aronstephy
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 300
- 618
Mabaraza yaliyowekwa na hii wizara ili kutatua migogoro kwenye ardhi na sio migogoro ya kifamili kwa sehemu kubwa yamefanyika kuwa kero kwa wananchi haswa wenye uhalali wa umiliki wa ardhi kwa viongozi husika kuendekeza rushwa sanaa.(Sijui posho zao haziwatoshi)
Kumekuwa na ucheleweshaji wa hukumu na pia kumekuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa sheria katika kutekeleza majukumu yao.Kuna kesi zimeshatolewa hukumu na mahakama za hakimu mkazi na hata mahakama ya rufaa lakini zinapopelekwa kwenye haya mabaraza kumekuwa na uzubaifu mkubwa wenye kutengeneza mianya mingi ya rushwa na hata kudhurumu mali za wananchi wanyonge walioshinda kwa uhalali kesi zao kwenye mahakama za mwanzo na hata za rufaa.
Nakuomba Mh Jerry Silaa peleka jopo la wataalam wako kwenye Baraza la ardhi mkoa wa Rukwa (kuanzia kata mpaka ya wilaya) wakawasaidie wananchi wanyonge wanaoibiwa haki zao na majizi yanatumia pesa na ushawishi walionao kwenye jamii kupoka maliza za wanyonge. Mwezi uliopita tu ulitoka kutoa maelekezo namna wanatakiwa kunya kazi ila bado wamekuwa kikwazo haswa. Kesi ya kusikilizwa mwezi mmoja inasikilizwa miezi mitatu na ukizingatia asaiv ni msimu wa kilimo.
Natanguliza Shukrani kwa Wizara husika nikijua hapa wapo wadau na wahusika watakao lifanyia kazi.