Mgomo: Madaktari waiangukia serikali!

Ina maana wamekubali kulipwa chochote ilimradi warudi kazini? Mi na wasiwasi watapewa sharti la kufanya kazi miezi 6 bila malipo kama adhabu ya mgomo waliofanya. Ina maana hata zile tuhuma za Joyce Nyoni, mama Nkya, Dr. Mpondo zilikuwa feki? Kama ndivyo wakawaombe msamaha Lucy Nkya na Dr. haji Mponda kwa kuwaharibia kazi

Waliotoa matakwa ya mawaziri kujiuzuru ni hao viongozi ambao wamewatekeza hawa interns ambao sasa wameamua kujitoa katika kundi lililopotea kimaadili na kuomba radhi.
 
Subirini tamko la wengine ndio mtajua kuwa mbinu ya 'wagawanye watawale" bado inatumika. Baada ya mgomo kuendelea kuuma hakuna jinsi nyingine isipokuwa kuwagawanya madaktari. Leo hii huko Chicago mgomo wa walimu wenye kuathiri wanafunzi karibu 350,000 unaingia wiki ya pili...
 
Mkuu mcfm40, can you really imagine eti baba wa familia yake au mama wa familia anadiriki kusema "alipotoshwa/alidanganywa" ... seriously? if they meant that sincerely, i then sincerely doubt the way they run their families...No offence.

Mbona kwenye nyumba za ibada kila siku wababu kwa wamama wanajazana kuomba radhi kwa Mungu kwa kupotoshwa na shetani. Kuifundisha familia kuomba radhi inapotambua imekosea ni jambo jema. Kung´ang´ania makosa siyo ujasiri. Ushajaa wa mtu huonekana katika uwezo wake wa kurudi kwenye njia sahihi baada ya kuposhwa na changamoto, sio kung´ang´ania kwenye chaka la upotofu.
 
Subirini tamko la wengine ndio mtajua kuwa mbinu ya 'wagawanye watawale" bado inatumika. Baada ya mgomo kuendelea kuuma hakuna jinsi nyingine isipokuwa kuwagawanya madaktari. Leo hii huko Chicago mgomo wa walimu wenye kuathiri wanafunzi karibu 350,000 unaingia wiki ya pili...

Wanaomba radhi si kwa sababu hawakuwa na madai ya msingi, ila ni kwa sababu wamesalitiwa. Hii inashangaza. Ninakubaliana na wewe mkuu wengi ni njaa inatusumbua hadi usaliti
 
Madaktari wanafunzi mnajifanya hamjui matatizo yanayowakabili wagonjwa na pia wafanyakazi wote wa sekta ya umma ya afya! Mfano mmoja, someni hapa KCMC hospitali wanalia kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa, kukosa vitendea kazi n.k

KCMC Hospital, Moshi Tanzania
MATATIZO
• Msongamano wa wagonjwa bado ni tatizo katika hospitali hasa katika wodi ya Wazazi, wodi za upasuaji na wodi za magonjwa ya kinamama.

Kulingana na takwimu za hospitali wagonjwa wanaokadiriwa kufikia milioni moja na laki sita wanatibiwa katika hospitali hii na ina jumla ya vitanda 300 na ina wodi 13.

WATUMISHI WA HOSPITALI
Hospitali yetu ina jumla ya watumishi 440 wa kada mbali mbali. Kati yao :-Daktari Bingwa ni mmoja, Madaktari wa Kawaida ni 8, Madaktari Wasaidizi 21, Matabibu 24, Daktari wa Meno 1, Madaktari Wasaidizi wa Meno 2, Wafamasia 2, Mafundi Sanifu Maabara 2, Wauguzi Wasajiliwa 69, Wauguzi Wakunga 72, na watumishi wengine wa kada mbali mbali.
• Bado kuna upungufu wa watumishi hasa Madaktari Bingwa.

• Upatikanaji wa madawa, vitendanishi na vifaa tiba bado ni tatizo toka katika Bohari ya Madawa.
MIUNDO MBINU:
Kwa kuwa hospitali hii imejengwa zamani, majengo yake mengi ni machakavu.

source: Kilimanjaro - muundo wa kiutawala
 
Ama kweli wataalamu wote wataendelea kuwa watumwa wa wanasiasa, I thought walivyodai kuwa madai yao ni ya msingi walikuwa na maana coz hata serikali mara kadhaa ilikiri kuwa madai yao ni ya msingi, sasa ina maana hizo huduma bora walizokuwa wanazipigania zimeshaboreka? mwanzo nilidhani wamejitolea kumkomboa mtz, kumbe JK alikuwa mkweli kuwa jamaa walichokitaka ni mishahara tu! hizo afya bora ilikuwa geresha tu! maana kukosa huo mshahara ambao waliudai hautoshi sana tena kwa miezi michache tu tayari kumewafanya warudi kudai kuwa walishawishiwa! so its obvious afya bora haikuwa lengo lao, eti jitu zima na midevu yake (hapo kwenye picha) linadiriki kusema lilishawishiwa, kwa hiyo mtu akikushawishi akuban**e utakubali kwa kuwa umeshawishiwa!? upungufu wa utashi na kuongozwa na busara za tumbo! Daktari kama hawa ni sumu kwa taifa na kamwe siwezi kuwa na imani nao, kama alishawishiwa aniache naye akakubali bila kuelewa kwanini ananiacha nife, akirudishwa akishawishiwa anichome sindano ya sumu si ataniua huyu!!
Hapa hatuna madaktari! sasa wakati wanagoma walifikiria nini?? JK timua wote bora tutibiwe na manesi kwani hata panado nao wanazijua!
 
ninyi watu kumbe ndio wehu namna hii? na ninyi mmekuwa kama wenzenu waalimu eeh? hovyo kabisa
 
Hapa kuna kesi ya msingi kabisa. Hawa madaktari wanafikiri ignorance of the law is an excuse to break the law.....La hasha sio hivyo. Umegoma na mgomo ulisababisha vifo una kesi ya msingi9 kabisa ya kujibu.

On a very serious note naomba contacts za mwanasheria atakayesoma taarifa hii niandikie kaziyangu@gmail.com nataka unipe quote za kufungua kesi kuwashtaki madaktari wote 200 waliokiri na kuomba msamaha kwa kosa la mauaji. Nataka kuwaburuza wote kotini ili nijue kama Watanzania tunatibiwa na watu mbumbumbu namna hiyo basi acha waende sero wakajifunze.

I am damn serious. Wanasheria kazi hii hapa.
 
Poleni interns! Ila naona hammjui JK vizuri. Ni mtu asiyegeuka nyuma, na akiamua ameamua
Viongozi walikuwa wapole sana kwa madaktari kwani ktk kipindi kifupi wameitisha migomo mara kadhaa na kila ikimalizwa wanarudi na ajenda nyingine na tuliwaeleza kwamba hawawezi kushinda vita hii kwani wanaoumia ni wasio na hatia.Kitendo kilichofanywa na serikali ni kuwatuliza mumkari madaktari ili warudishe uwezo wa kufikiri kwa kuwapokonya leseni za muda na baadae waombee msamaha na AMINI USIAMINI Serikali itawarudisha na hata hilo la kuomba msamaha wamefundishwa na waliomo ndani ya serikali na huo ndiyo mwanzo wa kuwarudishia leseni na kuwarudisha kundini.Natumai wamejifunza kama elimu dunia watakuwa wameipokea vyema.
 
Hivi vidaktari ni hovyo kabisa. Eti tutamfuata rais tumuombe msamaha!!!! Msamaha gani huo!!! Mmetumwa nini ninyi vitoto!!! Ni watanzania wangapi wanapoteza maisha kutokana na kukosekana kwa vifaa basic vya tiba? Njaa bwana haina adabu!
 
Waliotoa matakwa ya mawaziri kujiuzuru ni hao viongozi ambao wamewatekeza hawa interns ambao sasa wameamua kujitoa katika kundi lililopotea kimaadili na kuomba radhi.
Hao wa chicago si unaona nao hawakutimiziwa yote na wameshaanza kugawanyika vile vile na Meya ameshaanza kufuata taratibu za kisheria sinema kama ya Bongo tu!
 
Hivi vidaktari ni hovyo kabisa. Eti tutamfuata rais tumuombe msamaha!!!! Msamaha gani huo!!! Mmetumwa nini ninyi vitoto!!! Ni watanzania wangapi wanapoteza maisha kutokana na kukosekana kwa vifaa basic vya tiba? Njaa bwana haina adabu!

Sasa nyie Pro-Chadema mlikuwa mnachochea mgomo wa madaktari mmeshindwa kuwasaidia baada ya kufukuzwa, madaktari wameshtuka mnataka kuwatumia kisiasa kama mlivyomtumia Dr Ulimboka.

Ni pigo kubwa kwa Chadema.
 
Tumeyaona yote yaliyotokea kwa upande wa Wagonjwa wengi sana wamefariki kwa kukosa huduma muhimu wakati wa mgomo,kibaya zaidi Watanzania kwa ujumla wetu tuliwasihi Madaktari wasiendelee na mgomo ila wajipange katika mazungumzo ili kufikia muafaka. Matokeo ya yale ambayo tulikuwa tunawashauri ndiyo haya, madaktari wameshindwa kuuthibitishia umma wa Watanzania kuwa kile walichokuwa wamekigomea kuwa kimekwisha,mazingira mabovu ya kufanyia kazi bado yapo,ukosefu wa dawa bado upo,ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi bado upo,sasa kipi kimewafanya waombe radhi? Kwa mawazo yangu ni kuwa Serikali iliposema "Liwalo na Liwe" walikuwa wanafahamu udhaifu wa hao Madaktari Wanafunzi na ndiyo maana wakawafutia Leseni zao ili kuwanyima uwezo wakufanya kazi sehemu nyingine iwe ndani ya nchi ama nje. Nashukuru wamejifunza kutokana na makosa yao kuwa majadiliano pekee ndiyo njia nzuri ya kufikia suluhisho la jambo lolote lile,wengi wa Madaktari hawa walitumia hisia na mihemko na wala siyo akili katika ushiriki wao wa mgomo,ingawa ni haki yao kugoma lakini haipaswi kugomagoma hovyo wakati wanafahamu kabisa kuwa kwa taaluma yao inayoambatana na utii mkubwa na nidhamu ya hali ya juu haipaswi kuwekwa rehani kwa vitu ambavyo havina msingi. Mimi binafsi nimeridhishwa na kitendo chao cha kiungwana cha kuiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Raisi wetu,muungwana akivuliwa nguo huwa hasimami bali uchutama ili kujistiri. Tunamuomba Raisi awasamehe na awarudishe tena kazini kwa masharti magumu ili iwefundisho kwa wengine ambao watatamani kugoma.
 
Ha ha ha ha! Huko ni kukosa mbinu na mikakati katika maisha. Kwani ni lazima uidhinishwe kutibu? Mliona maslahi hayafai,mimi nilidhani mmeshapata mbadala wa kazi ya utabibu. Nikadhani mnaacha internship na kuingia kwenye utafifi, utaalamu elekezi au ujasiamali unaohusiana au hata usiohusiana na fani mlosomea! Poor short minded Doctors! Mlikuwa wajasiri kuwaacha watanzania wakafa leo eti mnajutia! Nunueni maua na mishumaa mkaomboleze katika makaburi ya watanzania waliokufa bila hatia mkimaliza nawakaribisha tufanye joint medical research on ethinomedicine.
 
Kuna jambo zaidi ya tunayoyasikia!! Siamini kuwa kudai haki ni lazima mtu aombe radhi. Yaani wanaomba radhi kwa kudai haki
Wasiishie hapo waende mbali na kumuomba radhi Ulimboka kwa kumsaliti hadi akaribie kupoteza maisha Kudai huduma nzuri kwa wagonjwa nako kunahitaji kuomba radhi!

Ni zaidi ya tunayoyasikia.Kitu kimoja ninachoshangaa ni 'ushujaa' wa hao Madaktari kusimama mbele ya kamera.Ushujaa huo ni wa aina yake.

Time will tell
 
Back
Top Bottom