Sina imani na Kamati Huru iliyoundwa na Ummy Mwalimu kufuatilia sakata la Madaktari Watarajali

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Nianze kwa kupongeza uamuzi wa Serikali kuamua kuitikia wito wa kuunda Tume ya kufuatilia suala la Madaktari Wahitimu Watarajali Nchini.

Uamuzi huo unaonesha wazi Serikali ipo kazini na ina nia ya kweli ya kuwasaidia Wananchi wake kwa kuwa ukifuatilia hoja za Wanataaluma hao wa Udaktari zina mashiko na kweli kuna vitu havipo sawa.

Sina haja ya kueleza mengi kuhusu hoja hizo, nitaweka link hapo chini usome mwenyewe.

Hoja yangu ni kuwa hii Kamati Huru iliyoundwa na Waziri kuchunguza nina mashaka nayo kama itafanya kile hasa ambacho kinatarajiwa kutoka kwa wahusika hawa waathirika au walalamikaji.

Waziri Ummy Mwalimu katika Kamati Huru amejumuisha jina la Dkt. Emmanuel Gambi ambaye ni MJUMBE na amemtambulisha kuwa ni Daktari Mtarajali na kiongozi wa Watarajali Morogoro.

Hapo ndipo tatizo linapoanzia, huyu bwana sio Mtarajali wala hakuwahi kushiriki katika mchakato wa malalamiko ya Watarajali.

Ruge alisema “Ogopa Mungu na Teknolojia”, ukiingia kwenye system ya Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) ambayo ipo wazi na hata wewe unaweza kuingia, utalikuta jina la Dkt. Huyo kuwa ni Daktari kamili na ana Leseni kabisa kama nilivyoambatanisha details zake.
Gambi.JPG

Kwa ambaye hana ufahamu kidogo, hao Watarajali ambao waliandika barua kwenda kwa Rais Samia, ni Wanataaluma wenye elimu ya udaktari lakini hawajakamilisha taratibu kwa maana hawana leseni za udaktari, sasa huyu Dkt. Gambi anaingiaje kuwa mwakilishi wao?

Kamati nzima haina mwathirika hata mmoja, tutaaminije hao wengine waliopo kwenye hiyo Kamati?

photo_2023-08-14_11-12-35.jpg

Gambi 2.jpg
Link: Madaktari Tarajali wanatoa malalamiko yao dhidi ya Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT)
 
Kesi ya nyani kapewa ngedere. Hawa watakaangwa kama wenzao wa sheria, wataambiwa hawana akili na wanaendekeza starehe badala ya masomo.

Bongo raha ya professor ni kuona wanafunzi wake wanafeli.
 
Tatizo serikali yetu haipo makini. Uhuni uhuni tu. Huku ni kumpa Gambi tonge mdomoni.
 

Attachments

  • Madaktari_DOSARI & MAONI-WPS_Office[1]_a.pdf
    6.6 KB · Views: 7
Back
Top Bottom