Military Politics: Is Magufuli in danger?

Hivi hata unaelewa maana ya Jeshi? Unajua hata JKT ni Jeshi pia? Sasa unajua kazi JKT wanazofanya?
Mimi nimefika Uswisi wanaolinda Balozi za nchi mbali mbali ni Wanajeshi wa Uswisi na siyo Polisi, yaani ukienda Ubalozini unakutana na Mwanajeshi wa Uswisi analinda!
Jeshi si mgambo wa kutumika kiholela.
 
Teknolojia ya mambo ya kijeshi inabadilika kila kuacha hivyo wanajeshi wetu wanatakiwa wawe mafunzoni na mazoezini kila uchao. Sio kubeba na kubangua korosho huku ikiuwa sekta binafsi
Hata yanayotufika huko Beni DRC,tungeweza kuepukwa nao kama mbinu na teknolojia mpya ingekua ndio kazi kubwa ya jeshi letu.
Mchezo wa kuwahusisha kila nyanja za biashara na utawala uraiani ni wa hatari sana
Mtoto akichezea wembe ........
Aliyeonja asali mwisho huchonga mjinga, time will tell..
 
Toeni ujinga wenu hapa..watu wanakaa hawana kazi wanakunywa tu bia na kula mishahara..Ni lazima washiriki na shughuli za uchumi..kaulizie nchi ya Misri ni Vipi imepiga hatua.
Wakianzisha operation Korosho kwa kulima Ekari 10000 Mtwara ndani ya miaka 5 watakua na shamba lao.
Watazalisha Korosho Nyingi sana. Wataamu hata kuuza bei wanayotaka hakuna atakayewauliza. Wataingizia Taifa fedha nyingi za kigeni. Naamini utakua ni ubunifu mzuri wenye Tija kwa Taifa.

Nia wanayo,
Ardhi ipo,
Uwezo wanao,
Sababu ipo wazi ni kulitumia jeshi kukuza uchumi.

Ni ushauri wa bure tu.
Wanachofanya kwa sasa hakiwezi kujenga uchumi mana ni kutumia nguvu zaidi kwenye mambo yanayoweza kujiendesha yenyewe kibiashara na serikali ikakusanya Chake.

Mkulima wa Korosho ,anapokea Sh. 3,300/- kwa kilo . Akiwa na Kilo 20,000 atakua amepokea Mil.66 kwa msimu Bila kulipa Kodi hata sh. mia moja. Ikumbukukwe kuwa mashamba Mengi ya Korosho yalikua ya Serikali na yaligawiwa wakulima yakiwa na korosho kama misitu , ... Wakati huo huo mfanyakazi anayepokea sh. Laki 4 kwa Mwezi anakatwa kodi sh.Elfu 40 ; ambapo kwa mwaka anapalipwa Jumla ya Tsh. Mil4.8 tu lakini analipa kodi sh. 480,000/- na makato mengine ambayo kimsingi yanaingia kwenye mzunguko wa Fuko la serikali kuu.
... Wanasiasa bhana!!Wanaangalia kura inayowaletea kula tuu !!!
 
ivi kwa raia ambao wanamiliki au wanaenda bureau kubadilisha vidolari unawapelekea jeshi kupambana nao na si mgambo wala polisi..
Mbaya zaidi hakuna onyo lililopiga marufuku watu kubadilisha fedha bureau na kwamba sasa ni BoT tu..
Na kwa nini ni Arusha tu ?
je ni kweli hata sekta ya utalii kuuliwa Kaskazini ili Mwanza na Chato wachukue nafasi ?
HUYU BABU SI LIMBUKENI PEKEE..
 
Sipingi kwamba waaifanye kazi.
Kazi gani zaid ya lindo? Kwa taarifa yako kada unaziona huku uraiani na kule kambini zipo. Watu wenye fani zote wapo na wanachapa kazi.muda wote. Labda.hujawahi kuishi kambini.. haya uwezi yajua.. lakin kama umewah utafaham wanavyochapa kaz
Ni kweli kabisa, wajeda wetu wanafanya kazi nyingi kama walivyo wajeda wengine dunia nzima.

Ujeda , dunia nzima upo kimataifa na unafanya mambo makubwa sana Kimataifa ,kisayansi na Kijamii kwa lengo la kuimarisha miundo mbinu yake na ya jamii.
Hii ipo miaka yote na nchi zote zenye amani kama ya kwetu . Lakini mambo mengi yalikua yanafanyika kimya kimya bila kukurupuka wala kuingiza mizuka ya wanasiasa.

Wajeda wetu wangeweza kujikita kwenye miradi yao ambayo ipo Tangu awamu ya kwanza na kama wanaona Kuna zao Fulani linalipa basi wangeanzisha maelfu ya Ekari na kuanza kilimo cha zao hilo bila kuingilia wananchi na wakulima wenye kutegemea vibiashara vyao vya mazao. Na faida itaonekana kwa kuongeza ajira na kukuza pato la nchi.
 
Najua na kukubali msisitizo wa matukio ambayo Amiri Jeshi mkuu amedhamiria kuyafanya, hasa yenye tija kwa Taifa.

Hata hivyo kwa maoni yangu, sikubsliani na matumizi ya Jeshi letu tukufu kwa mambo ambayo kimsingi na kikatiba ni ya kiraia.

Jeshi letu ni tiifu na proffessionals, lakini hili la kuwapeleka kusomba korosho, kwa kauli kuwa watazibangua na meno, na sasa kule Arusha kulinda maduka ya Forex!

Kuwachanganya wanajeshi na shughuli za kiraia kutaleta conflicts ambazo si za lazima, na mbaya zaidi kuwapunguzia morali.
Sokoine aliwahi kusema, wito wa jeshi ni ya vijana walio waliokalia harufu ya damu, kulinda nchi.

Tunaomba watumike kwa wito huo.
Afadhali mseme nyie wa huko huko mnaweza kusikilizwa
 
Toeni ujinga wenu hapa..watu wanakaa hawana kazi wanakunywa tu bia na kula mishahara..Ni lazima washiriki na shughuli za uchumi..kaulizie nchi ya Misri ni Vipi imepiga hatua.
Misri Imepiga hatua gani wewe?
Yani umeona Misri ndio nchi ya kutolea mfano kweli? Ni ya kawaida sana,nao wanjikongoja,wanategemea misaada na ndio wanaongoza kupokea misaada Afrika.
 
Povu la nini Mkuu

Ndugu yangu hakuna cha povu wala nini...yaani comments nyingine humu JF zinaudhi mno kwa kweli...Eti kinachomjia JPM kichwani ndicho anakifanya ..huu ni uzushi na udhalilishaji wa kiwango cha hali ya juu kabisa...Baadhi ya watanzania na ambao ni wengi na wazalendo kamwe hawawezi kukubaliana na kauli kama hii ya kizushi na udhalilishaji dhidi ya rais...Binafsi siwezi kukubaliana kamwe na kauli zinazomdhalilisha rais na ambaye ni mkuu wa nchi, dola na Amiri jeshi mkuu...rais ndiye kioo cha taifa letu...sasa kumuandika as if yeye ambaye hafikiri katika maamuzi yake ni wazi ni kumtusi na kumdhalilisha rais...wengine sisi hatuwezi kukubaliana na kauli hizi za kipuuzi na zenye mwelekeo siyo tu wa udhalilishaji bali hata wa usaliti kwa taifa hili...Wengine sisi tumeona mengi katika taifa hili ...tumebahatika kuziona awamu zote tano za uongozi wa nchi yetu...Tumemuona mwalimu Nyerere akifanya kazi na kweli niseme tumebahatika 'kufanya naye kazi' wakati huo tukiwa vijana wabichi kabisa...Tumemuona Mwinyi, Mkapa, JK na sasa JPM...tuna uzoefu wa kufahamu na kutambua mema na mabaya...Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu yake vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, JK na sasa JPM...lakini hatukufikia mahali kuanza kumntukana Nyerere wala Mwinyi wala Mkapa wala JK...UIla vijana wa siku hizi wasiojua hata nchi inaendeshwaje wakiwa wamejificha kwenye kitu kinaitwa uhuru wa habari na globalization wanadhani ni sawa sawa kumdhalilisha rais...hii siyo sahihi hata kidogo...Naanza kuwa na shaka kizazi kama hiki cha sasa kingekuwepo wakati wa mwalimu kingekuwaje?...
 
Toeni ujinga wenu hapa..watu wanakaa hawana kazi wanakunywa tu bia na kula mishahara..Ni lazima washiriki na shughuli za uchumi..kaulizie nchi ya Misri ni Vipi imepiga hatua.
Taasisi ya jeshi inaaminika,kuenziwa nakuheshimiwa sana na Watanzania.
Toka ukombozi Kusini mwa Afika, Vita ya Kagera na sasa Kongo, wanajeshi wetu wametujengea heshima kubwa.
Matumizi ya jeshi kwa mambo yasiyo ya dharura ya kuhatarisha amani ya nchi kidogo inaleta muonekano hasi.
Kuwachanganya wanajedhi ambso ni wanadamu, na raia laxima kutaleta uvunjifu wa discipline.
Mathalani, na siombei, kijana kama akiuza kotosho lorry zima Nangaurukuru, hata ukimkamata tayari umejenga kishawishi.
Aubkijana akiamua apatiwe dola zote kwenye Beureu De Change utamfanya nini.

Waswahili husema mla asali huchonga mzinga
 
Ndugu yangu hakuna cha povu wala nini...yaani comments nyingine humu JF zinaudhi mno kwa kweli...Eti kinachomjia JPM kichwani ndicho anakifanya ..huu ni uzushi na udhalilishaji wa kiwango cha hali ya juu kabisa...Baadhi ya watanzania na ambao ni wengi na wazalendo kamwe hawawezi kukubaliana na kauli kama hii ya kizushi na udhalilishaji dhidi ya rais...Binafsi siwezi kukubaliana kamwe na kauli zinazomdhalilisha rais na ambaye ni mkuu wa nchi, dola na Amiri jeshi mkuu...rais ndiye kioo cha taifa letu...sasa kumuandika as if yeye ambaye hafikiri katika maamuzi yake ni wazi ni kumtusi na kumdhalilisha rais...wengine sisi hatuwezi kukubaliana na kauli hizi za kipuuzi na zenye mwelekeo siyo tu wa udhalilishaji bali hata wa usaliti kwa taifa hili...Wengine sisi tumeona mengi katika taifa hili ...tumebahatika kuziona awamu zote tano za uongozi wa nchi yetu...Tumemuona mwalimu Nyerere akifanya kazi na kweli niseme tumebahatika 'kufanya naye kazi' wakati huo tukiwa vijana wabichi kabisa...Tumemuona Mwinyi, Mkapa, JK na sasa JPM...tuna uzoefu wa kufahamu na kutambua mema na mabaya...Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu yake vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, JK na sasa JPM...lakini hatukufikia mahali kuanza kumntukana Nyerere wala Mwinyi wala Mkapa wala JK...UIla vijana wa siku hizi wasiojua hata nchi inaendeshwaje wakiwa wamejificha kwenye kitu kinaitwa uhuru wa habari na globalization wanadhani ni sawa sawa kumdhalilisha rais...hii siyo sahihi hata kidogo...Naanza kuwa na shaka kizazi kama hiki cha sasa kingekuwepo wakati wa mwalimu kingekuwaje?...
Mkuu kwanini umejitwika jukumu la kumtetea.
Si kila ana mtazamo wako towards Rais ?
 
Ni kosa kubwa kufikiri as long as Mkuu wao upo sawa naye basi upo salama 100% no. Bregedi moja tu ikinogewa uongozi wa uraia ikasaliti aisee !!!

Tuwaache wafanye mambo yao na sisi tuhangaike na hizi siasa zetu za fitna fitna maana bila fitna siasa ya Tanzania huwezi kabisa hasa ukiwa mwana CCM.
 
Mkuu kwanini umejitwika jukumu la kumtetea.
Si kila ana mtazamo wako towards Rais ?

Kuwa na mitizamo tofauti dhidi ya rais siyo tatizo hata kidogo...tatizo linakuja pale baadhi na hasa vijana wa siku hizi wanapotumia lugha chafu, udhalilishaji, kejeli na matusi dhidi ya rais...
 
wahasimu wetu Malawi wanatu check tu. wajeda wetu wapo bize kubeba korosho na kukimbizana na wabadilisha pesa mtaani wenzetu wanaimarisha vifaru vyao kando ya Lake Nyasa.

kuna siku wajeda wetu tutawatuma kubeba viroba vya mahindi huko Sumbawanga sijui, wenzetu watatulia timing ya kufa mtu..... mara booooom!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom