Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,108
Mheshimiwa Mbowe nimefualtilia kwa makini mkutano wako siku ya leo huko Mutukula mkoani Kagera ambapo chama kina operesheni ya +255 Katiba mpya + Okoa bandari zetu. Lakini nimeshangazwa na hotuba yako nzima hukugusia kabisa suala la bandari wala katiba mpya nikashangazwa sana.
Iweje Mwenyekiti usahau theme ya operation ukaishia kuzungumza mambo yaleyale ya kawaida ya kukiintroduce chama lakini Ukaacha theme mama ya operation nzima?
Ndugu Mweneyekiti kwani bandari si ni mali ya wanamutukula pia?, kwa nini uache kutoa elimu na kuwahabarisha yanayojiri kuhusiana na jambo hilo?
Ndugu Mwenyekiti Katiba mpya si ni kwa manufaa ya Wanamutukula pia, kwa nini hotuba yako isizungumzie jambo hilo na kuwapa elimu wananchi juu ya umuhimu wa katiba mpya?
Ndugu Mwenyekiti ninahofia kuwa leo huko Mutukula umepoteza opportunity kubwa ya kisiasa, na kushindwa kuiangamiza CCM kwa wewe kushindwa kuzieleza hizo ajenda mbili muhimu sana katika siasa za nchi yetu.
Kumbuka CCM wako busy kuzunguuka nchi nzima kuuza ajenda yao ya bandari kwa wananchi. Nilitegemea wewe Mwenyekiti ungesaidia kuwafungua macho wananchi juu ya ajenda hiyo ili wasipotoshwe na CCM ila kwa bahati mbaya sana umepoteza opportunity nzuri sana kwa kuziweka pembeni hizo ajenda.
Ndugu Mwenyekiti ninahofia kuwa kama Utaamua kuziacha hizi ajenda katika mikutano yako basi lengo la chama kumobilize nguvu ya umma kunusuru Taifa letu dhidi ya mkataba huu mbaya itapata vikwazo na pia utakuwa umeisaidia CCM kukwepa kitanzi kizito cha kisiasa.
Ndugu Mwenyekiti, Hili jambo la kudadavua mkataba usimwachie Makamu Mwenyekiti tu katika mikutano yake, Na wewe lishikie bango katika mikutano yako. Kufanya hivyo utakuwa umetekeleza azimio la kamati kuu la majuzi.
Wananchi tunataka kusikia, Katiba mpya, Bandari, Na ugumu wa maisha mna solutions gani
Nawasilisha!