Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 941
MBUNGE NDAISABA AFUNGUKA MAZITO: MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA ILIVYOIBADILISHA NGARA
"Niwaombe wananchi wa Mumilamila kwa Umoja wenu endeleeni kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, endeleeni kumuunga mkono Mbunge Ndaisaba George Ruhoro. Hakika mengi tumeyafanya. Maendeleo ni hatua, hatua moja huanzisha hatua nyingine" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kipenzi cha watanzania amefikisha miaka mitatu tangu aingie madarakani. Wananchi wa Jimbo la Ngara wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara, Ndaisaba George Ruhoro tumeazimia kumpa kura nyingi mwaka 2025, ametufanyia mambo makubwa sisi Wananchi wa Ngara" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Rais Samia ametoa Shilingi Bilioni 100 kwaajili ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Nyakahora mpaka Rusumo katika Jimbo la Ngara, mradi huu umeanza kujengwa na Mkandarasi yupo Site. Ni Mama yetu, kipenzi cha Watanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Rais Samia ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 11 katika kipindi cha miaka mitatu hapa Ngara kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme. Umeme uko unakuja, Mkandarasi yuko site, nguzo zinaendelea kusogea, anatakiwa alete nyaya afunge transformer awashe umeme. Mpaka kufikia mwaka 2025 umeme utakuwa umewaka hapa Mumilamila" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 8 kwaajili ya ujenzi wa miradi ya Maji mpaka mradi wa Maji wa Bugarama ni sehemu ya fedha alizotoa Rais. Mradi umejengwa, umekamilika na unatoa Maji" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Mama Samia nilimkimbilia, nikasema watu wa Bushubi, Bugarama, Kihinga na Mumilamila wanapoenda hospitali ya Wilaya wanateseka sana wengine wanafia njiani kwasababu ya umbali mrefu wa kusafiri zaidi ya Kilomita 70. Rais Samia amenipa Bilioni 2 katika ya Bilioni 3 alizoahidi kutoa na Hospitali ya Wilaya inaendelea kujengwa Mbuba" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Barabara ya kutoka Bugarama mpaka Kabanga Nickel (Km 7.9) imetengewa Shilingi Milioni 8.98. Barabara ya kutoka Lunyana - Kihinga - Nyarukubala - Nyarulama imetengewa Shilingi Milioni 27.28. Barabara ya Nyarulama Sokoni - Mukivumu - Mumilamila Centre imetengewa Shilingi Milioni 27.9 kwaajili ya matengenezo" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara