Kama hutaki kurudi meza ya mazungumzo hadi waziri ajiuzulu, ina maana unataka mazungumzo bila waziri (common sense ni kwamba waziri hafanyi maamuzi binafsi, kuna kanuni, taratibu na maelezo mengine ambayo inabidi ayafuate wakati anafanya kazi- na hii inaaply kwa mfanyakazi mwingine yeyote). Kwa hiyo basi, Waziri akijiuzulu, au akaondolewa kwenye nafasi hiyo na Rais, basi lazima hiyo nafasi izibwe na waziri mwingine - ambaye atafanya kazi kwa kanuni, taratibu, sheria na maelekezo yale yale ambayo waziri msiyemtaka amekuwa akifanya kazi kwayo. Kumkataa waziri sio suluhisho la matatizo yeni, na hilo mnalijua fika.
Impliation ya madai ya kuondolewa waziri ili mkae meza ya mazungumzo ni kuwa hamtaki kuongozwa, mnataka mjiongoze ili mhakikishe mnapata vifaa, mazingira, posho, mishahara na stahiki zenu kadri mnavyopenda na mnavyoona inawasuit. Ingekuwa vinginevyo mngerudi meza ya mazungumzo (unless matakwa yenu mnayalazimisha kama vile sekta ya afya ndo muhimu kuliko sekta ya elimu, maji, kilimo nk ambao mnadhani wao hawana matakwa kama mliyonayo).
Wananchi malimbukeni kama mimi tunaona haina haja ya kuwa na madaktari wanaotaka kuua kwa maslahi yao binafsi badala ya kufa wao kwa ajili ya maslahi ya wengi. Mnastahili kuwajibishwa na nadhani mwenye mamlaka anachelewa sana kuwawajibisha.