Nijuavyo mimi, mgomo haukuwa na SHURUTI, ila HIARI..then if so, iweje leo wajitokeze na kusema "walidanganywa", hoping that we are great thinkers, does it ring a bell anyhow with their reason?..i dont think so...na hapa ndio walipokosea, kuchanganya kati ya SUBIRA na UKIMYA!!
Nadhani;
WIVU na KUTOJIAMINI:
Mkuu, takribani madaktari 400ambao watahitimu mwaka huu wamepangwa katika hospitali tayari, "wakichukua" nafasi yao, sasa nashindwa kuelewa kwanini baada ya kuona jambo hili likitokea ndio wakumbuke "msamaha" unapaswa kutoka...nisingependa kutoa maneno ya kashfa kwa madaktari wenzangu kwa kiwa ni wanafamilia(kitaaluma), lakini nina uhakika msamaha si wa DHATI ila kurudishwa.
SUBIRA:
Kwa daktari wa kitanzania akaaye masaa 30 macho kabla ya kukabidhi shift nyingine akiwa sehemu mbali mbali (wodini,chumba cha upasuaji,kliniki nk) ambaye amekwishazoea "kutingwa" na utitiri wa kazi, kusubiri bila kufanya kazi, ni MATESO, na hasa inapokuja suala la kimahakama...tofauti na hospitali, mahakama hutaja kesi kwa mpango wake, na huitaji SUBIRA ya hali ya juu kupata kusikilizwa kwa kesi yako..hii imetafsiriwa kuwa ni UKIMYA wa MAT hata mara baada ya MAT kutamka "tusubiri jambo hili lipo kisheria" katika mtandao wao kutokana na wengi(madaktari WALIOFUKUZWA kuwa nje ya jiji na hivyo kuwa ngumu katika kuitisha mkutano physically)
KIBURI:
Ilikuwa ni shida kwao(madaktari "WALIOATHIRIWA" na mgomo kuendelea kusubiri mtaani baada ya kushindwa kwenda nje au kuwa katika ajira binafsi but above all nielewavyo mimi...madaktari wa kitanzania "tuna viburi" at times..na ninasema hivi kwasababu ANTICIPATION before war/battle or any crisis for that matter it's not questionable, lakini kwa baadhi ya madaktari wakitambua kuwa mgomo unaweza kuwatoa kazini.
Kuna msemo unasema "usichague nguo ya kujisitiri ikiwa uko uchi" ..kama mtu aliondoshwa kazini, nijuavyo mimi katika kujisitiri angekuwa na vijikazi vidogo vidogo vimtunze kwa muda hadi pale maamuzi ya mahakama yatapotoka...lakini jambo hili lilikuwa next to impossible kwa baadhi ya madaktari..wakijifariji kwa maneno, "utaua fani", lakini ninachoshindwa kuelewa je fani hiyo ilikuwa "haifi" wakati ukiwa idle??!...but this was used as scapegoat, the truth being Kujishusha ili kufanya kazi hata kama ina kipato kidogo kuliko ulichokuwa unapata ni shida!! wengi walitaka kipato sawa au zaidi..na hicho ndio ninachoita KIBURI.
-lakini mtu anaweza kutafsiri ninawahukumu/kulaumu bure na kuwa sasa ndio "wamejishusha"..ofcourse they have, but is it genuine?..
ingekuwa ni jambo rahisi kuomba msamaha kama suala halipo mahakamani, na takribani wiki mbili zilizopita Mh. Hussein Mwinyi(Waziri wa Afya) alipokuwa pale MNH na MOI alisema "serikali haijawafukuza intern doctors, bali MCT itawaita mmoja mmoja kuwahoji".. sasa swali ni kwamba msamaha huu utabatilisha maamuzi ya Serikali? vipi mahakama na MCT?