Miaka 6 ya Hayati Magufuli mshahara uleule, miezi 3 ya Rais Samia Suluhu mshahara wangu umebadilika

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
250
Habari,

Ndani ya miaka 6 ya Magufuli niliambulia annual increment moja tu ya November 2017, ambacho ni kiasi kidogo sana.

Kwa ufupi mshahara haujaongezeka katika kipindi chote hicho.

Miezi 3 tu ya Rais Samia Suluhu salary slip yangu pale juu imebadilika.

Watu wa imani tunaamini kuwa mateso ni zao la uasi na Ibilisi bali Neema ni zao la haki na Mungu.

Hivyo basi huhitaji kuombewa ili upate kujua kati ya Rais Samia Suluhu na Rais Magufuli ni nani chaguo la Mungu na ni nani chaguo la shetani kwa watumishi wa umma.

Sizungumzii kwa wananchi, wafanyabiashara, wakulima au kundi jingine lolote, nazungumzia kwa watumishi wa umma.
Mshahara umebadilika lakini kumbuka bei ya mafuta ya petroli na diesel imeongezeka...maana yake ni kuwa bidhaa zinaenda kupanda bei
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
4,916
2,000
Mshahara umebadilika lakini kumbuka bei ya mafuta ya petroli na diesel imeongezeka...maana yake ni kuwa bidhaa zinaenda kupanda bei
Kwani JPM alipoingia na alipokufa vitu vyote bei ileile?
Mafuta ulimwenguni wote bei imepanda
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
16,603
2,000
Samia hajapandisha mshahara bwana ila ameanza kupandisha madaraja zoezi ambalo lilianza 2018 lakini kwa kusuasua
 

KingCobra95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,542
2,000
Mishahara upande au ushuke,it doesn't matter,cha msingi ni serikali ku+control inflation tu,,,,la sivo hio nyongeza haitakusaidia popote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom