Military Politics: Is Magufuli in danger?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,019
3,880
Nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha

JPM anatumia Jeshi katika operesheni mbalimbali lakini je anaelewa kwamba The army has no loyalty?Katika siasa za majeshi mwanajeshi hafundishwi siasa ya loyalty anafundishwa survival.

Unapoamua kutumia Jeshi katika operesheni yoyote ila lazima iwe na lengo moja Kutishia,kuogopesha na kushurutisha.Lakini unapolitumia Jeshi kushughulika na mambo ya raia unatakiwa ujue kwamba mahaba kati ya Jeshi na Raia yanaweza kufanya kuibuka kwa mawazo ya kimapinduzi kwa wanajeshi hasa iwapo unawatumia kukandamiza wananchi na wanyonge.

Kumbuka Soldiers have no Loyalty,they train to survive.

Nimshauri tu mheshimiwa raisi hata kama hana imani na watendaji wa serikali yake awe makini na matumizi ya jeshi letu.

Asiwageuze wanajeshi wetu vibarua wakutumwa kushughulikia hata issue zisizo na maslahi ya taifa.

Ha wa watu hawajawa trained kubeba magunia ya korosho na kubangu,Hawajawa trained kujenga kuta na kufanya shughuli za suluba.Wamefundishwa Vita,Kama usipowapa Vita watakuletea Vita.

Kama tunavyojua Jeshi ni kitu muhimu sana katika nchi yoyote ile duniani
Jeshi hulipa kiburi nchi yoyote kama linatunzwa vizuri na kutumika katika mambo yanayohusu sanaa ya vita

Siku zote kazi za jeshi katika nchi zinajulikana na likitoka nje ya nchi pia kazi zake zinajulikana

Je likiwa ndani ya nchi kazi yake ni nini?
Moja kati ya kazi kubwa za Jwtz likiwa ndani ya nchi ni kulinda mipaka yake na kusaidia mambo ya dharura kama mafuriko katika nchi, meli kuzama Yaani kazi zao pia ni kuhusu mambo ya uokozi katika nchi kwa ujumla wake

Katika nchi yetu tumeshuhudia kile kinachoitwa ni kulifanya Jwtz lisikae bila kazi.
Yaani kulitumia katika mambo mbalimbali ya kijamii!!!
Hilo silipingi lakini tuangalie ni mambo gani hayo ya kijamii katika kukitumia jeshi letu pendwa ili tusije kuliingiza kwenye tamaa yoyote ile

Pia kuna juhudi za maksudi kuliingiza jeshi letu kwenye mambo mbalimbali ikiwemo siasa,na pesa,
Siku wakielewa chochote kuhusu pesa ndani ya nchi hii basi tuandike maumivu kwa sababu wana uwezo wa kufanya chochote na hakuna wa kuwaambia kitu

Nimemsikia sijui ni gavana wa benki kuu akisema waliamua kulitumia Jwtz katika kupambana na utakatishaji wa hela ndani ya nchi, sio jambo baya ila ubaya ulipokuja ni kulitumia Jwtz katika kazi hiyo.

Tunaweza kufikiri tunafanya vizuri lakini Tamaa ameumbiwa binadamu na Tamaa hiyo ni bora akawa nayo mwingine lakini sio Jwtz

Nchi ambazo wanajeshi wamepindua nchi na kushika wao madaraka inaonyesha wanajeshi walikomba pesa zote na kujilipa bila kuangalia pesa hizo zilikuwa na matumizi gani katika nchi

Ni tahadhari tu tusilitumie sana jeshi katika mambo ya siasa au kuwaonyesha pesa maana siku isiyo na jina yaja

Nawasilisha

Nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha

JPM anatumia Jeshi katika operesheni mbalimbali lakini je anaelewa kwamba The army has no loyalty?Katika siasa za majeshi mwanajeshi hafundishwi siasa ya loyalty anafundishwa survival.

Unapoamua kutumia Jeshi katika operesheni yoyote ila lazima iwe na lengo moja Kutishia,kuogopesha na kushurutisha.Lakini unapolitumia Jeshi kushughulika na mambo ya raia unatakiwa ujue kwamba mahaba kati ya Jeshi na Raia yanaweza kufanya kuibuka kwa mawazo ya kimapinduzi kwa wanajeshi hasa iwapo unawatumia kukandamiza wananchi na wanyonge.

Kumbuka Soldiers have no Loyalty,they train to survive.

Nimshauri tu mheshimiwa raisi hata kama hana imani na watendaji wa serikali yake awe makini na matumizi ya jeshi letu.

Asiwageuze wanajeshi wetu vibarua wakutumwa kushughulikia hata issue zisizo na maslahi ya taifa.

Ha wa watu hawajawa trained kubeba magunia ya korosho na kubangu,Hawajawa trained kujenga kuta na kufanya shughuli za suluba.Wamefundishwa Vita,Kama usipowapa Vita watakuletea Vita.

Tawala za kijeshi ulimwenguni pote huwa hazijianzii tu bali husukumizwa kwenye majengo ya ikulu na ngazi zote za maamuzi kupitia mifumo ya kiraia iliyoshindwa, kulegalega, kandamizi, dhalimu, kiimla na kikabila. Kwa muhtasari tu wa tabia za tawala hizi ni kwamba;-

1. Wanajeshi wa ngazi za juu wanaposhirikishwa kufanya maamuzi ya kiraia kwa kudhani huko kutaongeza utii wao kwa serikali iliyopo madarakani kama ilivyokuwa enzi za Hosni Mubaraka. Hali hii hufanya wanajeshi wa ngazi za juu kuwatumia wale wa vyeo vya chini kufanya mapinduzi ili wao wasionekane kuwa chanzo cha kutotii.( Field mashall Tantawi na Abdelfatah Al sisi).

2. Wanajeshi ni mjumuiko wa wananchi wenye elimu na mitazamo tofauti isipokuwa wenye falsafa inayofanana sana. Heshimu aliyejuu yako hasa akiwa mwanajeshi mwenzako hiyo ndio falsafa yao. Katika mazingira ya kawaida ambapo katiba huongoza maamuzi yote ya kiutawala na kuheshimiwa jeshi ni chombo cha kusimamia na ulinzi na kulinda mipaka ila pale katiba inapokuwa majaribuni jeshi laweza kuwa chombo cha kuongeza mtanziko wa kiutawala kwa kujiingiza kwenye uongozi wa nchi.

3. Watawala waoga hujikuta wamekabidhi mamlaka ya uongozi jeshini bila kujua. Pale inapotokea mtawala wa kikatiba ni mwoga dhidi ya wapinzani wake kisiasa kwa kushindwa kujibu hoja zao, kuminya democrasia, kuiba mali ya umma na kupora haki za wanahabari hujikuta amekuwa adui wa wa wananchi wenzake hivyo hujitafutia huruma toka vikosi vya majeshi ambavyo navyo hujikuta kuomba malipo ya fadhila kwa kuingilia maamuzi ya utawala na hivyo kujigeuza watawala halisi.

4. Raia wanyonge na makundi muhimu ya kuboresha uchumi katika jamii yakikandamizwa hupelekea taifa kuingia kwenye mtanziko wa kimaendeleo na kukwamisha huduma za kijamii na kiraia ambapo hiyo hupelekea hata wanajeshi kukosa baadhi ya stahili zao huku mafisadi wachache wakijilimbikizia mali. hali hii huishia kuwafanya wanajeshi kuingilia masuala ya maamuzi kama ilivyotokea Zimbabwe ambapo jeshi lilimpumzisha swahiba wao Mugabe na hadi leo Zimbabwe ina unafuu kabisa kuliko enzi za Dictator huyo katili.

5. Kwa ufupi utawala wa kijeshi sio mbaya kutegemea na muundo wa jeshi na malezi ya kiutamaduni yaliyojengeka kati ya wananchi na jeshi lao, uwezo wa kiutawala ambao jeshi linao mfano wasomi wa taaluma mbalimbali, uhusiano wa kimataifa ambao jeshi linao vyote hivyo huchangia utawala bora wa kijeshi.

Kuhusu jeshi letu kwa sasa linahitaji bado kujengewa uwezo wa kuongoza taasisi achilia mbali nchi kutokana na kuwa na wasomi wachache, wasomi wasio na ujuzi wa kivitendo, tamaa ya kuishi kifahari, mitazamo isiyo ya kijeshi mfano wengi wapo jeshini kutokana na kukosa kazi mahali pengine hivyo kuishi kama sio wanajeshi. Ushauri ni kwamba ili Jeshi liweze kuwa na uwezo ni vizuri likafanya recruit toka watumishi wa umma wenye umri, elimu na uzoefu unaohitajika ili kwa mikataba maalumu wachangie huo uwezo wao na kulijengea jeshi letu uwezo wa kiutalawala kwenye nyanja mbalimbali.
Jeshi oyeeeee

Jeshi la Wananchi Tz, (JWTZ) ni chombo adhimu, angalau bado linaheshimika. Kuna sababu nyingi za kuliheshimu jeshi letu, ingawa sababu hizo zinagawanyika katika makundi makuu mawili. Moja, ni sababu zitokanazo na kazi za jeshi lenyewe. Hapo kuna nidhamu ya jeshi na wanajeshi (bila kujali wachache wanaoharibu taswira hiyo), misheni mbalimbali za ndani na nje zilizofanikishwa na jeshi letu, shughuli mbalimbali za kijamii katika kujenga taifa pamoja na kutoa huduma za kijamii (elimu, afya nk)

Pili, ni sababu zinazotokana na wananchi wenyewe. Hakuna namna wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kuheshimu na kulienzi jeshi lao. Na kwa bahati nzuri, watanzania wamekuzwa kwa namna hiyo, ya kuliheshimu jeshi.

Natambua kuna baadhi ya watumishi wa jeshi wanaotumia 'sare' na vitambulisho vyao kujinufaisha mitaani, na wakati mwingine kufanya vitendo vya uonevu kwa raia. Hao ni wajinga wachache ambao leo sioni haja kuwajadili.

Pamoja na hayo, kuna jambo la kustua ambalo kama halitadhibitiwa, jeshi hili adhimu litageuka kuwa janga taifa; kutumiwa hovyo na serikali.
Narudia kwa msisitizo; "Kutumiwa hovyo na serikali".

Tulianza kuona jambo hili wakati Rais Magufuli akiwatunuku kamisheni wanajeshi waliohitimu mafunzo kule Arusha, Septemba mwaka 2017. Kwenye shuguli hizo za kijeshi, Rais alionekana kujadili jambo na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, liloashiria kuwapo kwa mpango wa kufanya tukio la kisiasa.

Mpango unaoatajwa kuwapo ni ule wa kuwaita watu walioandaliwa (miongoni mwa wananchi waliohudhuria) ili wamsifie Rais kwa maneno waliopandikizwa. Baada ya Gambo kushindwa kuandaa mpango huo, Rais alisikika akimtukana mkuu huyo wa mkoa. Ilikuwa ni ishara mbaya kwa matukio hayo kufanyika kwenye shughuli za kijeshi.

Haikuwa bahati mbaya, matukio ya aina hiyo yanaendelea. Inaonekana ni kama hulka ya serikali ya awamu ya tano kulitumia jeshi, hata kwenye mambo yasio ya lazima.

Kutumia jeshi kwenye sakata la korosho, ni muendelezo wa matumizi ya hovyo ya jeshi. Pamoja na mikurupuko mingine, karibuni tutaona mpango huo ulivyoleta matokeo mabaya.

Tunaambiwa pia, jeshi limepewa kazi ya kulinda maduka ya kubadilishia fedha, eti kuna operesheni maalum ya kudhibiti wanaotakatisha fedha, inastua.

Je! Serikali haina mifumo ya kudhibiti utakatishaji fedha badala yake inatuma wanajeshi wakae kwenye milango ya maduka ya kubadilisha fedha? Natamani kujua taaluma za wanajeshi waliosimama kwenye milango ya maduka kama wana ufahamu wa masuala ya utakatishaji fedha.

Rais ana wasiwasi?
Matumizi ya jeshi, au kukimbilia kutumia jeshi katika mambo yanayoweza kufanywa na taasisi zingine, ni ishara ya nini? Wasiwasi? Hofu? Ulimbukeni wa madaraka? Au vitisho?

Ikiwa sababu ni wasiwasi na/au hofu ya kushindwa kuongoza, maana yake tayari umeshinda kuongoza. Hapa nirejee maneno ya Profesa Mkandala, kwamba kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wa hiari. Ikiwa Rais anatumia jeshi kwa kukosa imani na taasisi zingine, maana yake ameshindwa kuongoza taasisi hizo.

Je! Ni vitisho? Kama ni vitisho, Rais anamtishia nani? Haiwezekani kutumia jeshi kuwatisha watu mmoja mmoja ambao wanaonekana kuwa maadui (wa kisiasa). Jeshi linapotumika kwa lengo la vitisho, maana yake wanaotishiwa ni wananchi. Kuwatisha wananchi unaowaongoza ni ishara ya kushindwa kuongoza.

Bado natafuta kujua lengo la matumizi ya jeshi yasiyo ya lazima.

Mwisho, mimkumbushe Rais Magufuli na wafuasi wake, madaraka ni kama mchanga. Kadiri unavyoukumbatia mchanga kiganjani ndivyo unavyokuponyoka, na ukilegeza vidole pia unakuponyoka. Unahitaji kuwa mtu wa kiasi (gentle), mtu wa hekima na maarifa.

Ni vema kujua kwamba hakuna mahala pengine baada ya jeshi. Ikiwa matumizi haya ya jeshi yana lengo la kujitutumua, kutunisha misuli, maana yake umejitutumua hadi mwisho, na umetunisha misuli hadi mwisho, kwa kuwa jeshi ndio mahali pa mwisho. Hakuna pengine pa kukimbilia. Kutumia jeshi badala ya taasisi zingine ndio tafsiri ya kuyakumbatia madaraka (kama mchanga kiganjani) kwa nguvu zote, kifuatacho ni madaraka hayo kukuponyoka.

Ni vema hatua za haraka zikachukuliwa kudhibiti matumizi haya ya jeshi yasio ya lazima.
Nimeandika.
 
Rais anatumia Jeshi kama vibaraka wake wa kutekelezasera zake za kisiasa.
Asichokijua Rais ni kwamba Jeshi(JWTZ)ni jeshi la ULINZI na sio KIKOSI cha uzalishaji mali.
JWTZ wanapaswa kulinda amani ya nchi na majirani zetu sio kwenda kufanya kazi za JKT!
Rais wetu hana staha kabisa ......JWTZ wapo kwa kazi za kifani sio kubangua korosho.....hawa wachache anaowateua kwenye nyadhifa za kisiasa sio wawajibikaji wa jeshi maana wengi wao ni wastaafu(wanajeshi hawastaafu kwenye fani zao za kijeshi)...!
 
Nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha

JPM anatumia Jeshi katika operesheni mbalimbali lakini je anaelewa kwamba The army has no loyalty?Katika siasa za majeshi mwanajeshi hafundishwi siasa ya loyalty anafundishwa survival.

Unapoamua kutumia Jeshi katika operesheni yoyote ila lazima iwe na lengo moja Kutishia,kuogopesha na kushurutisha.Lakini unapolitumia Jeshi kushughulika na mambo ya raia unatakiwa ujue kwamba mahaba kati ya Jeshi na Raia yanaweza kufanya kuibuka kwa mawazo ya kimapinduzi kwa wanajeshi hasa iwapo unawatumia kukandamiza wananchi na wanyonge.

Kumbuka Soldiers have no Loyalty,they train to survive.

Nimshauri tu mheshimiwa raisi hata kama hana imani na watendaji wa serikali yake awe makini na matumizi ya jeshi letu.

Asiwageuze wanajeshi wetu vibarua wakutumwa kushughulikia hata issue zisizo na maslahi ya taifa.

Ha wa watu hawajawa trained kubeba magunia ya korosho na kubangu,Hawajawa trained kujenga kuta na kufanya shughuli za suluba.Wamefundishwa Vita,Kama usipowapa Vita watakuletea Vita.
Ujumbe mzito sana huu.
 
Rais anatumia Jeshi kama vibaraka wake wa kutekelezasera zake za kisiasa.
Asichokijua Rais ni kwamba Jeshi(JWTZ)ni jeshi la ULINZI na sio KIKOSI cha uzalishaji mali.
JWTZ wanapaswa kulinda amani ya nchi na majirani zetu sio kwenda kufanya kazi za JKT!
Rais wetu hana staha kabisa ......JWTZ wapo kwa kazi za kifani sio kubangua korosho.....hawa wachache anaowateua kwenye nyadhifa za kisiasa sio wawajibikaji wa jeshi maana wengi wao ni wastaafu(wanajeshi hawastaafu kwenye fani zao za kijeshi)...!
Bado anataka aunde Timu ya Taifa yenye wanajeshi watupu.
 
Rais anatumia Jeshi kama vibaraka wake wa kutekelezasera zake za kisiasa.
Asichokijua Rais ni kwamba Jeshi(JWTZ)ni jeshi la ULINZI na sio KIKOSI cha uzalishaji mali.
JWTZ wanapaswa kulinda amani ya nchi na majirani zetu sio kwenda kufanya kazi za JKT!
Rais wetu hana staha kabisa ......JWTZ wapo kwa kazi za kifani sio kubangua korosho.....hawa wachache anaowateua kwenye nyadhifa za kisiasa sio wawajibikaji wa jeshi maana wengi wao ni wastaafu(wanajeshi hawastaafu kwenye fani zao za kijeshi)...!
In short tuseme tu kuwa ana-abuse power tuliyompa ya u-kamanda-in-chifu vibaya mno

Kuna haja ya Bunge kuanza process ya kumu-impeach huyu Bwana kabla nchi yetu haijatumbukia jumla jumla shimoni
 
Kwa mawazo yake anaona kama hakuna vita wanajeshi wanapata mishahara ya bure.
Kwa anachofanya sasa wanajeshi watajenga ushabiki wa kisiasa na watakuwa upande wa wanaoonewa.
Jambo moja la wanajeshi wote ulimwengu ni kusimama ama kwa maslahi yao wenyewe au maslahi ya wanyonge ila huwezi kuwatumia kwa maslahi yake.Hataelewa hilo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom