Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,504
- 51,099
Katika nchi yetu tatizo la msingi siyo sheria za uchaguzi, Tatizo la msingi ni katiba mbovu inayozaa mfumo mbovu wa uongozi na utawala, mfumo mbovu wa haki na mfumo mbovu wa uwajibikaji.
Nashangaa chama kikuu cha upinzani ambacho kinajua wazi kuwa mzizi wa fitina ni katiba mbovu, hakina interest ya kuifanya katiba mpya kuwa ndiyo KILIO KIKUU cha kuwaingiza watu barabarani, lakini chenyewe kinaweka mbele mambo ya uchaguzi as if uchaguzi ndiyo tatizo kuu.
Hii inatoa taswira gani?, inatoa Taswira kuwa viongozi wa CHADEMA wao kinachowakera zaidi hadi kupata ujasiri wa kutaka kuwaingiza watu mabarabarani ni sheria zinazowakwaza kuingia bungeni au kupata udiwani. Otherwise kama kweli wana uchungu na wananchi kwa ujumla wake kwa nini Maandamano wanayoitisha yasiwe na AJENDA KUU YA MSINGI AMBAYO NI KUDAI KATIBA MPYA?
Uchaguzi wa mwaka 2020 ulipofanyika, Magufuli akawapiga akina Mbowe na kitu kizito kichwani waliwaambia wananchi kuwa kamwe hawawezi kushiriki tena uchaguzi chini ya katiba ya sasa na tume hii ya uchaguzi. Sasa Magufuli hayupo, wanahisi wana chance ya kuingia mjengoni tena kwa hiyo wako tayari kusettle na "minimum" reforms za kuwawezesha kuingia tena mjengoni kula kodi za wananchi!.
Mimi nasema kama CHADEMA wanataka kuandamana kama chama ili watngenezewe sheria watakazozipenda za kuwawezesha kupata hivyo viti vya ubunge na ruzuku iongezeke, basi ni kheri kwao wacha waandamane, LAKINI sisi wananchi tatizo letu KUU na la MSINGI ni KATIBA MPYA!
BILA KUIFANYA KATIBA MPYA KUWA NDIYO AJENDA MAMA ya maandamano basi haya maandamano ni JOKE yaani ni KICHEKESHO na ni muendelezo uleule tu wa wanasiasa kutaka kututumia wananchi kama ngazi ili kufikia malengo yao ya kisiasa ambayo kimsingi siasa ni ajira yao!.
Haitoshi kuchomekea vijmaneno vya hapa na pale kuhusu katiba mpya ili kulainisha mioyo ya watu, tunataka ajenda KUU iwe ni KATIBA MPYA.
Nje ya hapo, Mbowe na Wanachadema wenzako kama mnadhani uchaguzi ndiyo tatizo kuu nchini basi kaandamaneni. lakini nawajulisha tu kuwa Ajenda yenu imekaa kivyama, haijakaa kitaifa na kwa hiyo hata wanaCCM ambao wangewaunga mkono kuandamana kama ajenda yenu kuu ingekuwa ni KATIBA mpya hawataandamana kwa sababu mmeweka mbele mambo ya uchaguzi.