Mgomo: Madaktari waiangukia serikali!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
17 September 2012

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo Dr. Paul Swakala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na Datus Boniface

Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors), wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.

Kwa upande mwingine wamekijua juu Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kuwa kimewasaliti katika kutatua matatizo yao kwa sasa.
Hata hivyo, wameomba radhi kwa Wananchi walioathirika na mgomo huo kwa usumbufu uliyosababishwa na mgomo huo.

Hadi sasa Madaktari 364, wako mtaani baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kushiriki katika mgomo ambao umeisha hivi karibuni, baada ya kushawishiwa na wenzao wakiwemo viongozi wa MAT.

Akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hao, Paul Swakala alisema “Tulikaa na MAT kuzun gumza juu ya kutusaidia kutatua kero zetu lakini wameshindwa kutusikiliza na baadala yake tumeamua kufika hapa na kutoa kilio chetu”

Kutokana na kusalitiwa huko, alitoa onyo kwa Madaktari wengine kuwa wanaweza kupima kama wataendelea kujiunga na MAT au la.

Alienda mbali zaidi na kusema, hawako tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania.
Alisema, kwa hakika wanajutia kosa lao la kushiriki mgomo na wako tayari kurejea kazini ili kuendelea na kazi ya kuwahudumia Wananchi kwa moyo mweupe.

Tuwatie moyo, kuomba msamaha ni suala la busara sana na kila mtu anapitia humo hakuna asiyekuwa mkosaji katika maisha yake, wenye mamlaka waangalie na kuona umuhimu wa kuwasamehe.
 
Usaliti wa MAT ulionekana toka mwanzo! Intern hawakujua kuwa wenzao wana-vioski vingi sana, na walirudi makazini haraka kwa kuwa kuna faida kubwa sana wanapata! Hawafanyi kazi muda wote, na muda mwingine wanatumia kwenye Hospitali zao binafsi!
 
Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors) wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.
Kwa upande mwingine wamekijua juu Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kuwa kimewasaliti katika kutatua matatizo yao kwa sasa.
Hata hivyo, wameomba radhi kwa Wananchi walioathirika na mgomo huo kwa usumbufu uliyosababishwa na mgomo huo. Hadi sasa Madaktari 364, wako mtaani baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kushiriki katika mgomo ambao umeisha hivi karibuni, baada ya kushawishiwa na wenzao wakiwemo viongozi wa MAT.
Akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hao, Paul Swakala alisema “Tulikaa na MAT kuzungumza juu ya kutusaidia kutatua kero zetu lakini wameshindwa kutusikiliza na baadala yake tumeamua kufika hapa na kutoa kilio chetu”.
Kutokana na kusalitiwa huko, alitoa onyo kwa Madaktari wengine kuwa wanaweza kupima kama wataendelea kujiunga na MAT au la.
Alienda mbali zaidi na kusema, hawako tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania.
Alisema, kwa hakika wanajutia kosa lao la kushiriki mgomo na wako tayari kurejea kazini ili kuendelea na kazi ya kuwahudumia wananchi kwa moyo mweupe.
 
wamejiharibia sana hawa ndugu zetu, kosa namba moja ni pale mlipoamua kugawanyika wakati wa kugoma. Kosa namba mbili ni sasa mnapowageuka MAT na kuwatupia mpira wa lawama wakati utashi wa kugoma ulikua juu yenu.
Mwisho kabisa nasikitika kusema ya kwamba JK au serikali yake haitawasemehe kwa kuwa imeshagundua wapi mna kasoro, tafadhali jaribuni tu kutafuta career nyinginezo maana inaonesha hamkuwa na plan B.
Suala na ninyi kugoma ama kutokugoma ilipaswa mliongee vizuri hapo awali kwenye vikao vyenu vya ndani huku mkishauri na kushauriwa kutoka MAT.
 
tuliwaambia msikize kilio cha wagonjwa maskini wasio nacho hamkusikiza.. haya sasa maji mmekandwa na mtoto kafa.. ndio tabu ya kutumika kama condom bila ya kuangalia consequences..haya kiko wapi? na mabalaa yatawaandama mpaka siku mnaingia kaburini..laana ya watz wanyonge iwafuate ninyi na serikali, wote wauaji wakubwa nyie.
 
MAT sio watu kumbe ni wabinafsi kwelikwel, kwa nini wao wanaendelea kufanya kazi na interns ndo wafukuzwe? kwa nini hawajachukua hatua ili mrudishwe kazini?
 
Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors) wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.
Kwa upande mwingine wamekijua juu Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kuwa kimewasaliti katika kutatua matatizo yao kwa sasa.
Hata hivyo, wameomba radhi kwa Wananchi walioathirika na mgomo huo kwa usumbufu uliyosababishwa na mgomo huo. Hadi sasa Madaktari 364, wako mtaani baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kushiriki katika mgomo ambao umeisha hivi karibuni, baada ya kushawishiwa na wenzao wakiwemo viongozi wa MAT.
Akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hao, Paul Swakala alisema "Tulikaa na MAT kuzungumza juu ya kutusaidia kutatua kero zetu lakini wameshindwa kutusikiliza na baadala yake tumeamua kufika hapa na kutoa kilio chetu".
Kutokana na kusalitiwa huko, alitoa onyo kwa Madaktari wengine kuwa wanaweza kupima kama wataendelea kujiunga na MAT au la.
Alienda mbali zaidi na kusema, hawako tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania.
Alisema, kwa hakika wanajutia kosa lao la kushiriki mgomo na wako tayari kurejea kazini ili kuendelea na kazi ya kuwahudumia wananchi kwa moyo mweupe.

Mie hapo pekundu tu...
 
...mganga njaa always hana msimamo, hawa ndiyo hununuliwa kwa vitumbua na ubwabwa na kupelekwa Diamond J kukonfesi...! Huyu anafikiri atapewa ukuu wa wilaya...!!

Hakuna mtu asiyeaminika kama mtanzania. umasikini ni kitu kibaya sana. mwingine atauza hadi utu wake
 
Kama hii ni kweli basi naamini vifo vingi vya wagonjwa vinatokea kutokana na upumbavu wa madaktari, hatuna madaktari wenye weledi unaotakiwa ndio maana wameenda kupiga magoti badala ya kutafuta kazi kwenye nchi nyingine!
 
hongera swakala kwa uongozi mzuri, ulikuwa rais mzuri sana Bugando kumbe bado uko vizuri kaka. Maana MAT wameliweka jambo hili kuwa la mtu mmoja mmoja jishughulikieni wenyewe na mkisamehewa hakuna cha mgomo wa MAT wala jumuia ya madactari kuuunga mkono. mimi nimeboreka sana kwa jambo hili kwanza limetudharirisha hata wale ambao bado tunasoma.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom