Ndugu yangu hakuna cha povu wala nini...yaani comments nyingine humu JF zinaudhi mno kwa kweli...Eti kinachomjia JPM kichwani ndicho anakifanya ..huu ni uzushi na udhalilishaji wa kiwango cha hali ya juu kabisa...Baadhi ya watanzania na ambao ni wengi na wazalendo kamwe hawawezi kukubaliana na kauli kama hii ya kizushi na udhalilishaji dhidi ya rais...Binafsi siwezi kukubaliana kamwe na kauli zinazomdhalilisha rais na ambaye ni mkuu wa nchi, dola na Amiri jeshi mkuu...rais ndiye kioo cha taifa letu...sasa kumuandika as if yeye ambaye hafikiri katika maamuzi yake ni wazi ni kumtusi na kumdhalilisha rais...wengine sisi hatuwezi kukubaliana na kauli hizi za kipuuzi na zenye mwelekeo siyo tu wa udhalilishaji bali hata wa usaliti kwa taifa hili...Wengine sisi tumeona mengi katika taifa hili ...tumebahatika kuziona awamu zote tano za uongozi wa nchi yetu...Tumemuona mwalimu Nyerere akifanya kazi na kweli niseme tumebahatika 'kufanya naye kazi' wakati huo tukiwa vijana wabichi kabisa...Tumemuona Mwinyi, Mkapa, JK na sasa JPM...tuna uzoefu wa kufahamu na kutambua mema na mabaya...Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu yake vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, JK na sasa JPM...lakini hatukufikia mahali kuanza kumntukana Nyerere wala Mwinyi wala Mkapa wala JK...UIla vijana wa siku hizi wasiojua hata nchi inaendeshwaje wakiwa wamejificha kwenye kitu kinaitwa uhuru wa habari na globalization wanadhani ni sawa sawa kumdhalilisha rais...hii siyo sahihi hata kidogo...Naanza kuwa na shaka kizazi kama hiki cha sasa kingekuwepo wakati wa mwalimu kingekuwaje?...