Sura za viongozi wa dola ya Rumi zinajulikana lakini sura ya Yesu Kristo haijulikani

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,548
6,102
Dola ya Rumi au unaweza kuiita Roman Empire ni moja ya falme nne zenye nguvu zilizo tokea kuitawala duniani kama ilivyo tabiriwa kutoka kwenye maandiko matakatifu. Soma kitabu cha (Danieli sura ile ya pili)

Dola hii iliyo anza kuitawala Dunia kuanzia mwaka wa 27BC mara baada ya kuanguka kwa utawala wa Wayunani (Ugiriki ya Kale). Iliitawala Dunia kwa karne zisizo pungua tano mpaka hapo ilipo kuja kuvunjika yenyewe mwaka wa 476AD ikitoka katika mfumo wa Rumi ya kipagani na kuja Rumi ya kidini.

Dola hii iliongozwa na viongozi mbalimbali kama Julius Caesar aliye zaliwa mwaka wa 100BC na kufariki mwaka wa 44BC. Huyu ndiye chanzo cha viongozi wa dola hii ya Rumi kuanza kuitwa KAISARI yaani kama saivi tunavyo waita viongozi wa nchi Rais,

Basi bhana cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba tangu utawala wa Dola hii ya Rumi uanze viongozi wao wote sura zao zipo mpaka leo zinajulikana lakini sura ya Yesu Kristo haijulikani mpaka leo.

Ilikuwaje mtu ambaye alikuwa maarufu kipindi hicho kwa maajabu na miujiza yake aliyo kuwa anaitenda sura yake isijulikane mpaka leo maana Yesu Kristo popote alipo kuwa anaweka mguu maelfu ya watu walimfuata.

Inakuwaje mtu huyu sura yake mpaka leo iwe kitendawili lakini sura za watawala ziwepo tena wengine waliishi kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo mfano ni huyo Julius Caesar.

Kipindi Yesu Kristo anazaliwa Duniani mtawala alikuwa ni Kaisari Augustus akafuata Kaisari Tiberias, akafuata Kaisari Caligula, akafuata Kaisari Claudias, Kaisari Nero na wengine wengi ambao sura zao zipo.

Sura tunazo aminishwa ni za Yesu Kristo ni sura za binadamu ambao tunao hapa hapa duniani ambao ni wasanii wacheza filamu wakina Brian Deocon. Jim Caviezel, Diego Morgado na Robert Powell.

Chakushangaza na kusikitika ni kwamba watu hawa wamekuwa wakiabudiwa na kusujudiwa sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye nyumba za ibada majumbani mwa watu n.k.

Madhehebu yanayo fanya ibada siku ya Jumapili ndio vinara wa kuwaabudu hawa wasanii wakina Brian Deacon na genge lake. Je ni sahihi kuwapotosha maelfu ya watu kuamini hao ndio Yesu ilhali sura ya Yesu Kristo hakuna aijuaye?

Biblia inakataza katika zile amri kumi za Mungu kuwa tusiwe na miungu wengine ila Mungu pekee na wala tusiabudu chochote isipo kuwa Mungu pekee(kutoka 20).

Mwisho Namalizia kwa kusema shetani ananguvu sana hapa Duniani tuzidi kumuomba Mungu sana.
Screenshot_20220504-133809.jpg
 
Kwanza, wakuu wa makuhani na kikosi Chao walihitaji yuda iskarioti ili kumtambua Yesu. Hakuwa maarufu kwa sura hasa maeneo ya Yerusalemu. Alifahamika zaidi maeneo ya galilaya.

Pili hizo sura ziliweza kupatikana kwasababu Walikuwa kwenye sarafu za wakati huo na baadhi zilipatikana kwenye archeology.

Tatu, kuabudu sanamu (au tuseme kuwa na sanamu) ni hasa katoliki (ambayo mimi sijawahi kuhesabu kama ni kanisa). Hao Wana dini yao ila wameificha kwenye jina la kanisa. Wanaabudu pia kitu kinaitwa bikira maria.

Nne, unaonekana kuwa msabato. Huwa nawakubali kwa kusisitiza watu kujua kwamba maisha hayaishii duniani LAKINI ninamfahamu pia kwamba na nyie mnayo sanamu yenu mnaiita siku ya sabato. Kwamba usipoabudu siku hiyo basi umepotea.

Tano, mimi nikwambie kwamba ndani ya Yesu tunamwabudu Mungu katika Roho na kweli. Hatuabudu siku maalumu Bali kila siku. Kukutanika kama mwili wa Kristo ni kutegemeana na makubaliano japo makanisa mengi yamefuata utaratibu wa mitume kukutana siku ya kwanza ya juma.

Amani iwe pamoja nawe.
 
Mkuu, kwamba unataka kusema nini? Hebu funguka zaidi ili tuweze kuchangia kwa urahisi.

Kitu natamani ufahamu ni, kama umeamini shetani ana nguvu sana. Ni dalili kwamba umeamini Shetani yupo, na kupitia huo ujasiri ni ishara unaamini na Mungu naye yupo. Na hili linakwenda mbali zaidi kumaanisha unafahamu Mungu ndiye aliyemuumba Shetani. Kwa sababu hiyo, ni wazi kwamba kama Mungu hajachukua hatua yoyote mpaka sasa inamaana ni labda hakuna tatizo au yanayoendelea ni madogo hayana ulazima wa yeye kuingilia kati.

Imani ni kitu pekee kwenye duania hii chenye uwezo wa kuushinda ukweli. Tuchague kwa makini vya kuviamini. Vingi tunavyoamini vipo havipo na tunavyoamini havipo vipo.
 
Mi Pia binafsi kuzaliwa ni Roman Catholic...
Ila kuna mambo matatu kwakweli huwa moyo wangu huwa na sita angali sijajua Biblia.

1. Siku ya Ijumaa kuu kupiga goti na kubusu msalaba wenye sanam ambayo haifanani kwa zote na makanisa yote.

2.Kwenda kumsimulia Padre dhambi zangu kwa kificho aseee.

3.Kumuabudu Bikira maria li hali hata yeye baada ya Yesu kupaa alianza kujifunza mafundisho ya Kristo.

Shida nilio nayo Makanisa mengine ya Kiroho hayako katika kufundisha kweli ya Biblia na kuishia kufundisha maisha ya mtaan na kuuza bidhaa.
Pia mpaka sasa huwa na pata hata kigugumizi juu ya kifo changu.
Japo sikupenda kufanyiwa mazishi ya Kiroma kweli aslan.
Lakini ndipo nilipo kulia kiimani na kuoa na hata ubatizo.

Ila kweli tuna pata taabu sana sisi tulio na kiu ya kujifunza Biblia na kuwaaminisha kweli wale walio potoka
 
Hayo maswali mfwate padri atakupa majibu yote
 
Tatu, kuabudu sanamu (au tuseme kuwa na sanamu) ni hasa katoliki (ambayo mimi sijawahi kuhesabu kama ni kanisa). Hao Wana dini yao ila wameificha kwenye jina la kanisa. Wanaabudu pia kitu kinaitwa bikira maria.

3.Kumuabudu Bikira maria li hali hata yeye baada ya Yesu kupaa alianza kujifunza mafundisho ya Kristo.
Achane kudanganya watu humu wakatoriki hawaabudu sanamu, wala hakuna mkatoriki ambaye ibada yake inaishia kwenye sanamu za kuchonga ni kiwasinvizia tuu. Kama hamuelewi kitu muwe mnauliza kwanza mahali husika kusaidiwa.

Pili hakuna mkatoriki anaemuabudu bikira maria, wala bikira maria haabudiwi popote pale ndani ya kanisa katoriki. Moja ya Sheria zenyenye za hao wakatoriki inasema wakuabudiwa ni Mungu pekee, hakuna kingine chochote che kustahili kuabidiwa zaidi ya Mungu. Iweje sisi tulio nje tuwahukumu kwa mambo tusiyoyajua ?.

Anayepaswa kuabudiwa ni Mungu peke yake. Kwa wakatoriki wao Zipo heshima za viwango tofauti:

1: Mungu kwanza (latria) wanamwabudu.

2: Bikira Maria (Hyperdulia), wanamuheshimu hawamuabudu

3: Watakatifu wengine na vitu wanavyohusika navyo (dulia), wanawaheshimu hawaabudu

4: Picha na sanamu pia hupewa heshima isiyoizidi ile ya watakatifu na Bikira Maria.

Hayo ndiyo madaraja ya heshima ambayo wanazitoa, 2 hadi 4 ni heshima tu na siyo ibada kwa hivyo.
 
Sura tunazo aminishwa ni za Yesu Kristo ni sura za binadamu ambao tunao hapa hapa duniani ambao ni wasanii wacheza filamu wakina Brian Deocon. Jim Caviezel, Diego Morgado na Robert Powell.

Chakushangaza na kusikitika ni kwamba watu hawa wamekuwa wakiabudiwa na kusujudiwa sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye nyumba za ibada majumbani mwa watu n.k.

Madhehebu yanayo fanya ibada siku ya Jumapili ndio vinara wa kuwaabudu hawa wasanii wakina Brian Deacon na genge lake. Je ni sahihi kuwapotosha maelfu ya watu kuamini hao ndio Yesu ilhali sura ya Yesu Kristo hakuna aijuaye?
Sanamu ya Mungu haipo kwani tangu mwanzo Mungu baba hajawahi kuonwa na mtu isipokuwa kupitia kwa mwanae ambaye watu walimwona na waliishi naye wakamfahamu na kumbe kuchonga sanamu ya kufanana naye Isingeliwezekana.

Sanamu za Yesu zafanana naye kwa vile watu walimfahamu alivyofanana lakini zimeletwa kwetu kama ukumbusho wa jinsi alivyokuwa si kwa lengo la kuziabudu au kuwaabudu watu wanaoigiza maisha ya Yesu kwa njia ya video na picha.

Kwa kuziona izo sanamu, picha, video za maigizo ya maisha Yesu nk. hatuna mashaka kuwa alikuwepo kuliko kama tungekuta masimlizi tu.Hivyo hivyo kizazi kijacho kikiambiwa juu ya Nyerere kitaelewa zaidi kikioneshwa picha na sanamu zake lakini hizo picha na sanamu zake hawatasema ndo Nyerere mwenyewe labda kama ni vichaa, na pia hata akitokea mtu akaigiza historia ya maisha ya nyerere au matukio makubwa makubwa kuyafanya tanzania hakuna atakayesema huyo ndio nyerere mwenyewe labda kama ni punguani.
 
ngoja waje wa kanisa takatifu la mitume, maana wao ukiwaambia kupiga goti mbele ya sanamu ni haramu hawasikii ( ilhali wamejifanyia sanamu ya kuchonga)
Kwanza Mungu hakatazi wala hajakataza mtu kuchonga sanamu ila alikataza na anakataza kuzifanyia ibada izo sanamu za kuchonga sababu wa kuabudiwa ni yeye Mungu pekee.
1. Siku ya Ijumaa kuu kupiga goti na kubusu msalaba wenye sanam ambayo haifanani kwa zote na makanisa yote.
Kitu cha msingi ni kusikiliza maneno ya Padre au shemasi anapowaalika watu kuja kuanza kuabudu.

Padre au shemasi husema, Huu ndio mti wa msalaba, ambao wokovu wa dunia
umetundikwa juu yake, njooni tuuabudu
.

Ukifuatilia kwa makini kiswahili sanifu utagundua kuwa, Padre hufanya mambo haya yafuatayo katika mwaliko huo:

1: Huonesha mti wa msalaba.
2: Huambia watu waumini kuwa juu ya mti huo,wokovu umetundikwa
Kisha huwaalika wakauabudu.

Kwa maelezo hayo hapo juu labda ningekuuliza hivi, huyo padre au shemasi huwaalika wakauabudu mti wa msalaba au wokovu ambao umetundikwa juu ya huo mti wa masalaba ?

Hivyo Kwa mwaliko huo,wakatoliki hualikwa kwenda kuuabudu WOKOVU ulio juu ya msalaba.WOKOVU NI NINI? WOKOVU ni jina lililoandikwa kwa kiswahili.Jina wokovu kibiblia na kwa lugha asili ya Biblia ni sawa na jina YESHUA kwa kiebrania au YOSHUA.

Kristo ndiyo WOKOVU wetu tunayepaswa kumwabudu kwani alipokuja aliamua kuanzia kazi yake ya kutuletea wokovu katika mto Yordan pale ambapo Yoshua kahitimishia kazi yake.Yoshua aliwavusha watu toka ng`ambo ya mto kuwaingiza katika nchi ya ahadi ambayo ni Kanaan ya duniani na Yesu anapokuja,kama mwokozi,anataka awatoe watu wake kutoka katika nchi ya ahadi ya kidunia,kuwapeleka katika nchi ya ahadi ya mbinguni.Kumbe Yesu ni mwokozi wetu anayetutoa kutoka katika dunia kwenda mbinguni wakati Yoshua anaitwa mwokozi kwa kuwa aliwatoa Misri akawaleta Kanaan nchi ya ahadi.

Yesu na Yoshua kwa mantiki hii ni hilo jina WOKOVU kama nomino wakati kazi waliyotenda ni ya kutuokoa na kikitamkwa kama kitendo,Yesu au Yoshua, anaitwa Mwokozi.

kueleza kile wanachokiabudu wakatoriki ile Ijumaa Kuu. Padre au Shemasi husema Huu ndiyo MTI wa msalaba ambao WOKOVU wa dunia Umetundikwa juu yake, njooni tuUabudu.

Katika sarufi ya kiswahili hasa tunaposema juu ya upatanisho wa kisarufi, bahati mbaya ni kwamba nomino MTI na nomino WOKOVU zote zimechukua viambishi ngeli U, ili kuwa na upatanisho wa kisarufi. Tunasema kwa mfano, mti umaanguka, wokovu umetujia. Katika sentensi hiyo anayotamka padre au shemasi, ina maneno yote mawili, yaani mti na wokovu yenye kiambishi kimoja tu U kinachotuletea shida kuwa kimerejea nini, wokovu au mti. Kiambishi U, hakirejerei mti bali kinarejea wokovu yaani Yesu.

Kwa hiyo wanaposema njooni tuuabudu, hwamaanishi tuuabudu mti la hasha! Bali wauabudu Wokovu uliotundikwa juu ya mti wa msalaba katika akili zao. Ndiyo kusema, ibada hii kama mtu hawezi kutoka nje ya pale na kupeleka mawazo yake kwa Yesu, aliye Wokovu wetu , bila shaka anaweza kuwa anaabudu sanamu au mti wa msalaba.
 
Yesu kristo wa Nazareth hajawahi exist popote kina Constantine walimpa character mpigania uhuru aliyemiliki genge la kimapinduzi hapo Palestine ya zama zao Umasihi wakitumia character ya Heru/Horus wa accient Egypt na mamaye
Osiris aliyemzaa Kwa uweza wa miujiza au roho mtakatifu Kwa babaye ISS
Total christian moral and Dogma ni copy & paste ya
Accient civilization na sio Yesu tu Bali wale wote wanaojinasibu ni manabii na mitume walisha wahi exist kitambo kabla hao characters wa Bible hawajaexist!
 
Kuondoa huo utata wa kilugha kwani asisema "Mti huu umetundikwa uokovu. Njooni kuuabudu uokovu uliotundikwa kwenye mti huu. "
Itakuwa kweli wanauabudu huo mti jamaa wanajaribu kujitetea tu hapa.
 
Madhehebu yanayo fanya ibada siku ya Jumapili ndio vinara wa kuwaabudu hawa wasanii wakina Brian Deacon na genge lake.
 
Dola ya Rumi au unaweza kuiita Roman Empire ni moja ya falme nne zenye nguvu zilizo tokea kuitawala duniani kama ilivyo tabiriwa kutoka kwenye maandiko matakatifu. Soma kitabu cha (Danieli sura ile ya pili)

Dola hii iliyo anza kuitawala Dunia kuanzia mwaka wa 27BC mara baada ya kuanguka kwa utawala wa Wayunani (Ugiriki ya Kale). Iliitawala Dunia kwa karne zisizo pungua tano mpaka hapo ilipo kuja kuvunjika yenyewe mwaka wa 476AD ikitoka katika mfumo wa Rumi ya kipagani na kuja Rumi ya kidini.

Dola hii iliongozwa na viongozi mbalimbali kama Julius Caesar aliye zaliwa mwaka wa 100BC na kufariki mwaka wa 44BC. Huyu ndiye chanzo cha viongozi wa dola hii ya Rumi kuanza kuitwa KAISARI yaani kama saivi tunavyo waita viongozi wa nchi Rais,

Basi bhana cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba tangu utawala wa Dola hii ya Rumi uanze viongozi wao wote sura zao zipo mpaka leo zinajulikana lakini sura ya Yesu Kristo haijulikani mpaka leo.

Ilikuwaje mtu ambaye alikuwa maarufu kipindi hicho kwa maajabu na miujiza yake aliyo kuwa anaitenda sura yake isijulikane mpaka leo maana Yesu Kristo popote alipo kuwa anaweka mguu maelfu ya watu walimfuata.

Inakuwaje mtu huyu sura yake mpaka leo iwe kitendawili lakini sura za watawala ziwepo tena wengine waliishi kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo mfano ni huyo Julius Caesar.

Kipindi Yesu Kristo anazaliwa Duniani mtawala alikuwa ni Kaisari Augustus akafuata Kaisari Tiberias, akafuata Kaisari Caligula, akafuata Kaisari Claudias, Kaisari Nero na wengine wengi ambao sura zao zipo.

Sura tunazo aminishwa ni za Yesu Kristo ni sura za binadamu ambao tunao hapa hapa duniani ambao ni wasanii wacheza filamu wakina Brian Deocon. Jim Caviezel, Diego Morgado na Robert Powell.

Chakushangaza na kusikitika ni kwamba watu hawa wamekuwa wakiabudiwa na kusujudiwa sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye nyumba za ibada majumbani mwa watu n.k.

Madhehebu yanayo fanya ibada siku ya Jumapili ndio vinara wa kuwaabudu hawa wasanii wakina Brian Deacon na genge lake. Je ni sahihi kuwapotosha maelfu ya watu kuamini hao ndio Yesu ilhali sura ya Yesu Kristo hakuna aijuaye?

Biblia inakataza katika zile amri kumi za Mungu kuwa tusiwe na miungu wengine ila Mungu pekee na wala tusiabudu chochote isipo kuwa Mungu pekee(kutoka 20).

Mwisho Namalizia kwa kusema shetani ananguvu sana hapa Duniani tuzidi kumuomba Mungu s
Ukweli ni kuwa Yesu sio langi yao nahicho ndicho kinachowapa shida uzao wa nyoka

Wamejitahidi kuuficha ukweli kwa miaka mingi lakini ni kama inashindikana

ukitaka kujua Yesu alikuaje basi jaribu kutafuta sura na langi za ndugu zake alipokimbia kuuwawa na mfalme herode na kuenda kujificha misri;

misri ile ya kale acha hii wanayokaa wavamizi misri ile ya kimeti,
 
Kwanza Mungu hakatazi wala hajakataza mtu kuchonga sanamu ila alikataza na anakataza kuzifanyia ibada izo sanamu za kuchonga sababu wa kuabudiwa ni yeye Mungu pekee.

Kitu cha msingi ni kusikiliza maneno ya Padre au shemasi anapowaalika watu kuja kuanza kuabudu.

Padre au shemasi husema, Huu ndio mti wa msalaba, ambao wokovu wa dunia
umetundikwa juu yake, njooni tuuabudu
.

Ukifuatilia kwa makini kiswahili sanifu utagundua kuwa, Padre hufanya mambo haya yafuatayo katika mwaliko huo:

1: Huonesha mti wa msalaba.
2: Huambia watu waumini kuwa juu ya mti huo,wokovu umetundikwa
Kisha huwaalika wakauabudu.

Kwa maelezo hayo hapo juu labda ningekuuliza hivi, huyo padre au shemasi huwaalika wakauabudu mti wa msalaba au wokovu ambao umetundikwa juu ya huo mti wa masalaba ?

Hivyo Kwa mwaliko huo,wakatoliki hualikwa kwenda kuuabudu WOKOVU ulio juu ya msalaba.WOKOVU NI NINI? WOKOVU ni jina lililoandikwa kwa kiswahili.Jina wokovu kibiblia na kwa lugha asili ya Biblia ni sawa na jina YESHUA kwa kiebrania au YOSHUA.

Kristo ndiyo WOKOVU wetu tunayepaswa kumwabudu kwani alipokuja aliamua kuanzia kazi yake ya kutuletea wokovu katika mto Yordan pale ambapo Yoshua kahitimishia kazi yake.Yoshua aliwavusha watu toka ng`ambo ya mto kuwaingiza katika nchi ya ahadi ambayo ni Kanaan ya duniani na Yesu anapokuja,kama mwokozi,anataka awatoe watu wake kutoka katika nchi ya ahadi ya kidunia,kuwapeleka katika nchi ya ahadi ya mbinguni.Kumbe Yesu ni mwokozi wetu anayetutoa kutoka katika dunia kwenda mbinguni wakati Yoshua anaitwa mwokozi kwa kuwa aliwatoa Misri akawaleta Kanaan nchi ya ahadi.

Yesu na Yoshua kwa mantiki hii ni hilo jina WOKOVU kama nomino wakati kazi waliyotenda ni ya kutuokoa na kikitamkwa kama kitendo,Yesu au Yoshua, anaitwa Mwokozi.

kueleza kile wanachokiabudu wakatoriki ile Ijumaa Kuu. Padre au Shemasi husema Huu ndiyo MTI wa msalaba ambao WOKOVU wa dunia Umetundikwa juu yake, njooni tuUabudu.

Katika sarufi ya kiswahili hasa tunaposema juu ya upatanisho wa kisarufi, bahati mbaya ni kwamba nomino MTI na nomino WOKOVU zote zimechukua viambishi ngeli U, ili kuwa na upatanisho wa kisarufi. Tunasema kwa mfano, mti umaanguka, wokovu umetujia. Katika sentensi hiyo anayotamka padre au shemasi, ina maneno yote mawili, yaani mti na wokovu yenye kiambishi kimoja tu U kinachotuletea shida kuwa kimerejea nini, wokovu au mti. Kiambishi U, hakirejerei mti bali kinarejea wokovu yaani Yesu.

Kwa hiyo wanaposema njooni tuuabudu, hwamaanishi tuuabudu mti la hasha! Bali wauabudu Wokovu uliotundikwa juu ya mti wa msalaba katika akili zao. Ndiyo kusema, ibada hii kama mtu hawezi kutoka nje ya pale na kupeleka mawazo yake kwa Yesu, aliye Wokovu wetu , bila shaka anaweza kuwa anaabudu sanamu au mti wa msalaba.

Tafuta ujue kitu kinaitwa Sanduku la Agano/the covenant box. Halafu ujiridhishe sanamu ni nini na kuabudu sana kunakuwaje? Hivyo tu.

Fanya vivyo hivyo kwa kitu inaitwa nyoka wa shaba aliye nyanyuliwa na Musa kule jangwani wana wa Israeli wakapona walio mtazama huyo nyoka wa shaba.
 
Kwanza Mungu hakatazi wala hajakataza mtu kuchonga sanamu ila alikataza na anakataza kuzifanyia ibada izo sanamu za kuchonga sababu wa kuabudiwa ni yeye Mungu pekee.

Kitu cha msingi ni kusikiliza maneno ya Padre au shemasi anapowaalika watu kuja kuanza kuabudu.

Padre au shemasi husema, Huu ndio mti wa msalaba, ambao wokovu wa dunia
umetundikwa juu yake, njooni tuuabudu
.

Ukifuatilia kwa makini kiswahili sanifu utagundua kuwa, Padre hufanya mambo haya yafuatayo katika mwaliko huo:

1: Huonesha mti wa msalaba.
2: Huambia watu waumini kuwa juu ya mti huo,wokovu umetundikwa
Kisha huwaalika wakauabudu.

Kwa maelezo hayo hapo juu labda ningekuuliza hivi, huyo padre au shemasi huwaalika wakauabudu mti wa msalaba au wokovu ambao umetundikwa juu ya huo mti wa masalaba ?

Hivyo Kwa mwaliko huo,wakatoliki hualikwa kwenda kuuabudu WOKOVU ulio juu ya msalaba.WOKOVU NI NINI? WOKOVU ni jina lililoandikwa kwa kiswahili.Jina wokovu kibiblia na kwa lugha asili ya Biblia ni sawa na jina YESHUA kwa kiebrania au YOSHUA.

Kristo ndiyo WOKOVU wetu tunayepaswa kumwabudu kwani alipokuja aliamua kuanzia kazi yake ya kutuletea wokovu katika mto Yordan pale ambapo Yoshua kahitimishia kazi yake.Yoshua aliwavusha watu toka ng`ambo ya mto kuwaingiza katika nchi ya ahadi ambayo ni Kanaan ya duniani na Yesu anapokuja,kama mwokozi,anataka awatoe watu wake kutoka katika nchi ya ahadi ya kidunia,kuwapeleka katika nchi ya ahadi ya mbinguni.Kumbe Yesu ni mwokozi wetu anayetutoa kutoka katika dunia kwenda mbinguni wakati Yoshua anaitwa mwokozi kwa kuwa aliwatoa Misri akawaleta Kanaan nchi ya ahadi.

Yesu na Yoshua kwa mantiki hii ni hilo jina WOKOVU kama nomino wakati kazi waliyotenda ni ya kutuokoa na kikitamkwa kama kitendo,Yesu au Yoshua, anaitwa Mwokozi.

kueleza kile wanachokiabudu wakatoriki ile Ijumaa Kuu. Padre au Shemasi husema Huu ndiyo MTI wa msalaba ambao WOKOVU wa dunia Umetundikwa juu yake, njooni tuUabudu.

Katika sarufi ya kiswahili hasa tunaposema juu ya upatanisho wa kisarufi, bahati mbaya ni kwamba nomino MTI na nomino WOKOVU zote zimechukua viambishi ngeli U, ili kuwa na upatanisho wa kisarufi. Tunasema kwa mfano, mti umaanguka, wokovu umetujia. Katika sentensi hiyo anayotamka padre au shemasi, ina maneno yote mawili, yaani mti na wokovu yenye kiambishi kimoja tu U kinachotuletea shida kuwa kimerejea nini, wokovu au mti. Kiambishi U, hakirejerei mti bali kinarejea wokovu yaani Yesu.

Kwa hiyo wanaposema njooni tuuabudu, hwamaanishi tuuabudu mti la hasha! Bali wauabudu Wokovu uliotundikwa juu ya mti wa msalaba katika akili zao. Ndiyo kusema, ibada hii kama mtu hawezi kutoka nje ya pale na kupeleka mawazo yake kwa Yesu, aliye Wokovu wetu , bila shaka anaweza kuwa anaabudu sanamu au mti wa msalaba.
Hayo uliyosem
Ukweli ni kuwa Yesu sio langi yao nahicho ndicho kinachowapa shida uzao wa nyoka

Wamejitahidi kuuficha ukweli kwa miaka mingi lakini ni kama inashindikana

ukitaka kujua Yesu alikuaje basi jaribu kutafuta sura na langi za ndugu zake alipokimbia kuuwawa na mfalme herode na kuenda kujificha misri;

misri ile ya kale acha hii wanayokaa wavamizi misri ile ya kimeti,
Hayo anayosema padri yanapatikana kwenye andiko gani katika bibilia?
 
Kwanza, wakuu wa makuhani na kikosi Chao walihitaji yuda iskarioti ili kumtambua Yesu. Hakuwa maarufu kwa sura hasa maeneo ya Yerusalemu. Alifahamika zaidi maeneo ya galilaya.

Pili hizo sura ziliweza kupatikana kwasababu Walikuwa kwenye sarafu za wakati huo na baadhi zilipatikana kwenye archeology.

Tatu, kuabudu sanamu (au tuseme kuwa na sanamu) ni hasa katoliki (ambayo mimi sijawahi kuhesabu kama ni kanisa). Hao Wana dini yao ila wameificha kwenye jina la kanisa. Wanaabudu pia kitu kinaitwa bikira maria.

Nne, unaonekana kuwa msabato. Huwa nawakubali kwa kusisitiza watu kujua kwamba maisha hayaishii duniani LAKINI ninamfahamu pia kwamba na nyie mnayo sanamu yenu mnaiita siku ya sabato. Kwamba usipoabudu siku hiyo basi umepotea.

Tano, mimi nikwambie kwamba ndani ya Yesu tunamwabudu Mungu katika Roho na kweli. Hatuabudu siku maalumu Bali kila siku. Kukutanika kama mwili wa Kristo ni kutegemeana na makubaliano japo makanisa mengi yamefuata utaratibu wa mitume kukutana siku ya kwanza ya juma.

Amani iwe pamoja nawe.
Mungu akubariki awe pamoja nawe
 
Tafuta ujue kitu kinaitwa Sanduku la Agano/the covenant box. Halafu ujuridhishe sanamu ni nini na kuabudu sana kunakuwaje? Hivyo tu.

Fanya vivyo hivyo kwa kitu inaitwa nyoka wa shaba aliye nyanyuliwa na Musa kule jangwani wana wa Israeli wakapona walio
Kwanza, wakuu wa makuhani na kikosi Chao walihitaji yuda iskarioti ili kumtambua Yesu. Hakuwa maarufu kwa sura hasa maeneo ya Yerusalemu. Alifahamika zaidi maeneo ya galilaya.

Pili hizo sura ziliweza kupatikana kwasababu Walikuwa kwenye za wakati huo na baadhi zilipatikana kwenye archeology.

Tatu, kuabudu sanamu (au tuseme kuwa na sanamu) ni hasa katoliki (ambayo mimi sijawahi kuhesabu kama ni kanisa). Hao Wana dini yao ila wameificha kwenye jina la kanisa. Wanaabudu pia kitu kinaitwa bikira maria.

Nne, unaonekana kuwa msabato. Huwa nawakubali kwa kusisitiza watu kujua kwamba maisha hayaishii duniani LAKINI ninamfahamu pia kwamba na nyie mnayo sanamu yenu mnaiita siku ya sabato. Kwamba usipoabudu siku hiyo basi umepotea.

Tano, mimi nikwambie kwamba ndani ya Yesu tunamwabudu Mungu katika Roho na kweli. Hatuabudu siku maalumu Bali kila siku. Kukutanika kama mwili wa Kristo ni kutegemeana na makubaliano japo makanisa mengi yamefuata utaratibu wa mitume kukutana siku ya kwanza ya juma.

Amani iwe pamoja nawe.
katoliki ambayo mimi sijawahi kuesabu kama kanisa 🙏 Mungu wa mbinguni akubariki kwa kuliona hili
 
Back
Top Bottom