Mhitimu unayeamini waliopata sifuri Form 4 ndio kutimiza ndoto zao basi elewa kwamba ulipoteza muda shuleni

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,120
27,126
Watu kadhaa wamenitag kwenye Uzi wa matokeo ya Necta ili nijionee jinsi vijana wa shule za Kayumba walivyo pata zero na 4 kwa wingi.

Ni kama vile wanasema "Wewe si ndo unajifanya kuzipigia kampeni shule za Kayumba ona sasa walicho kipata?" Hapo hapo ni kama vile wanasema tena "Hawa vijana waliopata zero ndio kwisha habari yao!"

Kama wewe ni graduate halafu unawaza namna hii ndugu yangu basi unapaswa kuanza kuwa na mashaka na degree yako kwa sababu ulicho enda kusomea chuoni ni ujinga kabisa. Kwanini?

Elimu ni nini?

Moja kati ya motto maarufu kabisa kuhusu elimu ni ile inayo sema "Elimu ni ufunguo wa maisha".

Kazi ya ufunguo ni nini?

Kazi ya ufunguo ni kufungua sehemu zilizojifunga au zilizo fungwa.

Kwa viwango vya ufahamu vya kundi fulani katika jamii ya watanzania ni kwamba mtu alie pata zero form four ndio amepoteza dira ya mafanikio yake.

Dhana hii hapo juu ni sawa na sehemu iliyo jifunga ama iliyo fungwa.

Wewe kama msomi hupaswi kufikiri hivyo kama watu ambao sio wasomi kwa sababu wewe tayari una ufunguo wa maisha.

Wewe ulipaswa kuwa na mtazamo kwamba hata huyu kijana alie pata zero kidato cha nne bado anayo nafasi kubwa sana ya kutimiza ndoto zake pamoja na kuwa na zero yake (na huo ndio ukweli wenyewe).

Zipo njia nyingi sana za kumuua paka.

Katika jamii hii ya kitanzania ambayo maisha yame prove pasi na shaka yoyote kwamba tofauti kati ya msomi wa kitanzania mwenye degree na std 7 leaver au form four failure ni sifuri.

Yapo maeneo mengi sana ya kifursa yanayo muweka kijana alie feli form four katika nafasi ya kutimiza malengo yake kimaisha kwa Asilimia nyingi zaidi na kwa uhakika mkubwa zaidi kuliko graduates wengi tu.

Ukiwa kama msomi unapaswa kuwaza nje ya boksi.

Unapaswa kuwaza beyond others.

Hata katika mambo ya kawaida tu unapaswa kuwa na ufahamu wa juu kushinda mtu ambae hajaenda shule.

Unapaswa kuwa una hoji maswali katika mambo yote unayo ambiwa na watu na sio kuyapokea tu kama yalivyo.

Sio msomi mwenzako alie somea ujinga kama wewe anakwambia presha haina dawa na wewe una rudia sentensi hiyo hiyo kwa wenzako kama kasuku badala kumuuliza Kwanini?

Unakuwa huna tofauti na mtu ambae hajaenda shule.

Yes hata mtu ambae hajaenda shule anajua mji mkuu wa Tanzania ni Dodoma ila wewe kama msomi unapaswa kuhoji kwanini iwe Dodoma na sio Singida . Kwani Singida Kwani Singida kuna nini ambacho Dodoma hakipo hadi Dodoma ifanywe kuwa makao makuu ya nchi na sio Singida.

Ukisha pata majibu uje utuambie kwanini Dodoma ndio mji mkuu na Sio Arusha Dar au Mwanza.

Jifunze kuwaza kama Injinia ambae hakupoteza muda wake shuleni.

Wakati ninyi mnaona mto Injinia anaona daraja.

Nyinyi mnaona msitu, yeye Injinia anaona shule au zahanati.

Msomi ndio anapaswa kuwa hivyo. Wakati watu wengine wanamuona alie pata zero kama ndio amesha haribu dira ya maisha yake wewe unapaswa kumuona ndio kwanza amepiga hatua moja kubwa sana kuelekea kwenye mafanikio yake.

Hata kwenye Biblia imeandikwa hapo Mwanzo ulimwengu ulikuwa umetawaliwa na giza kuu lakini giza hilo halikumzuia Mungu kufanya kazi ya uumbaji.

Wakati viumbe wengine walipo tazama juu ya uso wa dunia waliona udongo, Mungu aliona mwanadamu ndio maana kupitia udongo huo huo alimuumba mwanadamu.

Wakati huko duniani watu wanaumiza kichwa ili waweze ku- technolize (sic) maisha ya Yesu kwa kuyatoa kwenye imani kuyaleta kwenye teknolojia wewe bado upo kwenye giza la kufikiri kwamba mtu alie pata zero ndio amefika mwisho wa kutimiza ndoto zake.

Maisha ya Yesu kwa mujibu wa Biblia ni kwamba alizaliwa na mwanamke bikira bila kuwa na baba alikufa kisha akafufuka etc.Wana sayansi wanapambana kutafuta teknolojia itakayo saidia kufanya wanawake mabikira wabebe ujauzito bila kukutana kimwili na wanaume plus teknolojia ya kufufua watu walio kufa etc.

Style up bwana msomi unazidiwa akili mpaka na wachonga vinyago na masanamu. Wakati nyinyi mnaona mwamba mkubwa yeye anaona sanamu. Wakati nyinyi mnaona gogo yeye anaona kinyago.

Yote tisa, kumi mnazidiwa akili mpaka na waganga wa kienyeji. Wakati nyinyi mnamuona mtu wenu amekufa yeye ana muona (kwenye akili yake) akiwa hai na kwamba amechukuliwa tu msukule. Atachukua dawa atamnywesha na ndugu yenu atafufuka.

However if I go down to your level of seeing things. Kuna idadi kubwa sana ya wanafunzi kutoka shule za kata ambao wamepata division one na hawa ni wale ambae shule ya Msingi walisoma Kayumba.

Vivyo hivyo kuna kundi kubwa tu la wanafunzi kwenye shule za Private ambao wana 3, 4 na zero.
 
Kufeli shule siyo kufeli Maisha.

Mafanikio ni dhana Pana zaidi. Yanategemea na mtu husika. Elimu yetu imetutengeneza kuamini kuwa Kupata marks Nzuri na ufaulu mzuri kuwa wewe/Mimi ni Bora zaidi ya wengine . Nafikiri Taasisi ya elimu na wadau wote tunapaswa kuiondoa Hii mentality .

Tukajikita zaidi kwenye ujuzi na ushirikiano Tukiweka mazingira madhubuti Kwa Kila mwanafunzi/binadamu kufikia His potential.
 
Kufeli shule siyo kufeli Maisha.

Mafanikio ni dhana Pana zaidi. Yanategemea na mtu husika. Elimu yetu imetutengeneza kuamini kuwa Kupata marks Nzuri na ufaulu mzuri kuwa wewe/Mimi ni Bora zaidi ya wengine . Nafikiri Taasisi ya elimu na wadau wote tunapaswa kuiondoa Hii mentality .

Tukajikita zaidi kwenye ujuzi na ushirikiano Tukiweka mazingira madhubuti Kwa Kila mwanafunzi/binadamu kufikia His potential.
100% correct
 
Kuna classmate alipata zero ikabidi arudie tena mtihani kama mtahininiwa wa kujitegemea, akalamba tena zero, ikabidi aingie mitaani kupiga mishe zingine. Baada ya miaka kadhaa jamaa kafanikiwa kuliko sisi rafiki zake tuliosonga mbele kielimu.

Kajenga nyumba ya maana na anamiliki chombo cha usafiri wa abiria na ana familia wakati wenzake hatuna mafanikio kama yake na familia zetu bado changa tulichelewa kuoa tulikuwa masomoni kwa muda mrefu. Kusoma tusome kwani hakuna mwanafunzi anayeenda shuleni kufeli.

Hizo marks tunazopata kwenye masomo baada ya kujibu maswali ya mtihani ni abrakadabra tu wala hakuna uhalisia wa kufanikiwa kimaisha hapo while straggling is ongoing
 
Kuna classmate alipata zero ikabidi arudie tena mtihani kama mtahininiwa wa kujitegemea, akalamba tena zero, ikabidi aingie mitaani kupiga mishe zingine. Baada ya miaka kadhaa jamaa kafanikiwa kuliko sisi rafiki zake tuliosonga mbele kielimu. Kajenga nyumba ya maana na anamiliki chombo cha usafiri wa abiria na ana familia wakati wenzake hatuna mafanikio kama yake na familia zetu bado changa tulichelewa kuoa tulikuwa masomoni kwa muda mrefu. Kusoma tusome kwani hakuna mwanafunzi anayeenda shuleni kufeli. Hizo marks tunazopata kwenye masomo baada ya kujibu maswali ya mtihani ni abrakadabra tu wala hakuna uhalisia wa kufanikiwa kimaisha hapo while straggling is ongoing

umeongea madini matupu mkuu big up sana.

And this is what am talking about
 
Back
Top Bottom