Mikasa iliyotokea kipindi wanaigiza filamu za Yesu

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Haikuwa kazi nyepesi kuigiza movie za Yesu. Songombingo lilianza katika ile scene ya msalabani. Scenes zote ilikuwa rahisi sana isipokuwa ile ya msalabani.

Kwenye ile movie ya mwaka 1979 ya Yesu iliyoigizwa na Decon, Brian Deacon anasimulia kwenye interview kuwa wakati wa scene ya msalabani haikuwa nyepesi kuigizwa kwani walikumbana na dhoruba kubwa la radi kiasi cha kushindwa kuigiza hivyo wakasubiri siku inayofuata. Haikubadilika, Hali ilitulia lakini baada ya Decon kuwekwa msalabani upepo mkali ulivuma, lakini hawakukata tama. Movie ya yesu ya Brian Deacon ndio movie mpaka sasa inayoshikilia rekodi ya Dunia ya kutazamwa mara nyingi na pia inashikilia rekodi ya movie iliyotafsiriwa kwenda lugha mbalimbali Duniani. Movie hii ilichezewa huko katika milima ya nchini Israel. Na mpaka leo hii Director (Muongozaji) wa filamu huyo hajulikani ni nani. Na baadhi ya waigizaji walishafariki na muigizaji mkuu aliyeigiza kama Yesu sasa ana takribani miaka 75 mwaka huu 2024.

Mikasa Haikutokea kwao tu kina Deacon bali hata kwenye movie ya Passion of Christ ya 2004, Muandaaji wa hiyo filamu, Mel Gibson alielezea songombingo la namna hiyo, walisitisha kuigiza filamu hiyo kwa siku tatu mfululizo kutokana na radi za mara kwa mara zilizoibuka tu na tetemeko la ardhi, anasema hata Jim Caviezel aliyeigiza kama Yesu alinusurika kuuwawa na radi. Pia alikumbwa na magonjwa mbalimbali ya mapafu ikiwemo Pneumonia, pamoja na kuishiwa joto la mwili. Filamu hiyo iliigizwa huko Italia katika kipindi cha majira ya baridi kali.
 
YESU ni MUNGU

Hiyo Mikasa ni ishara ya kuwa hafananishwi na chochote.

Luka 18
19 Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema ila Mungu peke yake.

Yohana 17
3 Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma.

Mathayo 27:46​

Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
 
Haikuwa kazi nyepesi kuigiza movie za Yesu. Songombingo lilianza katika ile scene ya msalabani. Scenes zote ilikuwa rahisi sana isipokuwa ile ya msalabani.

Kwenye ile movie ya mwaka 1979 ya Yesu iliyoigizwa na Decon, Brian Deacon anasimulia kwenye interview kuwa wakati wa scene ya msalabani haikuwa nyepesi kuigizwa kwani walikumbana na dhoruba kubwa la radi kiasi cha kushindwa kuigiza hivyo wakasubiri siku inayofuata. Haikubadilika, Hali ilitulia lakini baada ya Decon kuwekwa msalabani upepo mkali ulivuma, lakini hawakukata tama. Movie ya yesu ya Brian Deacon ndio movie mpaka sasa inayoshikilia rekodi ya Dunia ya kutazamwa mara nyingi na pia inashikilia rekodi ya movie iliyotafsiriwa kwenda lugha mbalimbali Duniani. Movie hii ilichezewa huko katika milima ya nchini Israel. Na mpaka leo hii Director (Muongozaji) wa filamu huyo hajulikani ni nani. Na baadhi ya waigizaji walishafariki na muigizaji mkuu aliyeigiza kama Yesu sasa ana takribani miaka 75 mwaka huu 2024.

Mikasa Haikutokea kwao tu kina Deacon bali hata kwenye movie ya Passion of Christ ya 2004, Muandaaji wa hiyo filamu, Mel Gibson alielezea songombingo la namna hiyo, walisitisha kuigiza filamu hiyo kwa siku tatu mfululizo kutokana na radi za mara kwa mara zilizoibuka tu na tetemeko la ardhi, anasema hata Jim Caviezel aliyeigiza kama Yesu alinusurika kuuwawa na radi. Pia alikumbwa na magonjwa mbalimbali ya mapafu ikiwemo Pneumonia, pamoja na kuishiwa joto la mwili. Filamu hiyo iliigizwa huko Italia katika kipindi cha majira ya baridi kali.
Seen.
 
Back
Top Bottom