Tukio la Ubakaji shuleni: Wazazi muwe Makini na watoto mnaopeleka shule za Bweni

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
TUKIO LA UBAKAJI SHULENI: WAZAZI MUWE MAKINI NA WATOTO MNAOPELEKA SHULE ZA BWENI

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Mwaka 2016 nilipata kibarua cha kujiegesha katika shule ya binafsi maeneo ya Mwembe Mtengu, Kigamboni.
Ile shule nikakuta waalimu wengine vijana ambao ni rika langu. Hapakuwa na Mwalimu wa kike hata mmoja. Licha ya kuwa shule ilikuwa ni mchanganyiko wa wasichana na wavulana. Hiyo ilinishangaza lakini haikuwa inanihusu kivile. Unajua sisi Watibeli tunatatizo la kufuatilia vitu vidogovidogo. Kwa kweli hili ni tatizo kwetu. Sio kwamba tunaamua bali tunajikuta tupo hivyo.

Mimi ni wale Watu ambao tukikutana siku ya kwanza ninaweza kujua aliyesimama mbele yangu ni mtu mzuri au mtu mbaya. Aidha kwa kukuangalia machoni au moyo wangu kuwa na shaka na wewe. Moyo wangu ulikuwa na wasiwasi sana kila nikitazamana na Mmiliki wa shule ambaye alikuwa akija siku za Weekend. Basi bhana!

Katika kusoma mazingira nikagundua ile shule inamilikiwa na mtu binafsi ambaye ni Msabato, kumbuka hata mimi pia ni Msabato. Hiyo ilinifanya nijihisi Comfortable Kwa sababu si Msabato mwenzangu bhana!

Kuna wanafunzi wawili walikuwa wakinishangaza sana wakati nikiwa nafundisha. Mmoja alikuwa binti mdogo aitwaye Angel, huyu alikuwa kidato cha tatu. Tangu nifike shule hiyo sikuwahi kuona tabasamu lake. Alikuwa ni binti mpole lakini mara kwa mara mwenye huzuni nyingi. Siti ya Angel ilikuwa Katikati ya darasa katika Row ya katikati.

Kila nilipokuwa nikiingia kufundisha alikuwa mtu wa kulia, kuihamisha kichwa kwenye dawati. Sasa hali ile ilikuwa inanipa maswali mengi nikiwa naendelea kufundisha. Huwaga sina haraka katika kuyaendea mambo. Niliupa muda nafasi. Kuna wakati Angel alikuwa akitoka katikati ya kipindi na kusema anaumwa. Kwa jinsi alivyo ningempa tuu ruhusa.

Niliazimia kuwa ipo siku nitamuuliza anakabiliwa na jambo gani lakini sio kwa haraka vile. Nilikuwa na sababu zangu. Mosi, bado nilikuwa mgeni, sikuwa naelewa mambo mengi ya eneo la kazi, pili, yule ni binti na mimi ni kijana. Hivyo kuyaendea matatizo kwa binti kiharakaharaka niliamini ingeweza kujifanya niingie kwenye matatizo ambayo sikuyajua. Hivyo ndivyo niliamini.

Siku moja tukiwa Ofisini na Waalimu wenzangu niliwàambia kuwa Angel atakuwa na tatizo kubwa linalomkabili nje ya vile Watu tunavyoliona. Tatizo hilo halihusu magonjwa ya kawaida kama inavyoripotiwa. Kuna kitu Angel kinamkabili lakini anajaribu kukificha.

Wengi niliowakuta walinibishia na kuniona mbishi kama ilivyohumu JF. Nikawaambia ninyi hamuhisi yale ninayoyahisi. Hamfikiri vile ninavyofikiri na sio kama hamuwezi kufanya hivyo bali ni kwamba hamtaki ukweli. Niliwaambia Angel atakuwa aidha anatatizo la kifamilia au tatizo la ukatili wa kijinsia unaoendelea au anaofanyiwa na mtu ambaye hana uwezo naye. Wakanikatalia, na mimi sikuwa na ushahidi zaidi ya maneno matupu niliyokuwa nayaamini.

Hivi kama ni kuumwa ni kuumwa gani huko kwa muda mrefu alafu vitu anavyoumwa havifahamiki. Unajua sisi wengine tunaonekana wajuaji lakini ni kwa vile tunadadisi na kusoma mambo mengi Sana. Hivyo tukijieleza inaonekana ni wabishi na wajuaji. Lakini yakija kutokea wanakuita sijui kionambali, sijui akili, sijui nini wakati ni mambo yapo wazi.

Baada ya miezi miwili kupita nikiwa tayari nishazoea na kujua kwa kiasi fulani kipi ni kipi, yupi ni yupi, wanafunzi gani ni wakora, wanafunzi gani wanatabia za umalaya, wanafunzi gani ni informers wa mwenye shule. Majirani wa ile shule wanatabia zipi na nani wanaukaribu na ile shule. Na mambo kama hayo. Kuna kitu nikagundua ambacho hakikuwa cha kawaida.

Siku moja Mkurugenzi wa shule(Mmiliki) huku mkewe akiwa Mhasibu wa shule waliitisha kikao. Wakatuambia kuwa kuna mambo kwenye ile shule yanaendelea yasiyo ya kawaida. Habari hiyo ilitufanya tuwe na utulivu tukisubiri kwa hamu kujua nini kinaendelea.

Akaendelea, Ati eneo lile la shule limevamiwa na Majini na mapepo Wachafu. Na yamekuwa yakirandaranda hasa majira ya Usiku. Mmmh! Majini hayo yanasumbua wanafunzi Usiku hasa Mabinti na wanakuwa wakipiga Kelele usiku wakiwa wamelala.

Habari hizo licha ya kuwa zinatisha lakini mimi zilinivutia kwa sababu tangu nikiwa mtoto nilikuwa nasikia habari za majini, sijui uchawi lakini sikuwahi kushuhudia. Niliona kuwa wakati umefika na mimi nishuhudie zile hadithi za kale. Kwa kweli nikiri nilivutiwa sana na habari Ile.

Siku ya siku ya Wachungaji kuletwa ikafika. Hapa ndio nikaona kuna tatizo Mahali. Nilidhani wangeletwa wachungaji wa kisabato lakini haikuwa hivyo, waliletwa Manabii wa upako ambao kanisa lao tulikuwa tukilipita tukienda pale Mwembemtengu Center.

Unajua Wasabato haiwezekaniki kuombewa na hawa mitume wa kisasa. Yaani Msabato OG aombewe na Mtume sijui aposto yaani hilo haliwezekaniki. Yaani hapo kuna walakini sehemu. Hivyo ndivyo niliamini na mara nyingi kile ninachoamini huwaga ni kweli kwa sababu mara nyingi Siendeshwi na mihemko.

Tukaitwa, tukatambulishwa kwa wale mitume(walikuwa wawili), kisha baada ya neno maombi yakafuata. Tukasimama pale ofisini kwa Duara huku tukiwa tumeshikana mikono huku na huku. mtume mmoja ndiye alikuwa katikati ya duara akiwa anaomba. Mmiliki wa shule na mkewe walikuwa miongoni mwa waliokuwa duarani.

Sasa mimi kikawaida sifumbagi macho. Huwaga mtu akisema tuombe ninafumba macho kwa sekunde kadhaa kwani muombaji atahakikisha Watu wote wamefumba macho ndipo aanze kuimba. Basi nikafumba macho nikiwa nimeinamisha uso wangu chini huku nikiwa nimeshika mkono wa mwalimu wa upande wa kushoto(wakemia na physics) na Mwalimu upande wa kulia(Biolojia na Jiografia).

Baada ya dakika moja kupita Mtume akiendelea kuomba nikafumbua macho nikiwa bado nimeinamisha kichwa changu. Hivyo mtu wa mbele yangu asingeweza kuona kama macho yangu yapo wazi. Nikainua macho polepole nikiwa nachungulia wenzangu waliopo duarani, wote walikuwa wamefumba macho. Hapo nikasongesha macho kwa Mtume, naye alikuwa amefumba macho huku akiwa anaomba kwa kufoka na kukemea kama ilivyo ada yao.

Nikahisi kuna mtu ananitazama, kugeuka nikagongana macho na Mke wa mmiliki wa shule(ndiye Mhasibu wetu). Macho yake yalinimaindi lakini sikujali. Tunatazamana kwa kitambo kisha nikayaondoa macho yangu na kurudisha kichwa changu chini nikawa naangalia chini ya viatu vyangu.

Yule mtume akaanza kugusa vichwa vya Wafanyakazi na waalimu huku akiimba, mmoja baada ya mwingine, mpaka aliponikaribia, hapo nikawa najishauri aniguse kichwa au asiguse. Akili moja yaniambia acha akuguse, nyingine ikasema asikuguse. Basi ikawa mgogoro wa kinafsia. Nikaamua asiniguse ingawaje nilikuwa na woga wa kufanya tendo hilo. Huko ni kutokujiamini. Sasa hofu ya nini wakati mwili ni wako.

Akili moja ikaniambia kamwe usiwekewe mkono kichwani na mtu usiyemjua. Nikaiona unahoja hivyo nikashikamana nayo.

Akaniuliza akiwa bado kafumba macho. Kila akiniletea mkono nikawa nakwepesha kichwa au narudi nyuma jambo ambalo lilimfanya afumbue macho yake na kunitazama. Nikampa ishara ya kidole na kichwa kumkatalia. Akamfuata wa pembeni yangu. Hapo nikaangalia huku na huku kumbe Mke wa mmiliki wa shule alikuwa akishuhudia tukio lile, nikageuka kumtazama mmiliki wa shule yeye akakwepesha macho yake kwa kuangalia chini na kuyafumba. Nilihisi hivyo ingawaje tulipishana kama sekunde hivi.

Baada ya maombi tulitawanyika, lakini Mmiliki wa shule, na mkewe na lile jopo la mitume na watumishi wa kanisa wakaniita. Tukacheka tukawa tunapiga vistori vya hapa na pale lakini nilijua walikuwa wameniitia nini. Hatimaye Mke wa Mmiliki wa shule akaniuliza kwa nini nilikataa kuwekewa Mikono. Na hapo hiyo ndio ikageuka Mada, nilitoa jibu fupi tuu kuwa, Siwekewi Mikono na Watu nisiowajua na ambao nimewaona leo tuu.

Tukabishana hapo, kama mjuavyo Taikon kwa Hoja ambazo wengi huita ubishi hajambo. Nikawauliza kwani wao imani yao ni ndogo kiasi kwamba hawawezi kuimba bila kushika Watu vichwa. Wakawa wanajibu blahblahblah! Basi walimaindi lakini hawakuwa nalakunifanya.

Baada ya Wiki Mbili kupita tukio la kusikitisha likatokea.

Ilikuwa jumamosi siku ya ibada katika kanisa la shule. Mimi kikawaida nilikuwa nimekaa siri ya pili kutoka mwisho hivyo kila anayeingia na kutoka na matukio mengine yaliyokuwa yanaendelea mule Kanisani nilikuwa nayaona. Mmiliki wa shule akamaliza kuhutubia akatoka nje kabisa ya kanisa.

Kisha baada ya dakika kadhaa Akatoka Angel, kisha wakafuatia Wadada wawili (wanafunzi wakike wakubwa tunalingana umri). Nikasahau habari zao. Mara tukasikia sauti ya mtu anayelia kwa uchungu na kwikwi!. Kanisa zima likageuka huku na huku kuifuata hiyo sauti lakini kukawa kimya. Mke wa Mmiliki wa shule akatoka. Hazikuisha dakika tano wale wanafunzi wawili wakike waliotoka wakarudi. Kisha zikapita dakika tano Mmiliki wa shule naye akarudi. Alafu dakika tano akarudi mke wa mmiliki.

Lakini Angel hakurudi mpaka tunamaliza ibada.

Wanafunzi wameenda kula, nasi tulikuwa tunakula. Siku ya jumamosi kwa vile mmiliki wa shule alikuwepo basi tulikuwa tunakula vizuri sana. Tulikuwa tunakula kwa Pamoja yaani Waalimu, wafanyakazi na mmiliki.
Punde ile mada ya ile sauti tuliyoisikia ikazuka. Mke wa mmiliki wa shule akasema ati yale ni majini na mapepo ndio kulikuwa yakilia. Mmh! Ingawaje mazingira ya Mwembemtengu ni ya giza kutokana na kijani kibichi. Hivyo yanautisho fulani.

Punde Angel anasimama mbele yetu akiwa analia. Kumbuka tumemzoea Angel akiwa katika hali hiyo.
Sasa Mke wa mmiliki wa shule alikuwa akimfukuza, anamnyooshea fimbo. Mimi nikamuuliza Angel unashida gani? Mmiliki wa shule akadai, achana naye mimi namjua Angel. MKE wa mmiliki wa shule naye akadakia huyu mtoto ni mwongo sana anapenda kuigiza.

Unajua sisi wengine tunapenda kusikiliza na kutomzuia mwingine asijieleze kama sisi tusivyotaka kuzuiwa.
Nikasema, tusimzuie asiseme, nikamuuliza angel unatatizo gani? Angel akataka kusema lakini akaacha, kisha mke wa mmiliki akasimama akiwa kamshikia fimbo na kumfukuza.

Basi Watu waliokuwa pale wakaanza kumponda na kuponda wanafunzi. Kama mjuavyo Taikon mara nyingi ninakuwaga tofauti kidogo jambo ambalo wengi huliita ubishi. Nikawaambia, mngemuacha aeleze kilichomleta kusingekuwa na tatizo. Nikapondwà, nikataniwa ati au ninampenda Angel. Tobaa! Tukamaliza Kula na tukasahau mambo yote yaliyokwisha kutokea.

Kila mmoja akaenda anapopajua huku wanafunzi wakiwa mabwenini wengine darasani wengine kwenye miti yenye vivuli basi ilimradi hakuamini sheria inayovunjwa.

Punde nikawaona walewale wanafunzi wawili wakike wakiwa na harakati fulani pamoja na Angel, sikuwazingatia, mara nikawaona wakitoka nje ya Geti la shule wakiwa na Waalimu wawili, ni yule mwalimu wa kushoto kwangu na wakilia kwangu waliowekewa mikono. Sikuwazingatia sana. Imefika saa kumi na moja nashangaa Geti la shule linafunguliwa, gari la mmiliki wa shule linaingia kwa kasi.

Kisha linasimama alafu anashuka Mmiliki wa shule wakiwa haihai. Ananiona kwa mbali, ananisemesha kwa ukali kuhusu jambo fulani. Ninakuwa mkaidi kutokana na alivyoni-approach. Hasira zake zinaongezeka anamuagiza mwanafunzi fulani agonge kengele. Jambo hilo linafanyika.

Mimi nilikuwa nishawakaribia nikauliza kuna tatizo gani? Mnataka kukiharibia shule, hamtaweza. Nikatekewa nisijue nini maana yake. Mnabaka watoto wa Watu alafu mnataka kunisingizia. Akasema. Punde getini wanaingia mwanaume na Mwanamke ambaye ni Majirani wa ile shule ambao ni wanufaika wa ile shule kama kupata mbogamboga n.k. Walikuwa wangapi? Mmiliki wa shule anauliza.

Walikuwa waalimu wawili na wanafunzi watatu wamewatorosha wanafunzi. Hapo nikakumbuka Tukio la Wale wanafunzi wakike wawili na angel wakitoka getini na baadaye kufuatiwa na Waalimu wawili.

Wametoroshwa huku wamebaka! Mmmh!
Taarifa za Kubakwa kwa angel zikanifikia.
Kumbe Angel kabakwa. Sasa kabakwa na Nani?

Tukakaa kikao cha dharura, headmaster akaanza kusimulia hapo tupo mimi, headmaster, Mwalimu mmoja, Mmiliki wa shule, mke wa mmiliki, mtoto mkubwa wakiume wa mmiliki ambaye anafundisha shule ya binafsi ya St. Mathew, wale Majirani wawili, na mtume. Headmaster akasema, wakati tumemaliza kula akiwa anarudi nyumbani kwake kupumzika (nyumba ipo eneo hilohilo la shule) akasikia sauti ya wanafunzi wakimuita, walikuwa wale mabinti wawili waliotoka Kanisani muda ule. Alitaka kuwapuuza lakini walikazana kumuita. Akasimama, wakamwambia Angel kabakwa! Akahamaki, angel Kabakwa?

Ndio, na nani? Twende ukamuulize mwenyewe. Wakaenda. Akamkuta Angel analia sana.
Headmaster nimebakwa! Angel akasema,
"Unahakika Angel"
"Mwalimu nimebakwa" huku akilia.
"Nani kakubaka?"
Angel akawa analia,
"Mkurugenzi kanibaka"
"Angel! Unahakika?" Headmaster anashkwa na butwaa!

Kumbe Mkurugenzi alipotoka kuhutubia Kanisani, wakati anatoka alimuita Angel, ndio muda uleule wakafuatana kwa tofauti ya dakika kadhaa. Angel alipofika Ofisini (ofisi ya mkurugenzi) akamkuta Mkurugenzi amekaa kwenye kiti. Mkurugenzi akamwambia angel akae kwenye kiti. Alipokwisha Kukaa Mkurugenzi akaamka na kwenda kumpapasa na kumtomasa tomasa mtoto wa watu.

Angel alikuwa anakataa lakini Mkurugenzi alitumia mabavu huku akimtishia na hapohapo kumuahidi Pesa.
Akambaka! Akamharibu! Akamuumiza! Akamliza mtoto wa watu!

Ndipo Angel akatoka akiwa analia, akawa anataka kuja Kanisani kuja kushtaki mbele za Watu kuwa amebakwa, Wakati huo Wale mabinti wawili nao ndio wametoka Kanisani wakiwa wanaenda chooni, wanakutana na Angel akiwa analia, Angel anawapa taarifa kuwa amebakwa. Wanafunzi hao ni Khadija na Victoria.

Wakawa wanashauriana waingie wamuumbue Mkurugenzi ili wapate haki ya Angel. Ndipo ile sauti ya kilio inasikika, kisha Mke wa mmiliki wa shule anatoka. Anakutana na hiyo kesi hapo nje. Mke wa Mkurugenzi anawafukuza Khadija na Victoria na kuwaambia warudi ndani Kanisani. Kisha anabaki na Angel anamtishia na kuona kama anajifanyisha, akamfukuza Angel aende Bwenini.

Kisha Mke wa mmiliki wa shule anarejea Kanisani.

Headmaster anaendelea kusimulia kuwa hata muda ule wakati tunakula angel alikuja ili atoboe Siri hiyo lakini Mke wa mmiliki na mkurugenzi walikuwa walimtishia kwa ishara ya mkono na macho bila ya sisi wengine kujua.

Basi Khadija na Victoria wakiwa Wadada wakubwa wa shule hiyo kiumri na kimuonekano, wakalishikia jambo hilo kidete. Ndipo mwalimu wa Physical na Yule wa biolojia wakakuta hiyo habari ndio wakashinikiza kesi hiyo ipelekwe Polisi.

Wakati huo simu yangu ikaingia meseji kutoka kwa wale waalimu kuwa wapo Mwembemtengu wamekwama muda wakisubiri usafiri. Nikatoka kwenye kile kikao nikawapigia simu. Nikawaambia wasiwapeleke wao polisi kwani wao ni wanaume, wawape nauli Khadija na Victoria wampeleke angel polisi kwa sababu wao ni wakubwa na wanauwezo wa kujitetea alafu sisi tutafuata. Ili isijeikaonekana waliwatorosha hao watoto kisha wanataka kumpa kesi Mkurugenzi. Wakafanya hivyo.

Nikaingia ndani, sasa Mtoto wa mmiliki wa shule akamuuliza Babaake kuhusu ukweli wa taarifa hiyo. Mzee akakataa, akasema hao waalimu wanataka kuiharibu shule yake na wametumwa na adui zake, akasema atadili nao na ukweli utabainika.

Kwa jinsi alivyokuwa akiongea ungemuamini au ungeshindwa kujua nani mkweli baina ya Angel na Mkurugenzi.

Wakaondoka, kumbe Mkurugenzi alikuwa ametuma wale Majirani waende polisi kuripoti kuwa mtoto wao ametoroshwa shuleni na waalimu. Kwani wale Majirani binti yao mmoja aitwaye Vicky alikuwa miongoni mwa walipompeleka Angel Polisi.

Walipofika kule Wakasema kuwa Yao ametoroshwa lakini polisi wakasema kuna wanafunzi wanatoka shule hiyohiyo wapo hapo kituoni. Walipoitwa wale Majirani wakamuona Vicky binti yao. Wale Majirani wakakomaa kuwa Walitoroshwa na wanahisi wale waalimu wamewafanyia hao wasichana kitu kibaya. Khadija na Victoria wakapinga lakini Polisi wakaona isiwe kesi wakatuma pira likaja shuleni likakamata wale Waalimu.
Wakati huo kumbe pira jingine limeenda Kongowe kumkamata Mkurugenzi. Kwani mkurugenzi anaishi Kongowe.

Nasi tukaenda, polisi wakawa wapo katikati wasielewe wamsikilize nani. Tukawaambia wamsikilize Mbakwaji. Muda huo Mbakwaji baba yake ambaye ni mjeshi alikuwa yupo Njiani. Alipofika jamaa alikuwa na khasira sana. Mbaya zaidi Mkurugenzi alikuwa ni rafiki yake na wanatoka sehemu moja Watu wa kabila moja. Saa mbili usiku mkurugenzi analetwa msobemsobe, hajakaa vizuri Baba Angel anamdaka na kumuachia kipigo heavy. Huku akiwa amemshkia bastola akimtishia kumuua.

Lilikuwa tukio lenye kusisimua. Akawekwa ndani. Wale waalimu nao wakashikiliwa kwa muda lakini Baba Angel akaamuru polisi wawaachie tuu kwa sababu anaona hawana kosa isipokuwa hila za Mkurugenzi.

Tukarudi! Baada ya siku mbili hivi tukashangaa Mkurugenzi na polisi wakija pale shuleni kisha wakaondoka. Baada ya Wiki Mkurugenzi akaachiwa. Akaja Assemble Akasema amesingiziwa. Na kama alivyosema kuna majini na mapepo yanataka ile shule isiendelee. Na kwa uwezo wa Yesu wameshinda lile jaribu.

Aliongea kwa kujiamini sana kiasi kwamba wengi walimuamini na sisi wengine wachache tukiachwa Njia panda. Ujumbe pekee alioutoa kwa Wale walimu wawili alisema; Ninyi ni vijana wadogo bado mnasafari ndefu katika maisha, jiepusheni na mambo yasiyowahusu mtakuja kujiingiza kwenye matatizo.
Maneno hayo nayakumbuka.

Basi, nikaona isiwe kesi nikaona niondoke Pale. Baadae kama miezi sita hivi. Nikaja kupata habari kutoka chanzo cha uhakika kuwa yule mkurugenzi alikuja kufungwa. Kumbe walikubaliana na Mjeshi kuwa alipe kiasi fulani cha pesa kama milioni ishirini hivi. Ili kesi ifutwe vinginevyo afungwe miaka thelathini. Mkurugenzi akaona isiwe kesi, akampa Mjeshi gari ambayo thamani yake ni milioni tano hivi kama Advance, kisha akampa na hati ya Shule kama rehani. Alafu polisi akaacha kipesa Fulani. Ndio kipindi kilé tunamuona ametoka kumbe ilikuwa ni dili la makubaliano.

Baadaye alikuja kumgeuka vibaya yule Mjeshi akakataa kumlipa zile pesa Milioni 20 na akaenda kumshitaki kwa kesi ya Rushwa na hapo ndipo alipojikanyaga. Chanzo kinasema Mke na watoto wa mkurugenzi hawakuona ni kivipi wangeweza kulipa hiyo milioni 20 kwa muda waliokubaliana na kama wasilolipa hiyo ingrmaanisha shule ingeenda kwa Mjeshi nao wasingebakiwa na kitu.

Hivyo mke na watoto wakaamua wamtoe mzee kafara kwa ujinga wake. Ingawaje Utetezi wa mzee ni kuwa tukio lile alilifanya kwa sababu ya mambo ya kishirikina. Taarifa hiyo pia tuliipata kwa mkuu wa kituo cha polisi ambaye alisema huyo mzee ndio kawaidà yake kwani 2009 pia alifanya tukio linalofanana na hilo na akachomoa. Sema raundi huu kumfanyia mtoto wa mjeshi inaweza isiwe salama kwake.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Acha nipumzike niende kwenye maandamano!

Robert Heriel
Taikon WA Fasihi
Kwa sasa Dar es
 
Leo ndio nimemaliza kusoma stori yako mkuu,Ila mkurugenzi Gani wa shule anashindwa kopeshwa 20mil amalize janga?Zuzu Sana Huyo CEo
 
Mkurugenzi kama genzi yaani

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom