Najua na kukubali msisitizo wa matukio ambayo Amiri Jeshi mkuu amedhamiria kuyafanya, hasa yenye tija kwa Taifa.
Hata hivyo kwa maoni yangu, sikubsliani na matumizi ya Jeshi letu tukufu kwa mambo ambayo kimsingi na kikatiba ni ya kiraia.
Jeshi letu ni tiifu na proffessionals, lakini hili la kuwapeleka kusomba korosho, kwa kauli kuwa watazibangua na meno, na sasa kule Arusha kulinda maduka ya Forex!
Kuwachanganya wanajeshi na shughuli za kiraia kutaleta conflicts ambazo si za lazima, na mbaya zaidi kuwapunguzia morali.
Sokoine aliwahi kusema, wito wa jeshi ni ya vijana walio waliokalia harufu ya damu, kulinda nchi.
Tunaomba watumike kwa wito huo.