Angelica Zambrano: Binti kutokea Ecuador aliyeenda Mbinguni na Kuzimu

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Hii ni makala ya yule msichana wa kule Ecuador aitwaye Angelica Zambrano. Huyu alichukuliwa na kupelekwa Mbinguni na Kuzimu.

Kule kuzimu aliwakuta wasanii mbalimbali, akawakuta viongozi wa dini. Yaani yule mtu mliyemwamini sana, naye akakutwa huko. Tutaisoma yote. Ukiingia mitandaoni ipo ya Kiingereza, hapa nitakuletea ya Kiswahili.

Kama hupendi mambo ya dini dini achana nayo mapema tu manake utaona watu wananiuliza maswali utadhani mimi ndiye Angelica.

Inaanza:
Kwa kipindi cha masaa 23, binti mdogo wa ki-Ecuado aitwaye Angelica alioneshwa falme za Mbinguni na Kuzimu, na kurudi kwa Kristo mara ya pili.

Alishuhudia Yesu akilia kwa huzuni aonapo umati wa roho zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa yeye, kanisa lisilo tayari kabisa kwa ujio wake, watu wameacha kushuhudia kwa walipotea mbali na kweli, na anasa za dunia zimeteka hata watoto kwa shetani.

Alishuhudia watu maarufu wakiteswa katika moto, waimbaji, wanamuziki na hata Papa. Angelica alioneshwa jinsi ufalme wa Mbinguni ulivyoandaliwa kwa uzuri na utayari, utukufu usioweza kufikirika, ambapo hakuna uovu.

Japokuwa Yesu anakuja kwa ajili ya watakatifu tu; wengi wa wana wa Mungu hawatakuwa tayari kwa siku ile, na wataachwa nyuma katika ulimwengu utakaogawanyika vipande vipande. www.DivineUfunuo.info/23 (Mahojiano kwa video, mwanzoni ni kwa lugha ya Kihispania, huko El Empalme, Ecuador. Sept. 29, 2009).

Maxima (Mama yake Binti):

Jina langu ni Maxima Zambrano Mora, tunasali kanisa la "Casa de Oracion" huku El Empalme. Tulikuwa katika kufunga kwa siku 15, na kulia kwa Mungu.

Binti yangu Angelica aliungana nasi pia. Katika kipindi hicho cha siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi ya asili, ambayo sijawahi kuona kabla.

Tulikuwa tunaomba na kufunga katika kipindi maalumu cha kumtafuta Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri Mungu aseme nasi.

Bwana alitutia matumaini makubwa sana. Kwa ajili ya majaribu yetu tulikaribia kukata tamaa, lakini Bwana alikuwa pamoja nasi kutusaidia. Alitupa neno la Yeremia 33:3 "Niite, nami nitakuitikia, ame nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.”

Binti yangu alitia msisitizo sana katika neno hili kwa Bwana, japokuwa sikujua kwa wakati huo.

Angelica (Binti Mhusika):

Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina umri wa miaka 18, na ninasoma chuo cha "Colegio José María Velazco Ibarra", hapa El Cantón, El Empalme, Ecuador.

Kwanza nilimpokea Kristo nilipokuwa na umri wa miaka 12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata mmoja wa rafiki zangu aliyeokoka na nikajisikia aibu miongoni mwao", kwa hiyo nirudi nyuma mbali na Mungu na kuishi maisha mabaya lakini Mungu alinivuta nitoke huko.

Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 15, nikarejea tena kupatana na Bwana, lakini nia haikutulia sawa sawa.

Biblia inasema (Yakobo 1:8), "Mtu wa nia mbili husita-sita katika nia zake zote" na mimi nilikuwa sawa na mtu huyu. Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo, siyo vizuri, ni vibaya mwanangu" lakini nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo, nataka kuwa hivyo, hakuna mtu wa kuniambia namna nitakiwavyo kuwa, wala chakufanya, wala namna ya kuvaa, au mwenendo. Naye alijibu, "Mungu atakushughulikia na atakubadilisha wewe."

Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 17, nilimkaribia Bwana. Tarehe 28 mwezi Aprili nilimwendea Bwana na kumwambia, "Bwana, nijisikia vibaya sana, najua kuwa mimi ni mwenye dhambi” na nilimweleza jinsi ninavyojisikia. "Bwana, nisamehe mimi.

Natamani uandike jina langu katika kitabu cha Uzima na unipokee niwe mwanao."

Nilitubu na kutoa maisha yangu kwa Bwana rasmi. Nikasema “Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti ndani mwangu."

Nililia kwa moyo wangu wote, huku nikimwomba Bwana anibadilishe mimi. Lakini kwa kadri ya muda ulivyozidi kupita, sikuona madiliko yoyote. Badiliko pekee nikuwa nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma Biblia na kuomba. Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha yangu.

Ilipofika mwezi Agosti, nilikaribishwa katika mfungo wa siku 15. Niliamua kushiriki, lakini kabla ya kuanza nilisema: “Bwana, naomba unishughulikie hapa."

Katika kipindi chote cha mfungo, Bwana alikuwa anasema na karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile Bwana hajaniona, na hilo liliniumiza sana. Nikaomba, "Bwana, hutanishughulikia mimi?" Nikaomba na kulia peke yangu na kusema tena, "Bwana, je unanipenda? Je upo hapa? Upo nami hapa? Kwanini husemi nami kama unavyosema na kila mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu, hata maneno ya unabii, lakini siyo kwangu"

Nilimwomba ishara ya kuwa yu nami, na Bwana akanipa neno la Yeremia 33:3, "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua." Nikasema, “Bwana, je umesema nami?” Kwasababu nilisikia sauti yake na kupata maono ya maneno yaliyoandikwa katika Yeremia 33:3.

Nikasema “Bwana, hiyo ni kwa ajili yangu?” Nilitunza na kukaa nalo kimya mwenyewe wakati kila mmoja akishuhudia waliyopewa na Bwana na kuoneshwa. Lakini mimi nilitunza siri yangu na mara kwa mara nilijikumbusha na kutafakari maneno: " Niite" maana yake nimwombe, lakini nini maana ya: "mambo makubwa, magumu" niliwaza, “Huenda ikamaanisha Mbinguni na Kuzimu."

Kwa hiyo nalimwambia “Bwana, naomba unioneshe Mbinguni tu, lakini siyo kuzimu, kwa sababu nimesikia kuzimu ni sehemu ya kutisha na mbaya sana." Lakini baadaye nikaomba kwa moyo wangu wote, "Bwana kama ni mapenzi yako kunionesha, na iwe hivyo, lakini nibadilishe kwanza. Naomba ufanye tofauti ndani mwangu, nataka kuwa tofauti.”

Tulipomaliza kufunga, kulikuwa na majaribu na vipindi vigumu na mara nyingine nalijisikia kuishiwa nguvu, siwezi tena kuendelea na Bwana. Lakini alinipa nguvu.

Nilianza kusikia sauti yake na kumjua vema zaidi. Tukawa marafiki wazuri. Bwana ni rafiki yetu mwema, na Roho Mtakatifu pia. Niliwahi mwambia, "Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka kukujua vema," na nilishirikiana naye katika mawazo yangu yote.

Nilimwomba kipindi chote cha mwezi Agosti hadi Novemba, na mtumishi wa Bwana akaja nyumbani kwetu na kusema, "Bwana akubariki." Nikajibu, "Ameni." Kisha akasema, "Nimekuja kukuletea ujumbe toka kwa Mungu…...Jiandae, kwa sababu Bwana atakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Atakuonesha wewe Mbinguni na kuzimu kama ulivyokuwa unamwomba neno la Yeremia 33:3." Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini umepataje kujua? Sijamweleza yeyote." Akanijibu, "Mungu unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye, alinieleza kila kitu."

Mara tukaanza kuomba. Baadhi akina dada toka kanisani kwetu na wana familia wangu wakaungana nasi kuomba. Lakini mara tulipoanza kuomba, nilianza kuona Mbingu zikifunguka.

Mara nikasema “naona mbingu zikifunguka, na malaika wawili wanashuka kuja tulipo" Mtumishi wa Mungu akasema “waulize kwanini wamekuja hapa”

Walikuwa warefu na wazuri wakupendeza; wana mbawa nzuri. Walikuwa wakubwa na wenye kung’aa, na walionekana wakiangaaza, mng’ao kama wa dhahabu.

Walivaa sandozi za vito vya thamani na walivaa mavazi matakatifu. "Kwanini mko hapa?" Wakatabasamu na kusema, "Tupo hapa kwa sababu tuna kazi yakufanya….. tupo hapa kwa sababu unatakiwa utembelee Mbinguni na kuzimu na hatutaondoka mpaka yote yatakapopita." Nikawajibu “safi sana, lakini mimi natamani kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu” Wakatabasamu na kuendelea kuwepo na hawakusema lolote zaidi. Baada ya kumaliza maombi, niliendelea kuwaona wakiwepo.

Pia nilianza kumwona Roho Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa pote na yuko kila mahali wakati wote.

Ninamwona, anaangaza na kung’aa sana, naona tabasamu lake na mtazamo wake wa upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa sababu ni mzuri zaidi ya malaika.

Malaika wana uzuri wao lakini Roho Mtakatifu ni zaidi sana kwa yote. Naweza kuisikia sauti yake, sauti ilijaa upendo na matulizo makuu.

Siwezi kuelezea kabisa sauti yake; kama radi si radi wakati huo huo yakuvutia. Yeye husema “Niko pamoja nawe” Kwa hiyo nalijitahidi kuendelea kutembea na Mungu, japo majaribu yalizidi kutuzingira.

Tulikuwa tunapita kipindi kigumu sana, lakini chenye ushindi waajabu. Mie husema “Bwana, mapenzi yako yatimizwe.” Niliendelea kuwaona malaika wale hata nikiwa shule na pia darasani. Nilikuwa mwenye furaha ajabu kwa sababu niliwaona vema.

Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia nijiandae, kwa sababu nitakwenda kuona Mbingu na kuzimu. Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.” Haikuwa rahisi niliposikia neno hili.

"Nitakufa namna gani? mie mdogo sana", Nilimuuliza. Akanijibu, “Usihofu juu ya lolote, Kila kitu Mungu afanyacho hakina makosa wala mawaa, na atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu ya Mbinguni na Kuzimu, kwakuwa hilo ndilo Bwana anataka sote tujue” Nikasema “Amen, lakini nitagongwa na gari au nitakufaje?” Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana akaniambia nisihofu, kila kitu kiko katika uwezo wake. Nikasema, “Ahsante Bwana”

Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani toka shule, malaika wale walikuwa nami, hata nilipokuwa namsifu Bwana. Wao walikuwa hawaongei nami; bali walidumu kusema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah," huku wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba wa Mbinguni.

Roho Mtakatifu pia alikuwa na malaika wale huku akifurahi. Watu wengi husema injili/ wokovu ni wa kuchosha/kukera, lakini huo ni uongo mkubwa toka kwa mwovu ili kuwafanya watu wasitafute uwepo wa Mungu. Nami pia niliamini hivyo hapo kwanza, lakini baada ya kukutana na Bwana na Roho Mtakatifu, najua injili haikeri wala kuchosha, niburudisho la ajabu hapa duniani!

Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho Mtakatifu. Lakini malaika walikuwa hawaongei nami, ila walikuwa wakimsifu Bwana. Nikimwambia Roho twende nami nakufanya hili na lile huja na kuwa nami. Ninaweza kujihisi na kumwona vema.

Japokuwa wengi hawamwoni, yeye yupo! Mahusiano haya yamendelea, hata hakuna sababu ya kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha yake na faida za Roho Mtakatifu…… hakuna njia ya kujitenga naye jinsi alivyo mwema na wafaida, hasa nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa, ninamshukuru sana kwa rehema zake na upendo wake kwa wanadamu na kwangu mimi!

Tarehe 7, Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema “Jiandae, kwakuwa leo utakufa,” Nilijua kuwa ni Roho Mtakatifu kwa vile nilimwona vema.

Niliipuuza sauti yake na kusema “Bwana, Sitaki kufa leo!” Lakini alirudia, “Jiandae, kwakuwa leo utakufa!” Mara hii sauti ilikuwa ya juu zaidi na mkazo mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe unayesema nami; nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi yako yatendeke. Nitafanya kila utakalo niambia, najiachia kwako Bwana, japo naogopa, najua upo nami, nawe ni wa kweli.”

Niliomba, “Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia kunipa ujumbe mara ya kwanza, mlete muda huu, nimkute nyumbani, na umpe tena neno hili aseme nami kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.” Sasa mara zote Bwana hujua ya nyuma, yaliyopo na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo nilipofika nyumbani nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.

Maxima (Mama ya Binti):
Binti yangu alipofika nyumbani, tulikuwa jikoni. Mara Angelica alipomwona mtumishi wa Bwana, akasema, “Bwana akubariki.” Mtumishi wa Mungu akajibu, “Bwana akubariki nawe. Je uko tayari? Kwa kuwa leo ndiyo siku Bwana atakayo kuchukua, saa kumi jioni.” Angelica alisimama na kushikwa na mshangao kwamba Bwana amejibu ombi lake na kufanya vilevile alivyomwomba njiani.

Angelica:
Niliposikia hayo maneno ya mtumishi, nikasema, “Ameni... lakini sitaki kufa, sitakufa! Hapana, Bwana, naogopa, naogopa sana, ninahofu kubwa!” Mtumishi wa Bwana akasema, “Tuombe ili hofu ikutoke sasa kwa jina la Bwana.” Nikasema, "Ameni" na tukaomba. Ghafla nikajisia hofu yote imenitoka na furaha isiyoelezeka ikajaa ndani mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema kuliko vyote nikitamanicho kinifike! Nikanza kutabasamu na kicheka wakati huo kila mmoja aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika toka unyonge na kuwa mwenye furaha. Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.
Picha wakimwombea: (Mtandao rasmi una picha yake hiyo)

Maxima:
Binti yangu ghafla akawa mwenye furaha ndani ya moyo na kuanza kula. Alionja karibia kila kitu kilichokuwepo, huku akisema, “Kama sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”

Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka na kuuliza, “kwanini uko hivyo badala ya kuwa na huzuni, unafuraha na mwenye raha?” nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana, nitakuwa naye, lakini sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote wakastaajabu na kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama yangu yalinitazama kwa mshangao zaidi!

Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa vitu vyake. Aligawa vyote, vyote! Ma-dada wa kanisani walikuwepo, nao pia aliwapa baadhi ya vitu kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema, “Kama nikirudi, watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo.”

Angelica:
Niliwaza huzuni aliyokuwa nayo mama yangu niliposema maneno hayo. Lakini nilijisikia furaha tupu, kwa hiyo nikaendelea kugawa vitu: nguo, kitanda, simu ya mkononi, kila kitu, lakini kwa sharti: kama nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.

Maxima:
Binti yangu alikuwa na msimamo na nia ya dhati, lakini kama mama nilishikwa na huzuni sana. Haikuwa jambo rahisi. Niliwaza, “Bwana muda huo ukiwadia, itakuwajekuwaje?” Sikuweza kuelewa. Na walipoanza kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema, “Dada njoo tuombe.” Lakini niliwajibu, “Nyie endeleeni, nitajiunga nanyi muda si mrefu. Ngoja nimalizie kazi hii.”

Angelica:
Wote walikuwa wananiangalia mimi tulipokuwa tunaomba. Niliomba, “Bwana, nataka kufanya mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata useme uwongo au ujute, najua wewe ni mkweli. Kama nitakuaibisha, basi vema unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya mapenzi, basi unirejeshe tena, lakini nisaidie kusema ukweli, niandae mimi, nisaidie kuhubiri na kuwaambia watu kutubu.” Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana. Nilimwambia mtumishi wa Bwana.

“Usimwambie mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye akajibu, “sitamwambia sasa, lakini mara Bwana atakapokutwa, nitamwambia.” Tuliendelea kuomba na kuungana katika duara.

Maxima:
Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana akamwambia mtumishi wake ampake mafuta binti yangu. Kwa hiyo baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake mwili mzima, toka kichwani hadi chini, kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote amepakwa mafuta.

Mama yangu na dada mmoja, Fátima Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri walivyokuwa wananipaka, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika, kama kioo kilinizunguka mimi. Ni vigumu kuelezea, nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea nilivyokuwa najisikia. Baada ya hapo kila walipojaribu kunigusa walishindwa!

Maxima:
Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica, nilijaribu kuweka mkono juu yake, nilishindwa! Alikuwa amezingirwa na kitu. Ilikuwa ajabu, hakuna aliyeweza kumgusa tena! Uzio huo ulianzia kichwani hadi miguuni, karibia sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo lilinitisha zaidi mimi.

Nimewawekea mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili halijawahi kutokea! Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza kuomba na kumshukuru Bwana. Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni iliyokuwa moyoni ikanitoka, maumivu yakakoma na sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na ilipofika saa 10.00 jioni, binti yangu akaanguka sakafuni.

Angelica:
Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa kupumua. Nikasikia maumivu tumboni na moyoni. Nilijisiki damu ikisimama, na ghafla maumivu makali mwili mzima. Nililoweza kusema, “Bwana, nipe nguvu, nipe mimi nguvu!” kwasababu nilijisikia kushindwa kuendelea zaidi.

Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika roho, si kwa macho ya mwilini, niliona mbingu zikifunguka. Niliwaona malaika, siyo wawili au kumi, bali kwa mamilioni wakiwa pamoja wamekusanyika. Katikati yao niliona mwanga, mara 10,000 zaidi ya jua. Na nikasema, “Bwana ni wewe unayekuja!”

Maxima:
Alipoanguka chini, tulijaribu kumsimamisha, lakini hakuweza kusimama mwenyewe. Muda huu tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema, “Omba. Sina nguvu, mama, sina nguvu na ninasikia maumivu.” Mwanzo alisikia maumivu tumboni, na baadaye moyoni. Tuliendelea kuomba na kumsihi Bwana. Bwana alichukua maisha yake!

Sijawahi katika maisha yangu kumwona mtu akifa. Nilishuhudia binti yangu, akigugumia maumivu! Haikuwa rahisi hata kidogo! Sikuweza kuelewa maneno yake ya mwisho, na mwisho alitulia. Niliweka mikono yangu usoni pake, na kioo mdomoni kuona kama alikuwa anapumua. Hakuwa na pumzi tena, alitulia kimya kabisa. Nilimshika, alikuwa angali na joto kama kawaida. Nilichukua shuka na kumfunika na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa baridi sana. Nywele zake zikalala, kama za maiti na akabadilika ubaridi wa barafu.

Angelica:
Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili ukifa. Kadri Yesu na malaika walivyozidi kukaribia, nikajisikia kuondoka, na sikuwa mimi tena. Sikuwa hai tena, nilikuwa nakufa na kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka chini, walikuwa tayari wamefika.

Nyumba yetu ilijaa malaika, na katikati yao niliona mwanga mkali kuliko wa jua! Ilikuwa vigumu; nilisikia maumivu makali wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili.

Nilikuwa nalia na kupiga kelele, kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni. Nilimuuliza, “Bwana, nini kinachotokea? Nini kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa mwili wangu na kuurudia tena, lakini nilipojaribu, ilikuwa kama kushika hewa: sikuweza kuugusa, mkono wangu ulipitiliza. Hakuna kati ya waliokuwa wananiombea aliyenisikia! Na nikapiga kelele, “Bwana, nisaidie mimi!”

Maxima:
Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale. Bwana alinipa nguvu kwa kuwa sikujua la kufanya. Ilikuwa kama vile yuko mahututi (kwenye coma), lakini nilijua yuko salama, kwasababu ilikuwa ni kazi ya Bwana. Kwahiyo nikasema “Bwana, mapenzi yako yafanyike.”

BWANA YESU KRISTO

Angelica:
Wakati huo nasikia sauti ya Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya UPENDO, “Usiogope, Binti, kwa kuwa mimi ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa kukuonesha niliyokuahidi wewe. Inuka, kwa kuwa mimi ni Yehova, ninayekushika mkono wako wa kuume na kukuambia, usiogope, nitakusaidia wewe." Ghafla, nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini, ninauangalia mwili wangu, nikitaka kuurejea bila mafanikio. Niliposikia sauti yake, woga ukanitoka, na sikuwa na hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika wakaanza kufungua njia.

Kulikuwa na mwanga mkali ung’aao, na nilipouangalia nilisikia amani ya ajabu. Kadri nilivyoangalia, nilimwona mwanaume mzuri, mrefu, aliyevaa vizuri na kuvutia sana kumwangalia, mwenye siha njema.
Mwanga ulitoka kwake. Kulikuwa na mwanga mkali kiasi cha kushindwa kumwangalia uso wake! Lakini niliweza kuona nywele zake za dhahabu ing’aayo na vazi jeupe na mshipi kifuani pake. Ukisomeka, “MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.”

Nilimwangalia miguuni pake, alikuwa amevaa sandozi zenye mng’ao wa dhahabu, dhahabu safi. Alikuwa mzuri sana! Akaninyooshea mkono wake. Nilipomshika mkono wake, haikuwa kama nilipojaribu kuugusa mwili wangu, mkono haukupitiliza. Nikauliza, “Nini kinachotokea?” naye akasema, “Nitakuonesha wewe kuzimu ili ukirudi uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi; kuwa ni kweli ipo.

Na pia utukufu wangu nitakuonesha wewe, ili uwaambie watu wangu wajiaandae, kwa kuwa utukufu wangu ni halisi na mimi pia.” Akasema, "Binti, usiogope” akarudia kusema tena na mimi nikasema, "Bwana, nataka tu kwenda Mbinguni, lakini siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!” Akasema, “Binti, nitakuwa nawe. Sitakuacha huko na nitakuonesha huko mahali kwasababu wengi wanajua kuzimu ipo lakini hawaiogopi.

Wanaamini ni mchezo, na kuzimu ni mzaha, na wengi hawajui lolote juu yake. Ndiyo maana nitakuonesha wewe huko kwa sababu wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika utukufu wangu.” Aliposema hayo, niliona machozi yakitiririka kwenye vazi lake. Nikamwuuliza, “Bwana, kwanini unalia?” Akanijibu, “Binti, kwasababu wengi wanaangamia, na nitakuonesha hii, ili uende na uwaambie ukweli na wewe usirudie hapo.”

KUZIMU
Ghafla, alivyokuwa anaongea, kila kitu kikaanza kutembea. Ardhi ilitikisika na kupasuka, na nikaona shimo jeusi tii chini.

Shimo:
Tulikuwa tumesimama kama kwenye mwamba na malaika wakituzunguka. Nikasema, “Bwana, sitaki kwenda mahali huko!” akasema, “Binti, usiogope niko pamoja nawe.” Kwa sekunde chache tukashuka kwenye shimo jeusi. Nilijaribu kuangalia lakini kulikuwa na kiza kikuu. Niliona duara kubwa, na kusikia mamilioni ya sauti.
Nilipata moto. Nikajisikia ngozi yangu kuungua. Nikamuuliza, “Bwana, hiki ni nini? sitaki kwenda mahali huko!” Bwana akasema hilo ni lango tu la kwenda kuzimu. Kulikuwa kuna harufu mbaya, yakutisha, isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye akajibu, “Binti, ni muhimu ufike na kujua sehemu hii.” Nikalia, “Lakini kwanini, Bwana, kwanini?” naye akasema, “Ili ukawaambie ukweli wanadamu; wanadamu wanaangamia, wanapotea na wachache sana wanaoingia ufalme wangu.” (Mat.7:14) Akishasema hivi, hulia sana. Maneno yake yalinitia nguvu na kunihimiza, kwa hiyo nikaendelea kutembea.

Ziwa la Moto:
Tulifika mwisho wa tanuru/lango, nilipoangalia chini niliona umati umefunikwa na miali ya moto. Bwana akasema “Binti, nakupa hii.” Ilikuwa ni faili kubwa lenye karatasi ambazo hazijaandikwa chochote. “Binti, chukua na kalamu hii ili uweze kuandika yote nitakayokuonesha, utakayoyaona na kusikia. Utaandika kila kitu ukionacho na utaishi nayo.” Nikasema, “Bwana, nitafanya, lakini nimeshaanza kuona mengi mno, Bwana. Ninaona roho zikiteswa, na kuzamishwa kwenye moto.”

Maxima:
Muda uliendelea kupita, na binti yangu alikuwa bado kalala pale. “Bwana, nini kinachotokea?” Machozi yalikuwa yakimtoka kwenye macho, lakini kila nilipomfuta, yalitoka tena. Nikaweka kioo mdomoni pake kuona kama anapumua, hakukuwa na pumzi. Tuliangalia mapigo ya damu, wapi, hakuna kitu. Tuliweka mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu. Mtumishi wa Bwana akasema, “mahali alipo sasa, siyo mahali pa kutabasamu bali mahali pa mateso.”

Angelica:
Nikamwambia Yesu, Nitashuhudia kuwa kuzimu ni halisi, kwamba ipo, lakini nitoe hapa sasa!” na akanijibu, “Binti, hatuja ingia bado mahali penyewe, na sijakuonesha chochote, tayari unataka nikutoe huku?” nikasema “Bwana, tafadhari nitoe mahali hapa,” tukaendelea kushuka kwenye korongo/shimo lakutisha! Nikaanza kulia na kupiga yowee, “Bwana, hapana, hapana, hapana, hapana……… Sitaki kwenda!” naye hujibu, “Unatakiwa kuona haya.”

Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina, makubwa na madogo. Yalikuwa yanakimbia sana, na yameshika vitu mkononi. “Bwana, kwanini yanakimbia hivyo na yameshika nini?” akanijibu, “Binti, wanakimbia hivyo kwasababu wajua muda wao karibu kwisha, kwasababu muda wa kuwaharibu/kuwapoteza wanadamu, hususani watu wangu. Na walivyoshika mkononi ni mishale ya kuwaharibu wanadamu, kwasababu kila pepo amepewa jina na kwa kadri ya jina lake, ana mishale ya kumharibu mtu na kumleta huku kuzimu; malengo yao ni kumharibu mtu na kumleta kuzimu.” Na niliendelea kuona mapepo yakikimbia na kutoka kuelekea duniani na Bwana akaniambia; “Wanakwenda duniani ili kuleta na kuwatupa wanadamu huku." Alipokuwa akisema hivyo, Bwana hulia, hulia sana. Kila alipolia nami nililia pia.

Maxima:
Binti yangu alikuwa amekufa kwa masaa 23, lakini sikutoa taarifa kwenye mamlaka yoyote. Niliomba, “Bwana, nitasubiri kwa masaa 24. Kama binti yangu hatarudi ndani ya saa 24, nitampigia simu Daktari.” Lakini, Bwana alimrejesha kabla ya saa 24 hazijatimia.

Angelica:
Bwana akaniambia, “je uko tayari kuona nitakachokuonesha wewe?” Nikasema, “Ndiyo Bwana,”. Alinipeleka kwenye sero moja, ambapo nilimwona kijana akiwa matesoni katikati ya miali ya moto. Nikajulishwa namba sero yake, japokuwa sikuweza kujua ile namba, ilionekana kama imeandikwa kinyume hivi. Palikuwa na nembo kubwa mle ndani, na kijana alikuwa na namba 666 kwenye kipaji cha uso. Pia alikuwa na aina ya kipande cha chuma imebandikwa kwenye ngozi yake. Funza walikuwa wanamtafuna, haikuweza kuharibu kipande kile; wala moto haukuweza kukiunguza. Akapiga kelele, “Bwana, nirehemu mimi. Nitoe mahali hapa. Nisamehe mimi Bwana!” lakini Yesu alimjibu, “umechelewa, umechelewa sana: nilikupa fursa lakini hutaka kutubu.” Nikamuuliza Yesu, “Bwana, kwanini huyu yuko hapa?” mara nikajulishwa.

Akiwa duniani, kijana huyu alijua neno la Mungu, lakini ghafla akajitenga na Bwana na kuchagua pombe, madawa ya kulevya na kupita katika njia zisizofaa. Hakutaka kufuata njia ya Bwana. Yesu alimwonya mara nyingi juu la litakalompata. Yesu akasema, “Binti, yuko hapa kwasababu kila anayeyakataa maneno yangu, anaye amhukumuye: lile neno nilisema naye litamhukumu siku ya mwisho,” (Yohana 12:48) na Yesu akalia tena.

Bwana akilia, nitofauti nasi tuliavyo na zaidi yetu. Yeye hulia na maumivu makali moyoni na uchungu usioelezeka. Bwana akasema, "Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya wanadamu,” Nikamuuliza, “Sasa Bwana kwanini wanadamu wapo huku,” Akanijibu, “Binti, niliumba kwajili ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini, kwasababu ya dhambi na kukosekana kwa toba, wanadamu huishia hapa, na wengi wangamiao kuliko wanaofika katika utukufu wangu!" Akaendelea kulia na huniumiza sana nimwonapo akilia. "Binti, nalitoa maisha kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie hapa [Kuzimu]. Nalitoa maisha yangu kwa upendo na huruma, ili wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme wa Mbinguni.” Yesu kwa huzuni huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu, kadri aonavyo watu pale kuzimu.

Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie salama. Niliwaza, “kama nikimwacha Bwana aende, ninge-nasa kuzimu pale” Nikamuuliza, “Yesu, je nina ndugu yangu mahali hapa?” Akanitazama kwa jinsi nilivyokuwa nalia na akasema, “Binti, niko nawe,” Kwasababu nilikuwa mwenye hofu sana. Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi kuwaza kumwona ndugu yangu kwenye sero ile. Nilimwona mwanamke akiteswa, alikuwa na funza wakimla uso wake, na mapepo yakimchoma mikuki mwilini. Naye hupiga kelele, “Hapana, Bwana, nihurumie, nisamehe mimi, tafadhari, nitoe mahali hapa kwa dakika moja!” (Luka 16:24)

Kuzimu, watu huteswa na kumbukumbu za waliyoyafanya duniani. Mapepo hudhihaki watu na kuwaambia, “abudu na kusifu kwasababu huu ndiyo ufalme wenu!” na watu hupiga kelele wakikumbuka kuwa walimjua Mungu, kwasababu walijua neno. Walimjua Bwana waliteswa mara dufu ya wengine.

Bwana akasema, “Hakuna tena nafasi kwa walioko pale[kuzimu]; kungali na nafasi kwa walio hai.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini bibi yangu mkubwa yupo pale? Sijui kama alikujua wewe. Kwanini yupo kuzimu Bwana?” akanijibu, “Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa kusamehe….. binti, yeyote asiyesamehe, sitamsamehe huyu.”
Nikamuuliza, “Bwana, lakini wewe husamehe, na una rehema.” Naye akanijibu, “Ndiyo, binti, lakini nilazima kusamehe, kwasababu hawajawasamehe wengi, na ndiyo maana wengi wapo hapa, wameshindwa kusamehe…… nenda kawaambia wanadamu ni muda wa kusamehe, hasa hasa watu wangu, kwakuwa wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe. Waambie waache malaaumu, mafundo, chuki mioyoni mwao, kwa kuwa ni muda wa kusamehe! Kama kifo kikimsitukiza mtu aliyeshindwa kusamehe, huyo mtu atakwenda kuzimu, kwakuwa hakuna awezaye kununua maisha.”

Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na moto na akapiga makelele, "Aaaah," na akaanza kutukana jina la Mungu, na kumlaani Bwana; kila mtu kuzimu humtukana Mungu.
Tulipoondoka eneo lile, nikaona kuwa kuzimu imejaa roho ziteswazo. Watu wengi huinua mikono nje, wakimwomba Yesu msaada wa kuwatoa nje. Lakini Bwana hakuwa na lolote la kufanya kwao, nao huanza kumtukana Mungu. Mara Yesu hulia sana na kusema, “Inaniumiza sana kuwasikia, inaniumiza mimi sana wanavyofanya, kwasababu siwezi kufanya lolote kwaajili yao. Ninacho kueleza ni hiki; nina nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio hai, wanao muda wa kutubu!”

Bwana akaniambia kuna watu wengi maarufu huku kuzimu, na pia wengi waliomjua Bwana. Akasema, “Nitakuonesha upande mwingine wa tanuru.” Tukaenda mahali penye mwanamke aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu makubwa na kupiga makelele, akiomba huruma kwa Bwana. Yesu akanyoosha mkono kwake na akaniambia, “Binti, Yule mwanamke umwonaye pale, amezingirwa na miali ya moto ni Selena.” Kadri tulivyokuwa tunamkaribia, akapiga kelele, “Bwana, nihurumie mimi, nisamehe mimi Bwana, nitoe mahali hapa!” lakini Bwana akamtazama na kusema, "Umechelewa, umechelewa sana, huwezi kutubu sasa.”

Selena
Aliponiona mimi akasema, “Tafadhari, nakuomba wewe, waambie watu hivi, tafadhari sema na usinyamaze; nenda waambie wasije mahali hapa; nenda waambie wasisikilize nyimbo zangu, wala wasiimbe hizo nyimbo.”(1 Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi niwaambie hivyo?"

naye akanijibu, "Kwasababu kila wakati watu wanaposikiliza nyimbo zangu, nateswa zaidi na zaidi, na mtu anayeimba na kusikiliza nyimbo zangu, anaelekea mahali hapa. Tafadhari, nenda uwaambie wasije huku; nenda waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!”. Akapiga kelele na mapepo humchoma mikuki na Selena kulia, “Nisaidie mimi, nihurumie mimi Bwana!” lakini kwa huzuni Bwana alimwambia, “umechelewa sana.”

Nikaangalia pande zote za eneo lile, lilikuwa limejaa waimbaji na wasanii waliokufa. Walikuwa wakiimba na kuimba, bila kusimama. Bwana akanifafanulia, “Binti, mtu aliyepo hapa, lazima aendelee kufanya kile alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."

Kadri nilivyokuwa naangalia eneo lile, niliona mapepo mengi yakinyunyiza vitu kama mvua. Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona watu kwenye miali ya moto wakikimbia mbali na ile mvua na kupiga yowee, “Hapana, nisaidie, Bwana!..... Hapana, haiwezekani kuwa hivyo,” na mapepo yalikuwa yanacheka na kuwaambia watu, “Sifu na kuabudu kwasababu hapa ni ufalme wenu milele na milele!” Niliona miali ya moto ikiongezeka na funza za watu zikiongezeka zaidi! Hayakuwa maji yale bali kiberiti cha kuongeza miali ya moto na kuongea maumivu ya kila mtu. Nikamuuliza Yesu, “Ni nini kinachotokea?..... Bwana, ni nini hiki?” Bwana akanijibu, “Huu ni ujira wa yeyote asiyetubu.” (Zaburi 11:6).

Bwana akanipeleka mahali alipo mtu aliyejulikana sana. Kabla ya maono haya, nilishi maisha kama msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu anayekufa anakwenda Mbinguni; wale walifanyiwa ibada za mazishi watakwenda mbinguni, kumbe sikuwa sahihi, nilikosa. Alipofariki Papa John Paul II, marafiki zangu na ndugu walisema amekwenda mbinguni. Taarifa zote kwenye LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema, "Papa John Paul II amefariki, apumzike kwa amani. Anafurahia sasa kuwa na Bwana na malaika Mbinguni" na mimi niliamini yote kuwa ndivyo. Lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, kwasababu nimemwona kuzimu, akiteswa kwa miali ya moto. Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa John Paul II! Bwana akaniambia, “Angalia, Binti, Yule mwanaume umwonaye pale, ni Papa John Paul II. Yuko hapa; akiteswa kwasababu hakutubu.”

Papa John Paul II
Lakini nikamuuliza, “Bwana, kwanini yuko hapa? Alikuwa akihubiri kanisani.” Yesu akanijibu, “Binti, hakuna mwasherati, wala muabudu sanamu, hakuna mchoyo na hakuna mwongo atakayerithi ufalme wangu.” (Eph 5:5) Nikamjibu, “Ndiyo, najua ni kweli, lakini nataka kujua kwanini yuko hapa, kwasababu alikuwa akiwahubiria umati wa watu!" Na Yesu akanijibu, “Ndiyo, Binti, alisema mengi, lakini hakusema kweli kama ilivyo. Hakusema kweli na kweli aliijua na japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za wokovu. Hakutoa uhalisia; hakusema kuzimu ni halisi na mbinguni kupo; Binti, sasa yuko mahali hapa."

Nilipomwangalia mtu huyu, alikuwa na joka kubwa lenye sindano nyingi mwilini mwake, limemzingira shingoni, naye hujaribu kumtoa. Nalimwomba Yesu, “Bwana, msaidie!” Mwanaume hupiga kelele, “Nisaidie mimi, Bwana nihurumie; nitoe mahali hapa; nisamehe mimi! Ninatubu Bwana; Nataka nirudi duniani, nataka nirudi duniani nikatubu.” Bwana alimtazama na kumwambia, “Ulijua vizuri yote haya. Ulijua vema kuwa kuzimu ni halisi, ipo…….. umechelewa; hakuna tena nafasi kwaajili yako.”

Bwana akasema, “Tazama Binti, nitakonesha maisha ya mtu huyu.” Yesu akanionesha kioo kikubwa kama LUNINGA [TV]; nikaona alivyotoa misa mara nyingi kwa umati wa watu. Na watu wale walivyokuwa waabudu sanamu. Yesu akasema, “Tazama, Binti, wapo waabudu sanamu wengi hapa [Kuzimu]. Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa Binti. Ni mimi pekee niwezaye kuokoa, na nje yangu hakuna mwingine aokoaye. Nawapenda wenye dhambi, lakini nachukia dhambi Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa nawapenda na ninataka waje kwangu.”

Kadri Bwana alivyokuwa akisema, nilianza kuona mtu huyu akipokea makusanyo makubwa ya sarafu na fedha; vyote alivihifadhi. Alikuwa na fedha nyingi sana. Naliona sura yake imeketi katika mamlaka yake, lakini pia naliweza kuona zaidi. Japo ni kweli watu hawa hawaoi, ninakuhakikishia wewe, sizushi, Bwana alinionesha mimi, wanalala na masista; na wanawake wengi!

Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa uasherati, na neno linasema hakuna mwasherati atakayerithi ufalme wake. Kadri nilivyokuwa naona, Bwana akaniambia, “Tazama, Binti, yote ninayokuonesha, ndiyo yanayoendelea, ndivyo alivyoishi [Papa] na ndivyo yanayotokea katikati ya watu wengi, katikati ya mapadre na mapapa waliopo.” Kisha Bwana akasema, “Binti, nenda na uwaambie wanadamu ni muda wa kugeukia.”

Bwana akanionesha sehemu watu wengi wanavyoelekea kuzimu. Nikamuuliza, “Bwana, namna gani wanakuja huku?” akanijibu, “Nitakuonesha.” Akanionesha lango lenye watu wengi wakipita. Watu hawa walikuwa wamefungwa toka mikononi hadi miguuni. Walivaa mavazi meusi na kubeba mizigo mgongoni mwao. Yesu akasema, “Binti, hao watu uwaonao hawanijui mimi bado. Mizigo waliyobeba ni dhambi, lakini nenda waambie walete mizigo kwangu, nami nitawapumzisha; kwa kuwa mie ndiye mwenye kusamehe dhambi zao zote…. Binti, nenda na uwaambie waje kwangu, kwani nawasubiri na mikono yangu iko wazi kuwapokea, na uwaambie hapo wanaelekea mahali hapa [kuzimu].”

Kadri nilivyokuwa nawatazama watu wakitembea, nikamwambia, “Bwana, Yule mtu pale ni binamu yangu; na Yule kijana pia, Bwana, na Yule binti pale anayelekea kuzimu; oh familia yangu inakuja huku kuzimu!” Bwana akajibu, “Binti, wanakuja huku, lakini nenda uwaeleze wanakoelekea, nenda waeleze kuwa wanakwenda kuzimu. Nenda waeleze kuwa nimekuchagua wewe uwe mlinzi wangu…… nimekuchagua wewe kama mlinzi, hii inamaanisha kuwa unatakiwa uwaambie ukweli. Unatakiwa uende uwaeleze yote niliyokuonesha wewe.

Kama hutawaambia na jambo likampata mtu huyu, damu yake itakuwa juu yako, lakini ukiende na kufanya nilivyokueleza, hapo mtu huyu nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu ulionao utaondolewa, kwa kuwa atadaiwa mwenyewe na damu yake haitakuwa juu yako. (Ezekia 3:18)".

Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea huku [kuzimu], maarufu na watu muhimu. Kwa mfano, Michael Jackson. Huyu alikuwa maarufu duniani kote lakini alikuwa mjumbe wa shetani

Japokuwa wengi wanaweza wasione na kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo ukweli. Huyu alikuwa na mkataba na shetani: alikubaliana na shetani ili awe na heshima na sifa ilikuwa vutia wapenzi wengi.
Michael_Jackson.

Hizo hatua na mitindo aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona mimi mapepo yakicheza na kutembea yanapotesa watu kuzimu. Yalikuwa yanateleza kwa kurudi nyuma na siyo mbele, huku yakipiga kelele; yakifurahia mateso wanayopata watu. Ngoja nikuambia wewe kuwa Michael Jackson yuko kuzimu. Bwana alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael Jackson akiteswa kwenye miali ya moto.

Nikalia kwa Yesu, “Kwanini?” haikuwa rahisi kuona mtu huyu alivyokuwa anateswa na alivyokuwa analia na kupiga mayowe. Yeyote anayesikiliza nyimbo za Michael Jackson au kuziimba au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya kuwa shetani anakutega katika mtego wake ili mwisho uishie kuzimu.

Mara hii, jitoe na kumkana shetani kwa jina Yesu! Yesu anataka kukuweka huru wewe, ili usipotee milele. Bwana akaniambia, “Binti, kuna watu wanijuao pia wanakuja huku.” Nikamuuliza, “Bwana, inakuwa je mtu akujue harafu aje huku?” akanijibu, “Mtu Yule aliyeacha njia zangu na mtu Yule anayeishi aina mbili za maisha [wokovu na dhambi].”

Akaanza kunionesha watu wanaoelekea kuzimu. Walikuwa wamefungwa kamba toka mikononi hadi miguuni. Kila mmoja alivaa vazi jeupe, lakini limetobokatoboka, lina-mabakamabaka na limekunjamana. Yesu akaniambia, “Binti, angalia watu walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili ya watu hawa.

Nakuja kwaajili ya watakatifu, waliotayari, wasiolaumiwa, wasio na makunyanzi na wasio na mawaa…… nenda uwaambie warejee kwenye njia zao za zamani,” (Efeso 5:26-27) Nilianza kuwaona wengi miongoni mwa wajomba zangu na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha njia za Bwana. “Nenda kawaambie ninawasubiri, walete mizigo yao nami nitawapumzisha."

YESU alikuwa analia baada ya kusema hayo, “Binti, wanakuja huku [kuzimu]. Nenda kawaambie wajomba zako; nenda kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi hawatakuamini, lakini mimi ni shahidi wako mwaminifu, ni shahidi wako mwaminifu. Sitakuacha wewe. Hata kama hawataamini, Binti, nenda na uwaambie ukweli huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia Binti nitakuonesha jinsi watu wanavyofika huku.”

Tulikwenda kwenye lango, ambapo tuliona umati wa watu wakiangukia ndani ya shimo kubwa. Siyo elfu moja wala elfu mbili, bali wingi wake kama mchanga wa bahari, hawana idadi! Walikuwa wananguka kwa kila sekunde, mfano wa mkono uliojaa mchanga umwakikapo chini. Zile roho zilikuwa zinaanguka kwa kasi. YESU alikuwa akilia, na kusema, “Binti hivi ndivyo wanadamu wanavyopotea; hivi ndiyo mwanadamu apoteavyo!!!..... Binti, inaniumiza sana mimi nionavyo wanadamu wanavyoangamia.”

YESU akasema, “maapepo pia hufanya mikutano huku.” Na nikasema, “mapepo yanafanya mikutano?” Yesu akasema, "Ndiyo, Binti, wanakutana kupanga, kupanga watavyowafanya wanadamu. Wanakutana kila siku kwa siri.” Na kwa hilo, Yesu akanipeleka kwenye sero,

15
ambapo niliona meza ya mbao na viti vikizunguka meza. Na palikuwa na mapepo, aina zote za mapepo. Yesu akaelezea, “Binti, wanapanga kwenda kuharibu nyumba/familia za wachungaji, wamisionari, wainjilisti na wote wanijuao mimi. Binti wanataka kuwaharibu; wanamishale mingi.”

Mapepo hucheka na kudhihaki, na kusema, “acha tuwaharibu wanadamu na kuwaleta huku.” Yesu akasema, “Nenda na uwaambie nipo pamoja nao watu wangu. Waambie wasiache milango wazi, wasimpe nafasi shetani, kwa kuwa shetani anazunguka-zunguka kama simba angurumaye, akimtafuta wa kummeza. (1 Petro 5:8)" Lakini neno linasema, "anatembea kama", kwasababu simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti (Ufunuo 5:5)! Yesu akasema, "Binti, wanataka kuharibu/kuangamiza familia za wachungaji.”

Nikamuuliza, “Kwanini wanataka kuharibu familia za wachungaji?” na Yesu akajibu, “Kwasababu wanawajibu wa maelfu ya watu ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana aliowakabidhi wao. Wanataka watu hao warudie dunia tena; waangalie nyuma na kuishia kuzimu…. Nenda kawaambie wachungaji kusema iliyo kweli tupu. Waeleze wahubiri kweli tupu na kusema kila kitu ninachowaambia na wasinyamaze nayo haya ninayowaambia!”

Tulipokuwa tunaondoka hapo, akaniambia, “Nataka nikuoneshe kitu kingine…. Wapo pia watoto huku.” Na nikamjibu, “watoto huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako lasema, 'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wao." (Mathayo 19:14) Yesu akajibu, “Binti, ni kweli, ufalme wa mbinguni ni wao, lakini mtoto lazima aje kwangu, kwa kuwa kila ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37) Ghafla, Bwana akanionesha mvulana wa miaka nane akiteswa kwenye moto. Mvulana akalia, “Bwana nihurumie mimi, nitoe mahali hapa, sitaki kuwepo hapa!” aliendelea kupiga kulia na kelele. Nikaona mapepo yamemzunguka mtoto huyu, yaliyofanana na cartoon.

Kulikuwa na aina za Dragon, BoyZ, Ben 10, Pokémon, Doral, na nyingine nyingi. “Bwana, kwanini mtoto huyu yuko huku?" Yesu akanionesha picha ya mkanda wa maisha mtoto huyu. Nilimwona anavyotumia muda karibia wote kwenye LUNINGA [TV] akiangalia cartoon.

Cartoon ya Ben 10: Pokemon:
Yesu akasema, "Binti, hayo maigizo ya cartoon, sinema zake, michezo mbalimbali ya kuigiza inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya shetani atumiavyo kuwaharibu wanadamu….. tazama, binti ilivyotokea kwa mtoto huyu." Nilimwona jinsi mtoto huyu alivyokuwa mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi wake aliposema naye alikimbia na kutupatupa vitu ovyo na kuto-watii. Baada ya hapo akagongwa na gari na ukawa mwisho wa maisha yake. Yesu akasema, “Tangu hapo yupo mahali hapa.”

Nilimtazama mtoto Yule akiteswa. Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie wazazi wawaelekeze watoto wao kama ilivyo katika neno langu.”(Mithali 22:6) Neno la Mungu ni halisi,

16
linatuambia tumwonye mtoto kwa fimbo, lakini si kila wakati, pale tu mtoto anapoonyesha ukaidi kwa wazazi. (Mithali 22:15).

Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza mno. Akasema, “Binti, wapo watoto wengi sana huku kwasababu ya cartoon, kwasababu ya ukaidi.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini lawama ziwe hizi cartoon?” Naye akanieleza, “Kwasababu ni mapepo yanayobeba ukaidi, kiburi, ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na mapepo mengine huwaingia watoto ili wasifanye mambo mazuri, bali wafanye mabaya: vile waonavyo kwenye LUNINGA [TV] watoto hutaka kufanya vivyo hivyo.” Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi, na watoto lazima waamue watakwenda na nani. Nikasema, “Bwana, niambia, kwanini kuna watoto huku?” na Yesu akanijibu, “Mara watoto wapatapo kujua kuna mbinguni na kuzimu, hapo wanayonafasi ya kuchagua.”
UFALME WA MBINGUNI

Kuna mengi ya kusema juu ya kuzimu, lakini kwasasa niwashirikishe niliyoyaona Mbinguni. Yesu akasema, "Binti, sasa nitakuonesha nilichowaandalia watakatifu wangu.” Tuliondoka kule kuzimu kupitia lango lake. Tulipokuwa tukisafiri kutoka nje ya kuzimu, ghafla tukatokea mahali penye mwanga. Sikuona giza tena, mateso wala miale ya moto. Akasema, “Binti, nitakuonesha utukufu wangu,” na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme wa Mbinguni! Mara tukafika kwenye mlango wenye maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa dhahabu, yalisema: “Karibu kwenye Ufalme wa Mbinguni.”

LANGO LA MBINGUNI
Yesu akasema, “Binti, ingia, kwa kuwa mimi ni Mlango na kila aingiaye kupitia kwangu, ataingia na kupata marisho.”(Yohana 10:9)

Baada ya Bwana kusema maneno hayo, mlango ukafunguka na tukaingia. Niliwaona malaika wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa Mbinguni! (Ufunuo 7:11-12) Kadri tulivyozidi kutembea, tulikaribia meza niliyoweza kuona mwanzo wake laini siyo mwisho. (Ufunuo 19:9) Niliona enzi kubwa, na enzi ndogo zimezungukwa na maelfu ya viti. Katikati ya viti niliona mavazi na mataji. Bwana akaniambia, “Binti, taji unayoiona pale ni taji ya Uzima."(Ufunuo2:10).

Yesu akasema, “Tazama, Binti, hii ndiyo niliyowaandalia watu wangu.” Niliona ile meza imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu. Kulikuwa na sahani, glasi za dhahabu, matunda; kila kitu kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri ajabu. Kulikuwa na chombo kikubwa katikati ya meza, kilichokuwa na mvinyo tayari kwa mulo. Na Yesu akasema, “Binti, kila kitu kipo tayari kwa ujio wa kanisa langu.”

17
MEZA YA KARAMU YA MBINGUNI
Tulikwenda mahali pengine, niliwaona watu wengi wakiwa bustanini. Kulikuwa na watu wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa wazee, bali vijana. Palikuwa na kijana akiwa na kitambaa mkononi, akicheza na kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu akasema, “Binti, Yule kijana pale ni mtumishi wangu Daudi.” Alikuwa akimpa utukufu Baba yetu. Ghafla, kijana mwingine akapita na Yesu akaniambia, “Binti, huyu ni Joshua; Yule Musa; na Yule pale ni Ibrahimu.” Yesu huwaita kwa majina yao. Wote walikuwa na mwonekano mmoja! Ajabu sana Mbinguni! Yesu akasema, “Mwanamke Yule ni mtumishi wangu, Maria Magdalena; na Yule mtumishi wangu Sara."

Lakini pia akaniambia, “Binti, huyu ni Maria. Maria, aliyemzaa Yesu Kristo, ambaye ni mimi. Binti, nikwambie, yeye hana habari ya yanayotokea duniani. Nataka kukwambia, nenda kawaambie wanadamu, waambie waabudu sanamu kuwa kuzimu ni halisi, na waabuduo sanamu hawata urithi Ufalme wangu, lakini waambie kama wakitubu, wataweza kuingia makao ya mbinguni. Nenda waambie nawapenda na pia waambie Maria hajui chochote [kinachotendeka duniani] na pekee wanayeweza kuheshimu ni mimi, kwasababu si maria wala mtakatifu Gregory wala mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye na nje yangu- hakuna yeyote, hakuna yeyote, hakuna yeyote – aokoaye!” Alirudia mara tatu-kuwa hakuna yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye.

Wanadamu wamedanganywa na kuamini kuwa kwa kupitia wadhaniwao ni watakatifu, sivyo ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi kupitia sanamu zilizofanywa kwa mikono ya watu. Lakini ngoja nikueleze kwamba Bwana anataka kukupa kilicho bora. Anataka wewe uingie katika Ufalme wa Mbinguni; tubu na kuacha uabudu sanamu. Kwasababu ibada ya sanamu haitakuokoa wewe. Yesu Kristo wa Nazareti ndiye pekee aokoaye, aliyeutoa uhai wake kwaajili yako, yangu na kwaajili ya wanadamu wote. Bwana ana ujumbe mzito kwa wanadamu. Huku akilia aliniambia, “Tafadhari, Binti, usikae kimya; nenda na uwaambie ukweli, nenda na uwaambie nilichokuonesha wewe.”

Sanamu za Maria na Waumini wa kisujudia
Nilimwona Maria akimwabudu Bwana, na niliwaona wanawake wakiwa na nywele ndefu nzuri. Nikasema, “Bwana, wanapendeza sana walivyoweka nywele zao.” Akaniambia, “Binti, kile uonacho ni utaji niliowapa wanawake.” Akaongeza, “Binti, nenda na uwaambie wanawake watunze utaji niliowapa.”

18
Kisha akaniambia, “Nina kitu cha muhimu cha kukuonesha.” Nikatazama mbali kidogo na kuona MJI UNG’AAO, MJI WA DHAHABU! Nikasema, “Bwana, kile ni nini? Nataka kwenda pale.” Akanijibu, “Binti, nitakuonesha kilichopo pale. Ukionacho ni makao ya Mbinguni, majumba ya Mbinguni yaliyotayari kwaajili ya watu wangu.”
Tulianza kutembea, hadi tukafika kwenye daraja la dhahabu. Mara tulipovuka daraja, tukafika kwenye mitaa iliyotengenezwa kwa dhahabu safi! (Ufunuo 21:21)

Kila kitu kilikuwa kizuri sana, kuzuri sana pale, kunang’aa kama kioo, ni mahali pasipo pakawaida, hakuelezeki! Tuliona majumba ya ki-mbinguni na pia tuliwaona, maelfu ya malaika wakijenga. Baadhi ya malaika walikuwa wanajenga kwa haraka ya ajabu, na wengine pole pole na wengine walikuwa wamesimama kabisa kujenga.

Nikamuuliza Bwana, “Kwanini malaika wengine wanajenga haraka haraka, wengine polepole, na wengine wamesimama?" Bwana akanieleza, “Binti, hivyo ndivyo wafanyavyo watu wangu duniani, na malaika wanafanya kama wafanyavyo watoto wangu duniani…. Binti, watu wangu hawahubiri neno langu. Watu wangu hawafungi tena. Watu wangu hawaendi mtaani kusambaza ujumbe wa neno langu kwa vipeperushi vinavyoeleza ukweli. Watu wanaona aibu kuhubiri.

Nenda kawaambie watu wangu warudi kwenye njia za zamani. Wale malaika uliowaona hawafanyi chochote ni malaika wa watu wangu waliorudi nyuma na kuacha njia zangu… Binti, nenda waambie watu wangu warudi njia zao za zamani,” (Yeremia 6:16) na baada ya kusema haya akaanza kulia Bwana.

Nikasikia watu wengine wakiimba, hivyo nikamuuliza, “Bwana, nataka unipeleke kule, ambako watu wanaimba.” Yesu alikuwa akiniangalia, nakwambia jinsi alivyokuwa ananiangalia, sikuweza kuona vema uso wake bali alikuwa akigeuza uso wake. Wakati huo machozi yalikuwa yakimtiririkia kwenye vazi lake, nikamuuliza kwanini analia. Lakini hakuweza kunieleza.

Baadaye tulifika kwenye bustani nzuri sana. Pale katika majumba ya mbinguni, niliona maua yalikuwa yakiyumbayumba huku na huku kama yapulizwayo na upepo. Hizi huenda ndizo sauti za kuimba nilizozisikia. Bwana akaninyoshea kidole na kusema, “Binti, tazama, maua yananisifu mimi; yananiabudu mimi! Watu wangu hawafanyi hivi tena kama walivyokuwa wanafanya mwanzo. Watu wangu hawanisifu, hawaniiabudu mimi; hawanitafuti mimi kama mwanzo. Ndiyo maana nalikwambia mwanzo, Binti, nenda na uwaambie watu wangu wanitafute, kwa kuwa nitakwenda, nitakwenda, nitakwenda kwa wanaonitafuta kwa roho na kwa kweli, kwa watu walio tayari, kwa watakatifu!” na huku akilia akasema, “Ninakuja, ninakuja!” hapo nikaelewa kwanini alikuwa analia, kwasababu anakuja, lakini si kwa wasio na nia, watu wa nia mbili [vuguvugu]. Atarudi kwa wale tu wanaomtafuta katika roho na kweli.

Ndipo Bwana akaniambia ninatakiwa kurudi duniani. Nikasema, “Bwana, Sitaki kurudi duniani! Unamaanisha nini- duniani? Nataka kubaki na wewe Bwana. Umenileta huku na mimi siendi kokote kwasababu niko na wewe!”

Yesu akasema, “Binti, ni muhimu urudi duniani ili ukashuhudie kwamba utukufu wangu ni halisi, yote niliyokuonesha kuwa ni kweli; ili wanadamu waje kwangu, watubu na wasiangamie.” Bwana akaanza kulia, nami nikaanguka miguuni pake; nikaona vidonda kwenye miguu yake. Nikamuuliza, “Bwana, hivi ni vidonda vya nini?” akajibu, “Binti, ni vidonda ya jana, nilipotoa maisha yangu kwaajili ya wanadamu.”

19
MKONO WA YESU
Bwana akanionesha vidonda vyake vya mikononi, nilimuuliza, “Bwana, kwanini ungalinavyo hata sasa?” akaniambia, “Binti, ni vidonda vilivyobaki.” Hivyo nikamuuliza, “je vitapona?” akanijibu, “Vitapona na kufutika tu baada ya watakatifu wote kuungana hapa….. Binti, lazima nikurudishe duniani: Familia yako na mataifa yanakusubiri wewe.”

Nilijaribu kukataa lakini akanyosha kidole chake chini duniani na kusema, “Tazama, wale watu uwaonao chini pale ni ndugu zako; na mwili ule uuonao pale, ndiyo utakaoingia…… ni muda wa kuondoka mahali hapa.” Baada ya hapo akaanipeleka kwenye mto mzuri mwangavu na akasema, “Binti, ingia katika mto na jizamishe mwenyewe.” Kabla sijaingia ndani ya mto wa maji ya uzima, nilikuwa najisikia furaha ya ajabu, lakini baada ya kujizamisha na kutoka nje, nilipata furaha kuu. Nilidhani sitarudi tena nyumbani kwetu, lakini Bwana akaniambia, “Binti, unatakiwa kurejea duniani….. Binti, nitakuonesha kitu: jinsi nitakavyorudi mara ya pili kwaajili ya watu wangu watakatifu. Nitakuonesha jinsi siku ile ya kutisha itakavyokuwa.”

FURAHA NA MAOMBOLEZO
Tulitembea hadi sehemu yenye kioo kikubwa kama LUNINGA [TV], nikaona watu. Niliweza kuona dunia yote. Ghafla nikaona maelfu ya watu wakipotea. Wanawake wenye mimba, mimba zilipotea, na wakawa kama wamechanganyikiwa na kupiga mayowe.

Watoto walitoweka pande zote. Watu wengi walikuwa akikimbia huko na huku, wakipiga kelele, “Haiwezekani, haiwezekani, nini hiki kitokeacho?”

Niliwaona wale waliomjua Bwana na kuachwa nyuma. (Mat.24:40-41) Walikuwa wakisema Kristo amekuja, furaha imetimia. Walikuwa wakipiga kelele na kutafuta kujiua wenyewe lakini hakuwezekana. Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo kifo kitawakimbia; Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena.” (Ufunuo 9:6) kulikuwa na ajali nyingi lakini sikuona hata mtu mmoja aliyekufa: wote walikuwa wazima japokuwa wameumia [majeruhi].

Niliona mlolongo mrefu wa maelfu ya watu. Akaniambia, “Binti, tazama, hivi ndivyo kila kitu kitakavyokuwa.” Kisha nikaona watu wakikimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakipiga kelele, Kristo kaja, Kristo kaja!” wakisihi, “Bwana nisamehe mimi, nisamehe mimi, nichukue nawe!”

20
Baada ya Bwana kuwachukua watu wake [Unyakuo]
Lakini kwa huzuni Bwana akasema, “Watakuwa wamechelewa. Muda wa kutubu ni sasa…. Binti, nenda kawaambia wanadamu wanitafute mimi, wakati huo hakutakuwa na nafasi. (Isaya 55:6) Binti, watakuwa wamechelewa wote watakaobakia nyuma.” Baada ya Yesu kuona watu wataobaki nyuma akaanza kulia na kusema, “Binti, nitakwenda duniani kama neno lisemavyo katika 1 Thes. 4: 16-17: “Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo.”

SIKU YA MWISHO
Lakini si kila mtu atakwenda na Bwana, wale tu wafanyao mapenzi yake (Mathayo 7:21) na aishiye maisha matakatifu. Kwa kuwa Bwana aliniambia, “Wale tu walio watakatifu wataoingia Ufalme wa Mbinguni, (Waebrania 12:14) Hakuna ajuaye, siku wala saa nitakayokuja kwaajili ya watu wangu watakatifu, hata malaika hawajui.” (Mathayo 24:36)

Kwenye Kioo cha LUNINGA [TV] niliona watu wakikimbia huko na huku. Magazeti yalisema “KRISTO AMEKUJA.” Kioo kikafungwa, na Yesu akamalizia kwa kusema, “Ninakuja kwa watakatifu.” Hivi ndivyo alivyonionesha mimi. Baada ya hapo akanirudisha duniani hapa. Tukiwa na kusanyiko la malaika wengi wakituzunguka, tulianza kushuka ngazi nzuri kama nini; ngazi nyeupe na maua yakizunguka. Nilikuwa nalia njia nzima kushuka chini, nikimsihi Yesu, “Bwana tafadhari usiniache hapa. Nichukue niwe nawe!” Alinijibu, “Binti, mataifa yanakusubiri, familia yako wanakusubiri wewe…….. Binti, lazima urejee mwili wako. Lazima upokee uhai wako, Binti, ili uweze kwenda kushuhudia yote uliyoyaona. Wengi hawatakuamini wewe; wengi watakuamini, bali mimi ni shahidi wako mwaminifu. Niko pamoja nawe. Sitakuacha kamwe."

21
KURUDI DUNIANI KWA ANGELICA
Maxima:
Binti yangu aliporudi, tulikuwa tunamsubiri pale, na alikuwa amelazwa pale pale chini sakafuni. Nikasikia mguno, "uuhmm," bila kitu. Nikasema, “ahsante Bwana kwasababu Binti yangu amerudi!”.

Sote tulimshukuru Bwana. Mara akaanza kupumua polepole, kidogo kidogo. Baada ya muda wa masaa matano, alikuwa na uwezo wa kufumbua macho na kusema. Mwanzo tulipata shida kumuelewa asemacho; ilikuwa ni vigumu kumuelewa. Hakuwa na nguvu kabisa. Ilibidi tufunge madirisha kwasababu macho yake hayakuwa na uwezo wa kuhimili mwanga.

Kwakuwa wadadisi, sote tulitaka atueleze alichoona. Lakini kwa kuwa alikuwa dhaifu, aliweza kutueleza kidogo tu. Ilimchukua karibu wiki mbili hadi alipoweza kutushirikisha habari nzima ya ushuhuda wake.

Mapepo yalikuja kumtesa baada ya hayo yote. Aliweza kuyaona waziwazi; yalijaribu kujificha kwenye vivuli. Yalikuwepo hapa karibu siku tatu mfululizo tangu arudi, kabla hajaweza kutueleza. Aliyauliza yalikuwa yanataka nini, nayo yakamjibu, “tumekuja kufanya mkataba nawe…….

Ni lazima ufunge mdomo, ni lazima usiseme lolote ya hayo uliyaona kule chini, kwasababu ukisema, tutakuuwa.” Aliyaelezea yalivyo mapepo, yana sura mbaya, makubwa na manene yanatisha. Alisema hakuna maneno yakuelezea jinsi yatishavyo kwa mwonekano. Alijaribu kuyakemea lakini yalikataa kuondoka. Yakifika yalikuwa yanamrukia na kumchoma. Naye aliendelea kupambana nayo na kuyakemea, lakini hakuweza kwasababu hakuwa na nguvu. Siku moja alipokuwa anayakemea, mwanga mkali wa ajabu ulitokea na yakakimbia yote! Alikuwa ni Bwana.

Alichopitia Binti yangu hakikuwa rahisi. Alipewa ujumbe wenye maono ya ndani kwaajili ya wanadamu, ili wamtafute Mungu. Wanadamu wanadhani wafanyayo ni sahihi. Vijana wamezama kwenye madawa ya kulevya na pombe, na kuona ni sawa maisha hayo, lakini si sawa.

Miongoni mwa alioneshwa binti yangu ya kutisha ni wasanii wengi walivyojaa kuzimu, wanamuziki/wacheza dansi na pia Papa John Paul II. Ni wakati wa kumtafuta Bwana, kutubu, na kujishusha na kujidhiri mbele za zake. Neno la Mungu ni kweli lisemalo, “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”(Mark 13:31) Neno la Bwana litatimizwa katika muda wake. Bwana alimwonesha tanuru ambalo watu walikuwa wanatembea kuelekea kuzimu. Na watu wengi tayari wakiwakuzimu. Ni kweli haya, lakini hata watu wa Mungu hawaamini haya, wengi hawaamini.

Ujumbe mkuu ni kwamba tumtafute Bwana, siyo kwa kinywa/mdomoni, bali kutoka ndani ya moyo, kwakuwa kurudi kwa Bwana ku-karibu. Yesu alisema, “Siko tena mlangoni; niko zaidi ya mlangoni. Nakuja muda simrefu; kuja kwangu ku-karibu. Watu wangu wameniacha na wamerejea mambo ya duaniani……… waambie watu wangu warudie njia zao za zamani.”

22
Kanisa leo linatakiwa kurudia njia zake za zamani; hapa tulipo ni wa motoni, tumtafute Bwana. Pale parapanda ikilia tuwe tayari kukutana na Bwana, itakuwa ajabu sana!

UJUMBE WA MUHIMU WA BWANA
Angelica akiongea mbele ya haraiki:
Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena duaniani. Siku hizo hatakuwepo duniani.” (2 Thes. 2:7) Na nikaona msongamano mkubwa wa magari na ajali nyingi sana. Watu wengi walijaribu kujiua, lakini Yesu akasema, “Watatafuta kifo, lakini kifo kitawakimbia wanadamu. Kifo hakitakuwepo tena siku hizo.”(Ufunuo 9:6) Nikawaona watu wakitazama LUNINGA [TV] na kusoma magazeti yakisema, “Maelfu na maelfu wamepotea.” Wengi watajua kuwa Yesu ameshakuja kwaajili ya watu wake watakatifu. Wale waliomjua Bwana lakini wameachwa, wakakimbia mitaani wakilia, wakijaribu kujiua wenyewe lakini hawakuweza lolote.

Nilipokuwa mbinguni, Yesu alisema, “Nina kuja duniani kwaajili ya watu wangu watakatifu na ninakuja mapema kwaajili ya kanisa langu.” Lakini wiki mbili zilizo pita Bwana aliniambia, “Binti, ninafurahishwa na unavyotenda, kwa kuwa unatimiza niliyokuagiza na nakukupa, lakini usiwaambie watu wangu kuwa nitakuja mapema, waambie ninakuja sasa hivi.” Tena Bwana akasema, “Waambie watu wangu ninakuja sasa hivi na ninakuja kwa watu watakatifu. Waambie watu wangu nakuja kwa watakatifu tu, nao ndio wataoniona mimi!.... tena usinyamaze: endelea kuwashuhudia ninayokwambia.”

Angelica akiomba na haraiki:
Kila mmoja afumbe macho, na weka mkono wako wa kuume kifuani. Inua mkono wa kushoto juu, kama unajisikia kulia[toba], lia tu. Sasa mweleze Bwana kile unachojisikia moyoni. Kwa wale waliotayari kumpokea.

Bwana, wafuatiane nami ktika maneno haya:
Bwana, ninakushukuru kwa Upendo na huruma yako, ahsante Bwana kwa maneno yako yaliyotufikia mioyoni leo. Baba, ninaomba msamaha kwako, unisamehe. Unisamehe mimi. Unioshe kwa damu yako ya thamani. Andika jina langu katika kitabu cha uzima. Nipokee/nikubali mimi niwe mwanao Bwana. Sasa hivi, ninamsamehe kila mtu niliyeshindwa kumsamehe. Ninakana hali yangu ya kutosamehe. Ninayakana yote yalinizuia nisikufuate Bwana, ninaomba unibadilishe Bwana na unijaze uwepo wako ndani yangu kila siku. Ahsante Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Ameni.

23
Angelica:
Ushuhuda huu siyo uwongo; siyo mzaha; siyo hadithi; siyo ndoto, kuzimu ni kweli ipo! Kuzimu ni halisia! Kwa yeyote asiyeamini, nataka kukueleza kuzimu ni kweli ipo, ni kweli ni halisi. Ninakosa maneno zaidi mazuri ya kuelezea uhalisia wa kuzimu. Natamani kama ungeshuhudia wewe mwenyewe. Lakini tafadhari amini, tii na uonyeke kwa ushuhuda huu [ushuhuda ukuonye na kukubadilisha] ili uepuke moto wa milele.

Angelica akiongea na Mfasiri/Muelezeaji:
Muda ukaribu sana, Mungu anaruhusu ishara kwa wanadamu zitokee ili kuwaonesha kitakachotokea. Usibakie ukihukumiwa; ndilo shetani atakalo. Jiulize kama uko tayari ukitembea kuelekea shimo la kuzimu? Leo ni siku ya wokovu, leo ni siku ya kumkaribisha Yesu, kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako.

Haya ni maneno rahisi lakini ni makubwa sana kusema: “Ninakubali na kukupokea Yesu uwe Bwana na Mwokozi wangu. Ninakupa wewe maisha yangu na roho yangu kwa moyo wangu wote. Natakuwa kuwa nawe kwa maisha ya milele.”

Chagua hatima yako baada ya maisha haya: Uzima au mauti, Mbinguni au kuzimu, Yesu au shetani. Iko wazi, uko upande wa Yesu au upande wa shetani. Au unafanya yaliyo mema au unafanya yaliyo mabaya. Chagua mwisho wako: uzima wa milele au ziwa la moto. Fikiria jambo hili. Fanya uamuzi sasa. Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili yetu, kwa dhambi zetu, na akatupa fursa ya wokovu kwa huruma yake. Mpokee Yesu Kristo kuwa mwokozi wako!

“Sasa umesikia ushuhuda huu, usiipoteze nafasi hii ukaijutia milele na milele motoni.”

24
Marejeo:
Ufunuo 19:9 ….Heri walioalikwa karamu ya arusi ya mwanakondoo. ……..maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.

Ufunuo 20:15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Ufunuo 21:4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.

Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
“Hakuna waabuduo sanamu wataourithi ufalme wa Mbinguni.”

Kutoka 20:4-5 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu.

Ufunuo 21:21 Na milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.

Ufunuo 21:27 Na ndani hakitaingia kamwe chochote kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana koondoo wa Mungu.

Ufunuo 22:7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.

Ufunuo 22:11 Mwenye kudhuluma na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

Ufunuo 22:12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Ufunuo 22:13-15 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

MWISHO
 
Hii ni chai tupu iliyotungwa na wajinga ili kutisha watu hakuna kitu kama hii
Spiritual realm haipo hivyo kamwe!

Mungu ni Upendo hawezi kumuonesha mtu matukio ya kutisha hivyo.

huu upumbavu ndio unafanya watu wamuogope Mungu na kumuona katili badala ya kumpenda kwa Moyo wote
halafu kingine napoona hii ni chai ni pale mhusika anapodai kurudi Yesu mara ya pili wakati alisharudi miaka 2023 huko nyuma siku ya pentecoste na sasa tupo nae hapa hapa kwa kila amwaminie anapokea Roho mtakatifu ambaye ni roho wa BWANA na hiyo kusema atarudi tena ni ujinga wa watu kutojua Gospel code wakidhani atarudi katika mwili wakati kila alichofanya Yesu kilikua ni Spiritual realm na ndio maana wakati Pilato anamuuliza kama yeye ni Mfalme anajibu ndio ila sio wa Ulimwengu huu akiwa na maana hamaanishi katika mwili ila ni Roho na huo ndio Ulimwengu mkuu unaotawala kila kitu,

watu wasipoelewa Biblica code wataendelea kulaghaiwa na shuhuda fake za kuwajaza matango pori kama nipo wrong naomba Roho mtakatifu anifundishe ila kwa navyoujua Ulimwengu wa roho unavyotenda kazi hii story ina walakini!
 
Kaenda kuzimu, kaenda na mbinguni kisha akarudi duniani kutuletea huu ushuhuda?

Angefanya tu kama alivyofanya Yohana aliopewa Ufunuo na Roho Mtakatifu.

Kwa maana hiyo huu ungekuwa Ufunuo wa angélica ningeelewa zaidi, ila kwa hili la kwenda huko kisha akarudi duniani hata Yohana hakufunuliwa kwa namna hiyo bali alifunuliwa akiwa kifungoni ktk kisiwa cha Patmo na baada ya huo Ufunuo aliuwawa, iweje angalica akabaki hai?
 
Kaenda kuzimu, kaenda na mbinguni kisha akarudi duniani kutuletea huu ushuhuda?

Angefanya tu kama alivyofanya Yohana aliopewa Ufunuo na Roho Mtakatifu.

Kwa maana hiyo huu ungekuwa Ufunuo wa angélica ningeelewa zaidi, ila kwa hili la kwenda huko kisha akarudi duniani hata Yohana hakufunuliwa kwa namna hiyo bali alifunuliwa akiwa kifungoni ktk kisiwa cha Patmo na baada ya huo Ufunuo aliuwawa, iweje angalica akabaki hai?
Huko Equador mbona mbali? Nimeshaona clip za zaidi ya wanawake watano hapa Bongo wenye madai kama hilo
 
Duh nimescroll dakika nzima bila jusoma sijuii ukitaka kusoma utachukua siku ngap
Kilichoandikwa:

- Angelica Zambrano ni msichana kutoka Ecuador aliyesema kuwa alitembelea mbinguni na kuzimu.

- Aliongea na Yesu ambaye alimweleza juu ya hali halisi ya mbinguni na mateso ya kuzimu.

- Yesu alimweleza kuwa wale wanaomwamini lakini bado wana maisha ya dhambi watateseka kuzimu.

- Aliona watu wakiadhibiwa kuzimu kwa sababu mbalimbali ikiwemo uasherati, ulevi, kutomwamini Mungu n.k.

- Aliwaona wengine wakiungua katika ziwa la moto na wengine wakiteswa na pepo wabaya.

- Aliambiwa kuwa wale wanaomwamini Yesu lakini bado wanafanya dhambi hawataingia mbinguni.

- Anawaonya watu kutubu ili wasiende kuzimu baada ya kufa.

- Anasisitiza umuhimu wa kumfuata Yesu kwa nidhamu ili kuepuka adhabu kali za kuzimu.

- Anawataka watu kusamehe iliwapate usamehe.

Kwa ufupi, Angelica Zambrano aliweka mkazo kuwa ni muhimu kutubu na kuishi maisha safi ili kuepuka mateso makali ya kuzimu.

=
My take

  • Madai kwamba msichana huyo, Angelica Zambrano, alitembelea mbinguni na kuzimu hayana ushahidi wowote. Huu ni uso tu, haithibitiki kiukweli.
  • Maelezo kuhusu mateso ya kuzimu yanatokana na imani za kidini na hazijathibitishwa kisayansi. Hakuna uhakika kama kuna mateso hayo au la.
  • Ushauri kwamba watu watubu ili waepuke kuzimu unaweza kuwa na lengo zuri la kuwafanya watu waishi vema, lakini halina ushahidi wa kisayansi.
  • Ushuhuda kwamba aliona mateso halisi ya kuzimu hauwezi kuthibitishwa. Inawezekana ni ndoto au tafakuri tu za mwandishi.
 
Kwa Dunia ya sasa Habari bila picha/video clip sawa na takataka tu
 
Screenshot_20231003-180216.jpg

Kanuni ya Mungu ni hiyo juu.
Hutumia walio hai tu. Wala hahitaji mtu aliyetoka kuzimu au peponi.
Screenshot_20231003-180216.jpg
 
Huko mbinguni aliona walio kwenye Biblia tu, na siyo wengine tunaoweza kuwajua kama aliowakuta kuzimu?!!!

Interesting.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom