makazi nchini

Moja ya shida hizo ni kuwa na muundo mbovu wa maamuzi na kiutendaji katika idara zote za Ardhi na maendeleo ya makazi, watumishi wa idara hizo pia kuandamwa na mazingira magumu kiutendaji na kupekelea kukosa moral ya kazi.

Mh. Waziri; kwa hakika kabisa bila kuwa na muundo bora wa utendaji katika wizara yako, unayo isimamia madudu yataongezeka, maamuzi ya kiutendaji katika Halmashauri yatafubaa, kwa sasa ni jambo la kawaida kuikuta ofisi ya aradhi haina umeme wala printer au photocopy machine, ofisi za ardhi hazina hata kabati au shelf la kutunzia kumbukumbu watumishi hawana bajet ya kutekeleza majukum yao

Mh. Waziri; watangulizi wako katika wizara yako kuna jambo walilifanya huenda ni kwa nia njema lakin linahitaji maboresho makubwa sana, mambo hayo ni muundo, utoaji wa matamko kwa njia ya Waraka, maelekezo yasio tekelezeka.

Mh. Waziri; nilikusikusikia ukisema kwamba watumishi wa ardhi wakatae maelekezo ya Waziri wao kwa kuwa si alie waajiri, unasahau kwamba kwa sasa watumishi hao hawapo tena TAMISEM bali unao hapo ofisin kwako na muajiri ni Katibu mkuu wako maana yake chombo cha kinidhamu ambacho ni muajiri ni Waziri, mtumishi anawezaje kukataa maelekezo ya waziri au kuhoji maelekezo ya mwajiri wake??

Mh. Waziri; nia yako ni njema sana katika kuisimamia wizara pamoja na kuiratibu ili ikupe matokeo utakayo lakin bila kuondoa changamoto za kimuundo ya mikocheni utayakuta maeneo mengi nchini. Wataalamu wa mipangomiji si sehem ya CMT hawaingii katika kamati tendaji huu mfumo utaumiza hii sekta

Mh. Waziri; kwa heshima kubwa sana nikusihi kufanya marekebisho ya kimuundo katika wizara yako. Punguza urasimu katika idara hizi na buni mfumo tendaji utakao saidia kuratibu matumizi ya ardhi ili hayo ya Mikocheni yasijitokeze tena, migogoro ya utumiaji ardhi ipungue na kila Mtanzania apate stahiki sahihi ya kutumia Ardhi ya nchi yake.

Mh. Waziri; mimi nikiwa kama Mtanzania na mwenye kuipenda sekta ya ardhi naomba nikushauri yafuatayo;-

1. Boresha mfumo kimuundo wa wizara yako

2. Ondoa kauli ya kuwaachia madiwani kupanga au kuharibu mji wao

3. Peleka wataalam wa mipangomiji ngazi ya kata kusaidia kudhibiti ukuaji holela wa miji na makazi

4. Unda tume ikusaidie kuchunguza chanzo cha ujenzi holela wa vituo vya mafuta na katika muda ambao tume itakuwa kazin sitisheni utoaji wa vibal vipya na majibu ya tume yalete mapendekezo ya namna bora ya kujenga vituo vya mafuta mijin

5. Tengeneza kamati shauri katika ofisi yako itumie kama chombo chako cha kiintelijensia, kamati hiyo iwe na wataalam wa ardhi pekee yaani mipangomiji, Afisa ardhi, Mpima ardhi na mthamini mali na ardhi. Kamati hii iwe na watu wenye wered wa hali ya juu sana na wanao weza kukueleza ukwel bila kujal ni uchungu au utamu wake

6. Ikikupendeza simamisha kwanza ziara zako na kutana na wataalam wa ardhi wakueleze changamoto zao kiutendaji pamoja na wadau wengine ili kwa pamoja mtoke na njia mahususi ya kushughulikia migogoro ya ardhi na udhibiti wa maendelezo ya ardhi nchini

Mh. Waziri; nikuombe radhi pale nilipo tumia neno lisilo kuvutia machoni mwako lakin kwa sababu ile ile ya nia njema ya kutekeleza Ilani ya CCM na kudumisha maelekezo ya Rais wetu mpendwa ya kuitaka sekta hii iwe na mchango katika maendeleo ya Taifa letu

Wasalam
Na
Ismal Chingwele
(Dip.CE, Bsc. URP, Msc. PPM, Msc. CEM)
Land Development Consultant-East Africa
Naomba kuelewa jambo kuhusu huyo Mkurugenzi wa mipangomiji aliyeelekeza pia asimanishwe sababu ya kanuni za 2018…nimeona hapo umesoma Bsc URP , hizo kanuni huwa anaandaa mkurugenzi wa mipango nini mwenyewe au kuna taratibu za kufuata na kuhusisha watu wengine ??? Lakini wat I remember mwaka 2018 Mkurugenzi wa mipangomiji alikuwa Prof Lupala , why asimamishwe huyu wa sasa ?? Ni maswali ambayo yananitatiza kidg ….
 
Kuna maswali mengi kuliko majibu.

Mchakato umeanza tangu kwa Mzee Lupalla.

Na Kuna tafiti kupata wapi tunahitaji maboresho, ushirikishwaji wa wa wadau na baadae kutengeneza rasimu ambayo lazima iridhiwe na mamlaka ambayo ni waziri mwenyewe.

Mkurugenzi huyu amebebeshwa tuu zigo. Maana yeye ametekeleza tuu vilivyokuwa kwenye pipeline. Watanzania wanaotakiwa wajue hizi taratibu... maana wako wanaodhani mkurugenzi anaweza kukaa tuu ofisini akatengeneza kanuni kama wanavyotaka kuaminishwa na Mh. Waziri.

Kama Zina makosa kwann wasijiuzuru wote..ofisi nzima.. maana wote wanahusika kwa namna moja au nyingine. Kuna namna watu watamgombanisba Mh. Rais na wananchi kwa kuwa short-sighted.

Kudhania ukiwafurahisha madiwani utakuwa umefanikisha azma yako. Ukweli wasomi Iko siku watawaambia wananchi madudu kwa lugha ya darasa la pili na huko kwenye ballot kutaitika.
 
Back
Top Bottom