Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Chapinga kushirikishwa katika Mchakato Mzima wa Maoni ya "Bima Ya Afya kwa wote" Kama serikali ilivyosema

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,598
17,734
Chama cha Madaktari Nchini Tanzania (MAT) kimepinga na kusema kuwa hakikushirikishwa kwenye mchakato wowote wa kuandaa,Kutoa maoni au Kushiriki katika njia yoyote ile ya mchakato huo.

kinyume cha serikali inavyojinasibu kuwa Chama hicho kilishirikishwa kama Mdau Rasmi wa Afya..

Aidha Dr. Deusdedit Ndilanha, ambaye ni Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT)

ametangaza ya kuwa ameshitushwa na
taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuwa chama kilishiriki kwenye mapendekezo ya Kitita cha Mafao Cha Mwaka 2023 cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)

"Chama kinakanusha kushiriki au kushirikishwa kwenye mchakato huu ,Hatua zilizopitiwa wakati wa mchakato" anasema Dr ndilanha..

"Chama kinawaomba wanachama na wadau wa afya kuwa na subira, Chama kitatoa tamko rasmi na msimamo wake mara baada ya kikao na kamati tendaji kukaa" anamalizia Dr Deusdedit Ndilanha

20231220_081704.jpg

20231220_081655.jpg

Screenshot_20231220_083936_X.jpg
 
kama Hao MAT hawajashirikishwa kuna uwezakano mkubwa hato hao waliotajwa kama walishirikishwa watakuwa hawajashirikishwa.

wanafanya kwa faida ya nani? kwa lengo gani?
Nahisi Serkali inataka kukusanya mapato zaidi ila sheria hii ni Ngumu kumeza kwakweli..

Subri ianze kazi utaona kilio cha wananchi..

Japo wengine kupinga ni Vigumu.."Kuona wadau kama viongozi wa dini wakipinga hiyo sahau" pia vivo hivyo kwa Wamiliki wa Hospitali na Vituo vya afya
 
kama Hao MAT hawajashirikishwa kuna uwezakano mkubwa hato hao waliotajwa kama walishirikishwa watakuwa hawajashirikishwa.

wanafanya kwa faida ya nani? kwa lengo gani?
Hii Bima ni njia ya serikali kukusanya fedha ila huduma zitakuwa mbaya sana. Ukweli ni kwamba serikali haina uwezo wa kutoa bima kwa wote kwa maisha ya mtanzania asiyezingatia hata afya na ambaye kula kwake kwa tabu.
Kama elimu kwa wanafunzi bado changamoto ije kuwa bima.
Ni kitu kizuri kwa kila mtanzania kuwa na bima ila malalamiko yatakuwa mengi sana
 
Huyo Rais wa MAT hajui wenzake wanatafuta Kura kwaajili ya Uchaguzi 2025.

Amuulize Dokta Ulimboka alichofanywa na hiyo hiyo Serikali alipojaribu kwenda kinyume nao.

Ajue anaishi na kufanya kazi Nchi ya Giza hii 🤗
 
Hiki ndicho kilichomtoa Prof. Abel Makubi ukatibu mkuu wizara ya afya....

Baada ya professional assessment ikaonekana hii bima iko impracticle, akaipiga chini. Mwanzo waziri alimuelewa.

Namba moja aliposikia akanga'aka, waziri akajivua na kumtupia zigo la lawama Makubi..
 
Wataalamu walishaikataa, hakuna mdau wa afya (Madaktari,Wafamasia,Wauguzi) aliyeona hii bima itatoboa ndo maana mwanzo ilisitishwa...

Kimsingi hii ni bima ya Ummy na genge lake...
 
Halafu ujue mpaka leo huwa sijui kosa la proff Makubi kabisa..
Labda kwa sababu yeye ni Daktri na aliliona hili swala ni ngumu kuweza kufanyika unless mwananchi aumie
 
Chama cha Madaktari Nchini Tanzania (MAT) kimepinga na kusema kuwa hakikushirikishwa kwenye mchakato wowote wa kuandaa,Kutoa maoni au Kushiriki katika njia yoyote ile ya mchakato huo.

kinyume cha serikali inavyojinasibu kuwa Chama hicho kilishirikishwa kama Mdau Rasmi wa Afya..

Aidha Dr. Deusdedit Ndilanha, ambaye ni Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT)

ametangaza ya kuwa ameshitushwa na
taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha kuwa chama kilishiriki kwenye mapendekezo ya Kitita cha Mafao Cha Mwaka 2023 cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)

"Chama kinakanusha kushiriki au kushirikishwa kwenye mchakato huu ,Hatua zilizopitiwa wakati wa mchakato" anasema Dr ndilanha..

"Chama kinawaomba wanachama na wadau wa afya kuwa na subira, Chama kitatoa tamko rasmi na msimamo wake mara baada ya kikao na kamati tendaji kukaa" anamalizia Dr Deusdedit Ndilanha

View attachment 2847744
View attachment 2847743

View attachment 2847759
Huyu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari (MAT) aliyetangaza msimamo huu asije akajikuta anatekwa na "Watu wasiojulikana" kama alivyotekwa Dkt. Ulimboka miaka ile ya nyuma. Awe makini sana na mienendo ya maisha yake kuanzia sasa. Akumbuke kwamba Watekaji wamekuwa wakipongezwa siku hizi kwa kupewa 'shavu nono' la kulambishwa asali kama reward kwa "kazi zao nzuri za utekaji." Yule aliyemteka Dkt. Ulimboka naye amepewa reward nono ya kwenda kule "Mjengoni Dodoma" ili akafaidi mema ya nchi, awe mwangalifu huyu Dokta, yasije yakamkuta ya kumkuta.
 
Wataalamu walishaikataa, hakuna mdau wa afya (Madaktari,Wafamasia,Wauguzi) aliyeona hii bima itatoboa ndo maana mwanzo ilisitishwa...

Kimsingi hii ni bima ya Ummy na genge lake...
Jamaa wanaforce hiyo bima maana imehaidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Kwahiyo lazima ionekane inafanya kazi kuelekea chaguzi za 2024 na ule Mkuu wa 2025.

Wanasiasa wakiamua lao hakuna namna
 
Halafu ujue mpaka leo huwa sijui kosa la proff Makubi kabisa..
Labda kwa sababu yeye ni Daktri na aliliona hili swala ni ngumu kuweza kufanyika unless mwananchi aumie
Ile kamati iloundwa ya wataalam kuassess feasibility ilikuja na majibu yasiyo na furaha kwa wanasiasa, ndiyo sababu ya kuondolewa kwa Makubi sababu hakutaka siasa kwenye jambo serious kama hili...

Ukiona MAT wanakuwa na guts za kuikana serikali ujue wana uhakika na wanachokifanya..

Hakuna mtaalamu wa afya anaielewa serikali inachofanya kwenye hii bima kwa wote..

Iwapo NHIF tu inapumulia mipira, hii bima kwa wote itawezekanaje?
 
Huyu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari (MAT) aliyetangaza msimamo huu asije akajikuta anatekwa na "Watu wasiojulikana" kama alivyotekwa Dkt. Ulimboka miaka ile ya nyuma. Awe makini sana na mienendo ya maisha yake kuanzia sasa.
Wakimgusa ujue mgomo wa madaktari utaibuka palepale maana hii bima wataalamu walishaikataa❌
 
Back
Top Bottom