Fahamu zaidi baadhi ya matukio yaliyojitokeza katika shooting ya filamu ya PASSION OF CHRIST ya mwaka 2004 (Najua wajua ila acha nikujuze zaidi!)

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,726
10,019
Filamu ya passion of christ ilitoka rasmi mwaka 2004 tarehe 25 mwezi wa 2 ikiwa imeongozwa na mwongoza filamu maarufu Mel Gibson ambaye pia aliwahi kuongoza utengenezaji wa filamu iliyofanya vizuri miaka ya 2000; filamu inayokwenda kwa jina la apocalypo.

Passion of christ ni filamu maarufu sana ambayo maudhui yake yaliegemea zaidi katika sehemu inayoelezea mateso na kifo cha Yesu Kristo. Inaelezwa kuwa Mwigizaji mkuu aliyeigiza kama Yesu Jim Caviezel wakati wa shoot movie hiyo matukio kadhaa na mengine ya kushangaza yalitokea na kwamba Matukio hayo mengine yalimuacha na maumivu mwili mwake. Alieleza Jim Caviezel.

Matukio hayo yalikuwa;

• Alipigwa radi kadhaa yeye na baadhi ya watu waliokuwa katika shughuli hiyo.
• Aliteguka bega katika sehemu aliyokuwa anashoot scene ya kubeba msalaba.
• Alitakiwa kuwa macho saa 8 usiku kwa siku kadhaa kila siku ili afanyiwe makeup ya vidonda na uvimbe.
• Kwa bahati mbaya wakati kwa kushoot scene ya kupigwa mijeredi baadhi ilitokea kumpata ukweli mwilini mwake.
• Alijikuta akiugua ghafla pneumonia kwa sababu alitakiwa kuwa bila nguo mwilini msalabani na sehemu baadhi zilitakiwa kufilmiwa asubuhi kipindi ambacho kilikuwa na baridi sana.
• Mmoja wa waigizaji aliokoka kipindi hicho cha utengenezaji wa filamu na kuomba kubatizwa na Padre mmoja aliyekuwepo eneo la tukio. Baada ya pale aliwabatiza pia watoto wake na mke wake.
• Mwanamama aitwaye Maia Morgenstern aliyeigiza kama Mama yake Yesu alikuwa mjamzito kipindi hicho.

Filamu hii imetengenezwa kwa lugha 3 ambazo ni English Language, Aramaic, Latin name Hebrew. Bajeti iliyotumiwa kutengeneza filamu hii ni dolla za kimarekani $30million na kuingiza faida kwenye boxoffice zaidi ya kiasi cha dolla za kimarekani $622.3 million. Muda wa filamu hii ni dakika 127.
 
Kuna sehemu walibugi dhahiri!
Walipokua wanaugeuza msalaba ili wakunje misumari waliyomgongomea Yesu, mwili wa Yesu haukufuata kanuni za fizikia (haukunepa katikati)
Otherwise ni filamu fikirishi sana. Bonge moja la product.
 
Kuna sehemu walibugi dhahiri!
Walipokua wanaugeuza msalaba ili wakunje misumari waliyomgongomea Yesu, mwili wa Yesu haukufuata kanuni za fizikia (haukunepa katikati)
Otherwise ni filamu fikirishi sana. Bonge moja la product.
walitumia Cgi ila ni hatari sana.
 
Thank you, na utuelezee kidogo reaction/response ya watazamaji baada ya kuitoa, moja wapo ni watu walipinga kabisa kuwa mateso yalikuwa “ exagrated” na kuifanya jamii ya kiyahudi ionekane katili sana hapa duniani.
Mateso kwenye filamu hii ni too much hata mimi ningeungana nao tu.
 
Una Akili ya kumtoa Akili mzungu. Shukuran kwa Awamu ya tano ya Dkt John Joseph Pombe Magufuli...
Kuna sehemu walibugi dhahiri!
Walipokua wanaugeuza msalaba ili wakunje misumari waliyomgongomea Yesu, mwili wa Yesu haukufuata kanuni za fizikia (haukunepa katikati)
Otherwise ni filamu fikirishi sana. Bonge moja la product.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom