Tumeyaona yote yaliyotokea kwa upande wa Wagonjwa wengi sana wamefariki kwa kukosa huduma muhimu wakati wa mgomo,kibaya zaidi Watanzania kwa ujumla wetu tuliwasihi Madaktari wasiendelee na mgomo ila wajipange katika mazungumzo ili kufikia muafaka. Matokeo ya yale ambayo tulikuwa tunawashauri ndiyo haya, madaktari wameshindwa kuuthibitishia umma wa Watanzania kuwa kile walichokuwa wamekigomea kuwa kimekwisha,mazingira mabovu ya kufanyia kazi bado yapo,ukosefu wa dawa bado upo,ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi bado upo,sasa kipi kimewafanya waombe radhi? Kwa mawazo yangu ni kuwa Serikali iliposema "Liwalo na Liwe" walikuwa wanafahamu udhaifu wa hao Madaktari Wanafunzi na ndiyo maana wakawafutia Leseni zao ili kuwanyima uwezo wakufanya kazi sehemu nyingine iwe ndani ya nchi ama nje. Nashukuru wamejifunza kutokana na makosa yao kuwa majadiliano pekee ndiyo njia nzuri ya kufikia suluhisho la jambo lolote lile,wengi wa Madaktari hawa walitumia hisia na mihemko na wala siyo akili katika ushiriki wao wa mgomo,ingawa ni haki yao kugoma lakini haipaswi kugomagoma hovyo wakati wanafahamu kabisa kuwa kwa taaluma yao inayoambatana na utii mkubwa na nidhamu ya hali ya juu haipaswi kuwekwa rehani kwa vitu ambavyo havina msingi. Mimi binafsi nimeridhishwa na kitendo chao cha kiungwana cha kuiomba radhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Raisi wetu,muungwana akivuliwa nguo huwa hasimami bali uchutama ili kujistiri. Tunamuomba Raisi awasamehe na awarudishe tena kazini kwa masharti magumu ili iwefundisho kwa wengine ambao watatamani kugoma.