GE2025 Mgombea Urais, Coaster Kibonde: Nikishinda Urais, Rais Samia atabaki Ikulu

GE2025 Mgombea Urais, Coaster Kibonde: Nikishinda Urais, Rais Samia atabaki Ikulu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini, Coaster Jimmy Kibonde, amesema endapo atashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, atamwacha Rais wa sasa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndani ya serikali yake kwa nafasi maalumu ya kushughulikia diplomasia.

Kibonde, ambaye amezungumza kupitia kipindi cha Clouds360 cha Clouds TV, amesema amegundua Dkt. Samia ni mwanadiplomasia mahiri, hivyo atamkabidhi jukumu la kuongoza dawati maalumu litakalokuwa na idara tatu zinazoshughulika na masuala ya kisiasa, kiuchumi na ya kimataifa.

“Nimesema nikishinda urais, Mama Samia nitamwacha Ikulu. Nimegundua Mama Samia ni mwanadiplomasia mzuri mno. Kwenye diplomasia ya kisiasa, kiuchumi na mambo ya nje yuko vizuri. Kwa hiyo atakuwa mkuu wa dawati maalumu katika serikali yangu. Asiwe na presha, ajira nimeshamuahidi,” amesema Kibonde.
Yaani hawa ndiyo washindani wa Samia kwenye uchaguzi wa mwaka huu View attachment 3438558
Samia kakuona subiria teuzi
 
Huyo ni mwanafalsafa, anaongea kifalsafa. Ukiwa mijinga mijinga tu wa kupigwa tone tone huwezi kuelewa chochote hapo
 
Kuna haja gani ya kuweka taarifa za mtu kama huyu jmn - ihurumieni Tanzania jmn
 
Alafu kuna watu wanataka tupoteze muda wetu kwenda kupanga foleni kupiga kura

Huo muda bora niutumie shambani kwangu nikiandaa mashamba kuliko kupoteza kupiga kura
 
Tanganyika tuna utani mwingi. Tunajali matumbo yetu badala ya kupigania kupata mifumo bora ya kuongoza nchi yetu ifanyiwe marekebisho (Reforms).
 
Kuna vitu vinashangaza sana.
Huyu mtu ni mshindani wa Samia au mpiga kampeni wake?
Yani sijawahi kuona mpinzani ambae badala amwage sera zake yeye ni fully kumsifia mshindani wake?
Screenshot_20250812_034913_Instagram.jpg
 
Kuna vitu vinashangaza sana.
Huyu mtu ni mshindani wa Samia au mpiga kampeni wake?
Yani sijawahi kuona mpinzani ambae badala amwage sera zake yeye ni fully kumsifia mshindani wake?
Hapo tatizo liko wapi, au mmezoea hizo siasa za kufokafoka, za chuki, fitina, uhasama, visasi, za matusi. Hiyo ndiyo siasa za kistaarabu
 
Alitakiwa atukane na kufoka foka hadi mate yaloweshe microphone, mishipa imjae, jasho litiririke, na lugha mbovu mbovu ( ndiyo ataonekana ni mpinzani wa kweli)😏
 
Hii nchi bana
Yani mtu anakaa zake huko tu anaamua kuchekesha umma.
 
Back
Top Bottom