Mgomo: Madaktari waiangukia serikali!

Mgomo: Madaktari waiangukia serikali!

I used to know that they are SMART persons in the world? So disapointed by u guys, nimebakiza Wakaguzi wa mahesabu tu katika list yangu.

Hahaha mkuu Uhalisia Jr, we are SMART, just some of people who cant handle the pressure...that's all...and wont be fair to generalize the majority's judgement over consideration of a few!
 
1.0 MI NIPO TAYARI KUCHANGISHA PESA HAWA MADAKTARI WAPELEKWE MAHAKAMANI KWA KUDHALILISHA TAALUMA YAO;
2.0 KUANZIA SASA TAKUKURU ANDAENI PESA ZA MOTO TUWACHOMEKEE WOTE NA RUSHWA MAANA NDIO WALIYOIMISS;
3.0 WAFUTWE KABISA WASIWE TENA MADAKTARI HAWATUFAI, MBONA TUNATIBIWA BILA WAO, WAACHE WAENDE WAKALIME, hawakujua nini wanafanya?.
 
Lkn hapa kuna utata unanitatisha, kama vile serikali inataka kuwagombanisha madokta wasiwe na maelewano, umoja na mshikamano ili wasiweze kudai walichokuwa wanadai
 
Sijaona pahala ktk tamko hilo la madaktari walipokitaja au kukigusia CHADEMA..Iweje wewe uanze kukitaja chama hata pasipohusika?Wasiwasi wangu ni kuwa,ipo siku mkeo atashindwa kupata ujauzito na utakit upia lawama CHADEMA..

Wakati mwingine mnakuwa arrogant bila sababu. Hiyo post nilimjibu Molemo. Wewe unamjua Molemo ni nani?
 
17 September 2012




Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo Dr. Paul Swakala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na Datus Boniface

Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors), wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.

Kwa upande mwingine wamekijua juu Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kuwa kimewasaliti katika kutatua matatizo yao kwa sasa.
Hata hivyo, wameomba radhi kwa Wananchi walioathirika na mgomo huo kwa usumbufu uliyosababishwa na mgomo huo.

Hadi sasa Madaktari 364, wako mtaani baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kushiriki katika mgomo ambao umeisha hivi karibuni, baada ya kushawishiwa na wenzao wakiwemo viongozi wa MAT.


Akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hao, Paul Swakala alisema “Tulikaa na MAT kuzun gumza juu ya kutusaidia kutatua kero zetu lakini wameshindwa kutusikiliza na baadala yake tumeamua kufika hapa na kutoa kilio chetu”


Kutokana na kusalitiwa huko, alitoa onyo kwa Madaktari wengine kuwa wanaweza kupima kama wataendelea kujiunga na MAT au la.

Alienda mbali zaidi na kusema, hawako tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania.
Alisema, kwa hakika wanajutia kosa lao la kushiriki mgomo na wako tayari kurejea kazini ili kuendelea na kazi ya kuwahudumia Wananchi kwa moyo mweupe.


washikaji wamesoma alama za nyakati. wanajua batch ingine ya mwaka huu inaenda mahosipitali kwa hiyo itakuwa imekula kwao. wajinga kabisa hawa. hongera kwa wale madaktari waliotujali sisi walala hoi pamoja na dhulma za ccm lakini waliendelea kutuhudumia huku wakijua kuwa sisi hatuna makosa.
 
magamba bwana kila kitu chadema. umejuaje kuwa ni wafuasi wa chadema?udhaifu wa jk ndo chanzo cha yote. mgomo wkt wa mkapa haukudrag this long coz he made correct intervention kama rais. dhaifu alienda kutembea kama kawaida yake. mtasema hata ffu aliyemuua Mwangosi alikuwa cdm

Kwanza we ulizani ni ffu wa wapi kama sio cdm, mbona mliwapigania kule bungeni waongezewe maslahi kama sio jamaa zenu??????????????????
 
Jumanne, Septemba 18, 2012 05:45 Asifiwe George na Aziza Juma, Dar es Salaam *Wajutia mgomo wao uliofanyika hivi karibuni *Wasema hawapo tayari kushiriki tena mgomo MADAKTARI wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (Interns), wameomba radhi kwa wananchi na Serikali kutokana na madhara ya mgomo wao uliofanyika hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Walioathirika na Mgomo, Paul Swakala, alikiri kuwa mgomo huo umesababisha madhara makubwa. Swakala alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa chama chake pia kinakusudia kwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete, kwa lengo la kumwomba radhi. “Tunatumia fursa hii kupitia kwenu waandishi wa habari kuwaomba radhi Watanzania wote na kwa Serikali kutokana na madhara yaliyosababishwa na migomo ile ambayo ushiriki wetu ulikuwa hauepukiki. “Tunajua kuwa wapo watu walioathirika na mgomo ule, hivyo tunawaomba radhi kwa Watanzania wote walioathirika na mgomo, pia kwa usumbufu uliojitokeza. “Pamoja na kwamba utamaduni wa kuomba radhi hadharani kwa nchi yetu haujazoeleka, lakini tumeamua kufanya hivyo kwa sababu sisi ni binadamu na watu wote tuna upungufu. “Pia tunamwomba radhi Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake kwa usumbufu uliosababishwa na mgomo ule, vile vile tunatambua na kuunga mkono juhudi zake katika kuboresha huduma za afya nchini pamoja na changamoto nyingi ambazo zinaikabili sekta hiyo nchini. “Hata hivyo, tutazidi kuiomba Serikali iangalie zaidi sekta hii, kwani maisha ya Watanzania wengi yanategemea huduma bora za sekta hiyo. “Tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa sisi vijana wao hatupo tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania wenzetu,” alisema. Swakala alisema kuwa madaktari wanajutia sana kosa hilo na wako tayari kurejea kazini kuendelea kuwahudumia Watanzania kwa moyo wote
 
Jumanne, Septemba 18, 2012 05:45 Asifiwe George na Aziza Juma, Dar es Salaam *Wajutia mgomo wao uliofanyika hivi karibuni *Wasema hawapo tayari kushiriki tena mgomo MADAKTARI wanaofanya kazi chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (Interns), wameomba radhi kwa wananchi na Serikali kutokana na madhara ya mgomo wao uliofanyika hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Walioathirika na Mgomo, Paul Swakala, alikiri kuwa mgomo huo umesababisha madhara makubwa. Swakala alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa chama chake pia kinakusudia kwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete, kwa lengo la kumwomba radhi. "Tunatumia fursa hii kupitia kwenu waandishi wa habari kuwaomba radhi Watanzania wote na kwa Serikali kutokana na madhara yaliyosababishwa na migomo ile ambayo ushiriki wetu ulikuwa hauepukiki. "Tunajua kuwa wapo watu walioathirika na mgomo ule, hivyo tunawaomba radhi kwa Watanzania wote walioathirika na mgomo, pia kwa usumbufu uliojitokeza. "Pamoja na kwamba utamaduni wa kuomba radhi hadharani kwa nchi yetu haujazoeleka, lakini tumeamua kufanya hivyo kwa sababu sisi ni binadamu na watu wote tuna upungufu. "Pia tunamwomba radhi Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake kwa usumbufu uliosababishwa na mgomo ule, vile vile tunatambua na kuunga mkono juhudi zake katika kuboresha huduma za afya nchini pamoja na changamoto nyingi ambazo zinaikabili sekta hiyo nchini. "Hata hivyo, tutazidi kuiomba Serikali iangalie zaidi sekta hii, kwani maisha ya Watanzania wengi yanategemea huduma bora za sekta hiyo. "Tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa sisi vijana wao hatupo tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania wenzetu," alisema. Swakala alisema kuwa madaktari wanajutia sana kosa hilo na wako tayari kurejea kazini kuendelea kuwahudumia Watanzania kwa moyo wote

Hiyo habari tunajua tokea jana, kama ulikuwa usingizini ni wewe
 
Tuwatie moyo, kuomba msamaha ni suala la busara sana na kila mtu anapitia humo hakuna asiyekuwa mkosaji katika maisha yake, wenye mamlaka waangalie na kuona umuhimu wa kuwasamehe.

Walikosa nini ?, kwa hiyo walikuwa wanadai upuuzi! Shame up on them!
 
Sasa awasamehe kwa lipi ? Kwa hiyo madai yao yote yalikuwa uongo ? Basi kama yalikuwa uongo wafutwe kazi
Hawa vijana hawana akili kama kweli waliyoyasema ilikuwa sahihi sasa wanaomba msamaha wa nini ?
JK kuwasamehe ni Udhaifu
 
Sisi ni watu wa ajabu sana.
Kupita kiasi!
Nashukuru kwamba niko ktk sekta binafsi, vinginevyo ningekuwa daktari nadhani ningekuwa mmojawapo wa hao wa***avu wachache wanaoiangukia sirikali. Ina maana madai yao yameisha? Ina maana waendelee kuburuzwa na sirikali?
 
Pengine yanayotokea tuliyaandika humu na tuliwaasa kunguni waliojitokeza kuomba msamaha
wakati wa mgomo tuliwaasa sana kama mmeamua muwe makini sana na kama amko pamoja ni bora mkajipange na kabla ya kujipanga anagalieni madhara yake yanayoenda kutokea

Dk Ulimboka aliongea vya kuongea lakini mkono wa serikali mrefu na hapo ndipo walipoamini wakati aliporudi sipendi kusema mlikosea naamini mlifanya mkumbo kukimbilia mgomo sasa basi naomba kama mmeomba msamaha basi nendeni kwenye makaburi ya kinondoni ama ya Dar yote mkaombe mlichofanya na upumbavu wenu kabla ya kusamehewa na serikali

nawaambia hivi kwakuwa wakati watu wanakufa muhimbili mlikuwa mkiwaona sasa basi mkihisi serikali ikiwasemehe imetoka, la hasha mkono wa Mungu ni mrefu kuliko serikali yenu simameni mbele ya watanzania muombe radhi kwa wafiwa wote waliokutwa na upumbavu wenu.
 
Pengine yanayotkea tuliyaandika humu na tuliwaasa kunguni waliojitokeza kuomba msamaha
waakti wa mgomo tuliwasaa sana kama mmeamaua muwe makinisana na kama amko pamoja ni bora mkajipange na kabla ya kujipanga anagalien madhara yake yanayoenda kutokea

dk ulimboka aliongea vya kuongea lakini mkono wa serikali mrefu na hapo ndipo walipoamini wakati aliporrudi sipendi kusema mlikosea naamini mlifanya mkumbo kukombilia mgomo sasa basi naomba kama mmeomba msamaha basi nendeni kwenye makaburi ya kinondoni ama ya dar yote mkaombe mlichofanya naupumbavu wenu kabla ya kusamehewa na serikali

nawaambia hivi kwakuwa wakati watu wanakufa muhimbili mlikuwa mkiwaona sasa basi mkihisi serikali ikiwasemehe metoka la hasha mkono wa mungu ni mrefu kulikos erikali yenu simameni mbele ya watanzania muombe radhi kwa wafiwa wote waliokutwa na upumbavu wenu

mwisho nasema kuliko uwe dk bora uitwe mpumbavu kwa kweli

Mkuu Pdidy, nakushauri;

1. Jifunze Uandishi, UPYA...Habari au hoja haijengwi namna hiyo hapo juu, kuanzia kichwa cha uzi na yaliyo ndani yake.

2.Unajishushia HESHIMA, wewe na wale "unaotaka kuwawakilisha" kwa lugha yako ya kejeli zisizo na msingi.

3. Jifunze kustahimili HISIA(hasira na chuki), hasa unapotaka kuandika jambo.

Mwisho, kama mmoja wa wale uliowatukana na wewe KUSHAWISHI watu wenye akili zao TIMAMU bora wawe "wapumbavu" ..nakukumbusha kuwa " kutamani UPUMBAVU" kama ulivyosema hapo mwisho ni kujidhalilisha unless hujui MPUMBAVU ni mtu wa aina gani Mkuu.
 
i can see ur anger, wajinga wakubwa hawa. na nisiwasikie tena wakilalamikia upuuzi wao wa kuboreshewa mazingira ya kazi.
 
Pdidy umeandika ujinga hapa! Jifunze kujenga hoja na kuwa subjective
 
Back
Top Bottom