Military Politics: Is Magufuli in danger?

Military Politics: Is Magufuli in danger?

Najua na kukubali msisitizo wa matukio ambayo Amiri Jeshi mkuu amedhamiria kuyafanya, hasa yenye tija kwa Taifa.

Hata hivyo kwa maoni yangu, sikubsliani na matumizi ya Jeshi letu tukufu kwa mambo ambayo kimsingi na kikatiba ni ya kiraia.

Jeshi letu ni tiifu na proffessionals, lakini hili la kuwapeleka kusomba korosho, kwa kauli kuwa watazibangua na meno, na sasa kule Arusha kulinda maduka ya Forex!

Kuwachanganya wanajeshi na shughuli za kiraia kutaleta conflicts ambazo si za lazima, na mbaya zaidi kuwapunguzia morali.
Sokoine aliwahi kusema, wito wa jeshi ni ya vijana walio waliokalia harufu ya damu, kulinda nchi.

Tunaomba watumike kwa wito huo.
 
Ushauri mzuri huu. Wsnajeshi wabaki kwenye field yao. Maana sasa kufanya kazi za kiraia ni matumizi mabaya ya rasilimali
Wanajeshi wakitumika kufyeka nyasi mitaani it is ok, wakilinda forex bureaux sio ok. Wakibeba korosho sio ok.
 
Kuna kazi zao muhimu, za kufanya sasa Raia wa kawaida wafanye shughuli gani? Maana wajeda sio wanasiasa kulinda mabenki hufanywa na kampuni za ulinzi sasa ukitumia wajeda Raia wengine watapata wapi kazi.
Wanajeshi wakitumika kufyeka nyasi mitaani it is ok, wakilinda forex bureaux sio ok. Wakibeba korosho sio ok.
 
Nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha

JPM anatumia Jeshi katika operesheni mbalimbali lakini je anaelewa kwamba The army has no loyalty?Katika siasa za majeshi mwanajeshi hafundishwi siasa ya loyalty anafundishwa survival.

Unapoamua kutumia Jeshi katika operesheni yoyote ila lazima iwe na lengo moja Kutishia,kuogopesha na kushurutisha.Lakini unapolitumia Jeshi kushughulika na mambo ya raia unatakiwa ujue kwamba mahaba kati ya Jeshi na Raia yanaweza kufanya kuibuka kwa mawazo ya kimapinduzi kwa wanajeshi hasa iwapo unawatumia kukandamiza wananchi na wanyonge.

Kumbuka Soldiers have no Loyalty,they train to survive.

Nimshauri tu mheshimiwa raisi hata kama hana imani na watendaji wa serikali yake awe makini na matumizi ya jeshi letu.

Asiwageuze wanajeshi wetu vibarua wakutumwa kushughulikia hata issue zisizo na maslahi ya taifa.

Ha wa watu hawajawa trained kubeba magunia ya korosho na kubangu,Hawajawa trained kujenga kuta na kufanya shughuli za suluba.Wamefundishwa Vita,Kama usipowapa Vita watakuletea Vita.
Magufuli ameletwa kwama njia ya ukombozi wa watanzania, kwamba yeye ni njia ya kuiua ccm dhalimu na serikali yake ili ile nyingine iweze kuja. Na njia hizi ni sahihi kabisa ktk kuibonoa serikali hii ya kibabeli.

Acheni wafu wazikane.
 
Rais anatumia Jeshi kama vibaraka wake wa kutekelezasera zake za kisiasa.
Asichokijua Rais ni kwamba Jeshi(JWTZ)ni jeshi la ULINZI na sio KIKOSI cha uzalishaji mali.
JWTZ wanapaswa kulinda amani ya nchi na majirani zetu sio kwenda kufanya kazi za JKT!
Rais wetu hana staha kabisa ......JWTZ wapo kwa kazi za kifani sio kubangua korosho.....hawa wachache anaowateua kwenye nyadhifa za kisiasa sio wawajibikaji wa jeshi maana wengi wao ni wastaafu(wanajeshi hawastaafu kwenye fani zao za kijeshi)...!
Jeshi La Kubangua Korosho Tanzania ( JLKT)
 
Najua na kukubali msisitizo wa matukio ambayo Amiri Jeshi mkuu amedhamiria kuyafanya, hasa yenye tija kwa Taifa.

Hata hivyo kwa maoni yangu, sikubsliani na matumizi ya Jeshi letu tukufu kwa mambo ambayo kimsingi na kikatiba ni ya kiraia.

Jeshi letu ni tiifu na proffessionals, lakini hili la kuwapeleka kusomba korosho, kwa kauli kuwa watazibangua na meno, na sasa kule Arusha kulinda maduka ya Forex!

Kuwachanganya wanajeshi na shughuli za kiraia kutaleta conflicts ambazo si za lazima, na mbaya zaidi kuwapunguzia morali.
Sokoine aliwahi kusema, wito wa jeshi ni ya vijana walio waliokalia harufu ya damu, kulinda nchi.

Tunaomba watumike kwa wito huo.
A Country is Not a Company Running a Government is Not like Family Matters
 
Kuna kazi zao muhimu, za kufanya sasa Raia wa kawaida wafanye shughuli gani? Maana wajeda sio wanasiasa kulinda mabenki hufanywa na kampuni za ulinzi sasa ukitumia wajeda Raia wengine watapata wapi kazi.
Wanatumika sababu hao waliotakiwa wameshindwa timiza majukumu yao eidha kiutendaji kazi au uaminifu.
 
Toeni ujinga wenu hapa..watu wanakaa hawana kazi wanakunywa tu bia na kula mishahara..Ni lazima washiriki na shughuli za uchumi..kaulizie nchi ya Misri ni Vipi imepiga hatua.
 
Kwahyo had kutumia jeshi it means serikali ime prove failures kitu ambacho ni hatari nchi yetu haiko chini ya jeshi iko chini ya utawala wa kisheria. Sasa huoni tu kuwatumia ni hatari maana jeshi hutumika kama last card hasa nchi ikiwa kwenye critical stage. Maana huwezi sema huamini vyombo vingine vya dola huku ukiamini jeshi, watu if wakikengeuka wakaamua kuongoza nchi kinguvu
Wanatumika sababu hao waliotakiwa wameshindwa timiza majukumu yao eidha kiutendaji kazi au uaminifu.
 
Aliekwambia kuwa jeshini hakuna kazi ni nani. Wanazonyingi sana.., naish karibia na kambi.. wanajeshi wanachakarika muda wote.

Ww ndio hufaluatilii mambo
Toeni ujinga wenu hapa..watu wanakaa hawana kazi wanakunywa tu bia na kula mishahara..Ni lazima washiriki na shughuli za uchumi..kaulizie nchi ya Misri ni Vipi imepiga hatua.
 
ni kweli wanajeshi hufundishwa vita pekee!!??......tunawasubili wataalam mje mthibitishe.
 
Aliekwambia kuwa jeshini hakuna kazi ni nani. Wanazonyingi sana.., naish karibia na kambi.. wanajeshi wanachakarika muda wote.

Ww ndio hufaluatilii mambo
mbona wanafanya kazi nyingi tu mnataka wakae tu makambini bila kufanya kazi mimi binafisi na mshukru baba jesca kuwapa kazi waache kufuga vitambi tu
 
mbona wanafanya kazi nyingi tu mnataka wakae tu makambini bila kufanya kazi mimi binafisi na mshukru baba jesca kuwapa kazi waache kufuga vitambi tu
Nadhan hujanipata uzuri. Sipingi kuwa wasipangiwe kazi hapana, ila mule kambini kuna kada kama za uraiani, na wanachapa kazi muda wote.. amna mtu unamkuta amekaa kizembe mle ndani.
 
Back
Top Bottom