Jinsi Kesi ya Yesu ilivyovunja Sheria

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,640
697,940
Kesi ya Yesu Kristo hadi kuhumiwa Kifo ilipita katika sehemu Sita (6) katika Uendeshaji wake katika Mahakama mbili: MAHAKAMA YA KIDINI (KIYAHUDI) na MAHAKAMA YA KISIASA (KIRUMI). Na katika Mahakama hizi zote mbili, Mashitaka yalikuwa tofauti kulingana na Makosa yaliyoletwa kwenye Mahakama husika.
Katika kila Mahakama, kulikuwa na hatua tatu tatu kama ifuatavyo:

I. MAHAKAMA YA KIDINI
Hapa alipitia hatua zifuatazo:
1. Yesu mbele ya ANASI
2. Yesu mbele ya KAYAFA
3. Yesu mbele ya BARAZA (SANHEDRIN)

Katika Mahakama ya Kidini ya Kiyahudi, Yesu alishtakiwa kwa Makosa Mawili:
1. Kukufuru (Alisema atalivunja Hekalu na Kulijenga kwa Siku Tatu, hii ilikuwa Kufuru)
2. Kujiita Mwana wa Mungu (Masiya)


Makosa yote hayo yalikuwa ni Makosa ya Kidini na alitakiwa aadhibiwe kwa taratibu za Kidini katika Mahakama hiyo ya Kidini.

Lengo la Viongozi wa Kidini ya Kiyahudi lilikuwa ni LAZIMA Yesu afe kwasababu walimwona kama Mwiba kwenye Maslahi yako. Ni kama alikuwa anaweka Mchanga kwenye Kitumbua chao.

Kwa vile Mahakama ya Dini ya Kiyahudi haikuwa na Mamlaka ya kutoka hukumu ya Adhabu ya Kifo hasa wakati wa Utawala wa Warumi kule Palestina (pamoja na Israeli); Viongozi hao wa Dini wakaamua kumpeleka Yesu kwenye Mahakama ya Kisiasa (Kirumi) kwa Ponsio Pilato ambaye alikuwa Gavana akimwakilisha KAISARI. Pilato ndiye aliyekuwa anasimamia Mahakama hiyo ya Kirumi na ndiyo iliyokuwa na Mamlaka ya Kumhukumu Mtu Adhabu ya Kifo.

II. MAHAKAMA YA KISIASA
Hapa napo alipita katika hatua tatu:
1. Yesu mbele ya Pilato.
2. Yesu mbele ya Herode.
3. Yesu mbele ya Pilato tena.

Viongozi wa Dini ya Kiyahudi ndio waliokuwa walalamikaji (Washtaki). Walielewa kuwa wakienda kwa Pilato na yale yale Makosa au Mashtaka ya Kidini, Pilato atawaambia wakamhukumu kwa Sheria zao za Kidini (kwasababu walikuwa na hayo Mamlaka). Na endapo angeamua kutoa hukumu, basi hukumu hiyo isingekuwa ni Adhabu ya Kifo (kama ambavyo wao walitaka Yesu AFE).

Kutokana na sababu hizo, wakaamua kuyabadilisha Mashtaka yake kutoka Makosa ya Kidini na kumbambikizia Makosa ya Kisiasa.

Hapo kwa Pilato wakaja na Makosa Matatu:
1. Kuwataharakisha watu (Kuwachochea watu wagome na kuupinga Utawala wa Kirumi wa Kaisari. Hili ni Kosa la Uchochezi).
2. Kuwakataza watu wasilipe Kodi kwa Kaisari.
3. Kujifanya yeye ni Mfalme (dhidi ya Kaisari).


Makosa hayo yote kimsingi ni Makosa ya UHAINI (Trison). Na adhabu ya Makosa ya Uhaini kwa nchi zote duniani ni Kuhukumiwa KIFO (Death Penalty).

Pamoja na Hila zote hizo, bado walikosa USHAHIDI wa kumshawishi Pilato atoe hukumu hiyo. Pilato akaitupilia mbali hii kesi kwasababu ilikosa Hoja za Kimantiki ya Kisheria. Akawaambia wampelekee Herode hilo Shauri. Maana Yesu alikuwa Mwananchi wa Galilaya na Herode (Antipas) alikuwa Mtawala wake wa Kimila. Huyu ndiye aliyemkata Kichwa Yohane Mbatizaji (John the Baptist) kwasababu ya Ahadi aliyoitoa kwa Binti wa Herodia.

Herode ambaye alikuwa Yerusalemu kipindi hicho cha Sikukuu ya Pasaka, naye hakuona kosa lolote la Yesu. Zaidi alifurahi tu kumwona maana alikuwa anazisikia tu Habari zake akiambiwa na Watu; na alikuwa anamchanganya na Yohane Mbatizaji.

Wakaamua kumrudisha tena kwa Pilato huku wakishinikiza kwa nguvu zote na Makelele kuwa asipomhukumu Yesu Kifo maana yake hana ushirika na Kaisari. Na pia watamtaarifu Kaisari kuwa Pilato anawatetea watu wanaompinga Kaisari.

Pilato aliposikia hayo na kwa kuogopa KUTUMBULIWA na Kaisari endapo Viongozi hao wa Dini ya Kiyahudi wangemfikishia Kaisari hiyo taarifa, akaamua kufanya kama walivyotaka. Akamhukumu Yesu adhabu ya Kifo cha Msalabani chini ya usimamizi wa Askari wa Kirumi.

TARATIBU KADHAA ZA KISHERIA ZILIVUNJWA
Kesi ya Yesu ni Kesi ambavyo inaongoza mpaka sasa kwa Kuvunja Rekodi ya Uvunjifu wa Taratibu nyingi za Mshingi za Kisheria katika Shughuli za Uendeshaji wa Mashtaka. Na Rekodi hii haijawahi kuvunjwa. Taratibu zilizovunjwa ni kama ifuatavyo:

1. Baada ya Yesu kukamatwa alitakiwa apelekwe kwenye Gereza (Lockup) ya Hekalu mpaka hapo Baraza Kuu la Wayahudi litakapokaa kama ambavyo Mitume Petro na Yohane walivyowekwa (Matendo 4:3; 5:17). Lakini Yesu mara tu baada ya kukamatwa akapelekwa nyumbani kwa Kuhani Mkuu (Yohane 18:13-27).

Hii ilikuwa tofauti au kinyume na taratibu za kawaida: Kwanza kilikuwa ni kipindi cha Pasaka. Usiku huo ulikuwa ni Usiku Mtakatifu kadili ya Liturujia ya Wayahudi, na Makuhani walitarajiwa kuwa na familia zao na sio kusikiliza kesi ya Rabi tu fulani kutoka Galilaya. Pili, nyumba ya Kuhani Mkuu kwa vyovyote vile ilikuwa nzuri na ya kistarehe (luxurious) kiasi kwamba pengine isingeweza kuwatosha Wajumbe wote 72 wa Baraza hilo kama wangeweza kukusanyika wote kwa taarifa ya haraka na ya muda mfupi kiasi hicho.

2. Haikuruhusiwa kesi au shauri lolote kuendeshwa wakati wa Sikukuu au Maandalio ya Sikukuu (No Trial was to be held during Feast Time). Lakini hao hao viongozi wa sheria za Kiyahudi waliendesha shauri la Yesu wakati wa Sikukuu ya Pasaka.

3. Kila Mjumbe wa Baraza alipaswa kupiga kura binafsi/kwa siri kukubali au kukataa wakati wa maamuzi yoyote ya hukumu (Each Member of the Court was to vote individually to convict or acquit). Lakini Yesu alihukumiwa kwa kura ya pamoja (but Jesus was convicted by acclamation.)

4. Kama mtu akihukumiwa kifo, hukumu hiyo ilitakiwa itekelezwa siku inayofuatayo (If the death penalty was given, a night must pass before the sentence was carried out). Lakini Yesu alihukumiwa na Hukumu hiyo ilitekelezwa muda mfupi tu baada ya hukumu kutolewa.

5. Wayahudi hawakuwa na Mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo, lakini hukumu ya Yesu ilipendekezwa na Wayahudi na wakampeleka kwa Pilato kuomba ruhusa ya utekelezaji (The Jews had no authority to execute anyone death penalty; but the Jews announced the death penalty and suggested to Pilate for implentation).

6. Haikuruhusiwa shauri lolote kuendeshwa wakati wa usiku (No trial was to be held at night, but this trial was was held before dawn). Lakini shauri la Yesu liliendeshwa usiku kabla ya alfajiri.

7. Mtuhumiwa yeyote alipaswa kupewa Mshauri au Wakili na uhuru wa kuleta mashahidi (The accused was to be given counsel or representation). Lakini Yesu hakupewa nafasi hii (But Jesus was given none).

8. Mashtaka ya Mtuhumiwa yalipaswa kubakia hayo hayo katika kila hatua ya kesi. Lakini Mashtaka ya Yesu yalibadilika kila hatua ya kesi kutoka Kukufuru na Kujiita yeye ni Mwana wa Mungu (Masiha) alipopelekwa kwenye Mahakama ya Kidini hadi Kutaharakisha jamii na kusababisha uasi (Rioting), Kuwakataza watu kulipa kodi kwa Kaisari na Kujitangaza kuwa ni Mfalme wa Wayahudi wakati Wayahudi walimtambua Kaisari kama Mfalme wao (Uhaini au Treason) katika Mahakama ya Kirumi alipokuwa mbele ya Pilato.

9. Mtuhumiwa hakutakiwa kuulizwa Maswali ya kujifunga au Maswali ambayo majibu yake yatamfunga; lakini Yesu aliulizwa kama yeye ni Kristo. (The accused was not to be asked self- incriminating questions, but Jesus was asked if He was the Christ).

YESU HAKUWA NA KOSA
Kuna Mazingira kadhaa yanaonesha Yesu alihukumiwa bila kosa kuanzia Mwanzo wa Kesi hadi mwisho.
Throughout this trial, Jesus’ innocence is stressed:
1. Mke wa Pilato alioteshwa katika Ndoto kuwa Yesu hakuwa na Hatia na akamtumia Ujumbe huo Mumewe (Matayo 27:19)

2. Pilato alijitahidi sana kuepuka kumhukumu Yesu Kifo. Kulikuwa na desturi ya kumfungua Mfungwa Mmoja wamtakaye Kipindi cha Sikukuu ya Pasaka(Kama tu ambavyo Rais anatoa Msamaha kwa Wafungwa Kipindi cha Sikukuu ya Uhuru). Pilato alijaribu kuitumia Desturi hiyo ili aweze kumtoa Yesu. Akaamua kuwaletea Baraba Mtu Mharifu na aliyetea Taharuki kwa kuleta Fitina na kusababisha Uuaji katika Fitina ile. Akiamini watamchagua Yesu atoke na Baraba ahukumiwe. Lakini wakataka afunguliwe Baraba na Yesu asulibiwe (Matayo 27:15-18).

3. Pilato alijaribu sana kuuliza Makutano kutaka kujua Kosa hasa la Yesu ni lipi hadi kustahili Kusulibiwa. Akawauliza, "Kwani? Ni ubaya gani alioutenda?" (Matayo 27:23). Maana walikuwa hawajatoa ushahidi au uthibitisho wa kosa lake. Bado wakajibu tu, "Na asulibiwe" (Matayo 27:23)

4. Mwisho, Pilato akaamua kuosha mikono yake kuonesha kuwa yeye hana hatia juu ya Kifo cha Yesu. Akasema, "Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe" (Matayo 27:24). Kwa kulinda cheo chake kama Gavana akamtoa Yesu kwao asulibiwe.

Credit kwa John-Baptist Ngatunga
 
Vipi ile kesi aliyeifungua Mkenya mahakamani kuhusu mauaji ya Yesu iliishia wapi?
 
Kuna kipindi fulani,Kuna jamaa aliiibua hii kesi ya yesu,na kulishitaji dola la kirumi,jamaa alikuwa anadai fidia dhidi ya uonezi uliofanyika,Sasa sijajua rufaa ya huyu jamaa ilifikia wapi!!.
Yeah ilikuwa kama miaka nyuma hivi ..najiuliza tu angelipwa hiyo fidia angeipeleka wapi?
 
Yule aliemkana Yesu hadi jogoo akawika pia hana kosa.

Yaani nione mtu anapigwa mijeledi anagongelewa misumari kwenye mikono na miguu anavalishwa miba kwenye miti na ananing'inizwa juu ya mti kama nyama buchani na askari halafu askari haohao wananifuata wananiuliza

" unamjua huyu mtu ?"

Ndugu msomaji embu tuacheni unafiki pembeni we ungejibuje?
 
Back
Top Bottom