Mgomo wa madaktari - Updates

Mgomo wa madaktari - Updates

If by Madini you mean Dhahabu Almasi na Tanzanite you dont know what you say.
How many Watu wa Chini you want them to die before you realise that CCM Goverment has evil plan to kill your body and soul??
People are dying from eating imported contaminated and expired foods.
People are dying from taking Fake medicines damped in our country by hooligans which have contract with CCM and their Government to kill Tanzanians while they get rich quickly.
People are dying because of low income and sky rocketing prices of food and other important services and goods.

OPEN YOUR EYES MY FELLOW COUNTRYMEN!!!!

As we talk and write CCM government has allowed multinational Corporation to swindle our Madini under their supervision.
They are paid a one time Fungu worth SHANGA ZA VIUNO VYA WAKE ZAO to supervise these Thugs to steal,rape our land and kill PIPO as they wish.

NEVER EVER THINK THEY ARE WAITING FOR YOU TO DIE SO THEY WILL HANDOVER THIS COUNTRY BACK TO SLAVERY, THEY ARE DOING IT RIGHT NOW AND YOU ARE SUPPORTING THEM WITH ALL YOUR HEART AND STRENGTH UNKNOWINGLY.

Washatuchukua MSUKULE siku nyingi, TUAMKE kabla Hawajaanza kutukata NDIMI a POINT OF NO RETURN.

Jana nimesoma jinsi dawa za meno zenye madini ya Fluoride kama vile Colgate zinavyosababisha matatizo makubwa sana ya kiafya ikiwemo ugonjwa wa moyo, cancer na kisukari. nakaona pia jinsi nchi nyigi za ulaya zilivyopiga marufuku dawa hizi tangu mwaka 2006.

Nikasoma pia jinsi dawa za uzazi wa mpango maarufu kama njiti zilivyo balaa kuubwa katika afya ya mama na jinsi dawa hizo zilivyozuiliwa kuuzwa katika masoko ya ulaya na marekani

Sasa nikatafakari jinsi vitu hivi vinavyoshamiri ndani ya nchi yetu na jinsi ambavyo matatizo yake yanavyoongezeka kila kukicha. Nikagundua hatuna viongozi nchi hii kwani wanajua hili na wanafumbia macho.

Nilikua naongezea tu hoja yako kwa kifupi ili mlengwa aelewe zaidi
 
Madaktari msijione kuwa nyie mmesoma sana kuliko wengine au fani yenu ni ya muhimu sana kuliko zingine. Fani zote ni muhimu kulingangana na mahitaji ya muda huo. Msitake kuiyumbisha nchi. Tumieni uzalendo kwa Taifa lenu!

Utatumiaje uzalendo kwa viongozi wasio wazalendo. Ndugu usiwe unakurupuka.
 
Mdugu yangu;

Hayo aliyoyasema Pinda ndiyo kauli rasmi ya JK.

Pinda ametumwa tu kufikisha ujumbe ingawa alikuwa anajifanya kuongea hadi mishipa ya shingo inasimama, lakini ilikuwa siyo kauli yake.

Kauli ya Pinda ilikuwa katika mgomo wa kwanza ambapo kwa kinywa chake alisema kuwa "Serikali imechukua hatua ya kwanza kuwasimamisha Dakitari Mkuu na Katibu Mkuu, hatua ya pili itakuwa ni kuwasimamisha Mawaziri wa Wizaara"

Kitu ambacho juZi amekipinga, yaani amepinga maneno yake mwenyewe. Na hii ni kwamba alipomwambia JK aliikataa hoja yakuwasimamisha na ndio maana nasema kuwa aliyosema juzi Pinda ni kauli ya JK.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

na kwa hili ilitakiwa pinda ajiuzulu kwa kwenda kinyume na bosi wake. Makinda ajiuzulu kwa ishu ya posho, piinda ajiuzulu kwa ishu ya posho na arusha ila kwakuwa hakua uwajibikaji wataendelea kudunda tu
 
wewe ndiye kilazawa kwanza kwa sababu hujui umuhimu wa mawaziri kuondolewa unavyoinfluence muafaka wa madaktari

kama mawazo yako ndio hayo.....wewe ni kilaza...........

Ndugu sikufahamu vizuri;

Lakini napenda kukuuliza swali moja jepesi sana.

Hivi unakumbuka Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa Waziri enzi za Uraisi wa Hayati Nyerere; Ikatokea makosa yaliyofanywa na watendaji wake, lakini Mzee Mwinyi kwa busara na bila kuambiwa na mtu yeyote aliamua KUJIUZULU UWAZIRI??

Endapo kama ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa bado kupevuka naomba waulize wanaokumbuka.

(Samahani kama nimeongea maneno makali)

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Mazee.......hii tabia ya ku-copy na kupaste ndio UKILAZA wenyewe........samahani sana..........hebu fungua box kidogo....ndio utaelewa..........

Hivi waTanzania ni lini tutafunguka akili na kuacha kuendekeza ushabiki wa kizandiki katika suala kuwataka watu tunaowapa dhamana wawajibike!? Ni dhahiri kabisa kuwa hufuatilii hili sakata lilipoanzia wakati Intern doctors waliponyimwa stahiki yao kibabe na Wizara ya Afya na majibu ya kudhihaki taaluma ya uDaktari waliyopewa na CMO na Katibu mkuu..hali iliyopelekea MAT kuingilia kati, kisha Intern hao kulipwa na kutimuliwa Muhimbili. Hapo ndipo MAT ilipoitisha mkutano ambao pamoja na sakata la Intern ulijadili dhihaka za mara kwa mara wanazopata madaktari wakifuatilia maboresho ya maslahi yao pamoja maboresho ya huduma za afya wanazotoa kwa jamii.

Majibu ya dhihaka yaliyofutia hapo wakati MAT inafanya juhudi za kutatua tatizo toka kwa CMO, Katibu mkuu, Waziri na Naibu wake wizara ya afya nadhani kila mtu anayafahamu (kama Freema huyajui google utayapata, yaliandikwa everywhere) mpaka kupelekea mgomo! Waziri Mponda na naibu Nkya walidanganya umma wa waTanzania kupitia vyombo vya habari, walidanganya Bunge, walimdanganya na kumshauri vibaya waziri mkuu mpaka kupelekea kukurupuka mara ya kwanza kabla ya kujirudi.

Waziri wa afya na naibu wake, pamoja na wale wawili waliotimuliwa wamekuwa ni kikwazo kikubwa cha kuboresha maslahi ya madaktari na utoaji huduma za afya (hata kama wao hawakusababisha hali duni ya huduma za afya, kuzuia maboresho ni udhaifu)....hii imepelekea maDaktari kutowaamini na kuomba/kudai wajiuzulu au wawajibishwe. kitu ambacho waziri mkuu alikiri na kusema anamuachia rais aamue...rais haamui muda unakwenda, na papo hapo wanataka tuendelee na mchakato wa maboresho...kivipi, wakati hawa waliokuwa kikwazo ndio wasimamizi wakuu kwa upande wa serikali na hatuwaamini?! ili mchakato wa maboresho uendelee huku maDaktari wakiwa na imani na serikali, hawa wawili waliokuwa kikwazo waachie ngazi....

Nadhani sasa Freema umeelewa...anza kuchangia kuanzia hapo...acha kubwabwaja, wewe pamoja na wenzako mnaobwabwaja!

Mkuu Riwa......siku zote naheshimu sana maandiko yako........are you really serious.........hebu chukua mawazo yako hayo yaweke katika picha iliyo kubwa kidogo......toka nje ya madaktari kidogo...........please

..............Kwa hiyo wewe una akili nyingi kuliko madaktari wakiwekwa pamoja? Usilolijuwa ni sawa na usiku wa giza. Ina maana hata kama wewe ungekuwa kwenye nafasi ya Mponda ungegoma kujiuzuru kwa kuwa huoni mantiki?

yaani na wewe ndio unajiona umeona mantiki...........mantiki my foot.........na wewe ni Kilaza tu.......

Mkuu kwa hiyo wewe unataka mawaziri wajiuzuru kwa sababu madaktari wenye akili saana wametaka hivyo?.. Kwa nini wewe mwananchi mwajiri wa hawa wote usitake kujua hao mawaziri wamekosea nini kikubwa hadi ifikie wajiuzuru?
Kwa nini mazungumzo baina yao yanakuwa na usiri fulani wakati bunge lipo na mahakama zipo kwani vyombo hivi kazi yake ni nini? Hivi kweli leo hatma ya nchi yetu imeshikwa mikononi mwa watu sijui wasomi ambao ndio watoa hukumu bila kupitia hatua za kisheria.

Kugoma wagome hatuwakazi ni maamuzi yao lakini wasitegemee wananchi wote tunawaunga mkono kwa sababu waliua watu na wanaendelea kuua watu ati kwa sababu ya Mponda na Nkya. Kwa nini wasiseme JK ajiuzuru maana huyu ndiye kawawekea kifua mawaziri wote nchini. Yaani namkumbuka sana mwalimu Nyerere na tutamkosa sana!

Asante sana Bob............heshima mbele

Kama mnadai wana dhambi ni lazima dhambi zenyewe zitajwe.. Huyo mkurugenzi wa IMF kajiuzuru kwa sababu zake mwenyewe, hata wewe ukiwa mgonjwa unaweza jiuzuru kazi lakini sii kwa tuhuma za wizi au kumbaka mtu..
Kama makosa yapo kweli basi madai yafikishwe ktk vyombo vya sheria au hata kamati ya Bunge iwasikilize madai yao kutaka mawaziri hao wajiuzuru kisha kisha ndio maamuzi yatafuata. Kina Lowassa, Karamagi na wengineo wasingejiuzuru kama swala lile lisingefika bungeni, huu utaratibu kwa nini leo mnataka kukiuka na kuchukua mamlaka mikononi mwenu kama kumpiga mwizi wa Manzese!

Unajua nini Bob.......watu wanajisahau na kutekwa na ushabiki zaidi ya kufikiri.......Asante Mkuu..........
 
Kuna mtu aliandika kwenye blog ya michuzi kwamba mwajiriwa hawezi na hana haki ya kumlazimisha mwajiri amfukuze mwajiriwa mwenzake. kama hivyo ndivyo madaktari wanapata wapi hiyo nguvu ya kumlazimisha mwajiri atende kinyume na sheria za ajira?

Nijuavyo mie Waziri si mwajiriwa wa Serikali. Angekuwa mwajiriwa taratibu zake zipo tofauti lakini kwa kuwa si mwajiriwa ndio sababu hana 'tenure' ya kukaa ndani ya huo utumishi wa umma.
 
Mkuu Riwa......siku zote naheshimu sana maandiko yako........are you really serious.........hebu chukua mawazo yako hayo yaweke katika picha iliyo kubwa kidogo......toka nje ya madaktari kidogo...........please
QUOTE]

Labda hapo ndio kwenye tatizo na watu tunaojiita 'Great Thinkers' tunabaki tukibishana kwa siku kadhaa juu ya kitu ambacho kiko straight forward....pande zote hapa zinajitahidi kuwa selfish...si madaktari, si serikali, si wananchi/wagonjwa...tunatofautiana degree na lengo la ya u-selfish tu!

Sisi kama madaktari, bila kuwa selfish serikali haitaboresha maslahi yetu na utoaji huduma bora katika hospitali za umma, kwa sababu serikali ni selfish kushinda hata sisi, lakini uselfish wa maDaktari una component ya kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa jamii!

Serikali nayo ni selfish, lakini u-selfish wake haumsaidii Daktari wala mwananchi! Wananchi nao kwa upande wao ni selfish, wanajali afya zao tu, bila kujali madai ya msingi ya maDaktari wala serikali inafanya nini kuyatatua.

Sasa huu u-selfish wa pande zote ndio utakaodetermine urefu wa huu mgomo...serikali ikiamua kutokuwa selfish huu mgomo unaisha in a day...maDaktari wakiamua wasiwe selfish, huu mgomo unaisha in a day, lakini utaendelezwa na mgomo-baridi kutokana na frustration kitu ambach si kizuri kwa wagonjwa, na pia idadi kubwa ya maDaktari watakatishwa tamaa na kufanya kazi hospitalini au nchini, hivyo tutawapoteza...wananchi hawawezi acha kuwa selfish kwani kila mtu lazima ajali afya yake kwanza, lakini wanaweza kuutumia u-selfish wao kuishinikiza serikali kutatua huu mgogoro haraka, sababu wakiwaacha maDaktari wawe watatuzi wa huu mgogoro bado wananchi watatathirika na mgomo-baridi au kuondokewa na idadi kubwa ya maDaktari tabibu!
 
Wakuu,

Nilishaandika siku chache zilizopita kuwa Mungu amewapofusha macho na kufisha akili za viongozi wa CCM ili kila wakifanyacho kiharibike na hatimaye watoke madarakani ili tunusurike.
Kwa wanaofuatilia mambo ndani ya ccm watakubaliana nami kuwa hakuna lenye mwelekeo linalofanyika likafaa kwa wao wenyewe kwanza (ndani ya chama) na kwetu wananchi. Mungu amewafitinisha kila mmoja anaongea lugha yake. Kama kungekuwa na serikali makini (hasa Rais),leo hii viongozi wa wizara ya afya wangekuwa wamebaki na uwakilishi wa wananchi wao pekee. Akili ya kawaida inakataa Rais kuwang'ang'ania labda wanamsaidia kufanya uganga wa kienyeji!

Ushauri
Wananchi tuungane na madaktari kugoma ili hawa ccm waondoke nchi irudi kwenye mwelekeo.

Nawasilisha
 
kama mawazo yako ndio hayo.....wewe ni kilaza...........

Mazee.......hii tabia ya ku-copy na kupaste ndio UKILAZA wenyewe........samahani sana..........hebu fungua box kidogo....ndio utaelewa..........

Mkuu Riwa......siku zote naheshimu sana maandiko yako........are you really serious.........hebu chukua mawazo yako hayo yaweke katika picha iliyo kubwa kidogo......toka nje ya madaktari kidogo...........please

yaani na wewe ndio unajiona umeona mantiki...........mantiki my foot.........na wewe ni Kilaza tu.......

Asante sana Bob............heshima mbele

Unajua nini Bob.......watu wanajisahau na kutekwa na ushabiki zaidi ya kufikiri.......Asante Mkuu..........

Ni wapi wewe ulipopewa Moral Authority kwamba unachoandika wewe au mtazamo wako wewe ndio sahihi na wengine hawako sawa!?
Haya ndio madhara ya nchi kukubali kuhifadhi mpaka masokwe mahali patakatifu.
 
...suala la kuunganisha mgomo na kutaka kujiuzulu kwa Mawaziri............wagome kwa sababu zingine....sawa sio hii ya kutaka Mawaziri wajiuzulu........

kuunganisha suala la kugoma na kujiuzulu kwa Mawziri ni UKILAZA USIO NA KIFANI..............

Hawa madaktari wamelewa sifa baada ya kuwaunga mkono kwenye mgomo wao wa kwanza, wamekuwa juu ya haki ya maisha hasa baada ya kuingiza mambo yaliyo nje na matakwa yao kwenye mgomo wao. Wamelewa sifa na wawajibike, they have to be responsible for their actions.

Kuna fani muhimu zaidi ya udaktari i.e bila walimu (kama nao wangeamua kugoma uso kikomo) wengi wao wasingekuwa madaktari hivi leo.
 
Mimi naona tufute bunge na madiwani na pesa zinazotumika huko kwa sasa zielekezwe katika kuimarisha sekta ya afya nchini. Nadhani nchi hii inahitaji zaidi madaktari na manesi kuliko inavyohitaji wabunge na madiwani.
 
Hawa madaktari wamelewa sifa baada ya kuwaunga mkono kwenye mgomo wao wa kwanza, wamekuwa juu ya haki ya maisha hasa baada ya kuingiza mambo yaliyo nje na matakwa yao kwenye mgomo wao. Wamelewa sifa na wawajibike, they have to be responsible for their actions.

Kuna fani muhimu zaidi ya udaktari i.e bila walimu (kama nao wangeamua kugoma uso kikomo) wengi wao wasingekuwa madaktari hivi leo.

Siku mgomo wa kwanza ulipoisha maDkatari wakati wanatoa kauli ya kurudi kazini waliweka wazi kinachofuata...waliweka wazi kuwa watendaji waliobaki wa Wizara ya Afya (Waziri na Naibu wake) wajiuzulu au kutimuliwa, jukumu ambalo WM Pinda alimtwisha Rais...Madaktari waliweka wazi kuwa tarehe 3 march watakutana kujadili progress ya mchakato utakaojumuisha madai yaliyokuwa pending. Tarehe 3 March maDaktari walikutana na wakatoa tamko kuwa wanaelewa kuwa serikali iko katika mchakato wa kuangalia jinsi ya kuboresha maslahi ya watunishi wa afya na mazingira ya kazi, ila kuna jambo ambalo halihitaji mchakato....Mawaziri kujiuzulu! Na walitoa tamko nini kitakachofuatia iwapo hawatajiuzulu!

Badala yake Mawaziri hawakujiuzulu na serikali kutangaza ubabe na kuwakingia kifua....NANI ANATAKA SIFA HAPO?

Let me tell you...with or without public support, we reached the point of no return! Kurudi kazini ni iwapo tu Mawaziri watajiuzulu kupisha watu wengine tutakaowaamini kuwa wana nia ya dhati ya kuboresha maslahi na ubora wa huduma za afya, then tutarudi mezani...hata kama will take years, atleast tuwe kwenye mchakato na watu tunaojiaminisha wana nia ya dhati!
 
Tatizo letu ni mnapogoma 'eti kwa vile waziri na naibu wake hawajajiuzulu' .... mtarudi mezani baada ya waziri na naibu mpya kuteuliwa au mnataka hiyo wizara muindendeshe wenyewe?

Kiasi cha kusema with or without public support mko kwenye point of no return, ni kiburi, jeuri ukatili na uasaliti kwa wananchi. We better live without dr than kuwa na madrs wa kaliba yenu, wauaji.
 
Naogopa sana, kuwachokoza zaidi Madaktari. Nahisi mlipuko wa mgomo mkubwa zaidi. Hasa kama provocation itatumika, hapo busara inahitajika zaidi. We should learn to hit the route cause rather than scape goat (Wazee wa ilala na mdaktari wapi na wapi, hayo ni mambo yakizamani.)
 
Hawa madaktari wamelewa sifa baada ya kuwaunga mkono kwenye mgomo wao wa kwanza, wamekuwa juu ya haki ya maisha hasa baada ya kuingiza mambo yaliyo nje na matakwa yao kwenye mgomo wao. Wamelewa sifa na wawajibike, they have to be responsible for their actions.

Kuna fani muhimu zaidi ya udaktari i.e bila walimu (kama nao wangeamua kugoma uso kikomo) wengi wao wasingekuwa madaktari hivi leo.
Pleaseeeee................
...baada ya kuwaunga mkono?
hebu tueleze ulivyowaunga mkono!
 
Madaktari msijione kuwa nyie mmesoma sana kuliko wengine au fani yenu ni ya muhimu sana kuliko zingine. Fani zote ni muhimu kulingangana na mahitaji ya muda huo. Msitake kuiyumbisha nchi. Tumieni uzalendo kwa Taifa lenu!

Hayo siyo madai ya madaktari bali ni mawazo yako binafsi!!!
 
Mgomo utapita kama ilivyopita mingine, na huu sio wa kwanza wala wa mwisho.
 
Tatizo letu ni mnapogoma 'eti kwa vile waziri na naibu wake hawajajiuzulu' .... mtarudi mezani baada ya waziri na naibu mpya kuteuliwa au mnataka hiyo wizara muindendeshe wenyewe?

Kiasi cha kusema with or without public support mko kwenye point of no return, ni kiburi, jeuri ukatili na uasaliti kwa wananchi. We better live without dr than kuwa na madrs wa kaliba yenu, wauaji.

Hilo litakuwa ni dai jipya ambalo wewe ndio umeliongezea...madai yetu yako clear, na mpaka sasa unayafahamu!

Kiburi, jeuri, ukatili na usaliti kwa wananchi (wakiwemo maDaktari) walianza serikali wenyewe, na ndio maana leo tumefikia hapa...wewe kama Freema ulichonga chochote kuhusu mapungufu hayo ya serikali? au serikali inaweza fanya hayo..ila kwa maDaktari ni nongwa?!

Tangu mwanzo wa mgomo serikali pamoja na wananchi malimbukeni kama wewe mnaongelea kuhusu wajibu wa maDaktari tu kwa wananchi..na kwa serikali....nini wajibu wa mwananchi kwa Daktari wake? nini wajibu wa serikali kwa maDaktari wake? wewe kama mwananchi unadai niwajibike kwako, wewe umetimiza wajibu wako kwangu? serikali imetizimiza wajibu wake kwangu? kama kuua hata serikali ni wauwaji kwa kutotimiza wajibu wao, na wananchi pia ni wauaji kwa kutotimiza wajibu wao..

Pengine wananchi wenyewe wangedai maboresho ya huduma za afya wanazotoa maDaktari ikiwemu vifaa, madawa na mazingira bora ya kazi labda mimi kama Daktari nisingehitaji kugoma! Sasa kila kitu shaghala baghala, na tatizo linaonekana dhahiri wapi lilipo, au nani anazuia mchakato wa maboresho...maDaktari wanagoma kwa benefit ya wote wewe unawabeza na kuwaita majina ya ajabu! Wewe mpata huduma mwenyewe ndio unakuwa wa kwanza kunikatisha tamaa kukupa huduma bora ninazoamini unastahili..sababu tu ya ushabiki wa kipuuzi!
 
Back
Top Bottom