Wizara ya Afya: Taarifa ya uchunguzi - Baraza la adaktari Tanganyika linaendelea kuendesha Mitihani ya Watarajali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Madaktari Tanganyika kuendelea kuendesha mitihani miwili ya kabla na baada ya Utarajali kwa Madaktari wote nchini wanaomaliza vyuo na kuuanza mafunzo kwa vitendo.

Waziri Ummy amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa kamati huru kuhusu ufaulu wa mitihani ya watarajali inayoendeshwa na Baraza la Madaktari Tanganyika kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Prof. Mohammed Kambi.

Waziri Ummy amesema Daktari yeyote aliyemaliza masomo yake katika vyuo vya udaktari ndani na nje ya nchi ili apate leseni ya Udaktari ni lazima afanye mtihani wa kabla ya utarajali na baada ya kukamilisha kipindi cha utarajali.

Aidha, Waziri Ummy amelitaka Baraza la Madaktari Tanganyika kuzingatia miongozo ya alama za ufaulu kama ilivyoelekezwa ili kusimamia taaluma ya Udaktari na endapo Daktari atashindwa kufikia alama zilizopendekezwa kwenye muongozo itabidi arudie mitihani.

Waziri Ummy ameliagiza Baraza la Madaktari Tanganyika kutoruhusu daktari aliyefeli Mtihani wa utarajali kuendelea na mafunzo kwa vitendo badala yake itamlazimu arudie mtihani huo mpaka afaulu ndipo aendelee na mafunzo kwa vitendo (Internship).

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na na vyuo na taasisi za Ithibati ili kuboresha mafunzo kwa upande wa Madaktari wakiwa vyuoni.

Waziri amesema Wizara ya Afya itaendelea kutimiza jukumu la kumlinda Mwananchi kwa kuhakikisha anapata huduma bora kutoka kwa wanataaluma wa Afya waliothibitishwa na Mabaraza ya kitaaluma kuwa ulinganifu na ubora unaotakiwa utakaowezesha kutoa huduma za afya bora kwa wananchi.

Akiwasilisha mapendekezo ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo prof. Mohammed Kambi amesema Kamati imependekeza mitihani ya utarajali kuendelea kufanyika licha ya madaktari kulalamikia ufaulu mdogo huku akilitaka Baraza la Madaktari Tanganyika kutoa alama za ufaulu kwa madaktari waliofanya mitihani hiyo.

1699021631662.jpeg

1699021674657.jpeg

1699021744795.png

1699021842042.jpeg

Pia soma:
1.
Barua ya wazi ya Madaktari Watarajali kwenda kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
2. Baraza la Madaktari lawajibu Madaktari Watarajali waliodai hawana imani na MCT
3. UPDATE: Wizara ya Afya yaunda Kamati kuchunguza Malalamiko ya Madaktari Watarajali
4. Baraza Madaktari Tanzania (MCT) lamgomea Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu Madaktari Watarajali
 
Hizi habari sio nzuri kwa , Wanaoamini katika Vitendo, Waogopa mitihani, waliofaulu kwa mchongo,

Ngoja niulize, hii haiwahusu ma CO? Mbona kuna walio ajiriwa Ajira zile za juni hawakupitia huko? Au ni mfumo mpya?
 
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Madaktari Tanganyika kuendelea kuendesha mitihani miwili ya kabla na baada ya Utarajali kwa Madaktari wote nchini wanaomaliza vyuo na kuuanza mafunzo kwa vitendo.

Waziri Ummy amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa kamati huru kuhusu ufaulu wa mitihani ya watarajali inayoendeshwa na Baraza la Madaktari Tanganyika kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Prof. Mohammed Kambi.

Waziri Ummy amesema Daktari yeyote aliyemaliza masomo yake katika vyuo vya udaktari ndani na nje ya nchi ili apate leseni ya Udaktari ni lazima afanye mtihani wa kabla ya utarajali na baada ya kukamilisha kipindi cha utarajali.

Aidha, Waziri Ummy amelitaka Baraza la Madaktari Tanganyika kuzingatia miongozo ya alama za ufaulu kama ilivyoelekezwa ili kusimamia taaluma ya Udaktari na endapo Daktari atashindwa kufikia alama zilizopendekezwa kwenye muongozo itabidi arudie mitihani.

Waziri Ummy ameliagiza Baraza la Madaktari Tanganyika kutoruhusu daktari aliyefeli Mtihani wa utarajali kuendelea na mafunzo kwa vitendo badala yake itamlazimu arudie mtihani huo mpaka afaulu ndipo aendelee na mafunzo kwa vitendo (Internship).

Kwa upande mwingine Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na na vyuo na taasisi za Ithibati ili kuboresha mafunzo kwa upande wa Madaktari wakiwa vyuoni.

Waziri amesema Wizara ya Afya itaendelea kutimiza jukumu la kumlinda Mwananchi kwa kuhakikisha anapata huduma bora kutoka kwa wanataaluma wa Afya waliothibitishwa na Mabaraza ya kitaaluma kuwa ulinganifu na ubora unaotakiwa utakaowezesha kutoa huduma za afya bora kwa wananchi.

Akiwasilisha mapendekezo ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo prof. Mohammed Kambi amesema Kamati imependekeza mitihani ya utarajali kuendelea kufanyika licha ya madaktari kulalamikia ufaulu mdogo huku akilitaka Baraza la Madaktari Tanganyika kutoa alama za ufaulu kwa madaktari waliofanya mitihani hiyo.

View attachment 2802621
View attachment 2802623
View attachment 2802625
View attachment 2802627

Pia soma:
1.
Barua ya wazi ya Madaktari Watarajali kwenda kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
2. Baraza la Madaktari lawajibu Madaktari Watarajali waliodai hawana imani na MCT
3. UPDATE: Wizara ya Afya yaunda Kamati kuchunguza Malalamiko ya Madaktari Watarajali
4. Baraza Madaktari Tanzania (MCT) lamgomea Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu Madaktari Watarajali
Safi sana, itasaidia kuboresha huduma na viwango, nchi zingine wapo strict, ni Tanzania tu udaktari unaonekana mrahisi kila mjinga anasoma.
 
Back
Top Bottom